Dr. Mwigulu Nchemba
JF-Expert Member
- Feb 25, 2012
- 416
- 2,037
Bube nakushukuru nilikuwa na maana kuna usimamiz na kuna kujisimamia. Nchi za wenzetu kama Singapore malasia na zingine tulizowahi kufanana kimaendeleo kila mtu hujituma ktk eneo lake la kazi. Lakini tz kila mtu anajituma kuiba ktk eneo lake, mfano anayepewa kujenga zahanati ya kijiji anajitahidi kuiba bila kuwajali masikini hivyohivyo anayejenga maabara, barabara nk. Laiti kila moja angetenda haki kwa masikini hali ingekuwa tofauti. Rais hawezi kuwa kila kijiji ndio ilikuwa maana yangu. Sada madam uaminifu huo haupo ndio nasema tunahitaji sheria kali kwenye matumizi ya madaraka na uaminifu ktk rasilimali za umma. Kauli ya makamba sr ina angle nyingi hivyo maana halisi haitakuwa moja ila kujenga nchi kaka hata ubadili chama bila sheria kali na watu wenyewe kuacha ubinafsi badiliko linaweza lisiwe la kiwango hicho unachokipigia picha. Haya anayosema mrema naunga mkono na mimi natamani anayelipa mishahara hewa, anayepata hati chafu na aliyepata hati safi ila value for money haipo wawe na gereza lao