Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Hivi hizo kanuni za CCM wanaozijua ni Nape, Mangula na Kinana peke yao?
 
CCM kuna udikteta Na ukiritimba Wa Hali ya juu! Au Ni kumuogopa Lowasa, inakuwaje wanachama wengine waruhusiwe kuongea mambo yahusuyo urais-siyo kampeni lakini Lowasa haruhusiwi?

tutajie mgombea mmoja ambaye kaita makundi ya watu nyumbani kwake na waandishi wa habari ili kujitangaza.acheni ushabiki wa kifala nape ameongea ukweli.
 
Nape unatumika

Nape unatumikia kundi la wanaokutuma na sio Chama cha Mapinduzi.

Nape inatosha kwa Lowassa,Nape bakisha maneno,Nape kwa nini unakosa hofu ya Mungu kwa kuhakikisha wanaokutuma unawafurahisha na kumuumiza Lowassa,Nape bila aibu unasingizia Lowassa anawapa watu vyakula na kuwapa nauli na posho,naamini umetumiwa na shetani kwa sababu nimeshuhudia ujio wa watu hawa na wanahabari wenzangu hapakua hata na soda wala chakula kwa Lowassa,

Nape tamaa ya madaraka huwa tamu lakini punguza kwa maslahi ya nchi,unamtisha nani nape?

Nape unajua Membe amehonga basi kama kampeni kwa kanisa katoliki Tabora,askofu aligoma maana alihonga wakati askofu akiwa matibabu tuna picha za ushahidi siku membe Ameitwa kuonywa na Askofu wa Tabora,nape huyu kwa kuwa mungu wako wewe huwezi kumsema hadharani,

Nape mungu wako Membe na Gotham wamegawa rushwa zanzibar wakati nchi inaomboleza kifo cha Komba,kumbe Nape ulikua unaimba kishetani huku moyoni ukifurahia kufa kwa Komba maana Gotham na akina Makonda walikaa vikao kabla kufa Komba wakipanga kutafuta mtu wa kumpa band ya TOT hata kabla Komba hajafa,nape tunarekodi ya waliyoyasema walikuwepo wasanii akiwemo koppa na akina cheni haya tumeyatunza kwa wakati muafaka,

Nape tunarekodi ya mawasiliano yako na January makamba mlivopanga kuchafuana Edward,Nape unapinga simu kushinikiza gazeti la u huru kuipa coverage habari ya kishetani iliyofikia kwa Farisayo anayejifanya malaika wa asubuhi

Nape Farisayo mwenzio January huwezi kumkemea kwa sababu wakubwa mlitumia mbinu kumtoa kwa edward kumleta kambi yenu akagawa simu zaidi ya 790 kwa wana UVCCM na kuhonga wanavyuo Malaki,Nape Farisayo huyu Makamba akaanda kitabu alihonga magazeti akitoa machapisho yakafika kwa kila mjumbe wa mkutano mkuu ukiwa umefunga bakuli lako kwa kuwa anafanya kazi Za mabwana zako,

Ufarisayo wako haujaisha wewe umeanza kampeni mtama kila ilipotoa msaada tunajua na mahali ulipotoa pesa ,Nape Muogope Mungu Kakobe anakuuliZa Umeokoka Nape?

Nape unajua kanuni za chama chetu haziruhusu kufanya kampeni za kuligawa taifa

mtoto wa Rais Ridhwani aliandaa watu kuligawa taifa kuwa Rais wa nchi hawezi kutoka kaskazini Nape ulikua unajua hili linaweza kuligawa taifa lakini kwa kuwa ni bwana unaemtumikia ulikaa kimya Ridhwani hagusiki acha wanachama wanyonge tubaguliwe hata nyombo vya dola vilikaa kimya leo nasikia kwenye mzalendo eti vinafuatilia wanaofanya siasa kuligawa taifa hawawezi kuanza na Ridhwani kwa kauli yake ni mtoto wa mkubwa huyu hagusiki hata akitukana mashekhe wanyonge watatulia

Nape inatosha,maumivu uliyompa Lowasa tunanyenyekea kwako ewe mwenye kipaji cha kuzimu inatosha,Nape mnapanga mbinu ovu ili edward akatwe jina ili uendelee kuenjoy cake ya wanyonge,hawa wanaokuja kwa Edward Lowassa sio wana ccm ,ccm ni wewe Ridhwani,Gotham na Membe jengeni chama japo mlikiasi na kuunda CCJ,

Mh Jakaya Kikwete najua ujumbe huu utakufikia,utaacha mpaka lini viongozi wenye heshima watukanwe mpaka na watu ambao unaweza kuwaonya?Hivi tumekosa Jakaya huruma kwa Edward hata kidogo Ni kweli Edward amekua kinyago cha kushambuliwa ukikaa kimya?

