Nape, 'Kujivua Gamba' ni danganya toto??

Nova,
Waambie mafisadi, tafadhali fikisha salaam hizi kama ulivyozifikisha kwangu kutoka kwao, wao ndio watoke tu wawaombe radhi watanzania kwa unyama waliowafanyia badala ya kudhani hawana akili kiasi cha kutaka eti wanaowatetea wananchi ndio wakaombe radhi... Shame on you fisadis...

Jamvini wananijua mi si mwanaccm ama chadema kwangu Tanzania mbele,lakini I always salute to anyone mwenye kupigania Taifa au Mwananchi yoyote wa Taznania ambae ni mpenda haki na mtenda haki,hivyo basi kwa vita vya mafisadi kijana mimi nakupa tano,mkimaliza na madingi na wasure wote wasimamizi wa strategy za ufisadishaji wa Taifa Tanzania njoo kwa recruitment team ya mafisadi viijana.

Mkiwaacha ndani ya vikao vya maamuzi watawageuka na kurecruit vijana innocent hivyo bidii zote zitakuwa hazina maana,wapigeni chini wote na muaanzishe CCM ya vijana wanaotanguliza Tanzania mbele hakika mtakuwa na nafasi nzuri ya kuchuana vyema na Chadema vinginevyo mkiendeleza kuwapa nafasi vijana wa mafisadi hakika kiti cha urais cha mwaka 2015 mtakisikia Radioni hata kama ni sarakasi za mzee kama kinana zitagota ukuta kwa kuwa tayari Watanzania wanafunguka na wanakuwa na ufahamu mkubwa wa dunia inavyokwenda kulinganisha na miaka mitano iliyopita.

My concern to you Nape, be creative and genuine kuwashauri CCM wabadilike enzi ya ubabaishaji na mizengwe kuwa CCM ndicho chama Nchi zimekwisha na sasa kiwape wananchi kile ilicho wahaidi kupitia ilani ya chama chenu,nje ya hapo ITAKULA KWENU kwa kuwa WHAT GOES AROUND COMES AROUND.Unavyoona wewe na kujisikia dhidi ya Nchi yako ndio mamilioni ya vijana Watanzania huko mitaani wanavyojikia.

Tumejifunza kama Taifa na kupitia ufisadi Taifa na Wananchi wamepata mwanga, na ufahamu umeongezeka na kupima tuelekee upande upi je niule wa Taifa kwanza au ni ule wa kikundi cha watu [chama] kwanza?Ustawi wa Taifa unategemea integrity ya waale waliopewa dhamana ya utawala,lakini chama chako kilipotufikisha toka miaka 20 iliyopita hakika umeecha jeraha baya sana ambalo madhara yake itatugharimu miaka kumi na ushee kuyamaliza.

Si pabaya wapigana vita vya kifisadi walipofika na vita nzuri daima ni ile ya wapiganaji wachache,ndio maana Fidel Castro alipofanya mapinduzi Nchini Cuba baadae miaka kadha baada ya mapinduzi alipoulizwa kama angepewa nafasi nyingine ya mapinduzi angesemaje,akasema wakati wa mapinduzi ya wakati huo alikuwa na kikosi cha watu 70 lakini kama angepewa nafasi hiyo leo angeitaji watu 16.Nawe Nape mapambano yako na wenzio haitaji lundo la watu,hivyo watu kama hawa walioanzisha thread hii ni watumwa wape pole,toka lini mtumwa akawa na Free will.

Nami nakukubali kuwa una Free will kitu ambacho ni unique sana kwa vijana wachache walio kwenye siasa za kitanzania kwa kuwa wengi walio huko hasa upande wa CCM wengi wao wamebebwa na kuwa wamefika hapo walipo kwa kuwa na sifa moja huyu n mwenzetu mkono kwa mkono,kisha baadae ukolome, upinge, ukatae, usimamie ukweli, ujipendi wakati umebebwa.Wabebwaji wanawatumikia mabwana zao na si vinginevyo ndio maana tunawaona ni mzigo kwa Taifa.Na daima mtu mwenye Free will daima huwa hana hofu,umuogopa Mungu na kumuheshimu mwanadamu mwenzie.
 
Nape, you need to feel burdened for our nation in order to act. What you have just said is already something and God honours that. He will direct you on what more you can do for our country.

Meanwhile i am greatful for your presence and i believe in what you are trying to achieve and hope you succeed.
 
