mzee wa njaa
JF-Expert Member
- Jun 16, 2011
- 1,363
- 224
Who is Mwigulu by the way?
Kesha kiri CCM haiwezi kusimamia sera zake...
Kesha kiri CCM haiwezi kusimamia sera zake...
Who is Mwigulu by the way?
Kesha kiri CCM haiwezi kusimamia sera zake...
na
haya ndo maswala makuu ya msingi kujibiwa:
...(na Peter Serukamba ambae namfahamu kuliko anavyojifahamu kwa kuwa nimefanya nae kazi TANROADS japo sina uhakika kama huwa anatembelea JF), naomba mnijibu swali langu:
Mtanzania maskini aiamini ccm kwa lipi? Naomba mnijibu hilo, na mkiweza kuni-convice kwa hilo kadi yangu ya CHADEMA niliyokata juzi (ilikuwa sikukuu najua ila CHADEMA ina watu wanaojituma bila malipo na kufanya kazi nje ya saa za kazi walinipa) nitairudisha na niwe magamba kama wazazi wangu walivyokuwa zamani japo sasa wameikana ccm!
hari ya pasaka wana jf. Mtoboa siri swali lako pana mno cos sekita ziko nyingi hata ukiichukia ccm kiasi gani huwezi sema ni sifuri. Ni sawa kuna mapungufu lakini sio sifuri. Kwa upande wangu sioni kama chama ni tatizo bali tatizo ni kwa baadhi ya wasimamizi kukosa uaminifu na uzalendo. Tatizo sio kwenye sera bali tanzania kuna mipango ambayo ilipopelekwa nchi za jiran walibadili jina la nchi tu wakaisimia mia vizuri ngazi zote ikawapa matunda mazuri. Nchi haijengwi na mtu mmoja. Swali pana ndio maana nimeogelea kujibu. Ila ktk kukushawishi nakuomba tusiangalie chama kama gari tuangalie chanzo. Utakubali kuwa kuna watendaji wengine wa serikali wala sio wanaccm na ni wabovu hawana uzalendo kwa nchi laiti watanzania wote walio na nyadhifa wangejua kuwa hawapaswi kuitumikia ccm bali waitumikie tanzania uzalendo ungekuwa juu. Watumishi wa ccm waitumikie ccm wa serikali wawatumikie watanzania na wawe wazalendo
Nafikiri hakuna sababu ya kutukanana hapa, hii ni fursa nzuri sana ya kujadiliana na kijana mwenzetu ambaye yeye yuko kwenye system ya utawala. Tubadilishane nae mawazo kwa kuto hoja nina imani anazisoma na hawezi kuzipuuza. Kwa fursa kama hii hatuna sababu ya kumtukana mtu hata kama hatukubaliani na kile anachosema. Tutumie mtandao huu kuchangiana maana wakati mwingine hawa viongozi hawapati fursa za kupata mawazo mbadala kama haya tunayompa ukizingatia huyu ni kiongozi kijana.
Ndugu yangu haya maswali nimeyapenda sana naamini kama ndugu yetu Mchemba akiyajibu basi tutakuwa tuemfungua ukurasa mpya na matumaini mapya. Tumpe nafasi kama hana majibu hata mkuu Nape anaweza kutusaidia kwa takwimu zenye kuthibitika.
Mkuu ukiona kijana mdogo amesoma na si wale wazee wenye chichiemu yao anajiunga kule huyo ni opportunist na hana lolote.Nadhani kumekuwa na kumwingilia Mwigulu
Mtoa hoja alitaka ufafanuzi toka kwa Mwigulu/Nape/Serukamba
Mwigulu amejibu kisiasa na nilitegemea mjadala uendelee bila kushambulia personalities bali hoja
Ukweli hata mimi nashangaa vijana wenye akili kama yeye huwa wanatafuta nini ndani ya CCM hii ya sasa ambayo haifanani na CCM tuliyojiunga nayo miaka hiyo
Ila ili kujua sababu hatupaswi kumshambulia, tumpe nafasi naye aseme
Na kwa hili ningefurahi kumsikia Nape pia maana kuna wakati tuliamini ni mmoja wa watu makini ndani ya CCM
Kwa sasa nina mashaka na imani yangu ya awali ila nae si vema kumhukumu bila kumsikia maana hiyo ndio natural justice
Bwana Mwigulu,
Usikwepe wajibu wala usitetee uzembe wa serikali ya chama tawala, kwa kuwasingizia watendaji.
