Nape na Mwigulu naomba mnijibu...

Weka namba hapa mnaendesha nchi kwa facebook,shame on you
Nachukia mtu aliyeboronga kuhamishwa, hata mvivu tu kulelewa cos kuna watu wengi sana wanatafuta kazi. Inawekana awamu ya kwanza ilihamisha watu walioboronga sawa wasomi hawakwepo niliwahi kufuatilia nikaambiwa sheria zinawalinda waborongaji kuwa ukimfukuza utamlipa hela nyingi. Bila ubishi tuziangalie upya sheria hizo. Tuwasiliane kwa facebook nikupe cm kwa ushauri. Nakuelewa you have a point
 
Well spoken Nchemba lakini tatizo kubwa ni Serikali ya Chama cha Mapinduzi kushindwa kuwawajibisha watu hawa zaidi ya kuwahamisha vituo vya kazi kila wanapoboronga. Pia hao magamba wa kisiasa nani atawawajibisha, sitafuni maneno namaana Lowassa,Chenge,Rostam na wengine ngazi ya mkoa na wilaya.

Majizi wametumia siasa ama tiketi ya chama kujinufaisha still wanapeta.Tazama maisha ya viongozi wetu na waliowaweka madarakani ni sawa na mbingu na ardhi.Mtazame Nape alivyoota mbawa,hakubali ushauri wala mawazo ya vijana wenzie kisa eti kapanda Cheo (Katibu Muenezi) na Vx juu mali ya wanachama na watanzania.

Mwigulu kuna kazi kaka,kweli mimi ni wakuongea na Nape nimpe ushauri mdogo wangu, ananiambia yuko busy sana labda aniassign mtu eti niwasilishe mawazo yangu.Hii ni ishara ya kulewa madaraka, hapa ndipo pazito si watumishi wa chama wala serikali ''wote manzi ga nyanza''.

Mkuu ni kweli uyasemamyo,hakuna wa kuwawajibisha watu wazembe wasiofanya kazi yao serikalini,mifano ni mingi,angalai wizara ya ardhi ukiritimba ulivyokithiri,usiri wa miradi ya madini ,gesi na mafuta,expansion za miundo mbinu zikiwemo bandari na reli,nk hayo yote yanahitajin kusimamiwa kwa ukaribu kabisa on daily basis,achilia mbali waliofuja mali za umma toka enzi za mwalimu kuwajibishwa,mi nadhani muda wa madiiko umefika maana kila mmtu ccm anafikiria tu uchaguzi ujao wa 2015
 
Mkuu kesho kazini nakuomba leo usipate kinywaji tunahitaji sana nguvu kazi yako ili kuweza kujanga taifa letu
kazi yangu ni 24/7 iwe bar au jf bado niko kazini.au unapenda nije kukusabahi huko moshi?
 
kazi yangu ni 24/7 iwe bar au jf bado niko kazini.au unapenda nije kukusabahi huko moshi?

Ndio maana mkuu nimekuambia acha kuropoka, kwa vile naitwa makupa ndio unahisi niko moshi mkuu, tumia weledi kidogo tu mkuu acha kugenerelize.
 
Kama nyie wakubwa mnatoa hongo na kuiba wadogo wqafanyeje?
Bube nakushukuru nilikuwa na maana kuna usimamiz na kuna kujisimamia. Nchi za wenzetu kama Singapore malasia na zingine tulizowahi kufanana kimaendeleo kila mtu hujituma ktk eneo lake la kazi. Lakini tz kila mtu anajituma kuiba ktk eneo lake, mfano anayepewa kujenga zahanati ya kijiji anajitahidi kuiba bila kuwajali masikini hivyohivyo anayejenga maabara, barabara nk. Laiti kila moja angetenda haki kwa masikini hali ingekuwa tofauti. Rais hawezi kuwa kila kijiji ndio ilikuwa maana yangu. Sada madam uaminifu huo haupo ndio nasema tunahitaji sheria kali kwenye matumizi ya madaraka na uaminifu ktk rasilimali za umma. Kauli ya makamba sr ina angle nyingi hivyo maana halisi haitakuwa moja ila kujenga nchi kaka hata ubadili chama bila sheria kali na watu wenyewe kuacha ubinafsi badiliko linaweza lisiwe la kiwango hicho unachokipigia picha. Haya anayosema mrema naunga mkono na mimi natamani anayelipa mishahara hewa, anayepata hati chafu na aliyepata hati safi ila value for money haipo wawe na gereza lao
 
