Nape na Mwigulu naomba mnijibu...

Mwigulu nilikuwa najiuliza sana kuwa kitu gani kimekutokea cos nilikujua tukiwa iliboru ulikuwa na kipaji sana cha uongozi na pia nikasimuliwa kuwa ulionesha mfano mzuri sana mazengo na chuo kikuu, kupitia mjadala huu nimehakikisha kuwa Mwigulu wa enzi zile na wa sasa ni yuleyule na zaidi ume advance zaidi. Binafsi nakupongeza na kukutia moyo una nafasi ya kulikomboa taifa hili na yeyote anayekufaham vizuri hawezi kukulaumu kwa makosa ya watu wengine ktk chama au serikali bali atataman uwe na mamlaka. Mazengo wanakumbuka msemo wako wa Enough is enough, nataman haya mambo yanayokera watu ungekuwa na mamlaka labda ungesema enough is enough. Ilboru nakukumbuka kwa usemi leadership is showing the way, you can not show the way unless you know the way. Big up bro you ara the youth's role model
 
Kwa hili naweza kukuunga mkono. Hii hamisha hamisha ya watendaji wabovu inalea ubovu, tunakuwa tunahamisha tatizo toka sehemu moja kwenda nyingine. Lakini nadhani tuende hatua mbili mbele. Pendekeza katika chama chako na serikali, kwamba baadhi ya nafasi ambazo kwa sasa ni za kuteuliwa, zigeuzwe kuwa za kugombania katika soko la ajira, tuziondoe katika uteuzi wa Raisi. Hapa ninaongelea nafasi hizi:-
1. Makatibu wakuu wa Wizara
2. Wakurugenzi wa vitengo vya wizara
3. Wakurugenzi wa wilaya
4. Wakurugenzi wa miji na majiji
5. Watendaji mbalimbali wa Ikulu

Tukifanya hivyo itakuwa rahisi kuwawajibisha pale wanapoboronga, kama ilivyo kwenye sekta binafsi. Lakini kwa sasa inakuwa ngumu hata kwa waziri mkuu kumwajibisha mteule wa raisi, kisa? Hajamteua yeye. Hii ndio sababu inayofanya tunakuwa na akina Jairo na Nyoni kibao katika nchi. Hawa wanawajibika kwa aliowateua, si kwa wananchi, ndio sababu inayofanya wanakuwa na kiburi, nadhani unanielewa. Hizo nafasi tajwa hapo juu inatakiwa ziwekwe kwenye soko la ajira, zisiwe za uteuzi. Nadhani suala hili tuliingize katika katiba mpya!


Mkuu Idimi naomba nitaje sababu kuu ya Serikali ya CCM kuendelea kuweka wateule katika nafasi za kiutendaji ambazo tungetegemea zifuate taratibu za competition katika soko la ajira.
Hizo nafasi ulizozitajaa CCM hawawezi kukubali ziende kwa makundi mengine ya watu hasa wanaogopa zinaweza kuangukia mikononi mwa watu wa vyama pinzani au wanaharakati wa kweli wenye lengo la kufanya kazi bila ufisadi.
Kuna kipindi nilipata nafasi ya kuwa kwenye team ambayo ilizunguka nchi nzima kukusanya maoni ya wadau na kufanya utafiti kuhusu maendeleo ya zao fulani ambalo ni muhimu hapa nchini.
Moja ya wadau walikuwa hao namba 2.Wakurugenzi wa wilaya na wakuu wa wilaya.Kila ofisi niliyoingia nilikuta ilani ya CCM kwenye ofisi ya hawa watendaji hakuna kitu kilicho nitia simanzi kama hicho kwa kuwa ni conflict of interest ya hali ya juu.Pata picha mkuu wa mkoa ni mteule wa mwenyekiti wa CCM,Mkurugenzi wa mji pia,mkuu wa wilaya hali kadhalika,mkurugenzi wa wilaya pia.Kwenye vikao vya halmashauri mbalimbali ni nani atathubutu kumkosoa mwenzake wakati wote ni magamba na wanatokana na chanzo legelege,fisadi na dhalimu?

Illustration:
Naomba nitoe mfano hai ili tuone uhalisi wa hili suala.Tulipita wilaya ya Korogwe huku tukiwa na appointment na Mkuu wa wilaya Bw.Erasto Sima lakini yeye asubuhi hiyo hakuwa ofisini kwa hiyo tukaambiwa na Katibu Mhutasi ametoka kidogo ila twende tukazungumze na Mkurugenzi wa wilaya huyo akatuambia mkuu wake wa kazi ameenda vijijini kufuatilia masuala muhimu atarudi jioni sana.Tukajadiliana machache na huyo DED then tukaaga na kuahidi tutarudi kesho kutwa yake.
Kwa kuwa tulihitaji kuwahi wilaya nyingine na tulikuwa nyuma ya muda ikabidi tupate lunch ya mapema then tuwahi kwa wadau wengine wilaya ya Lushoto badala ya kupoteza siku Korogwe.Narudi zangu hotelini nilipofikia namkuta Mkuu ya wilaya yako counter/reception akipata vinywaji laini akiwa na mrembo aliyejazia na kwa kuwa hakuwa ananijua sikuwa na haja ya kusalimiana naye nikaendelea na shughuli zangu za kukusanya makabrasha na nguo zangu na kurudi(niliporudi sikumkuta pale reception na sitaki ku-speculate kilichoendelea) kwenye usafiri wetu kuanza safari ya Lushoto.
Kesho kutwa yake tukarudi tena Korogwe na kupata mahojiano na Bw.Erasto Sima huku akianza kwa kuomba msamaha kwa kushindwa kuonana na sisi jana yake kutokana na majukumu ya kiofisi.Pia hakutupa strategic inputs muhimu ikionyesha hakujiandaa wala hakujua lolote kuhusu mazao ya wilayani mwake.Bahati nzuri DALDO(Afisa Kilimo na Mifugo wa Wilaya) alikuwepo na akatusaidia sana.