1. Watendaji wakuu wote huteuliwa na JK ambaye ni Mwenyekiti wako wa Chama. Je, tukisema kwamba Mwenyekiti wako wa Chama anawalea hao watendaji, utakana? Je, majibu yako hayamuaniki JK kwamba yeye ndio anawalea hao watendaji wabovu?
2. Unasingizia kwamba sheria ziwe kali:
(a) Nani anatunga hizo sheria? Bunge letu limekuwa dominated na wabunge wa CCM ambao hupitisha hata pumba, unakuta mbunge anaji-contradict, anaweza kutoa kasoro nyingi kwenye mswada halafu mwisho wa mchango anasema ninaunga mkono 100 kwa 100, bila hata kuweka provision kwamba ataunga mkono iwapo marekebisho hayo yatafanywa.
(b) Sheria zilizopo zikitumika ipasavyo zinaweza sana kupunguza ufisadi unaoendelea. JK alitoa msamaha kwa wezi wa EPA, kwamba wakirudisha fedha wasipelekwe mahakamani, hivi ni sheria gani ambayo inasema mwizi akirudisha alichoiba au kupata kwa njia ya udanganyifu, then anakuwa si mwizi? Huoni kwamba Rais na Mwenyekiti wa CCM anaweka mfano mbaya kwa wananchi na watendaji wengine? Kama mwizi wa EPA anasamehewa baada ya kulipa, then na wengine nao wataendelea kufisadi kwa kuwa Rais ameishaonyesha sio kosa kuiba mali ya umma.
(c) Kamati Teule ya Mwakyembe ilipendekeza watu wafukuzwe kazi na wafikishwe mahakamani, je kuna chochote kilichofanyika? Juzi hapa Kamati iliyochunguza Sakata la Jairo, iliweka mpaka na ushahidi kwamba kuna wafagizi walilipwa Sh. laki moja na ushee, na kumbe walikuwa wanaongeza 1 kwenye malipo ili iweze kufikia fedha zilizokuwa zimetafunwa kwa magendo. Mwananchi wa kawaida anaposikia kwamba Waziri anavuta posho ya shilingi milioni nne cash kwa siku chache, unadhani ataipenda CCM? Je, Jairo na hao akina Ngeleja wamechukuliwa hatua gani? Au hata hili nalo utasema mlolongo wa sheria ni mrefu na ilihali nyaraka za kugushi zipo wapi?
Mwigulu inatakiwa mfike mahali mkubali kwamba tatizo siyo sheria tu, tatizo linaanzia kwa Mwenyekiti wenu wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa nchi. Pili linakuja Bungeni ambako wabunge wa CCM mmekuwa mkiutumia vibaya wingi wenu ili kuilinda serikali ya CCM. Bahati mbaya wewe huwezi kukwepa lawama hapa, maana ni mmoja wa wabunge wa CCM, pia ni Mjumbe wa vikao vyote vya juu vya maamuzi ya CCM. Wewe ni mmoja wa wanaondaa agenda za mikutano na pia ni mmoja wa wanaoandaa tathimini ya kampeni, mnatakiwa kuwa wakweli kwa kutoa taarifa sahihi kwenye vikao vyenu, maana ni wewe ndio unakwenda kutukanwa matusi yote na wapiga kura waliochanganyikiwa kwa ugumu wa maisha huku serikali ikiendelea kuwalea watendaji wabovu na ikiendelea kuwalinda mafisadi.
Kwa hapa tulipofika, swala sio kwamba baadhi ya wana CCM ni mafisadi au baadhi ya watendaji ni wabovu, tatizo ni kwamba CCM kwa kushirikiana na serikali inafanya kila inaloweza kuwalinda mafisadi au kufunika uozo. Swala la Richmond liliisha kiajabu ajabu, hata sakata la Jairo litapita. Sakata la TBS na Bwana Ekerege pia litapita, ni kwa kuwa serikali. Wapinzani walio Bungeni wakija na hoja zenye mashiko, hamuishi kuwapiga vijembe, lakini mwisho wa siku, vijembe hivyo vinakuja kuwaumbua mkija kuomba kura. Joto la Igunga na Arumeru nadhani limetuma salam. Pia Songea na Kiwira wamewa-beep, wanataka muwapigie simu. Msipowapigia simu then watawapigia moja kwa moja, ogopa sana mlalahoi anapokupigia simu, anaipiga kwa uchungu wa kila sekunde inayopotea wakati anaongea na wewe na matokeo yake unayajua.