Bila kujua tatizo huwelizi kulitatua, kama Nchemba ni miongoni mwa watendaji wanaotegemewa watutatulie matatizo yetu basi ni dhahiri matatizo ya nchi yatadumu hadi CCM itakapoachia ngazi.
Kama tatizo ni sheria nani anatakiwa kuzirekebisha kama siyo serikali ya ccm?

Kama tatizo ni watendaji nani anatakiwa kuwawajibisha?

Watendaji wote serikalini ni wateule wa wanasiasa wanaotoka CCM, ama wameteuliwa na rais au mawaziri (wote wanasiasa) au wameajiriwa na wateule wa wateule wa wanasiasa kwa hiyo tunawaomba Ncemba na wenzako muache kulialia na mtutangazie rasmi kuwa mmeshindwa!
 
collezion, you have a point na kwenye hilo we have the same thinking. Unajua kuna wengine wanaongea kama enzi ile ya chama kushika hatamu za uongozi ambapo chama kikiona ilani yake kwenye kata imetapeliwa kinachukua hatua lakini sio sasa. China ndio wanaweza hii lakini kwa tz hata mtendaji wa kijiji anaajiriwa na utumishi taifa hivyohivyo na weo. Hivyo akiboronga ninyi chama ngazi husika lazima mpeleke kwenye mlolongo. Ukiuliza kuhusu mlolongo ndio jibu lake unaambiwa ni sheria ya utumishi. Otherwise nachukua ushauri na pia sms zote hizi nachukulia kama mlio wa jogoo nitawambia wenzetu serikalin kuwa jogoo limewika waamke. Mtanzania yeyote anahaki ya kuguswa na hali yatanzania na kutafuta huruma kwa ajili ya watanzania kwa watu wenye role ya kuwatumikia watanzania ngazi zote wawatendee haki badala ya kuwaibia nadhani sio cha kulaumiwa. Kuna baadhi ya watumishi wasio waaminifu kwenye halimashauri kila mmoja ana kampun wanagawana tenda kuwa wewe chukua ya barabara mimi ya afya wewe elimu na mingine umeme na maji. Mimi mtazamo wangu ni sheria iwe kali kwa ngazi zote kwenye usimamizi wa rasilimali na uzalendo kwenye utumishi. Adhabu za kwenye chama mfano mimi kutolewa kwenye sekretariet kunaweza kusimzuie mganga mkuu wa wilaya asiye mwaminifu kuiba dawa na kupeleka kwenye kiosk chake nje ya geti la hosipitali na kila mgonjwa aandikiwe kuwa kanunue getini. Ila mtu anapopewa ilani kama waziri anapoboronga na ikathibitika nadhani tuanze mifano iwepo wasio tu kufukuzwa kazu bali na chama na kufikishwa mahakamani
 
Huyu mwenzetu tangu aanze kumfahamu mungu ana taabu sana! Hapa anaonekana ana upako ile mbaya..

Hakuna haja ya kubishana na wakina mwigulu na Pro ccm wote, kwani hawana Mungu ndio maana taifa wamelifikisha hapa kwa kuiba rasilimali zetu. 2015 ndo mtakubali kwamba hiki kizazi sio chenu CCM kwanza na moto utaanzishwa hivi punde na KAMANDA LEMA( mandela wa pili)

Lakini hapa naona kuna kingine zaidi kuliko hii siasa ninayoijua mimi....!

tatizo la hilo chama lenu CCM hamna Mungu wa kweli zas y daily mnafisadi nchi, na kufumaniwa igunga.
2015 ndo mtakubali mziki wa chama cha Mungu na watu CHADEMA.

Hapa chini unadhihirisha kwamba nawe huna lolote......ni mtu gani wa mungu mwenye kuongea lugha kali kama hizi?!

MNAFIKI mkubwa wewe! Kwa macho nilikushuhudia ktk kijiji cha Nsimbo- igunga kwenye uchaguzi mdogo mwaka jana ukikashifu wale wote wenye msimamo na nchi, ulimtusi sana slaa kwa kudhani kuwa mtaendelea kutawala milele? Hakya mungu yani nyie 2015 mtatoka tu iwe kwa kura ama kwa Vita kwani kheri kutawaliwa hata na shetani kuliko nyie wafuasi wake mnaosambaza ukimwi kwa wadogo zetu na dada zetu kwa kivuli cha madaraka pia na kutumia rasilimali zetu na kodi zetu kumvua mpiganaji wetu lema ubunge na kuwakosesha haki wananchi wa Arusha uwakilishi bungeni, ALAFU NA WALE WATOTO ZAIDI YA 430 AMBAO WENGINE NI YATIMA AMBAO HUWA WANASOMESHWA NA LEMA KWA KUTUMIA FEDHA ZA UBUNGE, je mtawasomesha nyie wakina mwigulu na ccm yenu?
MLAANIWE WEZI WA UTU NA RASILIMALI ZETU NYIE CCM.!

Hakuna mtu wa mungu mwenye ujasiri wa kuongea lugha kama zako hivyo acha kabisa kumtaja taja mungu kwenye thread zako!! Nakumbuka jana (April 08,) ulianzisha thread kabisa kuhusu CCM kutokuwa na mungu!! Hivi mungu gani unayemzungumzia wewe?! Mungu huyuhuyu ambae amezungumziwa kwenye vitabu vitakatifu au kuna mwingine?! Kama ni huyu wa kwenye vitabu vitakatifu, basi ningekushauri usimuhusishe na siasa za Tanzania; ambazo zote (Upinzani na Utawala) kumejaa uchafu!! Unadai Mwigulu alimtusi Slaa, na wewe unachofanya hapa ni nini? Sio matusi hayo kuwaambia wenzako wote wana-CCM ni wafuasi wa Shetani?! Kwani ukiongea lugha ya kawaida hutaeleweka kwamba huipendi CCM na mambo yake?! Siasa kali kama zako haziwezi kuisaidia nchi yetu hata siku....lakini yote kwa yote, achana na mambo ya kumtajataja mungu pasi na sababu za msingi! Halafu hiyo CHADEMA unayoitetea, itikadi zake si kama hizo za kwako haidhuru hata kama wapo watendaji wenye itikadi kama za kwako (msimamo mkali)! Hivi umewahi kumsikia Edwin Mtei anavyoongea? What abt Mbowe? Slaa? Zitto?! Bob Makani? Tangu kuanzishwa kwake, CHADEMA kinafahamika kuwa ni chama mlengo wa wastani na ndio maana hata Hayati Nyerere alikipenda! Hivyo, achana na siasa zako za kusambaza chuki!
 
Nachukia mtu aliyeboronga kuhamishwa, hata mvivu tu kulelewa cos kuna watu wengi sana wanatafuta kazi. Inawekana awamu ya kwanza ilihamisha watu walioboronga sawa wasomi hawakwepo niliwahi kufuatilia nikaambiwa sheria zinawalinda waborongaji kuwa ukimfukuza utamlipa hela nyingi. Bila ubishi tuziangalie upya sheria hizo. Tuwasiliane kwa facebook nikupe cm kwa ushauri. Nakuelewa you have a point
na wewe ni sehemu ya waborongaji kumbuka kule igunga ulipoingia kanisani KKT na kupanda madhabahuni ukatoa rushwa na kuwaomba waumini waichague ccm
 
Mwigulu,
Ni bahati mbaya sana nimekuta mjadala huu nikiwa on my way....nitarudi kujumuika!!
Awali ya yote, lazima nikupongeze kwa ku-join RASMI JF...!!! Ni matumani yangu kwamba utakuwa member wa kudumu na visitor wa mara kwa mara humu jamvini!!! Sina shaka yoyote kwamba utakumbana na mengi humu jamvini ikiwa ni pamoja na matusi! Lakini, karne hii kuikimbia mitandao ya kijamii, hususani JF kwa nchi kama Tanzania ni kukimbia kivuli chako!! Kama unataka kufahamu ni kwanini CHADEMA ni maarufu sana kwa kizazi cha dot.com, basi siri kubwa ipo katika kutoikimbia mitandao ya kijamii!! CCM, mnaikimbia...maningia humu kinyemela!!! Tunashangaa tu kwamba akina Getrude Lwakatare wakitaka JF ifungiwe; hapo watu ndo tunakuja kushituka, kwamba ala, kumbe hata mama wa upako nae anaingia JF!!!