Kwa ufupi hawa watu wameshajimilikisha ofisi ambazo zinaendeshwa kwa kodi za wananchi na wanatenda vyovyote vile watakavyo.Hayo ndio madhara ya mfumo wa uteule huku takwa mojawapo likiwa kuwa na kadi ya CCM.

Naunga mkono kuwe na badiliko katika katiba mpya.

Nawasilisha.
 
Mkuu Ambitious,
Nakupa pole kuhusu kadhia uliyopata kwa huyo mtendaji Mteule wa Raisi pale wilayani Korogwe. Nimefika wilaya nyingi za mko wa Tanga na nimekutana na kadhia kibao sana.
Ni hayo hayo yaliyonipata wilaya jirani ya Lushoto mwaka 2005 nilipoenda katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya, bwana Elias Goroi (sijajua kwa sasa yuko wilaya gani). Nilikwenda kuuliza kitu fulani cha maendeleo ya wilaya, lakini manyanyaso na lugha chafu niliyokutana nayo toka kwa mkuu mweyewe wa wilaya sitakaa nisahau maishani mwangu. Ilibidi RAS aingilie kati (alituita chemba mie na mwenzangu), baada ya kuona hatuelewani na mkuu huyo. RAS akasikiliza kilichotupeleka pale kwa makini na upole sana, kisha akatoa solution moja smart sana ambayo ilisaidia kuendelea na kazi.
Majibu yale ndio yananifanya nipendekeze kwa Mwigulu na Nape, waishauri serikali ya chama chao kwamba nafasi za watu niliowataja hapo juu ziwe za ushindani wa ajira, na si za uteuzi wa raisi. Hizi fadhila za kuteuana ndizo zinazochangia kupunguza tija katika ofisi nyingi. Ni chanzo cha uvivu, majungu na umbea kazini. Hali kadhalika, wilayani tungebaki na DED na RAS tu, sioni hasa kazi kubwa ya mkuu wa wilaya ilhali mwenye watendaji wataalamu na fungu la ruzuku ni DED.
 
Hari ya Pasaka wana JF. Mtoboa siri swali lako pana mno cos sekita ziko nyingi hata ukiichukia CCM KIASI GANI HUWEZI SEMA NI SIFURI. NI SAWA KUNA MAPUNGUFU LAKINI SIO SIFURI.

KWA UPANDE WANGU SIONI KAMA CHAMA NI TATIZO BALI TATIZO NI KWA BAADHI YA WASIMAMIZI KUKOSA UAMINIFU NA UZALENDO. TATIZO SIO KWENYE SERA BALI TANZANIA KUNA MIPANGO AMBAYO ILIPOPELEKWA NCHI ZA JIRAN WALIBADILI JINA LA NCHI TU WAKAISIMIA MIA VIZURI NGAZI ZOTE IKAWAPA MATUNDA MAZURI. NCHI HAIJENGWI NA MTU MMOJA. SWALI PANA NDIO MAANA NIMEOGELEA KUJIBU.

ILA KTK KUKUSHAWISHI NAKUOMBA TUSIANGALIE CHAMA KAMA GARI TUANGALIE CHANZO. UTAKUBALI KUWA KUNA WATENDAJI WENGINE WA SERIKALI WALA SIO WANACCM NA NI WABOVU HAWANA UZALENDO KWA NCHI LAITI WATANZANIA WOTE WALIO NA NYADHIFA WANGEJUA KUWA HAWAPASWI KUITUMIKIA CCM BALI WAITUMIKIE TANZANIA UZALENDO UNGEKUWA JUU.

WATUMISHI WA CCM WAITUMIKIE CCM WA SERIKALI WAWATUMIKIE WATANZANIA NA WAWE WAZALENDO
maneno haya ungeyasema arumeru, umechelewasana kujitambua au leo hujapiga mambo yako?(kiroba na sigara *****? means cha a town)
 
Kaka Mwigulu: I salute you.
Nakumbuka hekaheka zako toka ukiwa Mazengo school za kupata nafasi za kisiasa kama ubunge na uwaziri naona unanukia.

Naomba nikuonye Mr. Mwigulu Nchemba, Amini yakuwa watanzania wa leo si wa enzi za nyerere, watu wameamka na wana upeo wakupembua mbivu na mbichi.

Tumia wasaa huu kuwa karibu na wapiga kura wako wasije wakakushangaza kwa kukuvua bunge muhula ujao na kuwapatia wapinzani. Jiulize kama kuna jambo la maendeleao ulilofinya ili wakuchague tena...

Tumia mda wako vizuri kuelimisha wazee wa CCM ambao bado wamelala wakiamini wadanganyika bado wamelala...waambie tumeamka sasa na ahadi za miaka hamsini kwa sasa hazina nafansi..

Tumia mda wako kuwaeleza mafisadi waliojazana CCM pia wakae chini wapange mikakati mipya ya namna yaku endelea kupata amani kwakua sioni kama watazifurahia mali walizwaibia watanzania...

Wasalaaaaaaaaaaaaaam!
 
Back
Top Bottom