"KUSHINDWA KWA DHANA YA KUJIVUA GAMBA"

imekuwa ni ndoto na dua ya mafisadi wengi na walafi wa rasilimali za nchi kwa faida ya matumbo yao kuona swala la wao kuwajibishwa kwa usaliti wao linashindwa! Ndo maana wanadhani wanaweza kujidanganya kwa kuimba tu kuwa limekufa.... HUWEZI DHULUMU HAKI ZA WATU NA UKAIMBA TU TENA KWA SHIBE YA KIFISADI KUWA ETI ZOEZI LIMEKUFA... Kama matamanio yote yangekuwa farasi basi kila masikini angepanda ili awe tajiri bahati mbaya sio!

SASA UAMUZI WA NEC ILIYOKETI APRIL MWAKA JANA ILIYORIDHIA MAGEUZI NDANI YA CHAMA( kujivua gamba).. KUHUSU SWALA LA MAADILI ILIAMUA.... VIONGOZI WOTE WANAOTUHUMIWA NA JAMII KWA UFISADI NA RUSHWA, WAPIME NA WACHUKUE HATUA ZA KUWAJIBIKA WENYEWE KWA KUONDOKA KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI VYA CHAMA. WASIPOFANYA HIVYO CHAMA KICHUKUE HATUA YA KUWAONDOA BILA KUCHELEWA.

Wakati wa mjadala watu wakatajwa baadhi ya watu wanaotajwa sana na jamii hasa kwenye ngazi za juu kujihusisha na yanayosemwa kuwa ni ufisadi mkubwa ambao leo ukimwamsha Mtanzania yeyote usingizini ukamuuliza hivi matendo gani ya kifisadi unayoyajua makubwa nchini, bila shaka na bila kigugumizi atakwambia, RICHMOND, DOWANS, EPA, RADA nk. Na ukimuuliza kina nani wanahusika atakutajia majina bila kuuma maneno..

Na tukakubaliana KIKAO KINACHOFUATA TUTAFANYA TATHIMINI YA MWITIKIO WA WITO HUO WA WAO WENYEWE KUWAJIBIKA.... WENGINE WAKATAFISIRI SIKU TISINI, TUKAJARIBU KUFAFANUA LAKINI KWASABABU MAFISADI WANAPESA WASIZO NA UCHUNGU NAZO WAKAENDELEA KUPOTOSHA... SI NENO, TUKAKUTANA NOV. TATHIMINI IKASOMWA IKAONEKANA MWITIKIO SIO MZURI, JAPO TULIKIRI WAPO/ YUPO WALIOITIKIA MWITO HUO.

UAMUZI UKAWA SASA TUCHUKUE HATUA YA PILI YA KUWAONDOA KWANI YA KWANZA YA KUWAPA MUDA KUPIMA, NA NILICHUKUA MUDA MREFU KUPIGA KELELE KUTAKA KILA MMOJA ASIKIE ASIJE MTU KUSEMA SIKUSIKIA( nina hakika kwa wanyonge na wachukia ufisadi kelele zangu zilikuwa za kuamsha matumaini, lakini kwa mafisadi, kelele zangu ilikuwa ni kero kubwa ndo maana wanaziita uvuvuzela, am happy for that kwani lengo ilikuwa ni kuwakera pia mafisadi)..

SASA CHAMA KIPO KWENYE MCHAKATO WA HATUA YA PILI, NA JUZI MKITI WA CCM TAIFA, KASEMA " tuliamua jambo hili kwenye kikao na nila manufaa kwa chama, wanaosema ni la hovyo, wao ndio wa hovyo).

Wanaodhani limekufa wanajidanganya... Mafisadi wanajua hawana chao, sasa kama wanawadanganya ni kwasababu wanataka muendelee kuwasindikiza, kama shetani afanyavyo anajua kabisa mwish wake ni motoni lakini anadanganya watu ili aende nao
 
sasa mnasubiri nini muda wote huo kuwang'oa?
 
Ndugu yake nape agenda yako ya kupinga ufisadi ni nzuri na unastahili pongezi, ila unapokesea ni kuwa mafisadi wanaonekana mbele yako ni wale tu ambao hawako kwenye kambi yako ya 2015, ila wale ambao wako upande wako wao sio mafisadi hapo ndipo tunasema kuwa dhana yako ya kupinga ufisadi inalenga 2015
Kwanza sina kambi, nimewaomba kila mara kusema kambi yangu ipi, kila mara wanababaika tu, mara Sita, Ben, Mwandosya, Mwakyembe, Sumaye, nk. Niambie fisadi gani niliyembagua na kwamba namkumbatia...
Wengine wanadhani msimamo huu nimeanza jana, Mwaka 2008 nilipozungumza na kuokoa mkataba wa hovyo UVCCM nilisema... KWA SWALA LA UBADHIRIFU, UFISADI NA RUSHWA HATA ANGEKUWA BABAANGU MZEE NNAUYE NINGEMSEMA MPAKA AACHE.
 