Mwigulu, Bado wewe ni kijana mwenzetu....kama mnataka kuichimbia kaburi CCM hususani kwa kizazi cha dot.com basi endeleeni kuikimbia JF! Lakini endapo mnataka kuijenga, basi wewe na vijana wenzako; hususani Nape na January, tunawaomba muwe frequent visitor humu jamvini!!! Mnachotakiwa kufanya sio kukimbia mashambulizi, ni kujibu mashambulizi...wana JF wana hasira sana na nyinyi, lakini soln sio kuwakimbia!!!

NAWAKILISHA!
 
And your point is...? Yaani unamlaumu Mwigulu kusema ukweli wake??? Yaani tukichukua madaraka (na kwa ccm hii yenye watu wa aina yako hakuna cha kuzuia hilo kutokea) lazima tutawashughulikia kisheria!

Henge, Acha ujinga! Ayaseme haya kwenye kikao gani cha ccm? Na ccm yenyewe ni ipi hadi asikilizwe, hii ya Mukama? Give us a break!
Mtoboasiri, mbona unawa crash watu wanaomhoji Mwigulu?wanauliza kama wewe ulivyouliza....wewe umemuuliza Mwigulu wakati huo huo unamjibia tukuelewaje au ulitaka hii thread iwe yako na Mwigulu tu...pls give chance to others too.
 
Hari ya Pasaka wana JF. Mtoboa siri swali lako pana mno cos sekita ziko nyingi hata ukiichukia CCM KIASI GANI HUWEZI SEMA NI SIFURI. NI SAWA KUNA MAPUNGUFU LAKINI SIO SIFURI. KWA UPANDE WANGU SIONI KAMA CHAMA NI TATIZO BALI TATIZO NI KWA BAADHI YA WASIMAMIZI KUKOSA UAMINIFU NA UZALENDO. TATIZO SIO KWENYE SERA BALI TANZANIA KUNA MIPANGO AMBAYO ILIPOPELEKWA NCHI ZA JIRAN WALIBADILI JINA LA NCHI TU WAKAISIMIA MIA VIZURI NGAZI ZOTE IKAWAPA MATUNDA MAZURI. NCHI HAIJENGWI NA MTU MMOJA. SWALI PANA NDIO MAANA NIMEOGELEA KUJIBU. ILA KTK KUKUSHAWISHI NAKUOMBA TUSIANGALIE CHAMA KAMA GARI TUANGALIE CHANZO. UTAKUBALI KUWA KUNA WATENDAJI WENGINE WA SERIKALI WALA SIO WANACCM NA NI WABOVU HAWANA UZALENDO KWA NCHI LAITI WATANZANIA WOTE WALIO NA NYADHIFA WANGEJUA KUWA HAWAPASWI KUITUMIKIA CCM BALI WAITUMIKIE TANZANIA UZALENDO UNGEKUWA JUU. WATUMISHI WA CCM WAITUMIKIE CCM WA SERIKALI WAWATUMIKIE WATANZANIA NA WAWE WAZALENDO

Kiongozi

nashukuru kwa uwepo wako hapa JF,Na nikupe pole kwa kukubari kuacha kazi yako ili tu ukitumikie chama

mkuu,tatizo kubwa ni kwamba ccm bado inadhani wananchi ni mbumbu kana kwamba hawaoni na hawaelewi nini kinaendelea ktk nchi yao.
wanaelewa kuwa Tanzania ni ya 3ktk uzalishaji wa dhahabu,lakini pia ni wa kwanza Duniani kuzalisha Tanzanite,na watanzania hawa wanaelewa kuwa CCM imeshindwa,ama inawaonea aibu baadhi ya viongozi wanaoiongoza serikali ya CCM Kwa kuingia mikataba inayotumaliza hadi kesho

