Operation Vua Gamba, Vua Gwanda Vaa Uzalendo ni ya Nape au CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Operation Vua Gamba, Vua Gwanda Vaa Uzalendo ni ya Nape au CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Losambo, May 30, 2012.

 1. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Wanajamvi,

  Kwa muda kidogo nimekuwa nikifuatilia jukwaani na kuona au kusikia kuwa katibu mwenezi wa CCM Nape Nauye amezindua operation ijulikanayo kama Vua Gamba, Vaa Uzalendo akiwa mkoa Kagera kwa shughuli za chama.

  Kiukweli nilibaki na maswali mengi ambayo naomba wanajamvi akiwepo Nape mnisaidie.

  1.0 Ile operation ni ya kichama au ni ya mtu binafsi yaani Nape? Kwa nini? Nifahamuvyo mimi operation kubwa kama hizo ni lazima zifanyike kitaifa au ziwe na sura ya umoja wa kichama na si mtu mmoja mmoja.

  Mf. CDM walipozindua operation yao M4C Arusha ilikuwa na sura ya kichama kwa maana maandalizi na hata uzinduzi wake ulilenga kuwajulisha umma nini maana ya M4C n.k

  Lakini hilo sijaliona katika operation inayodaiwa kuanzishwa na Nape. Je hili linahalarisha ile kauli ya kuwa Nape anakifanya chama kama mali yake? Anaweza akaamka na kuja na operation yoyote bila ya Mkama au mwenyekiti wake kujua?

  2.0 Ikiwa Vua Gamba, Vaa Uzalendo ni operation ya kichama basi itakuwa imekidhalilisha sana Chama Cha Mapinduzi? Kwa nini? Chama cha Mapinduzi ni chama kikongwe hivyo hakiwezi kufanya mambo yake kienyeji namna ile!!!! Kimantiki kama Nape hakutumwa na Chama inapaswa achukuliwe hatua kali ikiwemo karipio la maandishi kwa kufanya mambo kienyeji yaani bila mawasiliano (Networking)

  3.0 Hata kama ni programme ya kichama bado CCM itakuwa imekosa ubunifu kwa kuiga kutoka CDM. Kama wao walipaswa kuja na programme tofauti ambayo itakuwa na manufaa kwa chama hasa katika kipindi hiki cha kupigana kubaki madarakani au kuondoka!!!! Mwanzo mbaya unaashiria mwishilizo mbaya.

  Naomba nihitimishe kwa kuomba nifahamishwe juu ya sintofahamu ya Vua Gamba, Vua Gwanda Vaa Uzalendo.
   
 2. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Wamefilisika Kimawazo Copy and Paste Kila kitu
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Natamani Nape aje apite hapa na kutoa majibu juu ya hili.
   
 4. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  "Kauli ya nape ni kauli yangu mie " JK
   
 5. English Learner

  English Learner JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 346
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Friends,
  Nape is our fellow youth jamani kwa nini tunamsababishia BP na msongo wa mawazo?

  Naombeni tumpumzishe midomoni na kumchapa na key boards zetu walau kwa siku 2, 3
   
 6. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #6
  May 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Duuuk kweli hili nilikuwa silijui.
   
 7. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  English Learner siyo kwamba anachapwa mdomo, ila nafasi yake ni muhimu sana na hawezi kuepuka hili. Yeye ndiye msemaji wa chama na propaganda aote sasa kuna kipindi tunapenda kufahamu mengi na kuondoa sintofahamu nyingi ikiwemo hii ya Vua Gamba, Vua Gwanda, Vaa uzalendo.
   
 8. Donyongijape

  Donyongijape JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: May 28, 2010
  Messages: 1,451
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  According to statement yake, ''Sasa nimekuja kuwashika,hivi karibuni Nitazindua kampeni ya Vua Gamba, Vua Gwanda, Vaa Uzalendo''. So, kampeni ni yake, km ingekuwa ya chama tungejulishwa sinc last week walipokuwa kwn CC.
   
 9. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #9
  May 31, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kampeni ya vua gamba, vua gwanda ni ya CCJ na siyo CCM na nape aliizinduaka kama mwanzilishi wa CCJ a.k.a CCK....
   
 10. S

  Seif al Islam JF-Expert Member

  #10
  May 31, 2012
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 2,158
  Likes Received: 141
  Trophy Points: 160
  Yani wewe unazungumzia yale mazoezi ya kucheza gofu aliyokuwa akifanya nape kule kagera?
   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  May 31, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  Ivi nape ana watoto?
   
 12. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #12
  May 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Basi CCM ipo so disorganized maana kampeni kubwa kama ile haiwezi kuwa lunched na mtu individual. Kweli naanza kuamini Nape Nnauye hakitakii chama mema.
   
 13. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #13
  May 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona huko umeenda mbali sana, utaharibu maada wakija akina ritz; Rejao; na kundi lake.
   
 14. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #14
  May 31, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndiyo huko aliposema kauli hiyo Seif al islam sasa njilitaka ufafanuzi kama ni kauli ya chama au ya kwake binafsi.
   
 15. kookolikoo

  kookolikoo JF-Expert Member

  #15
  May 31, 2012
  Joined: Mar 9, 2012
  Messages: 2,537
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  JK aliwaambia wajibu hoja za upinzani papo kwa papo bila kungoja vikao. ndo anachofanya nape!

   
 16. Y

  Young zee JF-Expert Member

  #16
  May 31, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 398
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mi kwanza naendelea kutafakari hili jambo kwa kina. Maana kama ni vua gamba, vua gwanda, vaa uzalendo!! Nape atakuwa ametuthibitishia pasi na shaka kuwa CCM sio wazalendo hata kidog6.

  Na itabidi tutafakari tena na tena, kuwa rasilimali zetu (nchi) zinatumiwa vibaya na viongozi wa serikali ya ccm kwa kuwa hawependi taifa lifaidike nazo.

  Baba wa taifa alikuwa na uchungu na nchi na rasilimali zake tofauti na hawa.
   
 17. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #17
  May 31, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ni ya Chama, kulingana na kauli ya Nape kuwa hata akibaki peke yake, CCM itaendelea kuwepo.
   
 18. segwanga

  segwanga JF-Expert Member

  #18
  May 31, 2012
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 2,790
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Ana mtoto mmoja alizaa baada ya kùfanyiwa operation ya mirija ya kupitisha mbegu
   
Loading...