Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Nape ni mwanzilishi wa CCJ

wacha wamchane..

Watu wanamponda sana yeye hata hajielewi jaman aibu gani hii hadi kitandani kwako? Nape achana na siasa umeanzia pabaya hutafika hata huko unapotazamia! Badili fani uwe mchungaji au shemasi kanisani
 
Wanamchana kitu gani nyie? sasa mbona hamjibu kuhusu hiyo picha? Na bado
 
Watu wanamponda sana yeye hata hajielewi jaman aibu gani hii hadi kitandani kwako? Nape achana na siasa umeanzia pabaya hutafika hata huko unapotazamia! Badili fani uwe mchungaji au shemasi kanisani

Hafai kwenye makanisa hata kwenye misikiti!
 
Wanamchana kitu gani nyie? sasa mbona hamjibu kuhusu hiyo picha? Na bado

Huijui siasa ukiijua utatulia! hebu soma matusi yote aliyoyapa hapo kwenye comments!
 
Nakuhakikishia Nape kuwa, JK akiondoka tu, utaona rangi zote toka kwa wanaccm wenzako na hasa hasa mafisadi!
 
Nakuhakikishia Nape kuwa, JK akiondoka tu, utaona rangi zote toka kwa wanaccm wenzako na hasa hasa mafisadi!

Huyu jamaa hatabaki kabisa, watamuua kwa ujanja ange achana na siasa kwa maslahi ya familia yake na watoto wake baadae
 
Akienda FB anachanwa mbaya, akirudi JF anachungulia kama Guest maana moto unawaka, hakika amejichumia janga vuvuzela la ****** huyu!

Watu wengine hawana fikra pevu, hizi shida zote zinapunguza maisha yake tu yeye angekula tu vizuri nyumbani!
 
SIASA!!Lol!! Watu wanakauka makoo!!. But na tuyaheshimu mawazo ya kila mtu!!. Hoo ndo TZ iliyoingiliwa!!!............ Kila mtu ..politician!!!!!
 
Nape anaitaji kwenda shule kwanza akasome, najitolea kumpa scholarship. simuelewi kama ana pinga au ana support ufisadi
 
dah, nilikuwa sijui kama Mlimani City ndio sehemu ya siri ambayo Usalama Wa Taifa hawawezi kuwaona......aisee, nani anataka tukapate vinywaji pale tuongee vitu vya siri?
 
Kumbe Nape nae Gamba!!!!!!!!!!!!!!! tehe tehe pole Lowassa, wanakuvunjia heshimma tu kumbe chama kizima kimeoza! dah! hii safi kabisa!
 
Nape anaitaji kwenda shule kwanza akasome, najitolea kumpa scholarship. simuelewi kama ana pinga au ana support ufisadi

Mpatie Scholarship Freeman Aikael Mbowe hana Degree ana Diploma ya Muziki katika fani ya U-DJ!
 
Siasa tamu sana! Kumbe Nape ana uchu wa madaraka kiasi hicho? Shame upon you Nape! Unaidhalilisha CCM
CCM ishadhalilika sana Kaka,Nape anajidhalilisha mwenyewe tu
 
Chadema mnataka Nape awasifie? Hivi hamjui siasa? Nashangaa mnamchukia Nape yupo kwa ajiri ya Chama chake! Jibuni hoja zake na sio kumchukia ndio Siasa ina raha na kero zake! Chadema siasa sio Uadui!
 
Na Grace Michael

SIKU moja baada ya Kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Fred Mpendazoe kuanika wazi kuwa, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Bw. Nape Nnauye alikuwa ndio injini ya uanzishwaji wa Chama cha Jamii (CCJ) na alikuwa akivujisha siri za Chama Cha Mapinduzi (CCM), amesema yuko tayari kuwajibika endapo siri hizo zitatajwa hadharani.

Bw. Nnauye aliweka msimamo wake jana baada ya kuhojiwa na Majira kuhusu tuhuma mbalimbali zinazoelekezwa kwake na CHADEMA.

