Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Crap...

Kaungane na Mzee Yusuf mtoe album ya Taarabu..
 
Pamoja na makala ndefu lakini imetulia sana mkuu wasiwasi wangu ni huyu Nape kama ataona kitu hapa hasa wakati huu ambao nguo za kijani kwakwe na mapokezi mikoani tokana na kodi zetu yanamlewesha kabisa. inawezekana umepigia mbuzi gitaa kaka
 
Hata kama hajasoma ila wajumbe wake watampa ujumbe,






Naamini ujumbe mrefu hufafanua kwa mzito wa kuelewa na akisoma ataelewa, na asipobadilika, ataangamia.
 
Nape kama ujumbe huu hautamwingia akilini basi ni sikio la kufa lisilosikia dawa,
 
Kwa asilimia nyingi nakubaliana na tahadhari hiyo! Hasa hili la wafanyabiashara waliobandikwa jina la Ufisadi ni danganya toto kwani si CCM si vyama vyengine walio huru na ufisadi. Ni ajabu Watanzania wanasahau kuwa viongozi walio madarakani na wanasiasa kwa nyakati mbali mbali walishafisadi taasisi za Taifa na ndio maana leo tuko masikini.
 
Naona kijana umeamua kumsimamia Nape kwa mguu mmoja, ohooohohoooo!!!!! mbona umemzidi kiwango?

Lainisha lugha nyakarungu yule jamaa hatakuelewa kabisaaaaaa!!!!!!!!!! piga kazi kijana taifa linawahitaji, tupo pa1.
 
Sasa tuone kama anaweza kusikiliza japo kidogo!!! Nape Kazi kwako.
 
Kiswahili ulichotumia kumfunda ndungu yangu, bado umemuacha porini. Sana sana ndo'atahisi umempatia nguvu za kupuliza zile "tarumbeta za afrika ya kusini'"
 
excellent, asipoelewa basi anamtindio wa ubongo. excellent guy
 
picture-6.jpg

Na Mbasha Asenga - Imechapwa 18 May 2011

Tafakuri

rizione-242.jpg


DINI zote duniani hufundisha watu kutenda mema. Kwa mfano, hukataza kusema uongo, na wazazi wakati wote huwa na wajibu wa kuhakikisha wanawarithisha watoto wao maadili mema. Ni kwa kufanya hivyo tu jamii hukuza maadili mema na kuchukia uovu.

Taasisi nyingine zilizoundwa na wanadamu nazo hujengwa kwenye misingi ya kiuadilifu ili zistawi kwa nia ya kufikia malengo yake; taasisi yoyote inayokwepa uadilifu hata ikistawi kwa kiwango gani, mwisho wake ni kuporomoka tu.

Wiki iliyopita kulikuwa na malumbano makali katika vyombo vya habari, yakihusisha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa upande mmoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa pili.

Hoja kubwa iliyokuwa inabishaniwa ni malipo ya ujira kwa makatibu wakuu wa vyama hivyo. CCM kupitia kwa Katibu wake wa Uenezi na Itikadi, Nape Nnauye, alikuwa akipaza sauti juu ya mshahara wa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Willibroad Slaa, kwamba Sh. milioni 7.1 anazolipwa ni nyingi sana.

Nape alikanusha kwa mdomo mpana habari zilizokuwa zimetolewa na CHADEMA kuwa Katibu wao Mkuu, Wilson Mukama, alikuwa analipwa mshahara wa Sh. milioni 11.

Nape alisema Mukama analipwa Sh. 1. 5 milioni tu na posho ya kila mwezi ya Sh. 300,000, fedha ambazo kwa Nape ni kidogo sana ikilinganishwa na za Dk. Slaa na kwa maana hiyo Dk. Slaa anaonyesha hana uzalendo kwa wananchi wanaoishi maisha ya ufukara ilhlai yeye anayejiita mtetezi wao akilipwa mshahara mnono.

Nape kwa maana hiyo ametaka kuaminisha umma kwamba Mukama analipwa posho na mshahara wa Sh. 1,800,000 tu kwa mwezi. Habari hii inahitaji tafakuri ya kina juu ya ukweli wa kauli ya Nape.