nakubaliana na wewe kuwa watendaji si wazarendo,lakini CCM hii ndio iliyo yalea hayo,kama kweli ccm ingekuwa inafuata sheria,kanuni na taratibu mlizojiwekea madudu haya yasinge tokea leo hii

nakupa mfano mdogo tu

Uk wamerudisha chenji ya rada,hebu nawe jiulize swali,inakuwaje biashara iliyofanywa kwa kufuata sheria za manunuzi ya serikali leo hii kiasi cha pesa kinarudishwa eti gharama ilikuwa juu zaidi ya kawaida,kwa nini wahusika ambao bado ni viongozi wa CCM na SERIKALI wanadunda mitaani bila hata ya kuchukuliwa hatua iwe ndani ya ccm ama nje ya ccm? hatua hiyo inawavunja moyo wanaccm na sasa wamekuwa ni wanaccm mfu na waliowengi wanapiga kura za hasira

Mwl Nyerere alisema

"wananchi wanahitaji mabadiliko,kama hawatayapata ndani ya ccm,watayapata nje ya ccm" mkutano mkuu 1995 Dodoma
 
na wewe ni sehemu ya waborongaji kumbuka kule igunga ulipoingia kanisani KKT na kupanda madhabahuni ukatoa rushwa na kuwaomba waumini waichague ccm

Ndg sikupenda sana kujibu personal issues cos huenda ikawa kujitetea au majibu yasiwe na msaada kwa watanzania. Sasa kama hiyo ya kanisani nilitoa hela kwa kwaya mbili za kutoka iramba walialikwa kuja kuimba wakaharibikiwa magari yao wamenikuta mbunge wao nikawapa hela na by the way waimbaji wa shelui sio wapiga kura wa igunga labda useme nimewahonga kwa miaka minne ijayo. Mimi sioni kama ni jambo jema hao watu wanashida na wameshanikuta kiongoz wao nisiwasaidie kisa niko igunga. Watu wengine mnapokuwa hampo eneo msichukulie kila mnachosikia kuwa ndio reality. Ni kweli nilitoa hela ila ilikuwa hadharan kwa kwaya za jimbon kwangu na hamna neno CCM NILITAMKA. TUACHE HISIA ZA SIASA TUNAPOJADILI MAMBO MHIMU YA NCHI MAANA KUPITIA MABISHANO TUNAPATA PICHA HOJA NA USHAURI. HEBU ANGALIA TUBISHANE MPAKA JIONI KUWA NILITOA AMA SIKUTOA HELA AMA MIMI MBORONGAJI AU SIO HAPO TANZANIA INAPATA NINI. NAWASHUKURU WOTE MLI BASE KWENYE HOJA
 
collezion, you have a point na kwenye hilo we have the same thinking. Unajua kuna wengine wanaongea kama enzi ile ya chama kushika hatamu za uongozi ambapo chama kikiona ilani yake kwenye kata imetapeliwa kinachukua hatua lakini sio sasa. China ndio wanaweza hii lakini kwa tz hata mtendaji wa kijiji anaajiriwa na utumishi taifa hivyohivyo na weo. Hivyo akiboronga ninyi chama ngazi husika lazima mpeleke kwenye mlolongo. Ukiuliza kuhusu mlolongo ndio jibu lake unaambiwa ni sheria ya utumishi. Otherwise nachukua ushauri na pia sms zote hizi nachukulia kama mlio wa jogoo nitawambia wenzetu serikalin kuwa jogoo limewika waamke. Mtanzania yeyote anahaki ya kuguswa na hali yatanzania na kutafuta huruma kwa ajili ya watanzania kwa watu wenye role ya kuwatumikia watanzania ngazi zote wawatendee haki badala ya kuwaibia nadhani sio cha kulaumiwa. Kuna baadhi ya watumishi wasio waaminifu kwenye halimashauri kila mmoja ana kampun wanagawana tenda kuwa wewe chukua ya barabara mimi ya afya wewe elimu na mingine umeme na maji. Mimi mtazamo wangu ni sheria iwe kali kwa ngazi zote kwenye usimamizi wa rasilimali na uzalendo kwenye utumishi. Adhabu za kwenye chama mfano mimi kutolewa kwenye sekretariet kunaweza kusimzuie mganga mkuu wa wilaya asiye mwaminifu kuiba dawa na kupeleka kwenye kiosk chake nje ya geti la hosipitali na kila mgonjwa aandikiwe kuwa kanunue getini. Ila mtu anapopewa ilani kama waziri anapoboronga na ikathibitika nadhani tuanze mifano iwepo wasio tu kufukuzwa kazu bali na chama na kufikishwa mahakamani

Mwigulu haya yote kumbe mnayajua. Ila siku zote mko kimya. Mnajifanya mmeweka pamba masikioni.

