Nape: Lowassa kapoteza sifa ya kugombea

Nape: Lowassa kapoteza sifa ya kugombea

Mkuu Nape huwa ni mdomo lakini kwenye mambo ya kumwaga damu hapo ninamtetea.

hujui igunga waliua wakala wa chadema na sikichache walishasema... hata hivyo nilikuwa nazungumzia nape kupanda jukwaa moja kumnadi mkwe wa lowasa...
 
Ila nape kiukweli kabisa, Muambie Katibu Mkuu aache hii biashara ya Meno ya Tembo inatutia aibu sana watanzania aisee.
Kama vipi tumpe kisiwa cha mafia basi aachane na hiyo kitu, Mbona kuna biashara nyingi tu.

hawezi mkoromea kwasababu serikali iluyoko madarakani ni juhudi zake na huzo dili..
 
hujui igunga waliua wakala wa chadema na sikichache walishasema... hata hivyo nilikuwa nazungumzia nape kupanda jukwaa moja kumnadi mkwe wa lowasa...

Hivi kumbe Nape alihusika swala la Igunga? Si Mwigulu Nchemba kweli? Maana ninachojua ni kuwa Nape walimpiga marufuku kukanyaga Igunga.
 
Last edited by a moderator:
Duh!
Nape anafananisha Kitimoto Msikitini eti ni sawa na CCM na Rushwa ?
Hivi Kumbukumbu hana au amesahahu au alikuwa wapi wakati CCM wabavariki Rushwa kuitwa Takrima ?

Huku ni Kuudhalilisha Uislam Dini Yetu na hakika napinga na napinga kwa nguvu zote kamwe Uislam auwezi fannaishwa na Shetani CCM.
CC: Nape Nnauye
 
Last edited by a moderator:
Nape punguza mdomo usijifanye mungu mtu,mimi naunga mkono lowasa kuwa mgombea kwasababu uweza anawo sababu anayo mwisho anamaamuzi magumu nchi itanyooka
Hivi utajiri wa Lowasa kaupataje vile?
 
Kweli Maccm ni manafiki sana, yanamshadadia Zitto kutangaza kugombea huko wao wakizuiana kutangaza nia

Wanamshadadia kwa kuwa haja-acomplish mission waliyomtuma. Kumbuka IDs zinaficha mengi, huwezi kujua!
 
Acha kupotosha watu weka chote nilichosema. Nilichosema ni kuwa yeyote anayekiuka taratibu za chama katika mchakato ANAJIONDELEA SIFA za kuwa mgombea wa chama hichi!(Labda Chama kiamue kutofuata taratibu zake chenyewe, na kikiziacha hakina namna ya kuendelea kuaminiwa)!

Sasa si swala la Lowassa ni swala la KILA ANAYEKIUKA TARATIBU!kama naye anakiuka anaingia kwenye mkumbo huo, sio kwasababu ni Lowassa ila kwasababu ni mwana CCM na taratibu za CCM haziruhusu! Sio swala la Nape ni swala la taratibu,kanuni na sheria zilizowekwa kabla hata Nape hajazaliwa!

Haiwezekani watu wagawe rushwa hovyo tukae kimya tu kisa anayegawa flani!!!! Hivi kuna uwezekano wa kuingia na kiti moto msikitini ukapigiwa makofi?!! Unaweza kupigiwa makofi na kupewa uongozi wa kanisa wakati humwamini Yesu Kristo?!! Watanzania tusiogope kusema ukweli maana ndio utakaoiponya nchi yetu.

Kama mnamgombea ana sifa atachaguliwa tu huna haja ya kuongezea sifa zake kwa rushwa! Haya si yangu ya CCM, na ni kwa madiwani, wabunge na hata urais!

HERI YA MWAKA MPYA 2014!

Ndugu yangu Nape, unachosema ni sawa. Lakini kutokana na mazingira yaliyopo, nashauri mambo mengine kaa kimya kama wengine wanavyofanya. Kuna watu wengine wapo tayari kufanya lolote ili apate anachohitaji. Mengine nyamaza ndugu yangu. Tumesikia mengi yakifanyika CCM. Wengine wameumwa kidogo wafe, wengine wamekufa, wengine ajali n.k. Ukiuliza unaambiwa alipewa sumu.

Hayo ni maoni yangu, waweza pokea au kataa
 
Kila chama na funza wake anayepekenyua. CCM Lowassa, Chadema Zitto. TLP Mrema mwenyewe, Cuf Hamad Rashid, NCCR-Mageuzi Kafulila. Duh, noma!
 
Mkuu Crashwise kwa maana hiyo ww upo upande wa Lowasa bega kwa bega? Na kwanin unatoa onyo kwa Nape asiseme ukweli kwani Lowasa kawa Mungu hadi aogopwe?

Mda mwingine tuwe tunaacha unafiki na ushabiki Nape hana kosa lolote hapo pia hata siku 1 mwanamageuzi aliye timamu hawez kutetea jambazi ambalo lipo hadi kwenye list of shame ya sept 2007 iliyotajwa na Rais Slaa.
 
Last edited by a moderator:
Nape: unazunguka tu ila ulimlenga lowasa. Sasa ckia cc vijana ndio changuo . Huyo mnaemfikilia hata kwao .....hakubaliki.
 
Ok... CHADEMA walipoamua kuchukua hatua kwa watu ambao sio tu kwamba walianzisha mchakato nje ya taratibu, bali waliifanya michakato hiyo kwa kueneza chuki dhidi ya viongozi wa juu - kina Nape walisema CDM inaminya demokrasia!
Sasa hapa Lowassa anaposema ameanza safari ya ndoto zake Nape anatokwa mapovu!!!
 
Ccm hawana mtu mwingine zaidi ya EL!HAPA MTAJIANZISHIA THREAD NA KUJIJIBU WENYEWE!
 
Mkuu Tuko hawa CCM ni wanafiki tu, na wameshindwana wao kwa wao wanaingilia mambo ya ndani ya CHADEMA sasa.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Tuko hawa CCM ni wanafiki tu, na wameshindwana wao kwa wao wanaingilia mambo ya ndani ya CHADEMA sasa.

Wanaitumia CDM kama sehemu ya kujisahaulishia matatizo yao, lakini wanashindwa kujua mwisho wa siku watapambana nayo...
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom