Nape, 'Kujivua Gamba' ni danganya toto??

DSN

DSN

JF-Expert Member
Joined
Feb 2, 2011
Messages
2,793
Likes
132
Points
160
DSN

DSN

JF-Expert Member
Joined Feb 2, 2011
2,793 132 160

Sometimes wazee wa kijani wanajua kucheza draft au bao,manake walipo si ajabu wanatathimini athari za kujivua gamba Igunga waone na kusikia pia kwa kupima upepo wakisaidiwa na mapungufu ya vyama vya upinzani.

Pressure toka kwa wapinzani wao ndiyo mwamko wa kuibua kwa changamoto [challange] za kujivua gamba.Kama hakuna pressure au external force SIONI SABABU YA KUJIVUA GAMBA.Hii ni kanuni ya kisayansi na wazi wala halina mjadala kwa walio pitia masomo ya Physics wanajua kanuni ya FORCE.Kama hakuna nguvu kutoka NJE basi HAKUNA UMUHIMU WA KUJIVUA GAMBA,gamba liatavuliwa na NGUVU TOKA NJE sio Ndani hizo ni kanuni za maumbile ya Kisayansi.Wao CCM watakachofanya kama HAKUNA EXTERNAL FORCE maisha yataendelea kama jana na bata mwendo mzima,lakini wakikumbana na nguvu kutoka Nje [External Force] itabidi wajivue kwa kuwa wanajua wauwezo wa kuzia nguvu ya ndani [Internal Force] lakini hawana nguvu au mbinu ya kupambana na nguvu za Nje ya uwezo wao bali kuzifuata zinakowata waende.

TUFIKE HATUA TUJIFUNZE KUPAMBANA NA UKWELI [REALITY], binadamu tuna utashi,na CCM ni binadamu pia, pamoja na matendo yao bado wanatamani kuishi kwenye utawala na kutawala kama utashi mwingine wowote.Hivyo basi kanuni za kisayansi ndizo zitakazo waibua wao kukumbuka na kuibua mzozo wa utashi wao dhidi ya utashi wa jamii nzima, ambayo ni mgongano wa kimaslahi kijamii [Conflict of Interes].

Hivyo wenye wajibu wa kuwafanya CCM kuendeleza utashi wa kujivua gamba waendeleze mkakati wa kujivua utashi huo basi wendeleze jukumu hilo la kuwaambia wajivue kwa mujibu wa maelekezo ya Nguvu ya Nje ambayo kila Mtu anaafiki kuwa ni sahihi,na si kuwaachia CCM kwa kuwa wajivue, kiuhalisia CCM walipofika hilo LA KUJIVUA GAMBA KUPITIA WAO WENYEWE HALIWEZEKANI NA HAWALIWEZI TENA KUJIGEUZA.
 
U

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
20,357
Likes
1,840
Points
280
U

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
20,357 1,840 280
View attachment 38967

Mkuu analysis yako ni nzuri kweli.
 
Mtanzania1

Mtanzania1

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2010
Messages
1,169
Likes
0
Points
133
Mtanzania1

Mtanzania1

JF-Expert Member
Joined Dec 30, 2010
1,169 0 133
Labda wanatafuta mashoka........ujumbe uliwafikia
 
C

chuwaalbert

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2010
Messages
3,587
Likes
1,859
Points
280
C

chuwaalbert

JF-Expert Member
Joined Sep 17, 2010
3,587 1,859 280
Nakubaliana na DSN. Bila msukumo toka nje hamna mabadiliko.
Pili, kujivua gamba ni mchezo wa watawala wakiwashirikisha waandishi wa habari kupeleka hisia za watanzania nje ya hoja ya msingi, mtakumbuka kuwa wakati JMK akitangaza propaganda hiyo kulikuwa na msukumo wa DOWANZI kulipwa mamilioni! Upepo umebadilishwa sasa kuvuana magamba hatukusikii! Wanavuta muda, siku zinakwenda na watamaliza siku za kutawala na matatizo ya wtanzania yataendelea!
 
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Messages
1,478
Likes
12
Points
135
Makene

Makene

JF-Expert Member
Joined Nov 1, 2010
1,478 12 135
hiyo ndiyo ccm kumbe ulikuwa huijui. hicho ni chama cha ma'idea' kila siku wanabuni mbinu nyingine dhidi ya ile waliyokuwa wameibuni awali.
kama vile tu simba akiona jike anachelewa kuingia kwenye heat kwa ajili ya watoto, basi yule dume atauwa watoto aliosababisha wazaliwe ili aweze kujamiiana na yule simba jike.
 
mikatabafeki

mikatabafeki

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Messages
12,827
Likes
2,119
Points
280
mikatabafeki

mikatabafeki

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2010
12,827 2,119 280
sumu bado ni kaali mno na inaua watu kama kawaida
 
U

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined
Mar 18, 2011
Messages
20,357
Likes
1,840
Points
280
U

Ulimakafu

JF-Expert Member
Joined Mar 18, 2011
20,357 1,840 280
Nakubaliana na DSN. Bila msukumo toka nje hamna mabadiliko.
Pili, kujivua gamba ni mchezo wa watawala wakiwashirikisha waandishi wa habari kupeleka hisia za watanzania nje ya hoja ya msingi, mtakumbuka kuwa wakati JMK akitangaza propaganda hiyo kulikuwa na msukumo wa DOWANZI kulipwa mamilioni! Upepo umebadilishwa sasa kuvuana magamba hatukusikii! Wanavuta muda, siku zinakwenda na watamaliza siku za kutawala na matatizo ya wtanzania yataendelea!
Mambo mengine ni aibu tupu mkuu.chama hakina msimamo.
 
K

KAMBOTA

Senior Member
Joined
Mar 21, 2011
Messages
176
Likes
16
Points
0
K

KAMBOTA

Senior Member
Joined Mar 21, 2011
176 16 0
Na Nova Kambota,

Wapo watanzania wanaoamini kuwa itawachukua muda sana kumsahau mwanasiasa Nape Nauye kutokana na kile kinachoweza kutafsiriwa kuwa jinsi mwanasiasa huyo kijana alivyojigeuza kichekesho kila anapopata wasaa wa kuzungumza na wanahabari naam! Huyo ndiyo Nape Moses Nauye yule katibu wa itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi ambaye amejipachika jukumu la kuitikia kiitikio cha wimbo maarufu wa Jakaya Kikwete wa ``CCM lazima ijivue gamba``.

Sifahamu mara ngapi huwa Nape anazisoma makala zangu lakini nina uhakika kila anapopata wasaa wa kufanya hivyo huwa hakosi kuzisoma hivyo niweke wazi kuwa nina uhakika makala hii itamfikia iwe kwa kuisoma yeye mwenyewe au kwa kusikia kutoka kwa wapambe wake.

Ni Nape Moses Nauye huyu ambaye sasa ameamua kupunguza ``uvuvuzela`` baada ya kumaizikuwa alichodhani ni mapambano kumbe ni fitna za makundi ya ndani ya chama chake. Huyu aliwahi kujitapa kuwa CCM sharti ijivue gamba tena ndani ya siku tisini tu!, wenye akili tulishabaini kuwa hizi ni kelele za mlevi aliyenyimwa pombe, sasa Nape ni shahidi kuwa hivi sasa ni takribani miezi tisa sasa lakini hakuna gamba lililovuliwa au hata hiko chama chake kukiri uzito wa gamba hilo .

Nape ni aina ya wanasiasa wanaopenda kubebwa kwa mbeleko , hii ndiyo sababu hata alipokuwa anajitokeza na kuzungumza na waandishi wa habari kuhusu dhana ya kujivua gamba kila mwenye akili timamu alijua pasi na shaka kuwa ametumwa na wanaomtumia, alahaula! Lakini Nape kwa kutojua amefuta jina lake kwenye orodha ya wanasiasa wakubwa wa Tanzania wa miaka ijayo, hakuna ubishi naposema kuwa amejifuta mwenyewe naweza nisieleweke , bilashaka hii ni mantiki dhaifu lakini naomba wasomaji wangu muikubali kwasasa licha ya udhaifu wake kwa kuwa pasipo kukubali mantiki hii ya Nape kujimaliza itakuwa vigumu sana kwenu kuuelewa mwelekeo mbovu wa CCM na watendaji wake wa aina ya Nape.

Labda nitoe mfano wa mwanaharakati na mwanamapinduzi aliyetutoka hivi karibuni hayati Regia Mtema ambaye aliwahi kufanya tendo la ujasiri la kuomba msamaha mara Baada ya matamshi yake makali dhidi ya wale aliowaita ``wafugaji wavamizi`` huko katika wilaya ya kilombero, nachotaka kukisema hapa in ule ujasiri wa Regia kujitokeza hadharani na kuomba msamaha ndiyo maana namuuliza Nape anangoja nini kuomba msamaha kwa kuwaghilibu watanzania? Si Nape aliyejifanya mafisadi watang`oka ndani ya siku tisini? Si Nape aliyewapotezea muda wananchi masikini wa nchi hii kwa kuwadanganya kila uchao? Anataka mpaka Kikwete amtume kuomba msamaha?.

