NAPE: Kukabidhi nchi kwa wapinzani ni sawa na kumkabidhi Fisi Bucha

WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Points
1,195
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 1,195
Katibu wa itikadi siasa na Uenezi wa CCM Nape Nauye amesema kuikabidhi Nchi kwa wapinzani ni sawa na kumkabidhi Fisi Bucha,ambaye mwisho wa siku bada ya kula na kushiba atakimbia na kuiacha bucha kama ilivyo.

Nape alitoa Kauli hiyo mchana huu wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Mji mdogo wa Katoro wilayani Geita Mkoani Geita,ambapo alihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Alisema serikali ya Chama cha mapinduzi ka sasa inafanya mikakati ya kuhakikisha kamba inatekeleza ahadi zake zote ilizozitoa kwenye uchaguzi uliopita,na kwamba propaganda ambazo zimekuwa zikitolewa na wapinzani hazitakuwa na nguvu mwaka 2015 kwa sababu CCM itakuwa imetekeleza ahadi zake.

Amewataka wananchi kuiamini CCM kwa sababu kwa sasa imepata viongozi makini ambao wako mstari wa mbele kusimamia maslahi ya wanyonge,huku akimfagilia Katibu mkuu mpya wa Chama hicho Abdulhaman Kinana kwamba ni kiboko ya viongozi wabovu ndani na nje ya chama.

Wilaya ya Geita na haa katika majimbo ya Busanda na Geita yamekaliwa vibaya na upinzani,na inavyoonekana ziara ya Nape pamoja na katibu mkuu ambaye yeye alikuwa amebaki mjini Geita kwenye jimbo la Geita ni moja ya mkakati wa kuhakikisha kwamba wanazima harakati za vyama vya upinzani na hasa cdm katika kujikita kwenye majimbo hayo.
 
sosoliso

sosoliso

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Messages
8,210
Points
2,000
sosoliso

sosoliso

JF-Expert Member
Joined May 6, 2009
8,210 2,000
Amewataka wananchi kuiamini CCM kwa sababu kwa sasa imepata viongozi makini ambao wako mstari wa mbele kusimamia maslahi ya wanyonge,huku akimfagilia Katibu mkuu mpya wa Chama hicho Abdulhaman Kinana kwamba ni kiboko ya viongozi wabovu ndani na nje ya chama.
Mkuu mbona mlianza kuaminiwa toka mwaka 1961.. wakati huo ikiitwa TANU..! Umegeuka wimbo..?

Huyo Kinana c ndo anasafirisha meno ya tembo kwenda mashariki ya mbali huko..? Leo unadai ni kiongozi kiboko..? Labda kwa wizi wa nyara za nchi..!
 
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2007
Messages
4,820
Points
2,000
Mchambuzi

Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2007
4,820 2,000
Nisingependa kuamini kwamba Mwenyekiti alipomsifia Nape pale Mnazi Mmoja kwamba anafanya kazi nzuri sana na ya kusaidia Chama kwa kuwajibu wapinzani, alikuwa ana maana ya kauli za ovyo ovyo kama hizi; Haya ni matusi sio kwa wapinzani bali watanzania wanaotumia haki yao ya kikatiba kuunga mkono chama cha siasa wanachoona kinawafaa, bila ya kujalisha kama wanafanikiwa kukiweka chama hicho madarakani au hapana; Hii ni aibu sana kwa chama chetu, na sisi huku 'site' tumekuwa tunapata sana shida na maneno ya Nape, tunaonekana majuha kuunga CCM mkono, hata hoja za kukitetea zinaisha kwani mbali na chama kuvurunda kwenye mambo ya msingi, sasa kinaingia nguoni mwa watu na kuwavujinia heshima; kilichobakia ni kuwapiga tu na kuwapora mali zao;
 
Wingu

Wingu

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2011
Messages
4,323
Points
1,225
Wingu

Wingu

JF-Expert Member
Joined Jan 14, 2011
4,323 1,225
Hakika ni ukweli mtupu Nape umenena
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
90,368
Points
2,000
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
90,368 2,000
Mkichakachua uchaguzi 2015 basi damu ni lazima imwagike kwa kiasi cha kutisha. Watu wamechoshwa kabisa na magamba. Magamba wanaendelea kuwepo madarakani kwa kutumia wizi wa kura na utoaji rushwa kwa wapiga kura.
 
