Uchaguzi 2020 Nape Nnauye ateuliwa kuwania Ubunge jimbo la Mtama peke yake baada ya wagombea wengine kukosa baadhi vya vigezo

APITA BILA KUPINGWA UBUNGE MTAMA Lindi:

Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Mtama mkoani Lindi, Samuel Warioba Gunza amemtangaza Nape Nnauye mgombea ubunge kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi kuwa mgombea pekee wa jimbo hilo.

Pia soma => Uchaguzi 2020 - Nape Nnauye anaelekea kupita bila kupingwa Jimbo la Mtama, mgombea CHADEMA alikamatwa jana huku ACT-Wazalendo wakiwa hawana mgombea
Huyu mtu ana uwezekano mkubwa sana wa kurudi kwenye nafasi yake ya mwanzo kwenye Baraza la Mawaziri linalofuata. Kuna dalili hizo.Asipoingia mwanzoni, basi anaweza akaja akaingia baadaye kule mbele ya safari kama kuna chochote kitatokea! Aliachia ngazi kwa haki kabisa, ila kwangu mimi ni kati ya watu ambao niliwahi kusikitika kuwakosa ndani ya Baraza letu la mawaziri. Mungu azidi kimbariki.
 
Sioni faida ya kuwa na wabunge wa CCM! Hata sijui huwa wanafanya nini pale bungeni....!.
Huwezi ukaiona faida yao kwa sasa mpaka siku itakapotokea umewakosa. Kuna baadhi ya watu wamejaliwa kuona yaliyopita tu, yajayo hapana
 
.
Pole. Figisu hata kwa Trump uko zipo. Hilo la kutotakiwa kila kijiji nenda nalo kwa umakini
Huo ndio ukweli mkuu....

Sumu iliyopo ni mbaya zaidi..
Imeua biashara
Imeua kilimo
Imeua wafanyakazi
Imeua wanafunzi
Imeua mahusiano yetu ya kimataifa..

Hakika hii ni serikali ya kishetani ambayo ni lazima iondokewe maana Mungu katuletea Tundu Lissu na chadema...
 
Huo ndio ukweli mkuu....

Sumu iliyopo ni mbaya zaidi..
Imeua biashara
Imeua kilimo
Imeua wafanyakazi
Imeua wanafunzi
Imeua mahusiano yetu ya kimataifa..

Hakika hii ni serikali ya kishetani ambayo ni lazima iondokewe maana Mungu katuletea Tundu Lissu na chadema...
Ukweli ni relative.. na mitazamo yetu ya kisiasa inatufanya tuone vitu tunavyotaka.
 
NEC mnawadhalilisha CCM kwa kuwapa wanaume ubunge viti maalum. Yaani mwanaume kabisaaaaa unachekelea kupewa ubunge wa vitu maalum?
CCM ya sasa ni CCM ya kishetani na hovyo Sana, katibu mkuu mzaliwa wa Rwanda, Mwenyekiti Mrundi, lazima CCM ilaaaniwe kwa nguvu kubwa
 
Tumekuwa taifa la madhulumati. Watu hawaoni aibu kusifia na kushabikia huu ushetani.
Halafu hilo jamaa nalionaga linafiki sana.
Mnafiki na dhulumati.
 
Membe ameshatoa tamko lolote juu ya huo?

Hapo si ndo ilifaa iwe ngome ya ACT bara kwa uchaguzi huu.
 
Hivi Zitto si katamba juzi tu kuwa majimbo yote Lindi wanabeba na kuwa Nape ameshapaniki?!?

Nakukumbusha kuwa Mhe Membe alitamba kuwa majimbo yote ya Mtwara na Lindi yaani pamoja na jimbo alilokuwa analiwakilisha bungeni wakati akiwa waziri wa mambo ya nje, Mtama ACT-Wazalendo watayachukua!! Sasa hata jimbo lake la Mtama lishamponyoka!!!! Naamini kwa Tz Bara Act-Wazalendo watapata wabunge 0 yaani ZERO!! Sasa kama Mtama tayari ni lipi limebaki? CCM mbele kwa mbele, hiki siyo kipindi cha 2015.
 
Hata kama wakati wa kupiga kura 28/10 akipiga yeye mwenyewe na mkewe, basi ushindi itatangazwa kura 2 na humna mshindani!! just simple logic!
Ndio maana nimesema huo ubeunge wake hautokani na "mapenzi" ya wananchi wapiga kura. Au hujanielewa?
 
Back
Top Bottom