Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Nape na madai ya uchagga ndani ya CHADEMA

Jeykey toa mifano ya ushahidi wa chama kupoteza mvuto kulikosababishwa na Nape... Ukabila upi nilioeneza? Nimekuomba fanya utafiti kabla hujasema....

Nape tunakutegemea lakini unaanzakutukatisha tamaa
Propaganda sio nzuri ukilenga hisai za watu kabila fulani
 
Henge namaanisha katika yote niliyoyaandika,sisukumwi na hisia bali ukweli ninao uona...
Siko tayari kabisa kuhusisha chama chochote na udini au ukabila wakati sijapata kusikia yeyote akipigwa marufuku au kunyimwa uanachama katika chama chochote cha siasa hapa nchini kwa sababu ya kabila lake au hisia zake, ndio maana namuomba Nape aondoe haya matamshi kwani ninachooona kama tunaelekea huko basi kama aliyoyatamka ameyamaanisha..
 
mkuu, sema hivi siku wakristo wote na wachagga wote waamue kuhamia chadema huyo nape ndiyo ahahakikisha hiyo kauli yake - hongera katibu mwenezi wa kueneza siasa za chuku, uzushi, uwongo uliotukuka bila kujua au kupima athari ( risk) yake.

acha kuwa kipofu wa fikira,nenda kamwambie tendwa akifute,hadithi za kitoto no nafas jf
 
Henge nakushukuru,lakini unahakika haikurekebishwa kwa kutoa ufafanuzi? Nenda kaangalie hata gazeti liloandika hiyo stori lilikuwa la mwananchi nadhani la tarehe 12 Mei na angalia la tarehe 18 Mei... Nashauri si vizuri kushutumu bila kuwa na hakika... Heshima ya JF ni kubwa mno ku accomodate haya.....
Nape hakuna ubishi ya kwamba wewe ni kijana unaekubalika na watanzania wote hata wale amabao wako CDM wanakubali uwezo wako. Hili swala la kunyanyapaa kabila fulani ni vizuri ukalitolea ufafanuzi ili umma ukuelewe,vinginevyo hawa CDM ndio inaonekana kuwa mtajo wao kisiasa hata sisi ambao ni CCM damu tulishutushwa kidogo ni hizi taarifa za ukabila
 
ha ha ha!

nape mimi swali langu dogo tu...

UNAHUSIKA VIPI NA CCJ?
 
Ndugu Nape,
Mke wangu mchagga, nafanya kazi na wachagga.
Kauli yako kuwa CDM ni chama cha wachagga imewashtua wengi kwani wewe ulikuwa tumaini pekee ndani ya CCM. Wengi ndani ya CCM tumewachoka kwa kukurupuka na prropaganda.

usipoangalia utapoteza mvuto wa kisiasa.
 
kaisha ingia mitini,usipo jibu post yangu namba 28 hapana shaka mimi binafsi nitaamini ulihusika na CCJ na ulisema vibaya kuhusu Wachaga hivyo basi nitahitimisha kuwa weweni mbaguzi(kwa kuwasema vibaya wachaga))
 
Henge ndugu yangu, mie naamini kwamba kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake,hapa natimiza wajibu wangu tu na niko hivyo kote nilikopita fuatilia historia ya utendaji kazi wngu na ndivyo nilivyofundishwa na babaangu,ukiamua kufanya kazi basi fanya kweli,ukiamua kupumzika basi pumzika kweli,huwa sijui unafiki
Kaka,kwanza hongera kwa kujitokeza live ndani ya jamvi.....ukizingatia kauli yako uliyoitoa siku ile ndiyo imetawala media karibu zote wiki hii. Kinachonisikitisha kutoka kwako ni kuona unaleta majibu mepesi mepesi kwenye swala zito kama hili!. Mie ningekushauri ni bora ungekiri na uiombe samahani jamii ya kichagga na watanzania wote kwa ujumla. Mwisho nataka kukushauri kitu.....hebu jiangalie,jithaminishe kuanzia umri wako,hekima na busara zako mbele ya kizazihiki cha Tanzania ya leo..... Je,ni kweli wewe ni mtu wa kutoa mapovu mdomoni kwa hajili ya ccm?.....kaa,tafakari kwa kina then.......
 