Kama ulivyosema, ndo hivyo jogoo ameshawika. You have only 3 years to prove. WaTanzani hatutaki tena story. Tunachotaka ni kazi tu.

And ngoja nikuambie Ndugu yangu. Nyie hamjui kuwa sisi wananchi ndio waajiri wenu???. Kodi zetu ndio zinawalipa nyie mshahara. Ndo zinawanunulia nyie ma_VX. Ndo hizo zinawapeleka India kutibiwa. Ndo hizo zinazo_mfanya JK kila siku yuko angani kama rubani.

Ila cha ajabu hamthamini wananchi kabisa... Mnachojua ni kuwaliwaza wananchi kwa pesa ndogondogo kipindi cha uchaguzi. Na uchaguzi ukiisha yote mmesahau.

Ninachowashauri, wasikilizeni kwanza wananchi na mtatue matatizo yao. Ondoeni siasa, rushwa, ufisadi, katika kutimiza sera. 2015 hatuitaji story tena, tunahitaji kuona ahadi alizotoa rais 2010 zimetekelezeka.

Otherwise, CCM mnakuwa out of the game.
 
Asante sana, naomba NIKU-PM kesho maana nimejipa ban Facebook. Huwa inanifanya nisifanye kazi!

kifupi na wewe ni kama wao tu. Huna lolote! Alokwambia ukabebe kadi ya cdm nani? Sasa inakuwia nzito unaanza visababu. Halafu unakubali kuhamishwa toka huko kupelekwa fb, huoni unafanyiwa kamchezo wewe. Kuambia kupewa namba tu umeshalainika.

Huyo mwigulu nae anaongea siasa. Kwanza anatumikia chama na serikali, kitu ambacho kinamnyima maamuzi. Angekuwa na uzalendo asingepiga propaganda kwenye kampeni. Angesema kile ambacho cdm huwa wanasema, na hapo angekuwa mzalendo kweli.

Najua hadi muda huu kama ungekuwa 'lulu', ungekuwa huna hata 'kianzio' hapo. Mtuachie cdm yetu tafadhali
 
Huyu mwenzetu tangu aanze kumfahamu mungu ana taabu sana! Hapa anaonekana ana upako ile mbaya..

Lakini hapa naona kuna kingine zaidi kuliko hii siasa ninayoijua mimi....!

Hapa chini unadhihirisha kwamba nawe huna lolote......ni mtu gani wa mungu mwenye kuongea lugha kali kama hizi?!

Hakuna mtu wa mungu mwenye ujasiri wa kuongea lugha kama zako hivyo acha kabisa kumtaja taja mungu kwenye thread zako!! Nakumbuka jana (April 08,) ulianzisha thread kabisa kuhusu CCM kutokuwa na mungu!! Hivi mungu gani unayemzungumzia wewe?! Mungu huyuhuyu ambae amezungumziwa kwenye vitabu vitakatifu au kuna mwingine?! Kama ni huyu wa kwenye vitabu vitakatifu, basi ningekushauri usimuhusishe na siasa za Tanzania; ambazo zote (Upinzani na Utawala) kumejaa uchafu!! Unadai Mwigulu alimtusi Slaa, na wewe unachofanya hapa ni nini? Sio matusi hayo kuwaambia wenzako wote wana-CCM ni wafuasi wa Shetani?! Kwani ukiongea lugha ya kawaida hutaeleweka kwamba huipendi CCM na mambo yake?! Siasa kali kama zako haziwezi kuisaidia nchi yetu hata siku....lakini yote kwa yote, achana na mambo ya kumtajataja mungu pasi na sababu za msingi! Halafu hiyo CHADEMA unayoitetea, itikadi zake si kama hizo za kwako haidhuru hata kama wapo watendaji wenye itikadi kama za kwako (msimamo mkali)! Hivi umewahi kumsikia Edwin Mtei anavyoongea? What abt Mbowe? Slaa? Zitto?! Bob Makani? Tangu kuanzishwa kwake, CHADEMA kinafahamika kuwa ni chama mlengo wa wastani na ndio maana hata Hayati Nyerere alikipenda! Hivyo, achana na siasa zako za kusambaza chuki!