Uzalendo unaouongelea ungeanzia Bungeni kwamba Taifa kwanza. Taifa kwanza inaanza kwa kuwa fair kwa kutunga na kupitisha sheria ambazo zitatenda haki kwa wananchi. Kutunga sera ambazo zitaleta maendeleo kwa watanzania bila kuwabagua. Kuisimamia serikali ipasavyo ili iweze kutumia vizuri fedha na kutekeleza miradi yote iliyo kwenye bajeti.
Kila mwaka CAG anatoa report, hivi kwanini hamuibani serikali itunge sheria kwamba wakurugenzi wa halmashauri za jiji/manispaa/miji/wilaya na watendaji wa idara za serikali na mashirika ya umma ambao watakubwa na hati chafu au kukutwa wamefanya ufisadi wachukuliwe hatua/kufikishwa mahakani? Ikitokea wakurugenzi wawili watatu wakafungwa nina uhakika kwamba watu wataanza kuogopa, lakini vinginevyo kila siku mtakuwa mnalia kwamba sheria mbovu, lakini hamtaki kutunga sheria nzuri. Miswaada ya sheria ikija Bungeni mnaipitisha kishabiki huku ikiwa na mianya kibao ya watu kuchomoka na lengo likiwa ni kuilinda serikali iliyo madarakani.
Kashfa nzito na kubwa kubwa zote huwa zina baraka za serikali na ndio maana serikali inakuwa nzito kuwachukulia hatua watuhumiwa, maana serikali inajua ikifanya hivyo kuna uwezekano wa kukuta kuna maelekezo au vimemo vya kutoka kwa watu wakubwa na matokeo yanaweza kuwa mabaya. Ndio maana akina Maranda wameishafungwa na akina Jeetu Patel bado kesi zao zinasua sua mahakamani.
Halafu mambo ya kuwaambia watu waje facebook sidhani kama ni sahihi, mana facebook mpaka watu mkubaline kuwa marafiki, hapa JF ni sawa na mkutano wa hadhara, hakuna anayealikwa kwa kutuma maombi, bali ni kujiunga tu sawa na mtu anavyotoka nyumbani kwenda kwenye mkutano hadhara bila kuombwa. Na uzuri mwingine ni kwamba hata wale ambao sio members wanaweza kusoma.
Nimekuambia hivi,
Wewe huna sifa hata moja ya kuitwa mwenye mapenzi ya mungu hakuna mtu wa mungu mwenye lugha chafu kama zako; labda kama ni mungu mwingine lakini sie huyu anayefahamika na wengi wetu!! Kwa tahadhari yako ni kwamba, usizani watu tunashindwa kutoa lugha chafu kama wewe, tunaweza lakini hapa ni kwenye kadamnasi ingawaje wengine kwavile wanatumia nick names wanazani wanaweza kuongea lugha yoyote. Last but not least, nakuonya .sitaona taabu kupigwa ban ukiendelea kunitusi! Kama unabisha, endelea!