Mkuu NAPE nakusihi ujaribu kuwa mkweli, wewe unadhani CCM haihitaji mafisadi? kama ni hivyo basi mbona ulifukuzwa wewe Igunga na nafasi yako akapewa fisadi namba 1 wa CCM; ROSTAM? Namaanisha kipindi cha uchaguzi mdogo kule Igunga. Plz nijibu swali langu mkuu!!
 
Nova,
Waambie mafisadi, tafadhali fikisha salaam hizi kama ulivyozifikisha kwangu kutoka kwao, wao ndio watoke tu wawaombe radhi watanzania kwa unyama waliowafanyia badala ya kudhani hawana akili kiasi cha kutaka eti wanaowatetea wananchi ndio wakaombe radhi... Shame on you fisadis...
Nape nakupongeza sana,najua uliyoyafanya ni wachache waliweza ndani ya CCM,nadhani ni Nyerere peke yake, ila wanikwaza padogo tu,huwataji live majina yao,ulimtaja yule wa mkoa tu kuwa mwaanzia chini kuwa mafisadi si juu tu, si useme EL ni fisadi?unamuogopa?tutakuona kweli mpambanaji na umma wote utakuwa nyuma yako.

Kila la heri
 
Kwanza sina kambi, nimewaomba kila mara kusema kambi yangu ipi, kila mara wanababaika tu, mara Sita, Ben, Mwandosya, Mwakyembe, Sumaye, nk. Niambie fisadi gani niliyembagua na kwamba namkumbatia...
Wengine wanadhani msimamo huu nimeanza jana, Mwaka 2008 nilipozungumza na kuokoa mkataba wa hovyo UVCCM nilisema... KWA SWALA LA UBADHIRIFU, UFISADI NA RUSHWA HATA ANGEKUWA BABAANGU MZEE NNAUYE NINGEMSEMA MPAKA AACHE.

Mwenyekiti wa chama chako yeye sio fisadi? Nape sijui what to believe and trust from any of our leaders anymore. Ambaye hakufanya maendeleo yoyote huko jimboni kwake na mzembe leo twampa ubalozi China....what do u think? Hata huo nauita ufisadi. Sorry to say.
 
Hoja nyingin: NAPE KAPUNGUZA UVUVUZELA...

Sina hakika uvuvzela upi uusemao, kama kelele zangu juu ya mijitu iliyojidanganya kuwa inaweza kupewa dhamana ikatumia dhamana hiyo kuifilisi nchi kwa kutumia wao na watoto wao kuingia mikataba ya hovyo ambayo inalazimu Watanzania wavuja jasho walipe, ni uvuvuzela basi nadhani uvuvuzela ni jambo jema sana na hapa nilipo nipo stage ya juu kabisa ya uvuvuzela. Maana nina hasira nao sana, kila nikikumbuka kuwa pengine wangekuwa makini na kutumia dhamana walizopewa vizuri tatizo la umeme leo ingekuwa historia, nasikia hasira sana...

Kila nikikumbuka kuna kina mama wanakufa kwa kukosa aspirini tu, wakati kuna watu walipewa dhamana wakaiingiza nchi kuwalipa bila huruma zaidi ya 152 Mill. Kwa siku, nasikia hasira sana.

Kuna vijana leo wanakaa chini, pesa walizofuja na kulipana bila huruma hao unaowatetea leo zingetatua tatizo hilo kwa kiasi gani?

Nape mdogo wangu, naanza taratibu.

Kwanza nikiri kuwa sina hakika kuwa huyu Nnauye Jr mwenye picha ya Nape ndiye Nape Nnauye kweli, maana bado nina kumbukumbu ya Nape kuikana hiyo ID lakini hakukana matumizi ya picha yake kama avatar ya hiyo ID. Hata hivyo naona Invisible kakupigia chapuo kwa mbali, kwa hiyo kidogo inanipa imani kuwa Nnauye Jr ndiyo huyu huyu Nape Nnauye tunayemjua.

Basi nirejee kwenye mada.

Umeanza vizuri sana katika majibu yako kwa Kambota. Kama ulivyo wewe, mimi pia si msomaji sana wa makala za Kambota ila mara moja moja napitisha macho, haidhuru kujielewesha katika machache. Dunia ni elimu.

Ni kweli kuwa katika siasa za Tanzania, na haswa za ndani ya CCM, Nape Nnauye bado atakuwa na mguso fulani kwa kipindi kirefu kijacho na ninachelea kusema hata kwa vizazi kadhaa vijavyo, kinyume na ambavyo Kambota anadhani kuwa jina hili litafifia katika medali za siasa. Na ni vyema kuwa hukujipigia debe katika hilo. Nitafafanua.