Mangula wewe unasema umeokoka,ni ukristo gani wakushangilia akina Makonda wakimtukana Lowassa mmekaa kimya,nawaambia mnapanga mbegu Ngumu katika nchi

Nape,Mangula,Ridhwani,na Gotham na Membe kwa nini mnatumia turufu ya kumkata jina Lowasa huku mkijua anakubalika kwa umma,mnayafanya haya kwa maslahi ya nani?je ni ya wananchi au ya wale wa mezani aliowasema Jerry Slaa?

Jakaya kiokoe chama,muhurumie Edward Naye ni Binadamu,kuna maisha baada ya siasa Nape,

Namaliza kwa kusema,Nape pamoja na kazi nzuri unayofanya kuwarishisha waliokuweka hapo ulipo kionee huruma na chama,Lowassa amevuja damu muacheni watu ninyi!

Mungu mbariki Edward Lowassa na kumlilia

Mungu ibariki Tanzania
 
Mwenyekiti wa mtaa pesa ya kumpeleka mtoto wake shule ya kata hana hiyo ya kwenda kumpa support lowasa kaipata wapi???????????..?????
 
Patachimbika kati ya nani na nani?

Lipi jema, kuacha pachimbike kwa usalama na ustawi wa Watanzania au kusaliti maisha ya watanzania kwa kumwogopa fisadi lowasa kwamba patachimbika?

Yaani tuendelee kufa kwa sababu yakuogopa vita vya mafisadi? Sasa wakatafute nchi yao, Tanzania hatutakubali kusaliti taifa kwa maslahi yao, na wala hatutaruhusu wachimbishane ndani ya ardhi ya Tanzania.

Kwanza jamaa ni mjinga tu kama alivyosema Mwl. Nyerere. Anakusanya watu wachovu na watoto wa shule wasiokuwa na hata uwezo wa kujikumu maisha yao, eti wagharimikie safari za kutoka usukumani huko walipie gharama za hotel Dodoma na wampe fedha za kumshawishi!. Kwa lipi alilolifanya zuri la kumg'arisha hivyo? Hakuna.

Yeye angesubiri kwanza kipenga kipigwe ndipo aanza kuwaambia waje kumshawishi!. Lowasa ni mjinga na wanaomshawishi ni wajinga kama yeye. Ninawasamehe wanfunzi wa Dodoma tu kwa sababu waliambiwa kuna fedha na chakula kimeandaliwa cha kumshawishi mgombea. Hawana namna, walikwenda kufuata fedha zao.

Huyu jamaa asipopitishwa kuwa mgombea, patachimbika.
 
Nape kuwa makini na JK maana mwenzako hubadilika kutokana na upepo.Maneno mengine mwaacha ayaseme yeye mwenyewe na usikubali kutumika kiasi hicho.
 
Nape haijui ccm kama Lowasa aijuavyo, Nape haijui siasa kama Lowasa aijuavyo. Kwa ufupi Nape kwa lowasa ni sawa na kiroboto juu ya mgongo wa Tembo.
Nakushauri bwana mdogo Nape uachane na Lowasa na uwe biz kutafuta uraiya wa nchi utakayokwenda kupumzika kwanzia October30

hakuna point ya maana umeongea hapa mkuu. Btw huyu mmasai mwenzenu labda aanzishe chama chake maana hata huku upinzani hatumtaki.
 
Huyu nape juzi monduli c alikua anamuita Lowassa Baba,sasa ameanza tena figisu figisu zake aangalie sana ukimbiz unamtafuta huyu.
 
Nape acha ropo ropo you will never know what tommorrow gonna be!! ! ,be wise / hata kinana sijui amekaaje na wewe?
 
Ikitokea EL apitishwe kuwa mgombea na of course baadae kuwa mwenyekiti wa CCM, sijui Nape atafanya nini. Mimi nadhani ataenda kwa kile chama walichokianzisha huko nyuma. Hivi kilikuwa kinaitwaje?

mkuu nape anajua hapiti huyu..
 
Wewe unalilia lowasa aachwe tu agombee na hata kama hafai, kwa maslahi ya nani? Ninawasiwasi mkubwa sana na utaifa wako wewe. Mzalendo yeyote hawezi kulalia upande wa fisadi akasaliti Watanzania wenye maisha ya tabu wanaolia usiku na mchana wapate uongozi utakaowajili na kuwalinda.

Kama vile mzazi mwema asivyoweza kuwapa watoto wake sumu ya kahawa wanywe kwa kuwa tu wanalilia kutokana na kwamba inarangi na harufu nzuri, vivyo hivyo kiongozi makini hawezi kupitisha fisadi nyangumi kugombea uongozi wa wananchi huku akijua kwamba halifai, eti kwa sababu wanalilia.

