Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,264
- 105,429
Nisingependa kuamini kwamba Mwenyekiti alipomsifia Nape pale Mnazi Mmoja kwamba anafanya kazi nzuri sana na ya kusaidia Chama kwa kuwajibu wapinzani, alikuwa ana maana ya kauli za ovyo ovyo kama hizi; Haya ni matusi sio kwa wapinzani bali watanzania wanaotumia haki yao ya kikatiba kuunga mkono chama cha siasa wanachoona kinawafaa, bila ya kujalisha kama wanafanikiwa kukiweka chama hicho madarakani au hapana; Hii ni aibu sana kwa chama chetu, na sisi huku 'site' tumekuwa tunapata sana shida na maneno ya Nape, tunaonekana majuha kuunga CCM mkono, hata hoja za kukitetea zinaisha kwani mbali na chama kuvurunda kwenye mambo ya msingi, sasa kinaingia nguoni mwa watu na kuwavujinia heshima; kilichobakia ni kuwapiga tu na kuwapora mali zao;
Bora umesema.
Swali kwa Nape. Ikiwa CCM (angalau makada wakubwa waliobarikiwa na Mwenyekiti kukisemea chama)wanapinga kukabidhi nchi kwa wapinzani hivi, halafu ikatokea wananchi wakawapa wapinzani kura nyingi zaidi ya CCM, CCM (uongozi) watakubali kuheshimu maamuzi ya watu na kukabidhi uongozi wa nchi kwa wapinzani au la?