Huo unaoitwa uvuvuzela mkubwa wa Nape katika siasa za Tanzania ni kuhusu kujivua gamba na mpambano dhidi ya kada fulani ya jumuia ambao wanaitwa 'mafisadi', na siyo lazima kuwa ni dhidi ya ufisadi wenyewe. Kwa maoni yangu, kama chochote kimoja katika haya kitatokea, basi jina la Nape litaendelea kuwa katika mtiririko.

Kama 'mafisadi' kweli watathibitiwa na kuwaona Keko au Segerea, ni wazi kuwa historia itamtaja Nape kama mmoja wa wapambanaji katika mafanikio hayo. Jina na jitihada vitakuwepo kwa vizazi kadhaa.

Kama 'mafisadi' watashindwa kuthibitiwa na tutaendelea kuwaona wakitanua na kujimwaga iwe Magogoni au Chimwaga, basi jina la Nape litaendelea kuwepo katika misamiati yetu kama yalivyokuwa ya akina Sokoine, Kolimba na wengineo kuwa walijaribu lakini hawakufanikiwa. Msisitizo hapa uwe katika neno 'walijaribu'. Kwa hiyo ni haki kabisa na ninakubaliana na Nape kuwa kama siyo sisi, walau watoto na uzao wa mafisadi watamkumbuka kwa moja au jingine.

Lakini hiyo peke yake isitoshe na isiwe sababu ya kukumbuka Nape katika ulingo wa siasa.

La pili, na hili labda ni zito kuliko la kwanza, ambalo nakubaliana na Nape ni kuwa hata kama 'uvuvuzela' wake hautazaa matunda ndani ya siku 90 kama alivyodai au hata miezi 90, lakini ukweli ni kuwa CCM kabla ya Nape siyo CCM ya sasa ya Nape na haitakuwa sawa na CCM baada ya Nape. Iwe kwa mazuri au mabaya, ufa katika msingi umeonekana na unazidi kupanda ukutani, na kama hatima itakuwa kubomoa na kujenga upya au kuhama nyumba na kuiacha iporomoke, lakini itaendelea kubaki kuwa kundi la Nape, Mukama, Chiligati, n.k. aidha kwa kutumiwa au kwa dhati kabisa wameitoa CCM toka ndani ya 'vikao vyetu' na kuiweka kwenye macho ya umma kwa njia ambayo CCM haijawahi kuiona na hivyo haijui jinsi gani ya kukabiliana nayo. Ile dhana ya huyu si mwenzetu sasa hivi ndani ya CCM inamgusa kila mmoja wao.

Sasa napenda nigusie kwa ufupi masuala mawili ambayo nitaenda kushoto kwa Nape. Ufisadi na Katiba ya CCM.

Nashukuru kuwa katika bandiko la Nape hapa juu amegusia madhara ya ufisadi katika kuelekeza vipaumbele kwenye huduma za jamii. Ambacho nasikitika kusema kuwa ni dalili za 'unafiki' ni kuwa haya yote yanayotokea ni matunda ya Serikali ya CCM kwa takribani miaka 50, chini ya sera za CCM kwa miaka si chini ya 35, na zinasimamiwa na makada wa CCM kwa kila ngazi kuanzia kitongoji hadi Taifa.

Ni vipi leo tudhani kuwa kwa kuwa tu Nape kasema anaona uchungu, basi hiyo iwe tofauti na Kikwete aliyesema Maisha Bora (na sasa tunasota na bora maisha), au tofauti na Mkapa aliyesema Ukweli na Uwazi (wakati anachukua Kiwira nyuma ya pazia), au Kikwete aliyesema kuwa "hiyo ni ajali tu ya kisiasa" na kwamba hajui Dowans ni ya nani na imetokea wapi wakati Mwanasheria Mkuu wake anasema lazima walipwe, Waziri wake wa Nishati na wa Fedha wanasimamia malipo hayo? Kwa nini tusidhani na kuamini kuwa Nape pia anapoona uchungu, ni mwendelezo wa yale yale ya CCM ya kauli nzuri, matendo maovu?