Ni dhahiri pasipo shaka yoyote kuwa falsafa yaw kujivua gamba imefeli hata mwasisi wake Luteni Kanali Jakaya Mrisho Kikwete anafahamu ukweli huo, tatizo lililopo ambalo linazidi kuimaliza CCM ni kuwa si Kikwete wala huyo Nape aliyetayari kukiri hadharani kushindwa huko, ndiyo maana kwa kutambua hilo nataka kumuuliza Nape kuwa baada ya kushindwa kutimiza alichowaahidi watanzania, sasa anasema nini kuhusu falsafa mufilisi ya kujivua gamba? Tafakari!, A luta continua!
 
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Messages
629
Likes
2
Points
0
Age
42
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2008
629 2 0
Nova Kambota,

Kwanza nikiri jambo moja la kweli ulilosema kwenye makala yako ndefu kuwa SINA MUDA WA KUSOMA MAKALA ZAKO! Sijawahi kuziona wala kuzisikia, pengine hata hao wanaoitwa wapambe wangu hawana muda huo. Pengine amua mwenyewe uthamani wa makala zako, na hasa kama lengo ilikuwa ni kunifikia mimi. Namshukuru Mungu kuiona hii. Nitajibu hoja moja baada ya nyingine.

OMBI.... Wachangiaji wengine tujadili bila jaziba wala matusi tuupate ukweli wa hoja zilizomo humu... TUBISHANE KWA HOJA SI MATUSI, KEJELI WALA JAZBA
 
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Messages
629
Likes
2
Points
0
Age
42
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2008
629 2 0
Hoja yako ya kwanza ni kuamini kwamba haitanichukua muda mrefu kabla sijafutika / kusahaulika kwenye akili na hata mioyo ya watanzania. Kujisemea kwa hili si vizuri sana. Lakini hata kama watanzania hawatanikumbuka kwa hakika mafisadi na vizazi vyao hawatanisahau na kwangu hili ni jema sana maana hata kama sijazuia kwa asilimia mia moja lakini hasara waliyoipata mafisadi si ndogo, kama wanajibaraguza kwako kwamba hawajaumia waulize kwanini wakisikia nape wananyamaza kwa muda!!???

nilipopata nafasi ya kuwatumikia wenzangu niliweka nadhiri.... Nataka nitakapokufa ninaowatumikia wasinitafute kaburini bali nibaki kwenye mioyo yao kwa wema niliowatendea.

Najua fika kwa mafisadi dakika moja ninayoishi ni kilio kikubwa sana kwao...na nitaendelea hivyo mpaka mwenyezi mungu atakapoamua kunichukua.
 
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Messages
629
Likes
2
Points
0
Age
42
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2008
629 2 0
Nova,

Kwamba naimba wimbo wa mtu, kwanza afadhali umepiga hatua wewe na mafisadi waliokutuma kusema ni wimbo wa Kikwete very soon, nasema very soon MTAKIRI KUMBE NI WIMBO WA CHAMA AMBACHO MIE NDIO MSEMAJI WAKE....

Mlipoanza mlisema kuwa ni wimbo wa Nape na Chiligati, kwa hiyo hatua uliofikia wewe na wenzako na hasa baada ya kuambiwa Mwanza tuliamua kwenye kikao, ni nzuri sana maana hata shule unaanza darasa la kwanza then unaendelea, kazana ukikua utasema vizuri na kwa usahihi zaidi.
 
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Messages
15,081
Likes
10,568
Points
280
J

JokaKuu

Platinum Member
Joined Jul 31, 2006
15,081 10,568 280
Nnauye Jr,

..zaidi ya hayo ya kujivua gamba, hivi CCM mmeridhika na matokeo ya mitihani ya kitaifa na mwenendo mzima wa sekta ya elimu hapa nchini?

..naona kama vile chama chako kinaliangamiza taifa letu kutokana na sera yake mbovu ya elimu. CCM na serikali zake imetufikisha mahali ambapo wahitimu wa mfumo wetu wa elimu hawaaminiki tena, na hiyo inadhihirishwa na matokeo ya mitihani na feedback tunayopata toka kwa waajiri[wawekezaji].
 
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Messages
629
Likes
2
Points
0
Age
42
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2008
629 2 0
JokaKuu naomba nijibu ya Nova nikimaliza tutajadili la elimu, pengine ukilianzishia thread yake itakuwa bora zaidi

Nnauye Jr,

..zaidi ya hayo ya kujivua gamba, hivi CCM mmeridhika na matokeo ya mitihani ya kitaifa na mwenendo mzima wa sekta ya elimu hapa nchini?

..naona kama vile chama chako kinaliangamiza taifa letu kutokana na sera yake mbovu ya elimu. CCM na serikali zake imetufikisha mahali ambapo wahitimu wa mfumo wetu wa elimu hawaaminiki tena, na hiyo inadhihirishwa na matokeo ya mitihani na feedback tunayopata toka kwa waajiri[wawekezaji].
 
Mwanajamii

Mwanajamii

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2008
Messages
7,080
Likes
24
Points
0
Mwanajamii

Mwanajamii

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2008
7,080 24 0
Nova Kambota,

Kwanza nikiri jambo moja la kweli ulilosema kwenye makala yako ndefu kuwa SINA MUDA WA KUSOMA MAKALA ZAKO! Sijawahi kuziona wala kuzisikia, pengine hata hao wanaoitwa wapambe wangu hawana muda huo. Pengine amua mwenyewe uthamani wa makala zako, na hasa kama lengo ilikuwa ni kunifikia mimi. Namshukuru Mungu kuiona hii. Nitajibu hoja moja baada ya nyingine.

OMBI.... Wachangiaji wengine tujadili bila jaziba wala matusi tuupate ukweli wa hoja zilizomo humu... TUBISHANE KWA HOJA SI MATUSI, KEJELI WALA JAZBA
Hongera kaka kwa kuingia jamvini, hii ndiyo tunayoitaka na viongozi wengine waige mfano wako!
 
Mwanajamii

Mwanajamii

JF-Expert Member
Joined
Mar 5, 2008
Messages
7,080
Likes
24
Points
0
Mwanajamii

Mwanajamii

JF-Expert Member
Joined Mar 5, 2008
7,080 24 0
Nova,

Kwamba naimba wimbo wa mtu, kwanza afadhali umepiga hatua wewe na mafisadi waliokutuma kusema ni wimbo wa Kikwete very soon, nasema very soon MTAKIRI KUMBE NI WIMBO WA CHAMA AMBACHO MIE NDIO MSEMAJI WAKE....

Mlipoanza mlisema kuwa ni wimbo wa Nape na Chiligati, kwa hiyo hatua uliofikia wewe na wenzako na hasa baada ya kuambiwa Mwanza tuliamua kwenye kikao, ni nzuri sana maana hata shule unaanza darasa la kwanza then unaendelea, kazana ukikua utasema vizuri na kwa usahihi zaidi.
Kaka huyu anaonekana ni wakala wao... lakini hajiulizi kuwa yule jamaa tuliyepata tetesi kwamba ameanza kufunga akaunti zake...ni kazi ya nani?
 
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2008
Messages
629
Likes
2
Points
0
Age
42
H

Honey K

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2008
629 2 0
Hoja nyingin: NAPE KAPUNGUZA UVUVUZELA...

Sina hakika uvuvzela upi uusemao, kama kelele zangu juu ya mijitu iliyojidanganya kuwa inaweza kupewa dhamana ikatumia dhamana hiyo kuifilisi nchi kwa kutumia wao na watoto wao kuingia mikataba ya hovyo ambayo inalazimu Watanzania wavuja jasho walipe, ni uvuvuzela basi nadhani uvuvuzela ni jambo jema sana na hapa nilipo nipo stage ya juu kabisa ya uvuvuzela. Maana nina hasira nao sana, kila nikikumbuka kuwa pengine wangekuwa makini na kutumia dhamana walizopewa vizuri tatizo la umeme leo ingekuwa historia, nasikia hasira sana...

Kila nikikumbuka kuna kina mama wanakufa kwa kukosa aspirini tu, wakati kuna watu walipewa dhamana wakaiingiza nchi kuwalipa bila huruma zaidi ya 152 Mill. Kwa siku, nasikia hasira sana.

Kuna vijana leo wanakaa chini, pesa walizofuja na kulipana bila huruma hao unaowatetea leo zingetatua tatizo hilo kwa kiasi gani?
 
Forum statistics

Threads 1,272,906
Members 490,197
Posts 30,464,049