Nape na mafisadi wa CHADEMA

fmpiganaji,

Mkuu usihangaike na huyo DOGO, amelewa madaraka!

Je, mfupa uliomshinda FISI mbwa koko atauweza? Yeye aendeleze vita yake na REAL ACHE na hata hao nao kesha-washindwa na asubiri mapigo toka MAPACHA WATATU (REAL ACHE).

Akumbushwe ya kuwa...."mambo ya Ngoswe aachiwe Ngoswe"
 
Ha ha! Sasa alitaka alipwe mshahara mdogo kuliko anaowaongoza..pole sana nape,.
 
Good and factual based analysis, badala ya kutoa barua kwa mafisadi anahangaika na kisiki cha mpingo, anatapatapa baada ya kukatazwa kuwaandama mafisadi. Siasa sasa inaanza kuwa tamu ila anagombana na tembo
 
NAPE HANA HOJA ZA MSINGI,NA INAWEZEKANA HAJUI MAANA YA UFISADI AWAULIZE WATANZANIA FISADI NI NANI?KAMA HAWATAANZAA NA BOSI WAKE JK,LOWASA,rOST YA AZIZA NA WENGINE WA CCM
 
Alitaka alipwe Shilingi ndio alizike kuwa ni sawa, Chadema siyo tawi ama jumuiya ya CCM kiasi kwamba anaweza kuhoji mishahara ya watendaji wake. Aende kuhiji mishahara ya UWT na UVCCM.

Ukiona Simba anawinda panya jua amezeeka.....pengine kufilisika mbinu za uwindaji
 
Mbona huo mshahara umepungua? Ningetaraji uwe zaidi, hata kufikia sh milioni 12 zilizoandikwa na magazeti ya Rostam wakati wa kampeni.
 
Hivi mke wa Marehemu Moses Nnauye si alikataa huyu siyo mtoto wa NNAUYE wakati ule wa sakata la jengo la UVCCM?......hii kauli ilishabadilika?
 
Nape na Mukama rudini kwenye mada mlioanzisha ya kujivua magamba, naona mmetoka kwenye topic yenu, mara kuetetea familia ya JK wewe ni housegirl wa JK ? Mara list ya mafisadi ya CDM, Maliza mada moja kwanza ndio uanze mpya.
 
Mwambieni huyo dogo mshahara wa slaa sio nyaraka za siri uko hadharani siku nyingi..

by the way Slaa deserves every penny of that money and much more!
 
Namkumbushia huu mzimu...........


2qd1u6b.jpg
 
Huyo kijana naona ana wakati mgumu. Ni dhahiri sasa kazi aliyopewa anaanza kuiona ngumu. Ametumwa kazi na wakubwa zake ya kuwaanika mafisadi katika chama chake na kuwavua magamba lakini ghafla mafisadi nao wakatoa makucha na kumtisha JK ikabidi kijana afungwe kipunguza mwendo. Bado ana kazi ya kuzunguka mikoani kuanika uozo wa chama chake na sasa baada ya kupigwa stop kuwasakama mafisadi ndani ya ccm sasa hana cha kusema katika majukwaa. Matokeo yake anafuata sasa nyayo za watangulizi wake akin Tambwe Hizza na Makamba mkubwa kuongea maneno yasiyoisaidia yata hiyo ccm yenyewe. Pumba pumba pumba tupu
 
Nape amekosa wa kumshauri? Kama kapotea mapema hivi, baada ya miaka mitano atakuwaje?
 
Nape bwana!!! Tatizo hajui kuwa kwa sasa thamani na uwezo wa kiutendaji wa Dr. Slaa ni mkubwa hata kuliko hiyo sekretarieti yao mpya.
 
Nape alionekana kivutio kwa vijana pale aliposimamia haki katika mkataba mbovu wa majengo ya uvccm, ikatabiriwa hata angekiama chama sababu asingeweza pigania haki kwenye chama ambacho haki imewekwa mifukoni. lakini sasa amerikubali anguko lake la kisiasa, amenasa mtegoni, sio wa kuaminika tena.
 
Kuna taarifa kua Nape nnnayuye atatoa list ya mafisadi ndani ya chadema,..
naomba mwenye updates atupatie huko aliko,...

update:
inasemekana kumbe alicho ongelea chenyewe ni kile kile cha siku zote,...
huyu mkuu atatueleza zaidi kilicho jili



na huyu anareport hivi:



Huyu ndio msemaji wa CCM au kuna mwingine tumngoje?

nape anaiga kunya kwa tembo.

ninamuonea huruma sana maana kuna maeneo ambayo kama atathubutu kushusha bendera za chadema, atajikuta yuko hospitalini ICU. Na hii sisemi kumaanisha kuwa CDM ni chama cha fujo, bali Watanzania hawataki tena siasa za CCM. kwa gia hii ya kushusha bendera za chadema hatavumiliwa na watanzania waliochoka.na porojo za chama chake.

namtakia heri bwana nape.
 
Back
Top Bottom