"Tuhuma ya mimi kuwepo kwenye mkakati wa uanzishwaji wa CCJ ni uzushi usio na mashiko kwani jana (juzi) niliposikia ndo nikaanza kuuliza hata ofisi zao zilipo...lakini kubwa waeleze pia CCJ ilikufaje na hizo siri wanazodai nilikuwa nawapa wazitaje hadharani nitawajibika," alisema Bw. Nnauye.

Kuhusu tuhuma za kula mishahara miwili wa CCM na wa Mkuu wa Wilaya, alisema kuwa tangu ateuliwe hata mwezi haujaisha tangua ashikea nafasi hiyo hivyo kukanusha kupokea mishahara miwili.

Tuhuma nyingine ambayo ilielekezwa kwake ni ya kuhusika na kula fedha zilizotokana na ufisadi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ambapo kwa hilo alidai kuwa wakati ufisadi huo ukifanyika yeye alikuwa masomoni India.

"Ushauri wangu kwa CHADEMA wajifunze kula vya kuchinja waachane na vya kunyonga," alisema.

Akifafanua usemi huo alisema kuwa CHADEMA wanatakiwa waishi kwa kufanya kazi halali na sio kupika majungu na kupandikiza chuki kwa Watanzania kwa kuwa mwisho wa uongo ni aibu na akasema kuwa mwisho wa chama hicho umefika.

Juzi Bw. Mpendazoe akihutubia wananchi wa Mbamba Bay mkoani Ruvuma alianika mpango mzima wa waliohusika na uanzishaji wa CCJ na kuweka bayana kuwa Bw. Nnauye ndiyeo aliyekuwa akitumika kuandaa katiba ya chama hicho na kukusanya siri mbalimbali za CCM.

Alisema kuwa "Nape ni mnafiki, msaliti na mhaini ndani ya CCM kwa kuwa alishakula njama za kukiangusha CCM...tulifanya naye vikao vya siri hadi tukaanzisha CCJ leo anaitetea CCM ambayo alikuwa ameiona haifai, ni mnafiki mkubwa," alisema Bw. Mpendazoe.

Alisema kuwa Bw. Nape ndiye alikuwa akitumika ndani ya CCJ kwenda kwa wafadhili kupokea fedha za kuanzisha chama hicho na ndiye aliyehusika kutafuta pango la chama.

Alikwenda mbali kwa kusema Rais Jakaya Kikwete anaongoza chama feki kwa kuwa kina watu wanafiki na walishamdharau kwa uongozi wake dhaifu lakini yeye aliwapa vyeo bila ya kuwajua unafiki wao.
 
kama amelalamikia facebook,si mngekwenda ku comment hukohuko facebook?kwanini na nyie mmeyaleta hapa jf?

teeh teeh teeh! Kijana,huku ndo kwa nguli wa hoja! Ujiulizi kwanini pia taifa stars haikubali kucheza mechi za mchangani?? Uliza kama stars pia wanacheza kule uwanja wa mchanga hananasif,hakuna! Waje huku jf turushe makonde ya siasa si kwenda fb ambako hata mwanangu anayesoma std2 huwa namuona fb pale home! Ukute nape huwa anachat na hawa ma under9?!?
 
* CCM hawaoni waliyoyaacha ndani ya chama hicho? Mlata It is true that you may fool all the people some of the time; you can even fool some of the people all the time; but you can't fool all of the people all the time.

Monday, 16 May 2011 08:27 newsroom


* Asema kauli za Mbowe zimejaa vituko, njozi
* Awaonya waache kubaka demokrasia nchini
* Mlata: Chadema wamekuwa kero kwa jamii