biblia inasema utawatambua kwa matendo yao! Au na wewe ni mchawi kam pro-ccm wenzako siku hiz hampendi kabisa kusikia neno Mungu, au na wewe unafurahia uchafu wa ccm yenu? Mrengo wa kati unaujua www jibwa wa shetani? Au unafurahia wale watoto zaidi ya 430 kukosa eilimu kwa upuuzi wa mahakama zenu ccm?
Mwisho wenu upo2 na hivi siku hizi hampendi kusikia Mungu.
 
kwa majibu ya Mwigulu inaonesha dhairi matatizo yote ya kijamii mnayafahamu..tatizo nani wa kumnyoshea kidole mwenzie ikiwa wote mmechafuka.?hapa ndio muda muafaka uma kufanya maamuzi mazito.
 
Mwigulu haya yote kumbe mnayajua. Ila siku zote mko kimya. Mnajifanya mmeweka pamba masikioni.

Kama ulivyosema, ndo hivyo jogoo ameshawika. You have only 3 years to prove. WaTanzani hatutaki tena story. Tunachotaka ni kazi tu.

And ngoja nikuambie Ndugu yangu. Nyie hamjui kuwa sisi wananchi ndio waajiri wenu???. Kodi zetu ndio zinawalipa nyie mshahara. Ndo zinawanunulia nyie ma_VX. Ndo hizo zinawapeleka India kutibiwa. Ndo hizo zinazo_mfanya JK kila siku yuko angani kama rubani.

Ila cha ajabu hamthamini wananchi kabisa... Mnachojua ni kuwaliwaza wananchi kwa pesa ndogondogo kipindi cha uchaguzi. Na uchaguzi ukiisha yote mmesahau.

Ninachowashauri, wasikilizeni kwanza wananchi na mtatue matatizo yao. Ondoeni siasa, rushwa, ufisadi, katika kutimiza sera. 2015 hatuitaji story tena, tunahitaji kuona ahadi alizotoa rais 2010 zimetekelezeka.

Otherwise, CCM mnakuwa out of the game.

Mkuu Collezione Mwigulu anakubali yeye ni kijana msomi ambaye anaweza kutoa mchango mkubwa katika kuleta maendeleo hata kwa kujifunza kutoka kwenye model za uongozi na utendaji za nchi nyingine na kuzitumia kufanikisha mstakabali mzima wa kuleta maendeleo kwa taifa hili lililokwama kwenye umasikini wa kupindukia(wa wananchi wa kawaida maana wao wako vizuri tu na wananeemeka zaidi kutokana na matatizo ya taifa hili).
Tatizo kuu ni uoga wa hawa vijana wa CCM ambao wamesomeshwa na kodi za mtanzania wa hali ya chini lakini wamewekwa kwenye nafasi kwa uteule wa mafisadi.
Mwigulu katika hayo maelezo yake anaonyesha kukata tamaa kwani anaona wazi kabisa sio rahisi kupingana na wazee nguli waliotia mizizi ya kifisadi katika CCM ya sasa na serikali yake dhalimu.
Nia yake njema inaishia kichwani mwake maana kwenye vikao vya kichama na hata bungeni hawezi kupinga sera mbovu wala matumizi mabaya ya ilani ya chama chake kwani ndio kinachompa ulaji na kumweka pale alipo na pia anajua kinachowapata wale wanaosimama kupinga udhalimu wa mafisadi wa CCM.
Amewasha indicator kwamba ni wakati wa sisi watanzania kutoa maamuzi kuhusu mstakabali wa maendeleo yetu.

2015 haturudii makosa.Acha wamalizie muda wao na kama wanaiba waibe na vya akiba maana wakati mgumu unakuja juu yao wakati ambapo hakuna pa kujificha tena wala kuhamishwa kitengo.

2015.
 
Back
Top Bottom