Kabla sijaenda mbali nikumbushe tu yapata wiki mbili au tatu hivi zilizopita, Ridhiwani Kikwete, kada wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) akiwa mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji na Baraza Kuu, naye alijitokeza hadharani akijibu tuhuma dhidi ya ukwasi wake baada ya kuitwa bilionea. Watu walitaka kujua ameupata katika njia gani ambazo zipo wazi.

Ridhiwani alisema hana utajiri wowote, ila anamiliki gari aina ya Toyota Camry ambalo ni la kawaida tu, wala si Hammer kama ilivyodaiwa. Halafu akasema ana akaunti yenye fedha kidogo tu, hakutaja kiasi halisi cha fedha zilizoko, na zipo katika benki zipi hasa; lakini pia akadai kuwa ana shamba la hekari moja kwao Bagamoyo.

Mtandao wa media ya kijamii wa Wanabidii wiki hiyo ulikuwa na jumbe nyingi juu ya suala la Ridhiwani, lakini nilivutika zaidi na mchangiaji mmoja aliyehoji: "hivi hilo shamba la hekari moja la Ridhiwani linajumuisha na kiwanja anachomiliki Burka, Arusha?"

Kiwanja hicho ni kati ya viwanja walivyomilikishwa vigogo mkoani Arusha na kuzua malalamiko ya wananchi wa kawaida ambao hawakupewa viwanja licha kuahidiwa kuwa wangemilikishwa. Jina la Ridhiwani lilikuwa miongoni mwa majina ya vigogo hao.

Nimechukua mifano hii miwili ya makada hawa vijana kujenga hoja moja muhimu ya ‘uadilifu'. Ridhiwani hadi leo hajawahi kukanusha kumilikia kiwanja Arusha, japokuwa binafsi sina ugomvi naye kumiliki kiwanja kokote atakako katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania au kwenye sayari ya dunia, ni haki yake, lakini tatizo ni pale anapokwenda hadharani, mbele ya vyombo vya habari kutaja mali zake, huku akiacha nyingine ambazo kwa bahati nzuri jamii inazifahamu.

Kwa hiyo, jamii inapoona kuwa habari zenyewe za kukanusha na kuweka rekodi sawa ni za kutengenezwa, inajawa na maswali kuliko majibu kwamba hivi hawa vijana wabichi wakitazamwa kama viongozi wa kesho wa taifa hili wanapata wapi ujasiri wa kusema mambo ambayo hayana uhakika hadharani? Je, wakianza kuzungusha maneno leo na ujana wao wakiwa wazee itakuwaje?

Nape naye kasema kuhusu mapato ya bosi wake, sawa, lakini hajasema kwamba Mukama ana gari alilolipiwa na chama, linajazwa mafuta na chama; hajasema kuwa Mukama analipiwa nyumba na chama; lakini pia hajasema kama analipiwa matibabu na wategemezi wake.

Kikubwa zaidi hajasema kama ana posho ya kukirimu wageni, posho ya simu na marupurupu mengine mengi yanayolingana na kufanana na nafasi yake kama mtendaji mkuu wa CCM.

Ni vigumu mno kusadiki kwamba kama makatibu wa CCM wa mikoa wanalipwa mshahara wa Sh. milioni moja baada ya kodi, na wale wa wilaya wakilipwa Sh. 700,000 baada ya kodi, na Katibu Mkuu wa UVCCM akilipwa Sh. milioni 1.7, inawezekanaje bosi wao wa juu kabisa kulipwa jumla ya Sh. 1,800,000 tu kwa maana ya mshahara na posho zote?

Nape anajua, na kama hajui hakutaka kutafuta taarifa sahihi kwamba Katibu Mkuu wa CCM hana kiwango maalum cha mshahara; inategemea mtu huyo katokea wapi. Kwa kawaida anahamishwa na mshahara wake kutoka alikokuwa, kwa maana kwamba analipwa sawa na huko alikokuwa na nyongeza ya posho kibao juu yake.

Nape atakuwa analifahamu hili, amekaa pale ofisi ndogo za makao makuu Lumumba kwa miaka kadhaa sasa, anajua vizuri habari hii. Lakini kwa makusudi tu ameamua kutokusema ukweli.

