Nape, 'Kujivua Gamba' ni danganya toto??

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,380
8,135
Mimi nimekuwa nikifuatilia kwa umakini zaidi kuhusu hii la CCM kujivua Gamba tangu siku ile Nape Nnauye aseme kwamba wale wote walio ndani ya chama hicho na wamezungukwa na kashifa, sasa muda wao umefika wa kujiondoa katika nyadhifa zao au la watatolewa kwa nguvu!

Hakuishia hapo aliwapa miezi mitatu na kwakuwa aliwalenga watu Kama Andrew Change, Rostam Aziz, Edward Lowassa. Nikasubiri mkutano mkuu nikijua watawavua gamba kama walivyo tangaza awali ila chakushangaza CCM iko kimya kama haijawai kusemwa kitu!

Je, CCM inawambia vipi wananchi wa Igunga kuhusu kashifa zinazo waandama viongozi wake?

Je, CCM inajikosha vipi kwa jamii kutokana na kauli yake ya kujivua Gamba?

Je, Nape aliropoka au aliyekuwa akitumiwa na mtu sasa kaona pazito kaamua kukaa kimya mbona sasa hatumsikii?

Au wameamua kuwasamehe watuhumiwa wa kashifa za ufisadi!?
 

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
37,376
64,441
Nape asivyo na mshipa wa aibu anaweza kukujibu tena bila haya.
 

Tata

JF-Expert Member
Dec 3, 2009
5,800
2,712
Tatizo gamba ni CCM yenyewe wala sio mtu mmoja mmoja kama Nape na wenzake walivyotaka kuaminisha watu. Ili wajivue gamba kiukweli inabidi watimue watu wote ndani ya CCM na wa mwisho kutoka wakabidhi funguo za ofisi zote za CCM kwa akina Kaduma na wazee wenzake wa enzi za TANU.
 

Queen Kyusa

JF-Expert Member
Apr 25, 2011
663
161
Ukifuatilia siasa za nape unapata kichefuchefu kabisa, hayo magamba wanayovuana juzi juzi katoka kumsifia RA tena mpaka humu jamvini kajitetea kwa hoja za kitoto sana. Unajua ukiamua kufanya jambo fanya kwa kujiamini sio unakuwa vuguvugu. Hakuna kuvuana magamba wala nn ni siasa uchwara tu ambazo wala haziwasaidii watanzania na matatizo yuliyo nayo sasa.

Mm naona wameamua kuwasamehe watuhumiwa wa kashfa za kifisadi tena kimyakimya
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
27,667
30,115
CCM ya sasa inaongozwa kimagumashi -- siamini haya yanayotekea igunga kama kweli hiki ni chama makini cha kumkomboa mtanzania kwenye wimbi la umaskini.
 

Albano

Member
Jul 21, 2009
41
10
Kijana mmoja wa kijapan anayeitwa Shinji Daiko aliwai kuitembelea Tanzania na kuishi hapa kwa zaidi ya miezi mitatu. Akiwasili nchini alisema Tanzania ni nchi ya kipekee, lakini hakusema upekee wake upo katika nini, siku namsindikiza uwanja wa ndege kwa ajili ya safari ya kurejea kwao, nlimkumbusha hoja yake ya upekee wa Tanzania yangu, alinijibu kama ifuatavyo:-

1. Watanzania ni wepesi wa kulaumu na kuhukumu.
2. Pia ni wavivu wakubwa wa kutekeleza majukumu yao kwa kisingizio cha kuzilaumu serikali zao.
3. Ni wazito wa kufikiri masuala muhimu na wepesi wa kufikiri masuala yasiyo muhimu.
4. Watanzania wengi hasa vijana wanaomaliza elimu ya juu, wanapenda miujiza katika kuelekea mafanikio, badala ya juhudi na maarifa katika kuhakikisha wanafanikiwa, ni wepesi wa kuakakuajiriwa badala ya kujiajiri, hawapendi maisha yenye changamoto badala yake wanapenda maisha yenye mlengo chanya.

Nilitumia muda mrefu kutafakari hayo, na sasa nimejiridhisha kuwa yule kijana alisema kweli, tena kweli tupu. Tanzania kwanza, mengine badae.
 

kiroba

JF-Expert Member
Sep 10, 2011
324
114
Unajua hili suala ni kubwa sana zaidi ya sisi na viongozi wetu tunavyofikiri. Nadhani hapa ndio ile dhana ya kuchukua maamuzi magumu inakuja kuingia hapa. Hapa sasa tunajaribu kupata picha ya kuwa kwenye CCM ya leo hii hakuna kuchukia ufisadi bali ni chuki kati ya mtu na mtu au kundi na kundi.