Sipendi na sitaki kuwatetea hao waliolipwa mabilioni na au kusamehewa kodi kwa mikataba ya madini/maliasili ya mabilioni, wakati akina mama na dada zetu wanajifungulia chini, wazee wetu wanakosa aspirini, watoto wetu wanasomea chini ya miembe, ila naomba niulize ni wakati gani haya yalifanyika au lini yaliacha kufanyika? Kwa kumbukumbu yangu ni kuwa bado yanaendelea hadi leo chini ya uongozi na utawala wa wale wale wanaosema kuwa wanaona uchungu kuwa yanafanyika. Haijalishi kubadili jina la nani kasema iwe Mkapa, Kikwete, Nape, Chiligati, Mukama, Mangula, Sitta, hawa si wale wale tunaowajua chini ya chama kile kile CCM? Lini walibadili madoa yao na ghafla wamekuwa si chui tena na sasa ni wema wana ngozi ya mbuzi au kondoo? Mtenda haachi asili.

Kwa hiyo katika hilo ndugu yangu Nape, sikubaliani na wewe. Sipingi kuhusu wewe kuona uchungu, ila sikubaliani kuwa kweli unaona uchungu. Tenda tuone, usinene tu siku ipite tukalale.

Hili la Katiba bado linanipa utata sana. Niliwahi kusema kitambo kuwa kuna jitihada za makusudi zinafanywa kuibadilisha katiba ya CCM bila kupitia Mkutano Mkuu na inaonekana kuwa lengo ni kumdhibiti mtu na siyo ufanisi wa katiba. Wakati huo sikuwa na mwelekeo sana wa nini kinaendelea. Sasa nina picha nzuri baada ya kuyaona na kuyapitia hayo mabadiliko na haswa baada ya kupitishwa na NEC mwezi huu.

Niliwahi kuandika pia kuhusu ushubiri wa CCM na Kikwete kama Raisi anayemaliza muda, lakini ataendelea kuwa Mwenyekiti hadi 2017 ambaye hatimaye itamuangukia kuamua ni vipi mrithi wake wa 2015 atapatikana. Kwa hapa naamini kwa dhati kabisa Kikwete atapita bila kupingwa 2012 ndani ya CCM. Unaweza kupitia hilo andiko hapa: https://www.jamiiforums.com/tanzania-2010-2015/78626-ushindi-wa-kikwete-2010-shubiri-kwa-ccm.html.

Sishangai sana kuona kuwa mabadiliko haya ya Katiba yameletwa kwa "dharura" kana kwamba CCM haijui ifanyacho na inahitaji udharura kwa suala la kudumu kama Katiba. Lakini dharura ni jadi yetu na ndiyo maana hadi leo tuna makampuni ya umeme wa dharura toka 2006 na hiyo dharura haiendelei kuisha kwa miaka mingine 15 kutegemeana na mikataba. Huu ni mjadala mwingine kwa siku nyingine.

Turudi kwenye mada.

Nape nadhani unafahamu fika kuwa suala la ufanisi halina dharura na pia sheria au kanuni yeyote inayotungwa kukandamiza mtu au kikundi kimoja, huishia kuumiza jamii nzima na siyo huyo mtu pekee au kundi hilo pekee.

Historia na mifano mingi duniani imetuonyesha hivyo kuanzia enzi za Farao na wayahudi, Wamarekani na utumwa, Hitler na unazi, Mubarak na Misri, Mobutu na Zaire, Makaburu na wazawa Afrika Kusini, Ian Smith na Rhodesia, Obote na Uganda, Amini na Uganda, Hayati Karume na Zanzibar, Siad Barre na Somalia, Lenin/Stalin na Urusi, na hata Gbagbo na Ivory Coast au Kenyatta/Ruto na ICC (Don't be vague, let's go to Hague!), na mifano mingi sana.

Lakini mbaya zaidi ni pale kundi lengwa linapofanikiwa kuchukua dhamana na hatimaye kuzitumia sheria na kanuni zile zile zilizopitishwa na mahasimu wao kuwakandamiza wale wale waliozipitisha. Mifano michache niliyoitaja hapo juu inahusika pia, ukiutoa wa Farao na wayahudi kwani historia ilimtangulia Farao. Katika mifano hiyo leo tunaona 'watunzi' wamekuwa 'majeruhi' wa sheria na kanuni kandamizi walizotunga. Kwa Urusi, Misri, Afrika Kusini, Ujerumani, Zaire, Somalia na kadhalika, wengine hawataki hata kutajwa kuwa wana undugu na hao waliotajwa hapo juu.

Binafsi naona huko ndiyo CCM inaelekea na haya mabadiliko ya dharura ya katiba hayaashirii mwisho mwema.