Kwa kauli za Nape na Ridhiwani katika muktadha tofauti, zinaeleza kitu kimoja kibaya ndani ya jumuiya za chama na katika chama kwa ujumla wake, kwamba kusema uongo ni sehemu ya utamaduni wa chama. Tena uongo huu unasemwa hadharani, mbele ya waandishi wa habari bila hata wahusika kuwa na chembe ya soni kwamba kauli zao zinaweza kuwageuka.

Kwa wenzetu wanaojali maadili, kusema uongo kwa kiongozi yeyote ni sababu tosha ya kumweka pembeni katika wajibu wa umma aliokabidhiwa, lakini kwa bahati mbaya sisi tunajenga mfumo wa kusema uongo, kutokuwajiba, yaani kiongozi anaweza tu kujisemea lolote na hakuna chochote kitakachompata hata kama alichosema ni uongo wa saa sita mchana.

Tatizo la viongozi kusema uongo ni kubwa. Lina madhara makubwa, ni janga la kiuongozi kwa sababu anayesema uongo akiwa amekalia ofisi ya umma anawasilisha taswira moja wazi, kwamba si mwaminifu, na asiye mwaminifu hawezi kusimamia ofisi ya umma. Inawezekana sana hili ndilo tatizo letu kama taifa, kuwa na viongozi wasiosema ukweli.

Ukiwatazama Nape na Ridhiwani katika kauli zao, mtu hatakuwa amekwenda pembeni kama akifikia hitimisho kwamba utamaduni wa kusema uongo umeruhusiwa kuwa sehemu ya kuendesha mambo ndani ya chama tawala, na kwa kuwa kuna ruhusa ya kusema uongo, ni lini basi wananchi wanaweza kuamini kwamba yasemwayo na viongozi wao ni ya kweli?
 
Nape huwa anajitakia mambo mengine bila kujali hatima yake.Ni Mwanasiasa kijana,anastahili kutulia

Hata hivyo wacha aendelee kuiua CCM

Never interrupt your Enemy when he's making a mistake-Napoleon Bonaparte

Ujumbe umefika ameuona, tatizo ni kwamba hana ujasiri wa kuchangia mada hapa JF tena.
Facebook ndiyo sehemu salama kwake tu.

Kule si hakuna hoja nzito nzito? Mwanasiasa anayejipambanua kuwa Jasiri, ni lazima angeonyesha ujasiri huo kuchambua hoja hapa JF na kwingineko kwenye kusanyiko la Watanzania wenye mawazo huru waliotapakaa kila kona ya sayari hii.
 
Nakushukuru sana Nyakarungu, kwa heshima kubwa na unyenyekevu nivumilie nami nitoe mawazo yangu, pamoja na kwamba naamini yatakejeliwa kama ilivyo desturi, lakini si kitu kwa sababu mie binadamu.

Nakushukuru kwa maneno yako juu ya Marehemu Babaangu. Sikujua kabisa kabisa kwamba kunyooshea kidole wizi ulokuwa ukifanyika kwenye ujenzi pale UVCCM ilikuwa ni ukosefu wa busara na kwamba wewe ulikuwa mmoja wa waliokerwa na hatua yangu hiyo.

Sikujua nasema sikujua kabisa kma niliwahi kuchakachuliwa UVCCM, nilidhani ulikuwa utaratibu wa kawaida kuchuja majina na kwakuwa tuligombea wengi basi ilikuwa lazima wengine wasipate nafasi na hiyo ndo demokrasia.

Sikujua asilani kuwa eti sababu ya kupelekwa Masasi nilikuwa nafichwa nisiropoke, huku uteuzi umekuja baada ya miezi kadhaa baada ya kushindwa, nasisitiza kushindwa kura za maoni.

Chama cha siasa ni Itikadi, Itikadi ni Imani ndo maana niliwahi kusema, KUHAMA CCM ni SAWA na KUMSILIMISHA PAPA ni ngumu sana.

Naamini natupiwa maneno ya kuwa na mtindio wa ubongo kisa nimemgusa mtu wenu sina shida na maneno yeyote yanayotupwa kwangu.