Hari ya Pasaka wana JF. Mtoboa siri swali lako pana mno cos sekita ziko nyingi hata ukiichukia CCM KIASI GANI HUWEZI SEMA NI SIFURI. NI SAWA KUNA MAPUNGUFU LAKINI SIO SIFURI. KWA UPANDE WANGU SIONI KAMA CHAMA NI TATIZO BALI TATIZO NI KWA BAADHI YA WASIMAMIZI KUKOSA UAMINIFU NA UZALENDO. TATIZO SIO KWENYE SERA BALI TANZANIA KUNA MIPANGO AMBAYO ILIPOPELEKWA NCHI ZA JIRAN WALIBADILI JINA LA NCHI TU WAKAISIMIA MIA VIZURI NGAZI ZOTE IKAWAPA MATUNDA MAZURI. NCHI HAIJENGWI NA MTU MMOJA. SWALI PANA NDIO MAANA NIMEOGELEA KUJIBU. ILA KTK KUKUSHAWISHI NAKUOMBA TUSIANGALIE CHAMA KAMA GARI TUANGALIE CHANZO. UTAKUBALI KUWA KUNA WATENDAJI WENGINE WA SERIKALI WALA SIO WANACCM NA NI WABOVU HAWANA UZALENDO KWA NCHI LAITI WATANZANIA WOTE WALIO NA NYADHIFA WANGEJUA KUWA HAWAPASWI KUITUMIKIA CCM BALI WAITUMIKIE TANZANIA UZALENDO UNGEKUWA JUU. WATUMISHI WA CCM WAITUMIKIE CCM WA SERIKALI WAWATUMIKIE WATANZANIA NA WAWE WAZALENDO
Hongera sana umeonyesha uwezo mkubwa wa kustahimili kuwepo hapa jf na kujibu hoja za wadau usichoke na wala usiwe kama nape aka nepi.Nashukuru sana, yakujifunza nayachukua nayaliyo wajibu wangu nitatekeleza na pale panapohitaji kusema kwenye vikao nitasema ukweli cos nisiposema watz watasema kwa kalamu. All in all tunapojadili Tanzania na vitu vinavyosababisha watanzania waendelee kuwa na hali mbaya tuko pamoja. Mtaamini tutakapokuwa tunaongelea katiba nawaomba watanzania rasilimali na uzalendo viwe msitari wa juu. Vyama vipo kwa sababu Tanzania ipo bila tanzania hakuna chama hata kimoja. Asanteni tutaendelea kubadilishana mawazo na mengine tuongee na kwa cm tupeane througj fb
Hivi swala hili la kuwa kila siku watanzania wanaminishwa kuwa kuna watumishi baadhi ni wabovu na ndio wanaoharibia CCM utendaji naomba msilitamke mtafute sababu nyingine sio hii maana hii inzuiilika na hao watendaji wakaondoka toka kwenye system. Nchi hii inapotea ila inahurumia chama changu cha CCM kwa kutosikia na kusoma nyakati bali wamebaki kupeleka watu wanaotoa matusi ya aibu kwenye kampeni ila anguko la chama haliji kama muujiza bali huanza taratibu tu. Kazi kwenu viongozi wa CCM.Hari ya Pasaka wana JF. Mtoboa siri swali lako pana mno cos sekita ziko nyingi hata ukiichukia CCM KIASI GANI HUWEZI SEMA NI SIFURI. NI SAWA KUNA MAPUNGUFU LAKINI SIO SIFURI. KWA UPANDE WANGU SIONI KAMA CHAMA NI TATIZO BALI TATIZO NI KWA BAADHI YA WASIMAMIZI KUKOSA UAMINIFU NA UZALENDO. TATIZO SIO KWENYE SERA BALI TANZANIA KUNA MIPANGO AMBAYO ILIPOPELEKWA NCHI ZA JIRAN WALIBADILI JINA LA NCHI TU WAKAISIMIA MIA VIZURI NGAZI ZOTE IKAWAPA MATUNDA MAZURI. NCHI HAIJENGWI NA MTU MMOJA. SWALI PANA NDIO MAANA NIMEOGELEA KUJIBU. ILA KTK KUKUSHAWISHI NAKUOMBA TUSIANGALIE CHAMA KAMA GARI TUANGALIE CHANZO. UTAKUBALI KUWA KUNA WATENDAJI WENGINE WA SERIKALI WALA SIO WANACCM NA NI WABOVU HAWANA UZALENDO KWA NCHI LAITI WATANZANIA WOTE WALIO NA NYADHIFA WANGEJUA KUWA HAWAPASWI KUITUMIKIA CCM BALI WAITUMIKIE TANZANIA UZALENDO UNGEKUWA JUU. WATUMISHI WA CCM WAITUMIKIE CCM WA SERIKALI WAWATUMIKIE WATANZANIA NA WAWE WAZALENDO
Nachukia mtu aliyeboronga kuhamishwa, hata mvivu tu kulelewa cos kuna watu wengi sana wanatafuta kazi. ..