Tetesi: Joseph Misalaba na kampeni chafu kuwania nafasi ya Ukatibu Naibu Mkuu ndani ya Chama cha Walimu Tanzania

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,399
6,077
Kama ambavyo tumekua tukiendelea kufichua namna ambavyo uongozi wa CWT unatafutwa kwa mbinu chafu na namna baadhi ya watu walivyokihujumu chama, leo tunamleta kwenu Joseph Misalaba Mgombea wa nafasi ya Unaibu Katibu Mkuu CWT. Mtajwa hapo juu ni katibu wa CWT wilaya ya Geita aliyeajiriwa kwenye Chama kinyemela na Deus Seif bila hata kupitia njia ya usaili ambayo ndio njia pekee ya kuwaajiri makatibu wa CWT tangu zamani.

Ili kuweka miundombinu sahihi kwa Deus, alim sapoti Simon Shija akawa mjumbe wa kamati ya utendaji ya Taifa (KUT) akiwakilisha mkoa wa Geita. Hivi sasa ndiye katibu wa timu ya mpira ya Geita Gold FC inayocheza ligi kuu. Huyu pamoja na Deus Seif ndio wanaomfadhili Joseph Misalaba ndio maana ana uwezo wa kutisha wa kumpa kila mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa CWT shilingi laki 2 kila mmoja. Hivi mwalimu wa kawaida kiwango hicho cha hongo anakipata wapi? Na hata akikipata pengine kupitia mikopo atakirejeshaje?

Ndugu zangu chama kinauzwa na walimu wanahujumiwa. Deus na genge lake wameamua kuwekeza nguvu kwaJoseph Misalaba kama walivyofanya kwa Magesa kuhakikisha kwamba anapata unaibu katibu mkuu ili wakifanikiwa katika hilo wavune pesa za walimu ili chama cha Walimu kiendelee kusapoti Geita Gold Football Club kama ilivyokua inafanyika kuisapoti Namungo Football Club kwa kusapoti benchi la ufundi na wachezaji kupitia ada za walimu. Hapa Walimu Mnapigwa.

Hivi Joseph Misalaba ana uwezo gani wa kugawa fedha anazogawa kwa wapiga kura kama hategemei kurejesha fedha hizo kwa kuwaibia walimu? Na kwa kulipa fadhila kwa Godfathers wanaompa ufadhili? Kwa leo niishie hapa ila tunaendelea kuufatilia uchaguzi tightly with a close eyes and ears.
 
Taarifa hizi na ushahidi vipelekwe TAKUKURU, ikiwezekana walimu mliohongwa mjitokeze Kama mashahidi. Anawadharau Sana huyu, laki 2 zitakupeleka wapi na kiongozi atayewaibia ili kurudisha hongo yake. Lazima atawaibia huyu ili arudishe chake.

Serikali iingilie Kati. Sasa nimejua kwanini wale walimu wa hiki chama walimgomea Rais Samia kuwa Ma DC.
 
Back
Top Bottom