Dingswayo

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2009
Messages
4,020
Points
1,250
Dingswayo

Dingswayo

JF-Expert Member
Joined May 26, 2009
4,020 1,250
Kwa wale waliosoma fasihi ya Kiswahili hapo zamani watakumbuka kuna mwandishi mmoja alielezea dhana ya 'kinyume cha maneno'. Simkumbuki ni nani alisema hivyo, nadhani kuna watanikumbusha humu. Nape ametumia kinyume cha maneno kuelezea hali ambayo ccm imetufikisha hapa. Wamekuwa kama fisi waliokabidhiwa bucha na mifano ni mingi. Hebu angalia utajiri wa kufuru wa viongozi pamoja na familia zao. Utajiri huo umepatikana mara baada ya wao kuwa viongozi. Kuna habari zimeenea kuwa mtoto wa kiongozi mkuu anamiliki utajiri usio na kifani, miaka michache tu baada ya 'kuhitimu' masomo. Chanzo cha utajiri huu kimeulizwa mara kadhaa lakini wameshindwa kujieleza.
i
Nani sasa atabisha kuwa ccm wamegeuka fisi waliokabidhiwa bucha?
 
Mimibaba

Mimibaba

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2009
Messages
4,559
Points
1,195
Mimibaba

Mimibaba

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2009
4,559 1,195
Nisingependa kuamini kwamba Mwenyekiti alipomsifia Nape pale Mnazi Mmoja kwamba anafanya kazi nzuri sana na ya kusaidia Chama kwa kuwajibu wapinzani, alikuwa ana maana ya kauli za ovyo ovyo kama hizi.
Mkuu mbona unahangaika na kitu dhahiri. Nape yuko sahihi kuwa wao wana Bucha na wanamadaraka ya kumkabidhi bucha kwa ye yote wanaemwamini kuwastiri na maovu yao. Sasa chambua bucha ni ipi na wenye madaraka ni akina nani? Ukishachambua hilo unganisha na kauli za mwenyekiti utagundua kuwa uongozi wa CCM ni genge, janga na ni kikundi kidogo kilichojitenga na na wanachama waaminifu wa CCM kama wewe.

Silkushawishi ukihame maana utakuwa mbali na imani yako na maudhui ya itikadi ya chama; ila nakushawishi tafakari chukua hatua kama mwananchi ambaye ameporwa "Bucha" na genge hilo na janga kwa taifa letu.
 
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Messages
39,393
Points
2,000
Daudi Mchambuzi

Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Joined Nov 25, 2010
39,393 2,000
Katibu wa itikadi siasa na Uenezi wa CCM Nape Nauye amesema kuikabidhi Nchi kwa wapinzani ni sawa na kumkabidhi Fisi Bucha,ambaye mwisho wa siku bada ya kula na kushiba atakimbia na kuiacha bucha kama ilivyo.

Nape alitoa Kauli hiyo mchana huu wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika Mji mdogo wa Katoro wilayani Geita Mkoani Geita,ambapo alihutubia mamia ya wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Alisema serikali ya Chama cha mapinduzi ka sasa inafanya mikakati ya kuhakikisha kamba inatekeleza ahadi zake zote ilizozitoa kwenye uchaguzi uliopita,na kwamba propaganda ambazo zimekuwa zikitolewa na wapinzani hazitakuwa na nguvu mwaka 2015 kwa sababu CCM itakuwa imetekeleza ahadi zake.

Amewataka wananchi kuiamini CCM kwa sababu kwa sasa imepata viongozi makini ambao wako mstari wa mbele kusimamia maslahi ya wanyonge,huku akimfagilia Katibu mkuu mpya wa Chama hicho Abdulhaman Kinana kwamba ni kiboko ya viongozi wabovu ndani na nje ya chama.