Sasa hivi tunaanza kuona na kusikia jitihada za 'walengwa' wa hayo mabadiliko wakipita kwa wajumbe wa Mkutano Mkuu na kuwashawishi kuwa wakubali na wayapitishe kwa kauli moja hayo mabadiliko, bila pingamizi. Ikumbukwe kuwa hao hao 'walengwa' walipinga haya mabadiliko nje ya NEC, ila wakati wa kura ndani ya NEC walikubaliana nayo kwa kauli moja na kupitisha, isipokuwa Kingunge. Tujilulize wameona nini au wanajua nini ambacho siye wengine tuko gizani? Je, tunawaadhibu watoto watukutu kwa kuwafungia stoo yenye peremende, maziwa na biskuti? Tujiulize.

Hapo ndiyo kwa kiasi fulani naona kuwa ndugu yangu Nape, ni bora wakati mwingine kusimama nje na kufurahia au kuona karaha za nyumba yako badala ya kubweteka ndani na viyoyozi/TV wakati kumbe nje kuna ufa na paa linaezuka.

Kwa hiyo mchukulie Kambota au hata Kiungani, kama majirani tu wanagonga mlango kukwambia kuwa tumeona nyoka anapenya kwenye ufa wa nyumba yako, na usituhukumu kwa kusema kuwa nyumba yako ina ufa.

Haya ni maoni yangu na ninafurahi kuchangia huu mjadala, na kama Mkuu Invisible alivyosema, matusi na kejeli si mahali pake hapa.
 
Nape anajibu kisiasa,maswali mengine kayakimbia,NAPE!Tunakuomba tutajie mafisadi japo wawili wakubwa kwenye chama chetu,na pia inawezekanaje waziri wa serikali ya chama chetu,akafanya ufisadi,na rais ambaye pia ni wetu asijue?kumbuka sentens hii cku ile"mwenyekiti,lipi ambalo nilifanya wewe hulijui"
 
Nape una kazi kijana mwenzangu hapa hao wazee ni vigumu sana kuwabadilisha hata kama si wala rushwa.

Mimi sijui sana siasa za Tanzania kwasababu niko nje kwa muda lakini naomba niseme haya:

Nape sisi kama vijana tungetemea "Big Ideas" za kuendesha nchi kutoka kwa vijana wenzetu walioko kwenye siasa na hizi 'ideas" ni kwa nchi na si siasa.

Mfano: Kama ilivyokuwa JKT ningependa kuona Kijana kama wewe unakuja na Idea ya Wanavyuo kufundisha kwenye secondari kama wamepewa mikopo na serikali. Kama ilivyokuwa JKT hupewi cheti mpaka ufundishe au utoe mchango fulani kwa wanafunzi.

Vilevile tunajua shule ambazo zinafelisha Tanzania mwaka hadi mwaka ningependa kusikia kutoka kwa vijana wazo kama hili:

Kama shule inafelisha ni lazima wanafunzi wafundishwe wakati wa Likizo na wanavyuo na wawalipe mafao shule ikiendelea kufelisha ifungwe. Sijasikia mawazo yeyote ya maana kutoka kwa vijana wenzetu.

Mfano mwingine nimeona unafanikiwa sana hapa Texas Kama kumegundulika njia bora ya kilimo kwenye sehemu moja kama Arusha (Wako Productive kwenye kilimo cha kisasa) basi wachukue hizo method na kuzitawanya sehemu nyingine ambazo zinasuasua. Kwahiyo vijana mngependekeza kufunguliwa kwa bodi ya statistics na kama ipo isiishie kuesabu watu tu bali ichukue statistics za kilimo na elimu ili tujue mafanikio na tuweze ku ya copy.

Vile vile CCM hata Vyama vya upinzani hamjajiuliza hili: Je serikali inatakiwa kufanya nini? Sasa serikali inafanya vitu kuliko uwezo wake na kila tatizo likitokea tunataka serikali itatue na iwe kubwa zaidi. Je nyie vijana mmekuja na mpango gani wa kuifanya serikali ya Tanzania kuwa ndogo na ya ufanisi? Sijawahi kusikia Idea yeyote ya maana kwenye hili.

Serikali ya Tanzania haitakuwa na uwezo wa kufanya kila kitu elimu, afya, barabara, bandari, Tanesco, Mashirika ya ndege , reli, Polisi na jeshi n.k. Kwasababu serikali ni kubwa sana rushwa haitaweza kuisha kwasababu viongozi wako loose sana! Mfano ATC ilikuwa loose watu waka sign mikataba mibovu, Tanesco ilikuwa loose watu waka sign mikataba mibovu isingekuwa ya serikali ingekuwa bora.

Nimeandika mambo mengi hapa lakini bado Nape nasikitika kwamba vijana hamna "Big Ideas" kabisa. Hata Nape ungeweze kuomba Ideas kutoka kwa watu hata hapa mtandaoni lakini hujawahi kufanya hivyo.
 
