Kwenu migogoro imeshakuwa sugu, ni sawa na mtu mwenye ukoma inafikia stage hasikii maumivu ya kidonda.Ni chama imara kisichokuwa na migogoro na ni chama mlezi!
Mh. Lema, napongeza kwa waraka huu, a friend in need? umenistua kidogo kumkaribisha Davi Arusha, Je unataka kujiuluzulu Ubunge? au ndio umestukia jimbo la Arumeru? Halafu ukiipongeza NCCR unadhani mchakato walioutumia ni shaihi? Je ni utovu wa nidhamu kudai haki ya kidemokrasia? kwamba asitokee mtu wa kuhoji kiti cha Mbatia? (uenyekiti NCCR!!) Ningpenda pia kupata maoni yako kama umesoma JF, unaonaje Dave kurudi CDM? (MWENDA TEZI NA OMO.........) Unaposema maamuzi magumu hudhani kwamba kuna vidole unavigeuzia kwenu kwa Vimeo vinavyowatesa kila uchao? (Shibuda etc) huoni kwamba kuna tikiti baya shambani kwako?.........mwisho kabisa MBONA UMESHAMVUA MWENZAKO UBUNGE MAPEMA HIVYO NA MWENYEWE AMEDAI BADO NI MBUNGE?
mi nilishasema huyu dogo hawezi kuninyea kichwani ndo maana nimeamua kumtimua kwenye chama changu. Ila nitarudi baadae kidogo
Kasema vyama vya siasa visitumie vikao vyao kama sehemu ya kukomoana bali vikao vitumike kama sehemu ya kukosoana na kulekebishana. kasema viongozi wa juu wasitumie vyeo vyao kuwakomoa walio chini yao.
Wakati huohuo nape naye kasema vyama viwe kama mlezi wa vijana. kijana anapokosea inabidi alekebishwe labda mzee utasema huyu kashindikana lakini kijana inabidi tukae nao karibu. Ova
Tendwa is talking strategically on CCM's point of views. Chaguzi ndogo si wimbo ambao CCM kwa sasa wanataka kuusikia ndiyo maana wanataka kupendekeza mfumo wa kuteua wawakilishi wa wananchi badala ya wananchi kuwapigia kura.
Kwanza Chaguzi ndogo zinatumika kama kipimo cha kuona imani ya wananchi kwa CCM uchaguzi wa Igunga ulitoa jibu kuwa Imani hiyo imeporomoka catastrophically.
Pili chaguzi ndogo ni hela, CCM ili ifute aibu ya kushindwa vibaya katika chaguzi hizi hutumia fedha nyingi sana kiasi kwamba naona wenye akili kwenye chama wanajiuliza je gharama hiyo ni value for money katika kutetea mbunge mmoja ambaye hata wakimkosa bado wana super majority bungeni.
Tatu wimbo wa kufukuzana katika chama ambao ulipachikwa jina la kujivua gamba umeonekana si mzuri sana kwa afya ya CCM. Hivyo vyama kama NCCR vinapouimba CCM haipaswi kuucheza wimbo huo maana, maana ni dalili mbaya kwao, unawakumbusha magamba era ambayo strategically wameachana na mchakato huo.
Nne CCM wanajua kuwa hata kama jimbo hilo litakuwa wazi kulichukua haitakuwa rahisi sana na huenda ikawa ni cheche ya mabadiliko makubwa ambayo wanayasikia Aljazeera na vyombo vingine vya habari tu.
Tano kufukuzwa huku kwa Kafulila kuna undermine hoja yao ya kupeleka uwezo wa kuziba jimbo toka kwa vyama vinavyoyashikilia majimbo hayo, kwani ni dhahiri kuwa kama utaratibu huo utapitishwa basi wengi watakuwa victim kama Kafulila kwa ajili ya kukomoana tu kwa kuwa mtu hakubaliani na wewe.
Kiujumla Tendwa ameongea kama mlezi wa vyama ila kama kada wa chama chake pia ambacho ndicho kinamuweka mjini. Kwani kwa sura nyingine kukubaliana na uamuzi wa Mbatia ni kukubaliana na tuhuma kuwa Mbatia ni CCM B. Kitu ambacho kwa sasa strategically CCM haitapenda ijulikane hivyo wakati ikiendelea na utafiti wa kuua nguvu ya CDM kabla ya 2015.
Tutafukuza Shibuda pia then muingie gharama nyingine za uchaguzi, najua mtaanda pesa nyingi za kuhonga ili mshinde.
Mimi kama Msajili siingilii mamlaka ya chama chochote na sina mamlaka ya kikatiba kufanya hivyo. Lakini, katiba haimruhusu (Kafulila) kuendelea na uongozi (mbunge) hadi awe na chama, hivyo kunatakiwa sasa, kuandaliwe uchaguzi mdogo,alisema Tendwa na kuongeza: "Kuandaa uchaguzi mdogo ni gharama kubwa. Uchaguzi mmoja gharama yake ni zaidi ya Sh19 bilioni. Kwa suala kama hili tujiulize nani amesababisha gharama, tusiishie tu kuupigia kelele ufisadi, tuangalie na sisi viongozi wa vyama tunaisaidia vipi serikali?
Mimi ninadhani ni njama za mwenjekiti wa nccr baada ya kujisafisha mbele ya
wazee wa chama na nec aka panga mbinu za kulipiza kisasi na ame fanikiwa.
Amgoje Hamad Rashid waunde chama chao halafu akagombee kwa ticket ya chama hicho!! Hamad atashinda kwao WAWI na Kafulila kwao Kigoma kusini hivyo watakuwa na wabunge wawili na kumpiku CHEYO na Mrema!!