Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Nape: Lowassa ameanza kufanya kampeni, yuko hatarini kuenguliwa

Unajidanganya yaani kama hakuchaguliwa fisadi hakuna mwingine?

Mwingine atoke wapi ccm!Msijifunge akili mkaacha watu makini toka UKAWA,mkabaki na hao ma ccm ambao kazi itakuwa kuwasafisha badala ya kuwa kampenia
 
Nnatumai Nape anao ushahidi wa anayoyasema na kutuhumu watu. Kwamba watu wanaoenda dodoma wamelipwa na nani, kwa njia zipi na kwa sababu gani, la sivyo atakiaibisha chama kwa mara nyengine tena! Wananchi wameamua....acheni uzushi na uongo. Kwa nini mnawadhalilisha wananchi kiasi hiki? Waache kazi zao kwa kulipwa na kupewa chakula? Hivi wote walioonekana huko hawawezi kujinunulia chakula? Tena tunawaingiza mpaka viongozi wetu wa dini; maimamu na wachungaji!

Nnaungana na mtu wa Mungu mmoja aliyemtaka aokoke.....atubu na aokoke!!

mwingine huyu hapa.wewe ulikuwa kwenye kundi la viongozi wa dini au wanafunzi? Njaa mbaya sana
 
Nape na Mzee Unafiki Sita umefika muda na nyie mkaimarishe chama chenu cha CCJ kama alivofanya Zitto. Halafu na ww ungepunguza mahaba niue kwa Mzee Mamvi make sijaona point ya maana hapa.
 
Nape kipaji chake ni cha kuimba taarabu.
 
Kesho ni zamu yangu mimi na mke wangu kwenda dodoma kumshawishi edo kuchukua fomu. Nape a.k.a nepi unyamae wewe sio saizi yetu.
una akili ndogo sana , kwanini wewe mwenyewe usichukue fomu , lowasa zaidi ya mvi kipi kingine alichokuzidi ?
 
mi nawashangaa wasiomtaka lowasa,kama lowasa amevunja kanuni,si wanyamaze mda ukifika,wamuadhibu,ili kwao iwe rahisi apite wanae mtaka,kuliko mikelele mengi
 
mara ya kwanza wakati watu wanamsema huyu mtu aitwaye NAPE MOSES NNAUYE nilijua ni fitina za kisiasa,lakin mwaka jana wakati akiwa katika ziara mkoa wa kigoma ndio niligundua kwamba ana matatizo ya malezi na uelewa mdogo na ni mtu anayependa kuabudiwa.
Alikuwa anawashurutisha watu kama watoto wadogo,ashukiriwe mzee kinana ana hekima,anaweka mambo sawa kila mara hali inapochafuka,Mwaka 2005 wakati kikwete akijiandaa kuwania urais alisema nchi haiwezi kuongozwa na shoga,leo ndio rais,
Akwawekwa pemben akapigika mpaka huruma,wazee wakamuombea msamaha akpewa udc masasi baadae katibu mwenezi,leo amesahau anatamba,anaringa,anajishebedua.
Nape hiki chama sio chako,Nape huwezi kuwachagulia watanzania wa leo rais,nape huwezi kuzuia mtu anayependwa asipendwe,waache watanzania waaamue ubwabwaje kama nguchiro wa mtwara,
Nape mtu akipewa kapewa maana mtoaji ni Mungu sio wewe,usiishi kwa hofu,kwa hisia,na mitazamo hasi,onesha uwezo katika kukijenga chama,tatua shida za watanzania,wambie watanzania ukweli kwa wanahitaji rais wa aina gani hawahitaji mdundiko kwa sasa bali maamuzi mgumu,vitendo na uwajibikaji na uzalendo wa kweli,
Nape acha kufukia hisia za watanzania,tuachie musa wetu atuvushe kwenda kanani,mwache mwanaume aoneshe uwezo,ipo siku nape utapigwa mawe,ila ushauri wa bure jifunze hekima,busara,ustarabu na kutafatari kabla ya kutamka,bila shaka sifa ya kijana mwenye weledi tanzania itakuwa nyuma yako,utaheshimika na kuthaminiwa,
LIFE IS PERFORMANCE,PERFORM BY ACTING WISELY

Achen mahaba kwa fisadi mamvi...mwiz wa richomnd
 
Lowassa asipogombea ccm,wemekwisha.
Hakuna Presidential candidate ccm anayemkaribia Lowassa hata kwa mbali."Quote my words"

haya ndio mliyobaki nayo wafuasi wake. Huyu hapiti haendi popote nakwambia.tutampata rais wa maana kuliko huyo mroho wa madaraka.kashaambiwa akatafute chama cha kugombea namshauri aende chadema act hatumtaki.
 
Lowassa angekuwa mwelewa angeachana na maigizo anaofanya kwani nisawa na kupiga mashut makubwa ambayo ayana magoli
huyu mzee hana washauri , kinachoendelea ni vituko sana ; kakusanya wasela eti ni maaskofu sijui wachungaji wa pentecost !
 
Lowasa atakufa kwa presha mwaka huu Nape amezidi kumpa presha.
 
yeye anajari nini !! asipopitishwa ataipasua CCM kama ilivyokuwa kwa Lyatonga 1995 na kwa mwaka ndo CCM itakuwa kwa heri.CCM sharti imubembeleze au isambalatike kwa yeye kwenda ACT.

wewe ishia hapo hapo ACT hatumtaki labda ajaribu chadema msituambukize ugonjwa sisi wazalendo.
 
Nape ni mtoto kisiasa. Hawezi shindana na Lowassa. Namhurumia siku akitinga Magogoni, Nape atahamia chooni kuishi
 
Navyomjua jk hataki kupiga kelele na Lowasa anamsubiri kwenye kanuni dakika za mwisho amtandike hataamini masikio na macho yake.
Maweeh!let us wait and see? Mzee JK anaweza kumpa Mzee EL pande kwani hawajakutana barabarani!hizo kanuni zenu wakina nape hazina nguvu zaidi ya chairman wetu wa CCM!mnaweza pigwa na suprise mkatafuta pakuweka nyuso zenu...
 
Back
Top Bottom