Nimefuatilia kwa makini mjadala, nami naongezea sehemu ya majibu ya Nape, kuwa moja ya uwezo wa kufikiri wa mtu aliye makini na jambo mahususi, ni kujipambanua mbele ya umma, mwelekeo, malengo na msimamo wake dhahili. Hapa Nape amefanya hivyo, ila kwa sababu ya ushabiki, hoja zinazoingia humu ni kutaka kuendelea kumkatisha tamaa.

Jamani binadamu, mbona ni wazito wa kuamini? Nape ni daraja la ukombozi ndani ya CCM, ambaye hataki tungoje 2015 CCM itakuwa wapi?
 
Kumbukeni ndugu, Daudi alivyomteketeza Goliati kwa Kombeo, na pia namna Yesu alivyokataliwa na Mafarisayo pia Makuhani na kumbukeni msemo wa Kiswahili usemao Nabii hakubaliki nyumbani. Haya pamoja na mengine kama ya Tomaso ya kutaka kuona makovu ya kiganja cha Yes undo asadiki kuwa huyo ndiye alikuwa Mnazareti, itatuletea shida kubwa
 
"KUSHINDWA KWA DHANA YA KUJIVUA GAMBA"

imekuwa ni ndoto na dua ya mafisadi wengi na walafi wa rasilimali za nchi kwa faida ya matumbo yao kuona swala la wao kuwajibishwa kwa usaliti wao linashindwa! Ndo maana wanadhani wanaweza kujidanganya kwa kuimba tu kuwa limekufa.... HUWEZI DHULUMU HAKI ZA WATU NA UKAIMBA TU TENA KWA SHIBE YA KIFISADI KUWA ETI ZOEZI LIMEKUFA... Kama matamanio yote yangekuwa farasi basi kila masikini angepanda ili awe tajiri bahati mbaya sio!

SASA UAMUZI WA NEC ILIYOKETI APRIL MWAKA JANA ILIYORIDHIA MAGEUZI NDANI YA CHAMA( kujivua gamba).. KUHUSU SWALA LA MAADILI ILIAMUA.... VIONGOZI WOTE WANAOTUHUMIWA NA JAMII KWA UFISADI NA RUSHWA, WAPIME NA WACHUKUE HATUA ZA KUWAJIBIKA WENYEWE KWA KUONDOKA KWENYE VIKAO VYA MAAMUZI VYA CHAMA. WASIPOFANYA HIVYO CHAMA KICHUKUE HATUA YA KUWAONDOA BILA KUCHELEWA.

Wakati wa mjadala watu wakatajwa baadhi ya watu wanaotajwa sana na jamii hasa kwenye ngazi za juu kujihusisha na yanayosemwa kuwa ni ufisadi mkubwa ambao leo ukimwamsha Mtanzania yeyote usingizini ukamuuliza hivi matendo gani ya kifisadi unayoyajua makubwa nchini, bila shaka na bila kigugumizi atakwambia, RICHMOND, DOWANS, EPA, RADA nk. Na ukimuuliza kina nani wanahusika atakutajia majina bila kuuma maneno..

Na tukakubaliana KIKAO KINACHOFUATA TUTAFANYA TATHIMINI YA MWITIKIO WA WITO HUO WA WAO WENYEWE KUWAJIBIKA.... WENGINE WAKATAFISIRI SIKU TISINI, TUKAJARIBU KUFAFANUA LAKINI KWASABABU MAFISADI WANAPESA WASIZO NA UCHUNGU NAZO WAKAENDELEA KUPOTOSHA... SI NENO, TUKAKUTANA NOV. TATHIMINI IKASOMWA IKAONEKANA MWITIKIO SIO MZURI, JAPO TULIKIRI WAPO/ YUPO WALIOITIKIA MWITO HUO.

UAMUZI UKAWA SASA TUCHUKUE HATUA YA PILI YA KUWAONDOA KWANI YA KWANZA YA KUWAPA MUDA KUPIMA, NA NILICHUKUA MUDA MREFU KUPIGA KELELE KUTAKA KILA MMOJA ASIKIE ASIJE MTU KUSEMA SIKUSIKIA( nina hakika kwa wanyonge na wachukia ufisadi kelele zangu zilikuwa za kuamsha matumaini, lakini kwa mafisadi, kelele zangu ilikuwa ni kero kubwa ndo maana wanaziita uvuvuzela, am happy for that kwani lengo ilikuwa ni kuwakera pia mafisadi)..

SASA CHAMA KIPO KWENYE MCHAKATO WA HATUA YA PILI, NA JUZI MKITI WA CCM TAIFA, KASEMA " tuliamua jambo hili kwenye kikao na nila manufaa kwa chama, wanaosema ni la hovyo, wao ndio wa hovyo).

