Nape Nnauye: Gari lililotumika kumshambulia Lissu limewahi kuripotiwa kuwa linawafuatilia baadhi ya wabunge

Hahah Nape chonde chonde japo sukuwahi kukupenda ila hapa nakuonya waliomkosa Lisu sina uhakika kama watakukosa wewe
 
Mm cna chama na sintakua mwanachama wa chama chochote cha siasa. Nape acha konakona na kutafta kick kama harmorapa kila kukicha, hama hata sasa. Tatizo la siasa za Tz, viongozi mnatoa matamko ya kujenga chuki baina ya watz kuptia vyama vyenu then yanaleta uadui kwa watz ksha mnapatana nasi kubaki maadui. Hua namtukana sana Mdee Twitter ni mnafiki sn yule Dada. Asbh ataongea hv kuhamasisha ukawa wasmpende kiongozi flani then jioni anamsifia eti siasa haina adui wa kudumu. Watz, hii ni nchi yetu sote tusiishi kwa matamko gombanishi ya wanasiasa. Ni watu wapuuzi sana hawafai hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
ukigombana na watu kwa ajili ya siasa hata wewe huna akili kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Dodoma. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ametoa yake ya moyoni na kusema;.

"Mimi hili nalisema hadharani. Hii gari imekuwa ikifuatilia baadhi ya Wabunge hapa, mimi nikiwa mmoja wapo. Tulienda tukaripoti kwamba jamani kuna gari inatufuatiliana hatuelewi ni gari ya nani.

Sasa gari hiyo hiyo, namba hizo hizo, idadi ya watu hao hao, halafu watu wanaripoti hatua hazichukuliwi mpaka mwenzetu anafikia hatua ya kupigwa risasi, mimi nadhani ni jambo kubwa.

Ndo maana nikasema, yeye lisu ambaye Maswahiba yamemfika, sisi wengine tuliambiwa wanatufuatilia na tukathibitisha kwamba kweli wanatufuatilia, lakini yeye yamempata kabisa!..kwa kushambuliwa. Nadhani yeye anaweza kutueleza mengi kabisa. Nina hakika Lissu, dereva wake, wana mengi ya kusimulia juu ya hili.

Kwa kuwa alililalamikia kwa muda mrefu basi nadhani ni vizuri yeye aje atueleze. Ukiacha vyombo vya usalama kuchukua hatua lakini na yeye aje atuambie experience, naamini yale aliyoyasema wakati wa nanii yake na wandishi wa habari hakuyasema yote, aje aseme na mengine ambayo hakuyasema". Ameongeza Nape.

Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe niwatuhumiwa, hama CCM mjomba.

”Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.
Nape%20Nnauye.jpg

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu walipokutana jana kabla ya mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Nape Nnauye jana kabla ya Tundu Lissu kupigwa risasi majira ya saa 7 mchana anadai alikutana naye na kuongea naye katika viwanja vya bunge na baadaye kuja kupata taarifa kuwa amepigwa risasi na watu wasiojulikana.

"Masaa machache kabla ya kushambuliwa kwa risasi jana! Naamini mjomba utarudi utueleze ukweli wa wauaji hawa! Hasa 'the T460CQV' uliyoilalamikia"aliandika Nape Nnauye kweye mitandao yake ya jamii.

Mpaka sasa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yupo nchini Kenya akipatiwa matibabu kufuatia majeraha ambayo ameyapata katika mwili wake
Nape%20Nnauye%20.jpg



Mmmmmmh
 
Watu wanapoona kuna adui anayewafuatilia inabidi kuchukua hatua dhidi yake.
Kuna tatizo hapa, wabunge wafuatiliwe wajue kuna watu wenye nia ovu dhidi yao, halafu waendelee kusubiri matokeo?
Kwa nini wasibuni mbinu ya kupambana na maadui? Hata kwa kutafuta picha zao tu?
 
Acha Upuuzi hiyo ni picha iliyopigwa na Mwananchi jana wakati wanatoka Bungeni.

Ukifuatilia alichokisema Nape Nnauye hakuna sehemu aliyosema kuwa ni Rafiki yake ila kabla ya kwenda kula baada ya vikao vya asubuhi Nape aliongea na Lissu.

Get life kijana, sisi ni Watanzania baadhi ya wapuuzi wanataka kusema ni lao chadema.

Wewe siyo mtanzania bali wewe ni mccm.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watanzania bhana...
Kila mtu kwa sasa ni rafiki wa Tundu Lissu!
Ni urafiki au ushahidi muhimu huu Nape anauleza !! tena kuusema haraka ndio salama ya maisha yake pia .nyie maccm kwanini ukisoma habari unakimbilia kufikiria jibu badala ya kutafakari kwanza !!!??? Sio bure ataa bosi wenu kudai alimtuma Mruma miaka nne iliopita kuwa undercover urgency !!!
 
Back
Top Bottom