Nape na Tendwa wanena kuhusu Kafulila

Kwaio akishikwa na kipanda uso ndio apelekwi tena India?tutapanga nae foleni pale Amana..watu wanalia kwa mengi jamani!
 
Je huyu kafulila alikuwa na maana gani haswa?
Je ana maslahi ya wanajimbo lake moyoni kweli au ana agenda ya siri?

Si unaambiwa alikuwa anapinga NCCR kuwa idara ya CCM?Kuhusu maslahi ya wanajimbo yeye hajajiuzulu ubunge ila amevuliwa uanachama kwa misingi ya kukomoana,chuki na hasira.
 
Heee...Kafulila leo Superstar yeye! haya haya Usisahau kuwapa masharti maana hawaaminiki.
 
Wanaume huwa hatulii hovyo. Tunapambana. Kulia lia tumewaachi jinsi kinzani. Tukuelewe vipi wewe mwenzetu.
 
Kwa kile ambacho sio matarajio ya wendi,Nape amesema kuwa sio sahihi wala yeye sio Muumini wa kuwatimua wanasiasa vijana pindi wanapokosea.Amesema " Hawa ni wanasiasa vijana wanapokosea inabidi warekebishe kama wanafukuzwa kila wanapokosea nani atawarekebisha?" Amefafanua zaidi kuwa Kafulila alitibuana na CDM ,wakaanza kumwita sisimizi akaamua kukimbilia NCCR leo wamemfukuza. Wakati huo huo msajili wa vyama Tendwa amesea sio sahihi kupiga kelele kila kukicha kuwa serikali inafanya matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi ili hali wakati mwingine matumizi hayo yanachochewa na maamuzi mabaya yasiozingatia hasara ya maamuzi hayo.Mfano wa hilo la kumfukuza Kafulila ni gharama kwa serikali kurudia uchaguzi. Chazo: KURASA EATV
 
Si unaambiwa alikuwa anapinga NCCR kuwa idara ya CCM?Kuhusu maslahi ya wanajimbo yeye hajajiuzulu ubunge ila amevuliwa uanachama kwa misingi ya kukomoana,chuki na hasira.
Vijitu vya Kigoma ovyo kweli kweli. havina masimamo na vinatanguliza njaa mbele. Ona Kaburu, Ona Zito, ona Kafulila. Vyote hivyo vinaongozwa na matumbo tu. Nimevidhazau kweli. Mwanamme mzima unaangua kilio huku unapapasa miguu ya mwanamme mwenzio? Bora hata huyo anayetuhumiwa kwa ufisadi kama Lowasa lakini ana msimamo kuliko hivi viganga njaa.Kimenikasirisha mno.
 
I am no Kafulila fan...ila suala la hizi by elections inabidi lipitiwe upya. Gharama za chaguzi ndogo ni kubwa mno, mie ningependekeza ikibidi iwe defined kwenye elections law as to what should lead to a by election like death of an MP, when the current MP is found guilt of corruption and vote rigging ( this in particular should be followed by a criminal persecution). But kufukuzana huku kwa NCCR is unnecessary cost kwa kweli kwa nchi, its petty and dubious....#jstthinkingaloud.
 
Kafulila kama ni kujifunza angejifunzia kosa alilofanya akiwa chadema, alijiona Star kuliko mwenyekiti wake wa chama. Sasa ndio atajifunza.

Kwa hiyo Tendwa anaunga mkono kitendo cha majambazi kutotimuliwa CCM kwa kuwa ni gharama kuandaa uchanguzi mdogo, non-sense.
 
I am no Kafulila fan...ila suala la hizi by elections inabidi lipitiwe upya. Gharama za chaguzi ndogo ni kubwa mno, mie ningependekeza ikibidi iwe defined kwenye elections law as to what should lead to a by election like death of an MP, when the current MP is found guilt of corruption and vote rigging ( this in particular should be followed by a criminal persecution). But kufukuzana huku kwa NCCR is unnecessary cost kwa kweli kwa nchi, its petty and dubious....#jstthinkingaloud.
na itakuwa vizuri chama kinachomuondoa mbunge wake kwa staili hii kisiruhusiwe kushiriki uchaguzi unaorudiwa... By the way... kafulila bado ni mbunge halali hadi taratibu zote zitakapokamilika... IKIWEMO YA KUTANGAZA RASMI KUWA JIMBO LAKE LIPO WAZI..
 
CCM bana, hizi busara mnazipata wapi sasa? mnahofia gharama kama zile za Igunga? poleni bana! mpaka 2015, mtatia akili
 
Tutafukuza Shibuda pia then muingie gharama nyingine za uchaguzi, najua mtaanda pesa nyingi za kuhonga ili mshinde.
 
mi nilishasema huyu dogo hawezi kuninyea kichwani ndo maana nimeamua kumtimua kwenye chama changu. Ila nitarudi baadae kidogo
 
Back
Top Bottom