Wanaodhani limekufa wanajidanganya... Mafisadi wanajua hawana chao, sasa kama wanawadanganya ni kwasababu wanataka muendelee kuwasindikiza, kama shetani afanyavyo anajua kabisa mwish wake ni motoni lakini anadanganya watu ili aende nao

Kaka waeleze maana sie wengine tukisema huwa tunaambiwa ni wewe kwenye ID tofauti au umetutuma,wakidhani tunajuana.....
 
Nape, I commend the way you are urgently reacting on issues raised - I like this kind of reaction it helps to clear issues outright without wasting G/thinkers times. Imagine if you delayed to react on this matter probably Nova would continue to post but now he is nowhere to be seen. I have seen several CDM leaders including Secretary General reacting in the same way they help to clear some issues of public concerns that require urgency. Hence spare time of great thinkers to other critical issues thereafter.

Gossiping is no good, Nova. You better show up and make your case while the alleged is online.
Too low. Nova anasubiri majibu ya Nape ambayo anaendelea kujibu. You are the one gossiping.
 
Something will never be right somewhere manake kuna chembe za unafiki hakuna ukweli unaoonekana ama unaoweza kuthibitishwa. Waungwana huyu NAPE naye aseme ndani ya CCM mafisadi ni kina nani??? Manake ndani ya CDM wanafahamika through list kf shame sasa yeye anasimamia wapi??? Huu unafiki wekeni kando kabla na baada! Na ni kwa nini Sera ya CDM ya ufisadi imebakwa!!!
 
Hivi ndugu yangu Nape, ni kweli unachokisema? au ni kutaka kuboresha muda hapa JF?

Hivi hizi kauli ni za Chama na mwenyekiti wake na wanachama wake au za kwako kwa sababu unahasira na mafisadi?

Nimekuuliza hivyo kwa sababu kama ulivyosema ufisadi ni kitu kibaya, na kwa ujumla wake ufisadi ni kosa la jinai, huko nyuma TANU ilikuwa inasema UBEPARI NI UNYAMAAAAAA! Na ndiyo kuna wakati iliundwa sheria ya uhujumu uchumi ambayo nadhani bado ipo.

Mimi kwa uelewa wangu wa kawaida, katika kutatua hili kusingekuwa na haja ya wewe kutoa mapovu na kuonyesha unahasira kiasi gani na hili. Si CCM ni chama tawala? kina serikali, polisi, majeshi, usalama na wanainchi?

Nilitegemea suala hili lingeshaisha muda mrefu na chama kingekuwa saaaaaaafi. Wote wangekuwa KEKO na UKONGA. Sasa ndugu yangu kuweka maelezo meeeengi hapa kusema ukweli ni kutokututendea haki.

Yaani kwa ninavyoona, hatua mnayochukua ni kuuma na kupulizia. Haisaidiii chama hata kidogo. Si unajua ngoja ngoja yaumiza matumbo? Hawa ni wakosaji na kwa maelezo yako mnawajua, lakini mnawaambia wajiangalie ili wachukue hatua. Are you serious? sidhani. Nadhani tunangojea sinema huko mbele, jambo ambalo si zuri sana kwa chama na nchi kwa ujumla.
 
Hoja nyingin: NAPE KAPUNGUZA UVUVUZELA...

Sina hakika uvuvzela upi uusemao, kama kelele zangu juu ya mijitu iliyojidanganya kuwa inaweza kupewa dhamana ikatumia dhamana hiyo kuifilisi nchi kwa kutumia wao na watoto wao kuingia mikataba ya hovyo ambayo inalazimu Watanzania wavuja jasho walipe, ni uvuvuzela basi nadhani uvuvuzela ni jambo jema sana na hapa nilipo nipo stage ya juu kabisa ya uvuvuzela. Maana nina hasira nao sana, kila nikikumbuka kuwa pengine wangekuwa makini na kutumia dhamana walizopewa vizuri tatizo la umeme leo ingekuwa historia, nasikia hasira sana...

Kila nikikumbuka kuna kina mama wanakufa kwa kukosa aspirini tu, wakati kuna watu walipewa dhamana wakaiingiza nchi kuwalipa bila huruma zaidi ya 152 Mill. Kwa siku, nasikia hasira sana.

Kuna vijana leo wanakaa chini, pesa walizofuja na kulipana bila huruma hao unaowatetea leo zingetatua tatizo hilo kwa kiasi gani?
kuna kiongozi wa juu wa chadema kaiba password ya Nape?
 
Back
Top Bottom