Nina hakika ipo siku nafsi zitawahukumu, mnyonge mnyongeni....

La mwisho kwa hili, i swala la kutumwa tu ila ninayofanya nayaamini na si lazima yafurahishe wote, hata Yesu aliowaponya ndo waliomsulubisha.

Nakushukuru sana kwa ujumbe wako.
 
Ben, ni kweli kabisa sina uwezo wa kujibu wala kuchangia jf wenye akili wanalijua hilo
 
Hivi umaarufu upi ninaoutafuta? Ili nipate nini?

NAPE naamini kabisa ya kuwa wewe ni kijana wa chama tawala unaekubalika kwa watanzania kwa kiasi kikubwa hilo halina ubishi. NINGEFURAHI SANA kama ungetoa ufafanuzi kwa kile kinachoaminika ya kwamba umenyanyapaa kabila fulani mbele ya waandishi wa habari. SIO SIRI hizi taarifa za kunyanyapa kabila fulani zimetushtusha hata sisi ambao tumekuwa tukikuamini ya kuwa wewe ndio kijana pekee ndani ya CCM mwenye kuweza kuvuta kadamanasi (ORATOR)
 
Nakushukuru sana Nyakarungu,kwa heshima kubwa na unyenyekevu nivumilie nami nitoe mawazo yangu,pamoja na kwamba naamini yatakejeliwa kama ilivyo desturi,lakini si kitu kwasababu mie binadamu.
Nakushukuru kwa maneno yako juu ya Marehemu Babaangu. Sikujua kabisa kabisa kwamba kunyooshea kidole wizi ulokuwa ukifanyika kwenye ujenzi pale UVCCM ilikuwa ni ukosefu wa busara na kwamba wewe ulikuwa mmoja wa waliokerwa na hatua yangu hiyo.
Sikujua nasema sikujua kabisa kma niliwahi kuchakachuliwa UVCCM, nilidhani ulikuwa utaratibu wa kawaida kuchuja majina na kwakuwa tuligombea wengi basi ilikuwa lazima wengine wasipate nafasi na hiyo ndo demokrasia.
Sikujua asilani kuwa eti sababu ya kupelekwa Masasi nilikuwa nafichwa nisiropoke!!!! Huku uteuzi umekuja baada ya miezi kadhaa baada ya kushindwa,nasisitiza kushindwa kura za maoni... Chama cha siasa ni Itikadi,Itikadi ni Imani ndo maana niliwahi kusema...KUHAMA CCM ni SAWA na KUMSILIMISHA PAPA ni ngumu sana....
Naamini natupiwa maneno ya kuwa na mtindio wa ubongo kisa nimemgusa mtu wenu sina shida na maneno yeyote yanayotupwa kwangu.Nina hakika ipo siku nafsi zitawahukumu, mnyonge mnyongeni....
La mwisho kwa hili.... Si swala la kutumwa tu ila ninayofanya nayaamini na si lazima yafurahishe wote,hata yesu aliowaponya ndo waliomsulubu...
Nakushukuru sana kwa ujumbe wako.
378278_ALMAJIRIS2_jpg2375ce8fbaf9d7692c89f511a17bed7e


For now You should stop making noises and concentrate on how to improve the lives of Masses ravaging the Land.Nadhani kwa kuwa wewe umejikita katika itikadi,na kwa nafasi yako ya Ukatibu mwenezi,basi itumie vizuri kuhakikisha chama chako kinatekeleza ahadi zake ili kusaidia watanzania.

Kama kweli wewe ulikuwa unapingana na Ufisadi,tueleze au weka wazi cordiality yako na Jeetu Patel.Kuwa na ujasiri.

