WABHEJASANA
JF-Expert Member
- Jun 22, 2011
- 4,225
- 869
Amewataka wananchi kuiamini CCM kwa sababu kwa sasa imepata viongozi makini ambao wako mstari wa mbele kusimamia maslahi ya wanyonge,huku akimfagilia Katibu mkuu mpya wa Chama hicho Abdulhaman Kinana kwamba ni kiboko ya viongozi wabovu ndani na nje ya chama.
Nisingependa kuamini kwamba Mwenyekiti alipomsifia Nape pale Mnazi Mmoja kwamba anafanya kazi nzuri sana na ya kusaidia Chama kwa kuwajibu wapinzani, alikuwa ana maana ya kauli za ovyo ovyo kama hizi.
Katibu wa itikadi siasa na Uenezi wa CCM Nape Nauye amesema kuikabidhi Nchi kwa wapinzani ni sawa na kumkabidhi Fisi Bucha,ambaye mwisho wa siku bada ya kula na kushiba atakimbia na kuiacha bucha kama ilivyo.
Nape alitoa Kauli hiyo mchana huu wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Mji mdogo wa Katoro wilayani Geita Mkoani Geita,ambapo alihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.
Alisema serikali ya Chama cha mapinduzi ka sasa inafanya mikakati ya kuhakikisha kamba inatekeleza ahadi zake zote ilizozitoa kwenye uchaguzi uliopita,na kwamba propaganda ambazo zimekuwa zikitolewa na wapinzani hazitakuwa na nguvu mwaka 2015 kwa sababu CCM itakuwa imetekeleza ahadi zake.
Amewataka wananchi kuiamini CCM kwa sababu kwa sasa imepata viongozi makini ambao wako mstari wa mbele kusimamia maslahi ya wanyonge,huku akimfagilia Katibu mkuu mpya wa Chama hicho Abdulhaman Kinana kwamba ni kiboko ya viongozi wabovu ndani na nje ya chama.
Wilaya ya Geita na haa katika majimbo ya Busanda na Geita yamekaliwa vibaya na upinzani,na inavyoonekana ziara ya Nape pamoja na katibu mkuu ambaye yeye alikuwa amebaki mjini Geita kwenye jimbo la Geita ni moja ya mkakati wa kuhakikisha kwamba wanazima harakati za vyama vya upinzani na hasa cdm katika kujikita kwenye majimbo hayo.
huku akimfagilia Katibu mkuu mpya wa Chama hicho Abdulhaman Kinana kwamba ni kiboko ya viongozi wabovu ndani na nje ya chama.
Kwa wale waliosoma fasihi ya Kiswahili hapo zamani watakumbuka kuna mwandishi mmoja alielezea dhana ya 'kinyume cha maneno'. Simkumbuki ni nani alisema hivyo, nadhani kuna watanikumbusha humu. Nape ametumia kinyume cha maneno kuelezea hali ambayo ccm imetufikisha hapa. Wamekuwa kama fisi waliokabidhiwa bucha na mifano ni mingi. Hebu angalia utajiri wa kufuru wa viongozi pamoja na familia zao. Utajiri huo umepatikana mara baada ya wao kuwa viongozi. Kuna habari zimeenea kuwa mtoto wa kiongozi mkuu anamiliki utajiri usio na kifani, miaka michache tu baada ya 'kuhitimu' masomo. Chanzo cha utajiri huu kimeulizwa mara kadhaa lakini wameshindwa kujieleza.
i
Nani sasa atabisha kuwa ccm wamegeuka fisi waliokabidhiwa bucha?
Mkuu mbona mlianza kuaminiwa toka mwaka 1961.. wakati huo ikiitwa TANU..! Umegeuka wimbo..?
Huyo Kinana c ndo anasafirisha meno ya tembo kwenda mashariki ya mbali huko..? Leo unadai ni kiongozi kiboko..? Labda kwa wizi wa nyara za nchi..!
Yaani hata mseme nini lazima hii mizee tuitoe madalakani.