Mi sio mtabiri,lakini niseme kimoja!! Huenda Mwisho wa JK 2015, ndio ukawa mwisho wa Nape!!Leo hii wakazi wa Ubungo wangeficha wapi nyuso zao kwa aibu unayoifanya Nnape majukwaani??Upepo sasa umebadilika mno,nahisi huwezi tena kukaa meza moja na hawa watu(RACHEL), wamekuzidi kwa kila idara,hujafikia kiwango chao kabisa kukakbiliana nao, na ndio maana hata CHADEMA wanaenda kwa step, hawastutumu direct kama wewe unavyofanya. Kama ulikashifu kwa majukwaa, then tumia majukwaa hayohayo kuomba radhi, na sio uende mapokezi kwa gazeti la Mwananchi eti ndio unaomba radhi, kuna majority nikiwapo mm sijalisoma hilo gazeti,sembese bibi yangu aliyoko kijijini kule.

N.B. Kumbuka mimi nakushauri hii kitu kama Batchmate wako, kule Bangalore-Acharya, India....inanisikisha sana.
 
Jeykey,
Ni vizuri kuwa na hakika kwanza na jambo kabla hujamshutumu mtu.Nape kapanda najukwaani!!!!!!! Si busara kueneza uongo au kwakuwa nimekaa kimya bila majibu kwa hoja hii???? Fanya utafiti uwe na haki ya kushutumu. Kwa hili nakusamehe kwani hujui utendalo.

nape utakapokuja kilmanjaro kuimarisha chama utawaambiaje wachagaa? wewe si umeshawaona sio wenzako kwenye ccm
 
nape chunga sana ulimi wako na siasa zako za kikabila waswahili walisema ulimi ulikiponza kichwa
 
nape chunga sana ulimi wako na siasa zako za kikabila waswahili walisema ulimi ulikiponza kichwa
 
Mh Nape! Kasi uliyoingia nayo kwenye Ukatibu Mwenezi wa CCM, ilitupa moyo sana! Kauli zako za kufukuza Magamba bila kutaja majina zilitufanya tuone huenda umejaa gas tu! Lakini ulipoanza kukinzana kauli na bosi wako Mzee Mukama jibu lilianza onekana wewe huna lolote heri ya yule Tambwe Hizza, Kubwa zaidi Juzi uliposema CDM ni wachagga. Hivi wachagga wako nchi nzima?
 
Henge ndugu yangu, mie naamini kwamba kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake,hapa natimiza wajibu wangu tu na niko hivyo kote nilikopita fuatilia historia ya utendaji kazi wngu na ndivyo nilivyofundishwa na babaangu,ukiamua kufanya kazi basi fanya kweli,ukiamua kupumzika basi pumzika kweli,huwa sijui unafiki

Usisingizie mzee Mnauye ndie aliyekufundisha siasa zako ukabila.OMBA RADHI YAISHE Mzee wawatu alikuwa mtu wa makabila yote hata hao wachaga alikuwa rafiki zake
 
Henge ndugu yangu, mie naamini kwamba kila mtu anapaswa kutimiza wajibu wake,hapa natimiza wajibu wangu tu na niko hivyo kote nilikopita fuatilia historia ya utendaji kazi wngu na ndivyo nilivyofundishwa na babaangu,ukiamua kufanya kazi basi fanya kweli,ukiamua kupumzika basi pumzika kweli,huwa sijui unafiki
Mkuu Nnape heshima yako, kuja kwako hapa na kujibub a moja kwa moja ni jambo jema sana la la busara, kwa sababu vijembe,uzushi ,na matusi ambavyo vilikuwa vinaelekezwa kwako vitapungua na kuisha kabisa kwani ukimkabili mtu facetoface unammaliza kabisa si unaona hata jeykey keshaishiwa nguvu na hoja yake umeshaipoteza ila usingekuja hapa na kumkabili hoja yake ingekuwa na nguvu na kuendelea kukumaliza ,,tegemea kukutana na kila aina ya watu humu jamvini
.tuko pamoja na Mungu akubariki
 
Jeykey,
Ni vizuri kuwa na hakika kwanza na jambo kabla hujamshutumu mtu.Nape kapanda najukwaani!!!!!!! Si busara kueneza uongo au kwakuwa nimekaa kimya bila majibu kwa hoja hii???? Fanya utafiti uwe na haki ya kushutumu. Kwa hili nakusamehe kwani hujui utendalo.

Haaaaaaa!!!!
Unabisha kabisa mwanaume?
ona aibu basi, duh!!!!!
Mbona huja lalamika kuwa quoted vibaya?
hadi mzalendo wana ku-quote vibaya?we vipi wewe unadhani uko kwenye
jukwaa una hubiria chipukizi wa ccm nini?
 
Back
Top Bottom