Pia kusema kwamba huwezi kuhama CCM kwa kuwa ni sawa na kumsilimisha Papa,nadhani hayo maneno yangekuwa na nguvu kama ungeweka wazi kuhusu ishu yako ya CCJ na kutaka kuhamia CHADEMA.Umesema umemgusa mtu wetu?Chadema haiogopi kukosolewa,je wewe ulijibu au ulizusha uliyozusha dhidi ya Dr.Slaa kwa sababu yeye au CHADEMA inawachachafya?Wewe kama mwanasiasa kijana na msomi,na kwa kutumia taaluma yako ya journalism unatakiwa kuchagua maneno ya kusema,wewe ni katibu mwenezi wa chama for God's sake.Sasa tuende kwenye hoja za kitaifa.Hatuna Ugomvi na individuals,wala hatuingii kwenye personal vendatta kama mnavyofanya.Ungetumia taaluma yako ya Journalism ykutoka Pale Acharya,Bangalore na uzoefu ndani ya chama chako kunadi Itikadi na kuwatangazia watanzania matokeo ya Evaluation mliyofanya juu ya utekelezaji wa manifesto yenu ya uchaguzi.Dont go too low on persnal attacks.We need Change.mabadiliko ndiyo lugha inayoeleweka na watanzania.Unaweza kutusaidia katika hili kwa kuanzia huko huko ndani ya chama chako ili tufike kanaani.

By the way , what do we gain in a country blessed with numerious resources? how long do we need to start living like human beings in a rich country? who do we trust to do this if CCM Government has refused to deliver? who do we trust now?

Ben, ni kweli kabisa sina uwezo wa kujibu wala kuchangia jf wenye akili wanalijua hilo

I like this,Nilifanya hivi ili nikulazimishe/nikushawishi uingie hapa kwa jina lako halisi ujibu hoja.Si ndivyo inavyotakiwa?Halafu sikusema huna UWEZO wa Kujibu,Nilisema huna UJASIRI wa kujibu.

Ni matumaini yangu kuwa utaendelea kuwa nasi hapa
 
Hata Kunyamaza Nalo ni Nibu....

Lingekuwa ni jambo la ajabu sana kwa mzee Sitta na busara zake ajihusishe na watu kama nyinyi, huna la kujibu nilishasema awali nafsi yako inakusuta, jifunzeni kusema ukweli hata kama unauma; tafuteni njia nyingine halali kujitafutia riziki, msitumie siasa kuganga njaa ni HATARI kwa jamii yetu.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Madai yaliyotolewa na kada wa CDM Fredrick Mpendazoea kwamba Samwel Sita,Mwakyembe,Porokwa, Nape Nauye na Victor Mwambalasa walishiri kuanzisha CCJ ,yamezidi kuwaumiza vichwa viongozi wa CCM kiasi cha kutetemeka

Kilichowafanya viongozi hao kutetemeka sio madai hayo ambayo wahusika walishatolea ufafanuzi,bali hatua ya kada wa CCM naye kuthibitisha kwamba yaliyonenwa na MPendazoea kuhusu Samwel Sita na Mwakyembe na Nape na wengineyo kwamba walihusika kuasisi CCJ ni sahii
Kiongozi wa kwanza kuzungumza na ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM bara Capt John Chilagati ambaye alionekana kuhofia sakata hilo ,Chilagati amesema kwa mujibu wa umri wake na cheo chake ndani ya CCM Suala hilo ni kubwa mno amesema kwamba hana ubavu wa kuhoji wala kuhojiwa juu ya sakata hilo ambalo hivi sasa linavuma kila pembe ya Nchi" Jamani mimi yote nimeyasikia ,lakini mimi chilagati nasema hii isue ya sita,mwakyembe na Mkuu wa ya mawasiliano Nape Nauyo ndio waasisi wa CCJ,kwa kweli yamenizidi umri hayo mimi siyawezi labda wakubwa zangu"",alisema chilagati

Naye Bosi wa Chilagati Katibu mkuu wa CCM Bw Wilson Mukama amekwepa kulizungumzia jambo hilo,huku akidai ni hivi majuzi tu alikuwa kweny msiba wa mama yake mdogo ,hivyo akataka wana CCM wasimuongezee majonzi


Makamu mwenyekiti wa CCM Taifa Mzee Msekwa ameonekana kuogopeshwa na suala hilo hivyo kama ilivyo kwa wenzake naye akahofu kulitolea ufafanuzi,Msekwa amesema kutokana na sakata hili na mtindo uliotumika kutoa madai hayo ,yeye hausiki na wala hataki kabisa kulumbana na Samwel Sita kwani anamfahamu ni mtu wa visasi na fitina
 
Back
Top Bottom