Wilaya ya Geita na haa katika majimbo ya Busanda na Geita yamekaliwa vibaya na upinzani,na inavyoonekana ziara ya Nape pamoja na katibu mkuu ambaye yeye alikuwa amebaki mjini Geita kwenye jimbo la Geita ni moja ya mkakati wa kuhakikisha kwamba wanazima harakati za vyama vya upinzani na hasa cdm katika kujikita kwenye majimbo hayo.
Hivi kuna mtu mwenye akili timamu anaweza kuzunguka mikoani kuwazuga wapiga kura kuwa ccm bado wanafanya mikakati ya kushuhulikia ahadi walizotoa mwaka 2010???

Hivi ni chama gani kinachoiba rasilimali za watanzania kwa kutorosha wanyama hai na kufanya biashara haramu ya pembe za ndovu?
Nitawaona raiya wa Geita ni wajinga kama wataishabikia CCM hili hali serikali hii inasaini mikataba mibovu kwenye migodi ya Geita na kuwaacha wakazi wa eneo hilo kuwa maskini wa kutupwa.

HATARI:
Weka mbali na Tembo.
 
Mwita Maranya

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2008
Messages
10,569
Points
1,250
Mwita Maranya

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2008
10,569 1,250
huku akimfagilia Katibu mkuu mpya wa Chama hicho Abdulhaman Kinana kwamba ni kiboko ya viongozi wabovu ndani na nje ya chama.
Mwenyekiti wa chama ambaye pia ni raisi wa JMT ambaye pia ni amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama ameshindwa kabisa kuwakabili hao viongozi wabovu ndani ya ccm na serikali, eti leo katibu mkuu wa chama fisadi kinana ndiye aweze kuwa kiboko ya viongozi wabovu?
Akawadanganye mandondocha ya ccm yaliyozoea kudanganywa, sio watu walio na akili zao timamu.
 
Kitoabu

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined
Jul 7, 2011
Messages
5,762
Points
1,250
Kitoabu

Kitoabu

JF-Expert Member
Joined Jul 7, 2011
5,762 1,250
Kwahiyo mika yote hawakutekeleza hadi kumbe walikua wakimngoja kinana? Mbona wame chelewa wadanganyika tmesha amka kwa sasa 2na jua ccm niwajuzi kubadi chupa lajini kilevi ni kilakilaee
 
M

MERCYCITY

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2012
Messages
466
Points
500
M

MERCYCITY

JF-Expert Member
Joined Jan 25, 2012
466 500
Nape kajipange tena, sina chama lakini kwa maneno yako unakiangamiza chama. Hii inaonyesha hata kwa kura hamtatoka madarakani maana mnajua mnachokifanya. Fisi akishiba anaachia wenzie sasa ni bora ya fisi kuliko mnavyofanya. Nimesoma mahali fulani wakati ulikuwa sumba ulitukana watu.(Mchana wakiwa kwenye mkutano wa hadhara eneo la Liboli, Nape aliwaudhi baada ya kuanza kutoa matusi ya nguoni na hivyo akazomewa kwa nguvu kiasi cha kudai wanaozomea wana mimba. kutoka gazeti la tanzania daima) Nape acha kujitafutia laana wewe na watoto wako, bado mdogo sana na
 
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2012
Messages
13,991
Points
2,000
THE BIG SHOW

THE BIG SHOW

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2012
13,991 2,000
Wakienda kanda ya kaskazini nina mashaka ni mbuzi na wanyama wa jamii hiyo pekee watakaokwenda kuwaskiliza,huko ndio hawataki hata kuskia jina lenyewe

c.c.m ikifa siwez hata kuizika,nitaitupa baharini iliwe na papa..
 
Hebie

Hebie

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2012
Messages
1,316
Points
1,500
Hebie

Hebie

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2012
1,316 1,500
Dingswayo-'kinyume cha mambo' nimeipenda.

Amsikilizaye mjinga yeye ndiye mjinga maana mjinga haelimishi ama hamfanyi mtu kuwa mwelevu bali humpotosha!

