Kwanza shukrani na heshima kwako Mwigulu, kwa kukubali huu mjadala. Mwenezi wenu akija hapa ni vijembe na kuondoka. Haya ndio matumizi mazuri ya technology, watu wengine kama mimi mikutano ya kina Lusinde hatuwezi kuja hata mtoe Lexus. Thanx for coming, Bravo for that.
Tukirudi kwenye mada, umeongea vizuri, tatizo letu kubwa hivi sasa ni kukosa uzalendo na kukithiri kwa ubinafsi. Swali kubwa la kujiuliza na kuwauliza ni je, hili tatizo lilikuwepo tangu uhuru? Kama halikuwepo, je limeanzaje, lini na nani kalileta? Baada ya hapo, tutaweza kujadili kuhusu jinsi la kulitoa.
TULIPOTOKA
Ukiangalia historia na mienendo ya wazee wetu wa kweli wa awamu ya kwanza e.g Kaduma, Nnauye Snr, Kawawa, Sokoine etc, utaona kitu kimoja in common, they were true patriots, walikuwa wazalendo kweli kweli. Waliamini katika kufanya mambo kwa manufaa ya watu wengi na nchi yao, the motherland, na sio kwa manufaa yao pekee, hawakuwa wabinafsi.
Wakati wa mjadala wa posho kupanda, kwenye kipima joto, Prof. Baregu alikuwa anasimulia jinsi walivyokuwa wanasafiri mpaka Ukerewe na sehemu nyingine zenye mazingira magumu kupeleka elimu ya watu wazima. Walifanya hivyo bila posho wala malipo ya ziada kwa sababu waliamini katika kujenga nchi yao, na hii ilikuwa reflected na tabia na mienendo ya viongozi wa juu. Watu walikuwa wazalendo kwa sababu walikuwa na viongozi wazalendo.
UZALENDO ULIISHAJE?
Tusaidiane katika hili.
TULIPO HIVI SASA
Tulipo hivi sasa ni uzalendo 0 ubinafsi 100. Hatuna viongozi wanaitumikia nchi yao, tutakuwaje na wananchi wanaoitumikia nchi yao? Mwigulu unajua uchafu uliopo serikalini ambao chama kinauangalia, unaujua! Tumeona mawaziri wakikwamisha miradi kwa sababu hawajapata nafasi ya kujipatia 10%. Najua unajua nini kilichelewesha mradi wa vitambulisho. Hakuna kiongozi mwizi anaefanya wizi peke yake, lazima ashirikiane na watu wa chini yake. Je huyu kiongozi anawafundisha nini hawa wafanyakazi wadogo? Hivi jiulize, mtu kama Blandina Nyoni, kama tuhuma zote ni za kweli, ana uwezo wa kuwakemea juniors wake na kuwafanya wafanye kazi kwa uzalendo? Je unataka kusema kuwa serikali ya CCM, pamoka na vyombo vyake vyote, haioni uchafu wote huu wa viongozi wake?
Ukweli ni kwamba haya mambo yanaumiza sana, ndio maana inafikia hatua mtu anasema bora jiwe kuliko CCM.