NA BASHIR NKOROMO, MANYONI

KATIBU wa Halmashauri Kuu Taifa (NEC) CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema madai ya CHADEMA kwamba watafanya nchi isitawalike ni ndoto za mchana na kuwatukana Watanzania. Amesema Watanzania wamefanya uchaguzi kwa amani na kuipa ridhaa CCM kuongoza dola, hivyo kauli za Chadema ni kupingana na maamuzi ya walio wengi na kuwaona hawana busara. Pia, amesema Tanzania ni nchi ya kidemkrasia na ambayo viongozi wake wanapatikana kikatiba, hivyo vitendo na kauli za viongozi wa Chadema ni kubaka demokrasia. Aliongeza jambo hilo kamwe halitavumiliwa na serikali ya CCM na Watanzania kwa jumla litokee, kwani inahatarisha amani na mustakabali wa nchi. Nape aliyasema hayo mjini hapa juzi, wakati akihutubia mamia ya wananchi na wanachama wa CCM wakati wa kuitambulisha Sekretarieti mpya ya Chama. "Sasa Watanzania wanapokuwa wamefikia maamuzi kwa hekima zao halafu mtu mzima kwa kukosa busara anakuja kuwaambia eti anataka nchi isitawalike, watamwelewaje?" alihoji Nape Alisema mara baada ya uchaguzi mkuu kumalizika viongozi wa Chadema chini ya Freeman Mbowe, wamekuwa wakifanya vituko mbalimbali, huku wakitamba kuwa watahakikisha nchi haitawaliki. "Ndani ya Chadema hakuna demokrasia na Mbowe hilo ameshindwa, sasa anataka kuvuruga nchi nzima. Hili haliwezekani hata kidogo, kwani Watanzania si wajinga na wanafahamu baya na zuri na manufaa ya demokrasia," aliongeza Nape. Pia, alitumia fursa hiyo kuwaasa Watanzania kupuuza kauli za Mbowe na wenzake, kwani zinaweza kuliingiza taifa hatarini na kuathiri wasio na hatia kwa manufaa ya wachache. "Tazameni Kenya, baada ya uchaguzi viongozi walizusha malumbano kila mmoja
alirusha maneno akiwa ndani ya nyumba yenye kiyoyozi na ulinzi, lakini mwisho wa siku wananchi ndio wakaingia kwenye maandamano na mauaji kutokea. "Leo wamepatana wanagonganisha glasi za mvinyo katika sherehe mbalimbali, ila maisha ya watu yalipotea na wengine kupata ulemavu mpaka sasa hawajapona. Chadema ndiyo wanataka nchi kwenda huko,haiwezekani," alisema Nape.

Kuhusu Chadema kutumia maandamano ili kupata uongozi wa nchi, Katibu wa NEC ya CCM, Uchumi na Fedha, Mwigulu Nchemba,
alisema hizo ni ndoto, kwani Tanzania ni nchi ya kidemokrasia. Alisema Tanzania ina utaratibu wake wa kufanya uchaguzi kila baada ya miaka mitano na kwamba, wananchi bado wanaipenda na wana imani na CCM, kwani ndiyo maana wameipa nafasi ya kuongoza tena. "Jamani hawa watu vipi, hapa Tanzania kila baada ya miaka mitano tunafanya uchaguzi kupata viongozi, waache kuota ndoto za mchana, kwani Watanzania wamewakataa kupitia uchaguzi sasa maandamano ya nini. Wanataka kuonewa huruma ili waangamize watu?" alihoji Nchemba. Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata, alisema maandamano ya Chadema ni kero kwa wananchi na wanarudisha nyuma maendeleo, kutokana na wananchi kujihusisha na uzalishaji mali. Alisema Chadema wameshindwa kwenye uchaguzi halali, na kwamba kama wana uchungu na maisha ya Watanzania wanapaswa kuwahamasisha kufanya kazi na si kuandamana kila kukicha. "Hawa vigogo wanaandamana kwa sababu jioni wanagawana posho na kujipongeza,
lakini wananchi wanarudi nyumbani na kuwaza familia itakula nini. Hawana nia njema hata kidogo, tusikubali kupotoshwa na kikundi
cha watu wachache wenye uchu wa madaraka," alisema Martha. Mkutano huo wa Manyoni, ulitanguliwa na mikutano katika mji mdogo wa Puma na baadaye Itigi, ambapo Naibu Katibu Mkuu wa CCM, John Chiligati alipokea wanachama wapya 70 na baadaye kupokea wengine wapya kwenye mkutano uliofanyika Manyoni. Mapema, Chiligati akifungua shina la wakereketwa wa CCM la Baghdad mjini Itigi, Wajumbe wa Sekretarieti ya CCM Taifa, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida na Kaimu Mkuu wa mkoa huo, Paschal Mabiti walifanya harambee ya papo hapo na kuchangia shina hilo sh. 700,000 kuanzisha mradi.
 
Back
Top Bottom