Nilimpa nafasi hadi kumpigia kura za maoni ndani ya ccm jimbo la Ubungo akigombea nafasi ya ubunge na mama Shamsa mwangunga, alichezewa mchezo akalopoka na kumshutumu EL akimshutumu na ufisadi wa jengo la UVCCM, wakampa ukuu wa wilaya (mtwara kama sikosei) akatuliza kitenesi, leo anakuja na swaga gani tena?

Nina kashahada kangu nafuatilia mambo hasa yaliyo na mustakabali wa nchi, nitapata wapi muda wa kumsikiliza Nape? Hanidanganyi huya jank!
 
M

Mkulia

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Messages
373
Points
225
M

Mkulia

JF-Expert Member
Joined Apr 26, 2012
373 225
Kila mtu hunena yale yaujazayo moyo wake. Kwa hiyo Nape anadhihirisha kuwa yeye na magamba wenzake ni mafisi wanaofikiria zaidi matumbo yao na siyo ya wenzao. Hivi kwa akili yake ya kitoto Nape anataka kutuamisha watanzania kuwa uwepo wa viongozi wezi,wazembe,majambazi na mafisadi ulikuwa unasubiri ujio wa Kinana? Kwani huyo Kinana ndiyo kwanza anajiunga na hiki chama cha mafisadi? Si alikuwepo tangu zama zile? Kwa hiyo imani ya Kinana kwa watanzania ipo wapi? P'se Nape acha utoto na kejeli kwani watanzania wa leo sio kama wale wa miaka ile.
 
yaser

yaser

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2012
Messages
1,371
Points
1,225
yaser

yaser

JF-Expert Member
Joined Jan 23, 2012
1,371 1,225
Kwa wale waliosoma fasihi ya Kiswahili hapo zamani watakumbuka kuna mwandishi mmoja alielezea dhana ya 'kinyume cha maneno'. Simkumbuki ni nani alisema hivyo, nadhani kuna watanikumbusha humu. Nape ametumia kinyume cha maneno kuelezea hali ambayo ccm imetufikisha hapa. Wamekuwa kama fisi waliokabidhiwa bucha na mifano ni mingi. Hebu angalia utajiri wa kufuru wa viongozi pamoja na familia zao. Utajiri huo umepatikana mara baada ya wao kuwa viongozi. Kuna habari zimeenea kuwa mtoto wa kiongozi mkuu anamiliki utajiri usio na kifani, miaka michache tu baada ya 'kuhitimu' masomo. Chanzo cha utajiri huu kimeulizwa mara kadhaa lakini wameshindwa kujieleza.
i
Nani sasa atabisha kuwa ccm wamegeuka fisi waliokabidhiwa bucha?
dah hii nchi bwana....mtoto wa mbowe ni mdogo tu pale mikocheni anatembelea VOGUE..
 
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Points
1,195
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 1,195
Mkuu mbona mlianza kuaminiwa toka mwaka 1961.. wakati huo ikiitwa TANU..! Umegeuka wimbo..?

Huyo Kinana c ndo anasafirisha meno ya tembo kwenda mashariki ya mbali huko..? Leo unadai ni kiongozi kiboko..? Labda kwa wizi wa nyara za nchi..!
Mkuu mimi sijui hilo na wala sio hoja yangu hiyo,hayo ya meno ya Tembo unayajua wewe na Kinana wako labda unafanya nae mimi sijui na wala si jukumu langu.
 
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined
Jun 22, 2011
Messages
4,225
Points
1,195
Age
40
WABHEJASANA

WABHEJASANA

JF-Expert Member
Joined Jun 22, 2011
4,225 1,195
Yaani hata mseme nini lazima hii mizee tuitoe madalakani.
Ni kweli lakini jambo hili linahitaji mkakati na utekelezaji na sin ushabiki tu wa kisiasa,kama ambao naona unafanyika humu ndani!!!
 
Forum statistics

Threads 1,296,633
Members 498,713
Posts 31,254,458
Top