Nape Nnauye: Gari lililotumika kumshambulia Lissu limewahi kuripotiwa kuwa linawafuatilia baadhi ya wabunge

Sio mda tutasikia naye kakamatwa kwa tuhuma za uchohezi. Hakika ukikaa nje ya uwanja makosa ya wachezaji yanaonekana kwa macho mawili.


Vyovyote iwavyo, kwa akili za kawaida tu hatihitaji mpaka Lissu apone aje kusema, ila ukweli uko mioyoni mwetu.


"LISSU YUKO HAI NA ATAENDELEA KUWA HAI KWA NGUVU ZA MUNGU"
Labda kuisaidia police lakini sio kwa uchochezi.
Taarifa kama hizi ni muhimu sana kuwatambua wauwaji.
 
Nadhani sasa hivi inabidi mbinu za self defence tuanze kuzitumia..hivi sasa mimi maanza kupiga counter attacks tu ikitokea nimekuhisi halafu kumbe siyo basi chukua kabisa pole yako in advance
 
INASHINDIKANA nini kufahamu hilo gari linawafuatilia limetoka wapi? Hii ni ajabu sana gari liko humuhumu halifafahamiki ni la nani.Mara lina watu wasiojulikana.Mpaka karne hii Tanzania mtu anaweza kupanga uhalifu na kuufanya na asijulikane akiwa humuhumu ndani.Hii ni hatari sana.
 
Troll JF you are a hypocrite, more dangerous than a dishonest man. A dishonest man deceives and cheats, and a hypocrite betrays and swindles.

Remember that, God has given you one face, and you always make yourself another.You were talking all dirty and inciting all evil towards Tundu Lissu.

Why today, you are trying to be on his side whilst we all know you do not mean it?

Shame on you
m
Not Nape i know. or you are talking about whom? Nape is one of the very few civilized and concious ccm members. period
 
Mnapotoka kwenye jambo muhimu mnaanza kujenga Chadema humu JF hapo ndipo mnakosa maana kabisa........++++++!!!

Hili ni jukwaa huru kila mtu anaweza kuhimiza analopenda litimie ikiwa ni kujenga chama, kukuza biashara au kupata mchumba, ili mradi huvunji sheria.
 
ad157fe7781064c216bdacb180445aa1.jpg
FB_IMG_1504880917630.jpg


try me
 
Sasa kwa kusisitiza kwamba 'aje atuambie' si ndio mnawaambia wale jamaa wahakikishe hiyo stori wanapelekewa kina Bob Marley na Martin Luther badala ya sisi....nadhani mngekauka kwanza apone arudi.
 
Dodoma. Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye ametoa yake ya moyoni na kusema;.

"Mimi hili nalisema hadharani. Hii gari imekuwa ikifuatilia baadhi ya Wabunge hapa, mimi nikiwa mmoja wapo. Tulienda tukaripoti kwamba jamani kuna gari inatufuatiliana hatuelewi ni gari ya nani.

Sasa gari hiyo hiyo, namba hizo hizo, idadi ya watu hao hao, halafu watu wanaripoti hatua hazichukuliwi mpaka mwenzetu anafikia hatua ya kupigwa risasi, mimi nadhani ni jambo kubwa.

Ndo maana nikasema, yeye lisu ambaye Maswahiba yamemfika, sisi wengine tuliambiwa wanatufuatilia na tukathibitisha kwamba kweli wanatufuatilia, lakini yeye yamempata kabisa!..kwa kushambuliwa. Nadhani yeye anaweza kutueleza mengi kabisa. Nina hakika Lissu, dereva wake, wana mengi ya kusimulia juu ya hili.

Kwa kuwa alililalamikia kwa muda mrefu basi nadhani ni vizuri yeye aje atueleze. Ukiacha vyombo vya usalama kuchukua hatua lakini na yeye aje atuambie experience, naamini yale aliyoyasema wakati wa nanii yake na wandishi wa habari hakuyasema yote, aje aseme na mengine ambayo hakuyasema". Ameongeza Nape.

Nape amesema Lissu alimwambia, “Wewe Nape ni mjomba wangu, kwa nini unabaki CCM? Mimi na wewe tunafuatiliwa na jamaa zako wakitumia gari moja. Mimi na wewe niwatuhumiwa, hama CCM mjomba.

”Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi mchana na kupelekwa chumba cha upasuaji katika Hospitali ya Rufaa ya Dodoma na baadaye usiku alihamishiwa Hospitali ya Aga Khan ya Nairobi nchini Kenya.
Nape%20Nnauye.jpg

Mbunge wa Mtama Nape Nnauye na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu walipokutana jana kabla ya mbunge huyo kupigwa risasi na watu wasiojulikana.

Nape Nnauye jana kabla ya Tundu Lissu kupigwa risasi majira ya saa 7 mchana anadai alikutana naye na kuongea naye katika viwanja vya bunge na baadaye kuja kupata taarifa kuwa amepigwa risasi na watu wasiojulikana.

"Masaa machache kabla ya kushambuliwa kwa risasi jana! Naamini mjomba utarudi utueleze ukweli wa wauaji hawa! Hasa 'the T460CQV' uliyoilalamikia"aliandika Nape Nnauye kweye mitandao yake ya jamii.

Mpaka sasa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu yupo nchini Kenya akipatiwa matibabu kufuatia majeraha ambayo ameyapata katika mwili wake
Nape%20Nnauye%20.jpg

Siasa rahisi hizi. Kwani mtu akiamua kuropoka hata kwa kukopi na kupaste ni lazima iwe kweli? Huyu nae aangalie wenzie kina Ngonyani na Chawene hawajapanic mbona?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Giza likizidi sana nuru ipo jirani! Watafahamika tu kwa uwezo uleule uliomwokoa! Msisahau hakuna siri chini ya mbingu na damu ya asiye na hatia humlilia aliyeimwaga daima na kumwandama yeye na uzao wake daima. Tubuni ili mpate kusamehewa!
Nape na Bashe walishasema kuwa usalama wa taifa ndo watesi wao, leo kaweka msisitizo tu
 
Acha Upuuzi hiyo ni picha iliyopigwa na Mwananchi jana wakati wanatoka Bungeni.

Ukifuatilia alichokisema Nape Nnauye hakuna sehemu aliyosema kuwa ni Rafiki yake ila kabla ya kwenda kula baada ya vikao vya asubuhi Nape aliongea na Lissu.

Get life kijana, sisi ni Watanzania baadhi ya wapuuzi wanataka kusema ni lao chadema.
Wewe ni mmoja wa maadui wa Chadema humu jf , nyuzi unazoanzisha kuhusu Lissu zinaangaliwa kwa jicho la tatu .
 
Back
Top Bottom