Nape Nnauye: Gari lililotumika kumshambulia Lissu limewahi kuripotiwa kuwa linawafuatilia baadhi ya wabunge

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,224
Dodoma. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ametoa yake ya moyoni na kusema;.

"Mimi hili nalisema hadharani. Hii gari imekuwa ikifuatilia baadhi ya Wabunge hapa, mimi nikiwa mmoja wapo. Tulienda tukaripoti kwamba jamani kuna gari inatufuatiliana hatuelewi ni gari ya nani.

Sasa gari hiyo hiyo, namba hizo hizo, idadi ya watu hao hao, halafu watu wanaripoti hatua hazichukuliwi mpaka mwenzetu anafikia hatua ya kupigwa risasi, mimi nadhani ni jambo kubwa.

Ndo maana nikasema, yeye lisu ambaye Maswahiba yamemfika, sisi wengine tuliambiwa wanatufuatilia na tukathibitisha kwamba kweli wanatufuatilia, lakini yeye yamempata kabisa!..kwa kushambuliwa. Nadhani yeye anaweza kutueleza mengi kabisa. Nina hakika Lissu, dereva wake, wana mengi ya kusimulia juu ya hili.

Kwa kuwa alililalamikia kwa muda mrefu basi nadhani ni vizuri yeye aje atueleze. Ukiacha vyombo vya usalama kuchukua hatua lakini na yeye aje atuambie experience, naamini yale aliyoyasema wakati wa nanii yake na wandishi wa habari hakuyasema yote, aje aseme na mengine ambayo hakuyasema". Ameongeza Nape.

Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe niwatuhumiwa, hama CCM mjomba.

”Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.
Nape%20Nnauye.jpg

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu walipokutana jana kabla ya mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Nape Nnauye jana kabla ya Tundu Lissu kupigwa risasi majira ya saa 7 mchana anadai alikutana naye na kuongea naye katika viwanja vya bunge na baadaye kuja kupata taarifa kuwa amepigwa risasi na watu wasiojulikana.

"Masaa machache kabla ya kushambuliwa kwa risasi jana! Naamini mjomba utarudi utueleze ukweli wa wauaji hawa! Hasa 'the T460CQV' uliyoilalamikia"aliandika Nape Nnauye kweye mitandao yake ya jamii.

Mpaka sasa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yupo nchini Kenya akipatiwa matibabu kufuatia majeraha ambayo ameyapata katika mwili wake
Nape%20Nnauye%20.jpg
 
Watanzania bhana...
Kila mtu kwa sasa ni rafiki wa Tundu Lissu!
Acha Upuuzi hiyo ni picha iliyopigwa na Mwananchi jana wakati wanatoka Bungeni.

Ukifuatilia alichokisema Nape Nnauye hakuna sehemu aliyosema kuwa ni Rafiki yake ila kabla ya kwenda kula baada ya vikao vya asubuhi Nape aliongea na Lissu.

Get life kijana, sisi ni Watanzania baadhi ya wapuuzi wanataka kusema ni lao chadema.
 
Aah..wamemuachia mbowe na Msigwa waende..tusije laumiana kwa lolote
 
Mungu ni mwema.

Kamfikirisha maneno mazito, kamthibitishia hayo maneno, halafu amemuokoa.

Get well soon Lisu
 
Hahahahhhaha nazidi kuamini hili jambo lilipangwa... Hahahaha eti Lissu na Nape ni mtu na mjomba wake na Wema naye anasema Lissu ni mjomba wake....

Unfiki Mbaya sana na sitoshangaa hata Simba chawene kusema Lissu ni kaka yake hahaha....maigizo tuu
Mkuu, unaukumbuka ule uzi wako uliosema, nanukuu.."hawa watu wapo tayari hata kumwaga damu ili wabaki madarakani"

Unaukumbuka?
 
Hahahahhhaha nazidi kuamini hili jambo lilipangwa... Hahahaha eti Lissu na Nape ni mtu na mjomba wake na Wema naye anasema Lissu ni mjomba wake....

Unfiki Mbaya sana na sitoshangaa hata Simba chawene kusema Lissu ni kaka yake hahaha....maigizo tuu
ndio maana nilishauri mkae kimya maana nguvu mnayo itumia vijana wa CCM kujiepusha na sakata hili naiona ni zaid ya hydroelectric mnatutia mashaka makubwa nyie watu naona mmekazana na wote hoja zenu zafanana
1. kiki
2. accacia

naona karibu watetezi wa ccm woote hasa wa mitandao hoja zenu hizo hizo jaman kaeni kimya muviachie vyomba husika vyenyewe ndio vitajua ni kiki au laa na niwaombe mkiombwa waje external investigators kuutafuta ukweli mkubali kwa moyo mmoja msikimbilie kusema vyombo vyetu havijashindwa
 
Hahahahhhaha nazidi kuamini hili jambo lilipangwa... Hahahaha eti Lissu na Nape ni mtu na mjomba wake na Wema naye anasema Lissu ni mjomba wake....

Unfiki Mbaya sana na sitoshangaa hata Simba chawene kusema Lissu ni kaka yake hahaha....maigizo tuu
Mama yake Nape ni wa wapi vile?
 
Back
Top Bottom