Hata hivyo wakimpitisha Lowasa, haitakuwa ajabu kwa taifa maana tumezowea kuwa na mama wa kambo asiyejali usalama wetu. Mbona hata katiba mmetuwekea madudu, huku mkijua kisha kwa unafiki mnajifanya kusema wananchi wenyewe wapige kura ya kukubali ama kukataa huku mkijua hawana ufahamu wala elimu ya kutosha bila kuelimishwa?

Kweli Tanzanai ina machungu mengi sana na ccm. Mchagueni Lowasa mzidi kujichora, lakini pia hata mkimchagua nani, Wtanzania wamekataa kuendelea kuongozwwa na chama chenu cha wauaji!. Hatutaki. Chezeni sinema tuburudike tu hapa. Mtauona mziki October.
 
mi nawashangaa wasiomtaka lowasa,kama lowasa amevunja kanuni,si wanyamaze mda ukifika,wamuadhibu,ili kwao iwe rahisi apite wanae mtaka,kuliko mikelele mengi

watu wanamshtua mapema angalau fedha zake zisiishe kabisa wewe unafikiri akiachiwa mpaka mwezi wa tano na jina halipo si atakufa kwa presha.
 
Wakati mwingine ni kuwapa WATANZANIA kile watakacho / nape na kikundi chako just kuweni fair MTAKIANGUSHA CHAMA NA ISITOSHE KUKIZIKA CHAMA CHETU NI HERI KAMA MMEAHINDWA KULETA MSHIKAMANO MUACHIE NYADHIFA CHAMA HIKI SIO MALI YENU KAMWE
 
Kwa taarifa tu ni kwamba Nape na kundi lake ndio wanapanga na kutengeneza watu wa kujichanganya na wananachi au raia wema wanaotoa fedha zao kwa ajili ya kwenda kumshawishi Lowassa achukue form za urais.
Hawa watu wa Nape wakisha gundua kuwa mikakati ya kwenda kwa Lowasa imekamilika na wenye moyo wameshatoa hela zao basi wao huja mwishoni na kujinadi kama watu wanaomkubali Lowasa ila hela za kuchanga hawana na Nauli hawana.Wanapoamua kuwakaribisha kwa lengo la kuongeza shamrashamra ndipo wanapoibuka na kusema hakuna hela zilizochangwa bali Lowasa ametoa hela zake Mwenyewe.

Lengo la Nape kufanya mchezo huu ni ili amwengue Lowasa kwenye kinyang'anyiro.
 
Natamka haya maneno kwa roho safi kabisa na bila kumumunya maneno kwamba: ikiwa lagwanani Edward Ngoyai Lowassa atatinga nyumba nyeupe ya magogoni mwezi wa Oktoba, january Makamba, Nape Nnauye na Paul Makonda mkahamie Somalia.

Sote ni mashahidi jinsi hawa watu wa3 wanavyomsukasuka Lowassa kwa muda mrefu huku wakitambua fika kwamba Lowassa sio saizi yao ila wanafanya hivyo kwa lengo la kutafuta cheap fame in politics. Nawashauri muanze kufungasha virago vyenu kuanzia sasa. Nawe Makonda nakushauri huo ulaji wa ukuu wa wilaya uule kwa haraka maana siku zako zinahesabika kwa vidole vya kiganja cha mkono mmoja. Hayo madaraka uliyozawadia na JK ndio yatakuwa ya mwisho katika harakati zako za uongozi wa kisiasa. Ulithubutu kumpiga mzee wetu Warioba ukazawadiwa cheo lakini safari hii utakula jeuri yako.

Sijatumwa na mtu yeyote kuandika haya maneno ila nawapa angalizo tu kwa roho safi. Tafuteni nchi ya kuhamia kuanzia sasa. Si mmejifanya jeuri kumtukana mamba kabla hamjavuka mto? Imekula kwenu!

:israel:
 
Last edited by a moderator:
Utakuwa falla yani wewe uchukuliww na gari hujui unakopelekwa? Atuondoleenupuuzi wake hapa
 
Haya yote unayo ya ongea kama hujui ama unajifanya kuwa mchungaji wa kondoo wako EL ukijua kuwa huyo ni kondoo wakati watu wanajua ni chui basi utakuwa unatenda dhambi kama anayo tenda NAPE kwa sababu unawashawishi watu na kusema uongo mfano unasema UMMA unampenda lowassa .nadhani neno umma hulijui mapana yake bora unge orodhesha makundi ya watu wanao muhitaji lowassa na si kujumlisha watu wote .inamaana hata NAPE ana muhitaji lowassa maana umma ni watu wote wenye lengo moja nia moja .
 
Back
Top Bottom