Mimi nilidhani kwa kuwa RA aliamua kujivua gamba kama slogan ya chama inavyosema basi ndio ulikuwa wakati muafaka kwa CCM kupaza sauti ya juu kwa kauli moja ya kupinga ufisadi na wale wanaotenda mambo ya kifisadi. Hapa sikuona mantiki ya kumwita RA kwenye kampeni wakati hana taswira nzuri katika jamii ya watanzania. Hapa ndipo pangetumika kupata mtaji wa kisiasa kwa kukataa kabisa kushirikiana na watuhumiwa wa ufisadi. Lakini cha kushangaza CCM kwa kuonyesha haina nia ya dhati ya kupambana na ufisadi basi imeamua kukumbatia watuhumiwa wake.

Wako wapi akina Samweli Sitta,Pius Msekwa,Mukama,Nape,Mwakyembe,Olesendeka,Anna Killango, na wengine wengi ambao wamejipambbanua kama majemedari wa kupambana na ufisadi? Mimi nimeingiwa sana na wasi wasi, hivi ni kipi haswa kilichopelekea kaanzisha mkakati wa kujivua gamba. Kujivua gamba ulikuwa ni mkakati mzuri sana wa kukitakasa chama kwa maovu yaliyotendwa na baadhi ya wanaCCM wasiokuwa na uadilifu.

Maoni yangu kwa viongozi waandamizi wa CCM, ni kuwa wajiandae kwa hoja zenye nguvu na za kueleweka kuwapatia wananchi ufafanuzi wa ni kipi hawsa kilipelekea kuwaalika tene kwenye chama watu ambao wametuhumiwa kuwa ni mafisadi? Zaidi ya hapo kwa kweli CCM imepoteza dira na haijui inakoelekea. Natoa wito kwa viongozi wa ngazi zote kuanzia shina hadi taifa, kuweni makini sana na myenendo yenu ya kukiongoza chama,vinginevyo hakitasalimika na kansa ya ufisadi.

Mungu ibariki Tanzania. Ahsanteni.
 

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,575
521
Nape hana jipya ni makapi na matapishi ya ccm sijaona jipya analofanya kama sio kuhadaa wananchi
 

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,380
8,135
Sijui nini lakini yaelekea chama kuna kitu kinafukuta na hakuna wakukiopoa kwani tatizo nikwamba wote siwasafi!!

Na zaidi watakuwa wamemuonya katibu mwenezi kwa achunge mwenendo huu anaokuja nao si mzuri unakigawa chama na kitakufia mikononi!!
 

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,882
1,124
mimi siku zote nawatetea wanawake wanaotupa watoto chooni kwa sababu bila wao kujua wanatuondolea mabalaa yanayowezakutufika mbeleni,
na wale wagumu wa kuchukua maamuzi ndio hawa wanatuachia vituko duniani.
 

Concrete

JF-Expert Member
Mar 12, 2011
3,605
538
@Kujivua gamba ni usanii wa JK kama tulivyomzoea, sasa wimbo umeshachuja inabidi warudi kwenye siasa yao ya kawaida ya kulindana wao kwa wao. @Namsikitikia Nape kwa kukubali kutumiwa na JK kwenye siasa hizo za kisanii, amepoteza kabisa uwezo wa kufanya siasa za hoja na kubakia kutetea kila kitu kinachofanywa na CCM kwa sababu tu yeye ni katibu mwenezi&itikadi. @Sasa Nape ameingia kwenye orodha ya waliokuwa makada wa CCM waropokaji ambao tumekwisha wasahau eg. Yusuph Makamba, Ramadhani Mapuri, Tambwe hiza. Na muda si mrefu CCM watamchoka pia Nape na kumpoteza kabisa kwenye ulingo wa siasa za Tz kama wenzie waliomtangulia. Lets wait&watch the movie..
 

chuda08

Member
Sep 12, 2011
5
0
CCM ya sasa inaongozwa kimagumashi -- siamini haya yanayotekea igunga kama kweli hiki ni chama makini cha kumkomboa mtanzania kwenye wimbi la umaskini.

hapo kwenye red uko sawa FUSO. wa kumkomboa mtz ni mtz mwenyewe, kosa letu tumekalia kulalamika tu hatuchukui hatua hivyo tutaendelea kutaabika siku zote!!
 

KakaKiiza

JF-Expert Member
Feb 16, 2010
11,380
8,135
Siasa za magamba utata!!Lakini ajabu ni huyu LA aliondoka kwa mbwembwe na matusi kibao kwakusema hawezi siasa za uchwara je leo siasa hizo zimeisha huko igunga?ajabu niyeye pekee kavua gamba au ililazimu avue gamba?
 

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
24,646
5,408
Ile falsafa maarufu ya kujivua gamba iliyoasisiwa na cha tawala yapata miezi kadhaa iliyopita sasa inaonekana kufifia na kutotajwatajwa tena.Ndio imeishia hapo au wenyewe wanafuta kasi mpya au imekuwaje?
 

measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,782
2,396
hilo ni swali kwa CCM na slogany hiyo ya gamba....wameshasahau mkuu. Watakuja na mpya ngoja tusubiri...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom