Nape: Jisahihishe, Unapoteza Vijana Wengi CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape: Jisahihishe, Unapoteza Vijana Wengi CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mchambuzi, Aug 14, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote, nikiwa kama Mwana CCM, naongozwa na kanuni muhimu sana ya chama inayosema:
  Kukosoa na Kukosoana Ndio Silaha ya Mapinduzi.

  Vile vile tuna kanuni nyingine muhimu sana ndani ya Chama chetu inayosema:
  Nitasema Ukweli Daima, Fitina Kwangu Mwiko.

  Moja ya mambo ambayo yamekuwa yanakivuruga chama chetu ni tabia ya viongozi na wanachama kuwa na unafsi, ambao ni ugonjwa mbaya sana. Hata Mwalimu Nyerere aliwahi kulizungumzia tatizo hili ndani ya kitabu chake cha TANU na Rais (1962) ambapo alikemea sana tabia za unafiki, fitina, uwoga na unafsi miongoni mwa viongozi na wanachama wa TANU.


  Kwa mfano, Mwalimu anatamka kwamba:

  "Makosa yetu mengine hutokana na woga; woga unaotuzuia kumlaumu mkubwa japo tunajua kuwa kakosa, au kumtetea mdogo anayelaumiwa na wakubwa japo tunajua hana makosa. Na msingi wa woga pia ni unafsi. Pengine huwa tunaogopa sisi wenyewe kulaumiwa au kupata hasara fulani. Pengine twaweza kuwa hatuna cheo chochote ambacho tunaogopa kupoteza; pengine hatuna wala tamaa yoyote ya kupata cheo fulani. Lakini woga unaweza kutokana na tamaa ya kila binadamu kupendwa na binadamu wenzake. Sisi wote tunayo tamaa hii, au sivyo tusingekuwa binadamu. Woga huu huweza ukamfanya mtu kuvumilia maovu, hasa kama maovu yale yanatendwa na walio wengi kwa walio wachache, au yanatendwa na wakubwa kwa wadogo. Kwa kuogopa kuwaudhi wengi tunaacha watende makosa bila kuwasahihisha, wasije wakatuchukia. Huu ni unafsi mbaya sana. Ni kweli kwamba demokrasia haiwezi kudumu ikiwa wachache hawatakubali matakwa ya wengi. Lakini matakwa ya wengi hujulikana katika majadiliano au mazungumzo ya wazi wazi."


  J.K Nyerere, TANU na Raia (1962, pp2-3).
  ----------------------------------------------------

  Katika siku za hivi karibuni, Nape kama kiongozi wa chama chetu amekuwa anatuchanganya sana sisi vijana wenzake ambao bado tuna mapenzi na CCM, na maoni haya sio yangu tu bali ya vijana wengi tuliopo site. Tumekuwa tunamtetea kwa nguvu zetu zote kwenye mijadala yetu vijiweni lakini kila siku zinavyozidi kwenda mbele, tunazidi kuishiwa na ammunition za kutumia kupambana kwa hoja. Kwa mfano, karibia mwezi mmoja uliopita, Nape alitoa tamko kwenye vyombo vya habari kwamba yeye haoni tatizo lolote Mzee Mustapha Sobodo kuchangia fedha Chadema. Lakini jambo la kushangaza na linalotufanya sasa tukimbie vijiwe ili kuficha nyuso zetu ni hili:

  Mzee Sobodo ni mtanzania kama watanzania waliokusanyika Serena Hotel na kuichangia Chadema milioni 70 hapo kwa papo (huku nyingine zikiwa ni ahadi/pledges). Kitendo hiki hakikumfurahisha Nape, ingawa ukweli ni kwamba ni kiwango kidogo kuliko kile alichotoa mtanzania mwingine – Mzee Sobodo ambacho nadhani ilikuwa ni fedha taslimu shilling milioni 100. Sasa iweje suala la Mzee Sobodo (mtanzania kutoa fedha taslimu milioni 100 kwa Chadema) lisiwe tatizo lakini watanzania wengine pale Serena kutoa fedha taslimu milioni 70 iwe tatizo? Yupo kijana mmoja wa chama cha upinzani ambae huwa tupo pamoja kijiweni kwetu alitoa kauli moja ambayo kidogo iliharibu hali ya hewa, na binafsi nisingependa kuamini kwamba yupo sahihi. Kijana huyu alitamka kwamba:

  ----
  "huyo Nape wenu anawachanganya tu, ‘inawezekana' (akasisitiza tena ‘inawezekana') suala la mzee Sobodo analiunga mkono kwa nia ya kujijenga na Mzee huyu mzalendo ili aje kumsaidia apate jimbo moja la ubunge mwaka 2015 huko kusini kwani Mzee Sobodo na Nape wote wanatokea mkoa wa Lindi. Isitoshe, ndoto za Nape ubungo zimemalizwa na John Mnyika."
  ----

  Maneno haya yalinishtua sana na nisingependa kuamini kwamba hii ndio dhamira kuu ya Nape kuwa na msimamo tofauti na suala la harambee ya chadema pale serena (milioni 70 fedha taslimu) vis a vis suala la Mzee Sobodo (milioni 100 fedha taslimu). Isitoshe, sina uhakika kama kweli mzee Sabodo anatokea Kusini.

  Haya ndio maoni yangu kama mwana CCM bila ya unafiki, fitina wala woga, na napata ujasiri wa kunena haya kwani hata Mwalimu Nyerere kama tulivyokwisha ona anahimiza kwamba kufanya hivyo ndio kukijenga chama, na kinyume chake ni kukibomoa chama. Hii ndio dhana nzima kanuni ya "Kukosoa na Kukosoana Ndio Silaha ya Mapinduzi."


  Vijana wengi waliopo ‘site' hawana access yoyote kwa Nape, na pia hawamjui in person, hivyo ni vigumu kwao kumpatia mawazo yao yenye lengo la kujenga chama ndani ya misingi niliyokwisha ijadili. Mitandao kama JamiiForums ndio huwa tegemeo la wengi towards that end. Isitoshe, Nape ni mtumiaji mzuri wa mtandao huu kwani tumemuona mara kwa mara akijibu hoja mbali mbali kwa uvumilivu wa hali ya juu. Vinginevyo, katika kipindi cha miezi ya hivi karibuni, Nape amekuwa anatoa kauli ambazo sisi watetezi wake huku vijiweni mara nyingine inabidi tukimbie ili kuficha nyuso zetu – kwa mfano kauli dhidi ya wanachama wa CCM wanaohamia upinzani n.k. Kila kukicha, vijana wengi ambao bado wana mapenzi na CCM licha ya Chama chetu kukosa (au pengine niseme kukoseshwa) mwelekeo, huwa wanasali sana Nape arudie katika hali yake ya zamani alipokuwa UVCCM kwani vijana wengi walikuwa wanajidai na kujivunia sana kuwa na kiongozi wa aina yake, na kijana mwenzao ndani ya Chama ambae hakika alikuwa makini sana kwa kila jambo.

  Nawakilisha.
   
 2. a

  andrews JF-Expert Member

  #2
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​mtanzania wa kweli mpenda mabadiliko na maendeleo akiwa kijana kujiunga na ccm atakuwa kaachiwa radhi na wazazi wake maana kimebakia kuwa chama cha watoto wa mafisadi tu
   
 3. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #3
  Aug 14, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Hoja yako inaeleweka, lakini ukweli ni kwamba chama ni watu, sio mtu mmoja mmoja; kwahiyo kuhusu suala la ufisadi na viongozi, watakuja na kupita, and as a matter of fact, hakuna kiongozi mwenye kashfa ya ufisadi ambae atakuwa active politically beyond 2025; otherwise wengi wetu tumejaa subira, wataondoka tu, na watakiacha chama na misingi ile ile (aidha kikiwa cha upinzani au kinachoshika dola),na tutapata tu viongozi wazalendo kutuongoza kwa misingi hiyo; Vinginevyo,kumbuka tu kwamba CCM ya Zambia (UNIP) ilipoteza uchaguzi kwa Chadema ya Zambia (MMD) baada ya kutawala kwa miaka zaidi ya 25; na Chadema ya Zambia (MMD), ikaja kupoteza uchaguzi juzi juzi baada ya kutawala kwa miaka 20, kwa chama kingine kipya kabisa cha Patriotic Front (PF) cha Rais wa sasa, Satta. katika siku za usoni, CCM ya Zambia (UNIP) na Chadema ya Zambia (MMD) bado vina nafasi kubwa ya kurudi madarakani kwani hawajakata tamaa; Hii ndio raha ya demokrasia ya vyama vingi;
   
 4. a

  andrews JF-Expert Member

  #4
  Aug 14, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​labda nyerere afufuke na kawawa lakini mfumo wa uchaguzi ndani ya ccm ni wa kirushwa sana umeingia mpaka serikalini na hakuna mtu anayeweza kuinusuru ccm labda chama kingine kiongoze nchi hapo labda mtajipanga kwa system mliyo nayo ya akina mukama na nape msitegemee mapya ila kuzama kwa manuwari yenu 2015.
   
 5. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Na kuhusu kauli yako kwamba CCM ni chama cha watoto wa mafisadi, ebu nikuulize: Chadema ni Chama Cha Watoto wa nani? Wakulima (asilimia 70) vijijini? Kwani kama Chadema au chama kingine chochote kitanithibitishia kwamba ni chama cha wakulima (watanzania waliopo vijijini), nitajivua uanachama wangu wa CCM haraka sana na kujiunga na Chadema au chama chochote kitakachofanikisha hilo. Angalau TANU/CCM kilikuwa chama cha wakulima awali, kimeyumba kidogo lakini kikipata uongozi makini, kitarudia hali yake ya awali kwani misingi yote ya chama in that context bado ipo intact;
   
 6. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #6
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  Uko sahihi sana mkuu! What i know ni kwamba Nape amesoma Political Science, sasa sijui anachofanya sasa ni siasa ambazo mimi hata simwelewi.

  The issue of today sio propaganda ni kuadmit failure then choose the right approach ili kurejesha mvuto wa chama unaotoweka kwa kasi mithiri ya rocket iendayo sayari ya mars! Siku za nyuma ccm ilikuwa imewekeza sana kwa vijana na hivyo kuwa na mtaji wa kudumu na ndio hao watu wazima wachache wanaoishilia.

  Kama Nape angesimamia mambo haya 4 angekuwa kijana wa kipekee!
  1. Serikali kuwa wazi kwenye mambo ya msingi kwa maendeleo ya taifa, mfano mikataba inayoingia na wawekezaji kama madini n.k.
  2. Serikali kutumia kwa umakini mapato ya ndani yanayotokana na kodi za ndani na kuepuka matumizi makubwa ya fedha za kukopa.
  3. Viongozi kuishi maisha yatakayo reflect uhalisia wa uchumi wa mtanzania na siyo kukopy na kupaste lifestyle za viongozi wa Bahrain, Brunei au Abu Dhabi.
  4. Kuchukua hatua kali kwa viongozi wanao hujumu uchumi wa nchi kwa kuiba na kufuja mali za umma na kujilimbikizia mali
   
 7. a

  andrews JF-Expert Member

  #7
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kuna ukweli ambao wanaccm mungewa kukubali basi ccm isingewza kuanza kusambaratika kama sasa kuna udini ambao ccm ndiyo inayoongoza kuwasema chadema na cuf lakini nyuma ya pazia ccm inaongoza na ukabila unakuja juu sana na kama huamini statistic zilizofanywa tanzania chini ya ccm 2020 lazima damu imwagike labda ccm ikubali kushindwa chaguzi kama ilivyoshindwa 2010 lakini kwa kutumia mapolisi uwt walishiriki kupora kura za watanzania hilo kina mwana ccm analijua na nilimrekodi mbunge mmoja wa ccm akinieleza mikakati yote wanayoitumia nitaieka siku moja humu muone ccm ilivyofilisika kisiasa
   
 8. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #8
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Tatizo la Nape ni kutumikia mabwana wawili

  upande mmoja anataka kuwa mpiganaji na kupinga ufisadi

  upande wa pili ni 'kutetea chama' by any means necessary

  na chama chenyewe kimejaa mafisadi

  its a very tough job....

  anatia huruma kwa kweli
   
 9. a

  andrews JF-Expert Member

  #9
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ​ni ukweli usiopingika kuibadilisha ccm ni kuongozwa na chama kingine hata kama ni miaka 5 tu
   
 10. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #10
  Aug 15, 2012
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,224
  Likes Received: 7,346
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi,
  Nadhani sio nwana CCM tu wanaoficha nyuso, ulimwengu wa vijana wa Tanzania unajisikia tutwee na fadhaa wanapomsikia mtu aliyetarajiwa kuonyesha vijana wanaweza akionyesha pengine wasivyoweza.

  Nape wa UVCCM si huyu wa CCM. Kule UVCCM alikuwa huru, huku amebanwa. Tambo zake alipoingia na sasa ni mithili ya 'paka aliyefungiwa nje' na anazunguka zunguka kupata mahali pa upenyo.

  Mimi huamini uwezo wa mtu na si umri, jinsia au wajihi. Kwa siku za karibuni nimekuwa natembea kifua mbele kule 'site' za vijiwe vyetu kwasababu nikitaka kuonyesha ubovu wa vijana huwa nina mifano rahisi sana kama wa Nape na wale walioko Bungeni. Wakati Mchambuzi ukiishiwa silaha kutokana na hoja za Nape, nashukuru mimi ananipa silaha za bure.

  Kisaikolojia Nape amechangyikiwa, ile dhamira yake aliyokuwa nayo amegundua ilikuwa ni njozi baada ya lunch.
  Juzi kapigwa kibao na mwenyekiti wake aache kuwasumbua mafisadi wa Radar.
  Huko nyuma amewahi kupigwa vibao ndani ya Halmashauri kuu, na kususiwa chama sasa anazunguka mwenyewe mikoani.

  In short Nape is frustrated, the only place he can vent out his frustration is through other political parties, engage in cheap politics, unorganized rhetoric and the likes of sewer politics.
  Nape has lost his strength on national issues as well as command of political language and intellect.

  Mr Nnauye is incapacitated and completely grounded. He is accepting heavy punches from fisadi and psychological trauma from cronies and allies. His best friend JK has distanced from him and rejoin his old club.
  Mr Nnauye has no vote of confidence from the public especially the youth wing who have shifted their loyalty from role model to Nape the puppet.

  Nnauye Jnr is a typical example of youth failures. Nape lost the battle against Fisadi now is loosing support from young blood. Nnauye must revist his strategy if he wanna endure in politics.

  Nape, take vacation and re-evaluate your career pathway. Spend time to learn modern politics.
  Who can tell the diffence between Nape of 2012 and Mustafa Songambele of 1962!
   
 11. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  You have raised an interesting point. Hivi is politics a profession? Mimi sidhani, at least kwa Tanzania kwani sote tunajua kwamba kila profession inahitaji training ya kila mara – kila mtu anayefanya kazi ya profession hulazimika kwenda kufanya training mara kwa mara ili kuwa up to date na his or her job requirements (na hii huwa ni lazima, sio hiyari). Kama politics kwa Tanzania ni profession, basi sio miaka ya sasa bali enzi za Mwalimu kwani yeye alijenga hadi Chuo cha siasa (Kivukoni) kwa ajili ya kuwanoa wanasiasa mara kwa mara. Vinginevyo Tanzania kwa miaka ya sasa, hakuna formal qualifications za mtu kuwa kiongozi wa kisiasa, not even relevant work experience is taken into account.
   
 12. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #12
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Lakini kazi za idara yake zipo very clear, kwani kwa mujibu wa katiba ya CCM, kazi za idara ya itikadi na uenezi ni hizi (samahani nina version ya kiingereza):

  (a) To deal with fundamental issues concerning the Ideology and Policies of Chama Cha Mapinduzi.
  (b) To disseminate and elaborate on the CCM ideology and policies.
  (c) To plan and supervise the training, agitation and involvement of CCM cadres and members in party work.
  (d) To supervise the Party’s media institutions, communication and mobilization of the masses in general.
  (e) To guide and supervise the preparation of CCM policies, programmes and the Party’s Election Manifesto.
  (f) To supervise research, library service and Party literature/documents.

  Unaweza kusaidia kufafanua kidogo dhana ya kutumikia mabwana wawili inachangiwa vipi na his job description/requirements?
   
 13. Anyisile Obheli

  Anyisile Obheli JF-Expert Member

  #13
  Aug 15, 2012
  Joined: Dec 13, 2009
  Messages: 3,304
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Kijana mwenzetu kapoteza dira kabisa maana ye kila kukicha awaza chadema tu, na kufwarafwaja kwingi mdomoni
   
 14. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #14
  Aug 15, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Mkuu Escobar nadhani wewe ni mmojawapo unayeamini kuwa elimu ya hii nchi ipo juu sana.Huku TZ huwa Mtanzania huwa anaendesha maisha yake bila kuweka Link na Elimu yake.Yaani anayejitahidi sana huw ani ele miaka michache ya mwanzo kabla hajapata mrija wa kula.Ukijataka jua angalia bunge,kuna wanasheria wengi ila mambo ya kisheria huwa hawawezi yatambua haraka na kujibu kwa ufasaha kwa kulinaganisha vipengele.Angalia Tafiti nyingi zilivyopikwa, angalia ugunduzi wa kusuasua VETA,SIDO etc.

  Nimeona na kusikia watu kibao kuanzia mahospital, maofisi ya kawaida watu wanakuwa na task upand mmoja upande wa pili wanavyeti vyenye GPA kubwa.Halafu wanashindwa solve problem akija mtu miwngine kisolve na kupewa maelezo anasema "ah haa aaah. sasa si ungeniambia kuwa topiki hii na hii ipo,sasa mimi ningejuaje?".

  Sisemi hivyo kwa mheshimiwa Nape ila kuna shida sana kwa wsomi wetu kutafsiri walivyovisoma viwasaidie kubuni njia mpya ,na majibu mapya ya matatizo ya kila siku.

  Na hii ndio shida hata kwa wanamichezo wetu,walimu wanawafundisha sana kabla ya mechi,ila sku ya mechi huwa wanakuwa hawaoni ni wapi pa kutumia yale maelekezo.Ila baada ya mechi wakianza elezewa ndio wanabaki "ah hah, aisee next time hawanipiti tena".Mechi ijayo wanaingia kama wanafunzi waliokariri tricks nyingi sana ila haziendani na pumzi yao,uwezo wao katika viungo pamoja na wakiwa wamepungukiwa na ubunifu ,Ubunifu unoweza fanya kitu na baadaye kujiliza ni "vipi ulifanya pale mpaka ukaleta ushindi", ila kwa wabongo wengi huwa "Ni vipi hawakuona alichofanya mpinzani hadi kutushinda". Hata wasomi wetu wenye sifa za kuwa na GPA kubwa huwa wanashangaa sana "Ni vipi jamaa wa facebook wamekuja na kitu kipya", wataalamu wa CCM "nao wanajiuliza ni vipi CDM wanakata mbuga?", "Ni vipi sasa wanapiga harambee na wanapa hela nyingi, huku wakiwa hawana hela nyingi kama za mafisadi?"Kwa vile hawajui hesabu rahisi kama "average ya watu 10,000,000 wakitoa 1,000/=" yaani hata kama watakuwa wachache lakini michango mikubwa kama ya Sabodo ita adjust na kuweka huo wastani. Sasa wanashangaa nini billion kumi kuchangwa katika vijiwe?

  Kucheza na number kumekuwa kukiwafaidisha wandesha michezo ya kubahatisha hata hapa Tanzania. Makanisa nayo yamekuwa yakicheza na number kiasi cha kuweza fanya shughuli zao za kimaendeleo bila watu kujua,wakidhani jamaa wanapata misaada nje.Kwa miaka mingi makanisa walishaambiwa kuwa wajifunze jitegemea kwa vyanzo vya ndani kwani siku zaja hawatapa misaasa ya nje.Sasa hili la ruzuku za vyama kukatwa na hali ya uchumi mataifa ya nje.Ni wazi kuwa vyama vinahitaji kuwa na watu makini wa kuhakikisha ukusanyaji wa hela haukatiki.nape alihtaji kuwa makini sana zaidi ya kuingia katika vita na CDM.Sijui hajui kuwa kushambulia CDM ni hatari sana kwa mwanasiasa mmoja mmoja.Hakumbuki Arumeru?Nape anahitaji hepuka washambulia CDM kwa staili ya kuwafanya wajibu.Alipaswa wajibu kwa staili ya kupunguza makali, na awatumie wasaidizi wake kutuma makombora.Normally CDM wakijibu hoja huwa wanajibu vibaya na ni ngumu kujitetea. Yupo wapi Wasira, Mkapa. Wassira kawa kituko hata mbele ya watoto mara wamuonapo katika TV.

  WASICHOJUA WASOMI WETU NI KWAMBA SHULENI MASWALI YANAULIZWA KIMAANDISHI NA MAJIBU YAKE YANAKUWA YANAJULIKANA.KATIKA REAL LIFE MASWALI HUULIZWA KWA PROBLEMS,NA MAJIBU YAKE YANASAHIHISHWA SI KWA KALAMU NA MAKSI.
   
 15. t

  tenende JF-Expert Member

  #15
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ............. Usichelewe mkuu, weka, ...tunaisubiri!!!!...
   
 16. t

  tenende JF-Expert Member

  #16
  Aug 15, 2012
  Joined: Jan 10, 2012
  Messages: 6,560
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  ............. Usichelewe mkuu, weka, ...tunaisubiri!!!!...
   
 17. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #17
  Aug 15, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  CCM wanakosoana jamii forums?

  Haina mshiko.
   
 18. k

  kisimani JF-Expert Member

  #18
  Aug 15, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 553
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nimekuwa nikitafakari sana juu ya kauli za CCM ikiwa ni pamoja na hii aliyoitoa Ndugu Nape juu ya cdm kufanya usanii katika kuchangisha fedha (M4C).

  Kauli za Rais Jakaya Kikwete katika migomo kuwa aserikali haiwezi kulipa walimu, madaktari mishahara waliyoomba (japo hakueleza wanaweza kufika kiasi gani), kauli za mawaziri wa CCM na viongozi wote kwenye serikali (pasipo mzee wa Sumu aka Mwakyembe), zote ni kauli za haiwezekani/ wanawadanganya ni ngumu mmno, itawezekanaje, tunakusanya kiasi kidogo ni ngumu mmno. Mbaya zaidi wanapoona wenzao wanaweza kufanya kama ishu ya M4C wanaanza kuleta propaganda kuwadanganya wananchi ni vigumu mmno/ haiwezekani. Wanaweka nchi rehani.

  Kinacho imaliza tanzania ni rushwa, migomo yote inatokea kwa sababu ya Rushwa, jiulize mbona Nyerere aliwaambia watu wafunge mikanda baada ya vita vya Uganda wakakubali?? Leo hii jaribu kuwaambia watu wafunge mikanda uone, kama hawajakupika mawe. Watu wanaona jinsi fedha zilivyo/zinavyo kwapuliwa kibinafsi. Tumesikiwa akaunti za Uswis, Mnadhimu wa Jeshi (Shimbo) anamiliki trilioni 3 huko South Africa, EPA, Richmond, Kiwira na mengine mengi. Hivi ndio sababu kuu za migomo na wala sio kingine.

  Nape, fedha zikitumiwa ipasavyo zinaweza kufanya kazi kubwa sana. Kwanza zinabaraka ya Mungu, usishangae M4C ikifanya mambo makubwa, ni kwasababu wanapambana na Rushwa na Mungu anaweka mkono wake.

  Acha kusema itawezekanaje, sema itashindikanaje??? Wenzetu wanampango wa kuama sayari sisi tunaangaika kununua madawati.
   
 19. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #19
  Aug 15, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni CCM kupigana vita mpya kwa mbinu za kizamani, mwambieni Nape passed are times for propaganda. Watu wenye akili wanawadharau. Nape ni mtu mkubwa sana kwenye chama anaponyanyuka na kusema CHADEMA wanapokea hela kutoka nje ya nchi ili kuvuruga nchi, swali ni je, hakuna sheria zinazotoa miongozo juu ya ufadhiri wa vyama, na kama zipo ni serikali ya chama gani iliyoshindwa kusimamia?

  Upinzani wa sasa hivi sio kama wa miaka ya 95 uliokuwa unaongozwa na vyama vya siasa, huu wa sasa hivi ni wa wananchi wenyewe. Na hapa ndio wanaposhindwa kuelewa kina Nape, it's not about the party, it's about the people who are tired of the life under their rule. Upinzani hautakufa Tanzania kwa kuiua CDM au kuwanunua viongozi wake. It is the people who are the opposition right now. Ndio maana ukiongea jambo baya kuhusu CDM hasa hasa bila ushahidi watu wanacheka.
   
 20. Escobar

  Escobar JF-Expert Member

  #20
  Aug 15, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 576
  Likes Received: 217
  Trophy Points: 60
  What i know ni kwamba a smart insitution or organization itaweka vitengo au idara kwa mujibu wa mahitaji ya kiutendaji na watawekwa watu wenye ujuzi husika kwenye nafasi hizo ili kurahisisha ufanyaji kazi na kuleta tija iliyokusudiwa i mean to achieve the intended goal. Kwa mfano mhasibu atapewa idara ya fedha, mhandisi asimamie majengo na ujenzi n.k. Wkati Nape anateuliwa nilidhani kuwa uteuzi wake umezingatia kuwa yeye ni msomi wa wa taaluma ya siasa hivyo angeweza kufikia malengo ya chama kwa ufanisi zaidi lakini sasa kinyume chake ndio imekuwa! Yeye anadhani au sijui ameelekezwa hivyo kuwa wabaya wao ni CHADEMA kumbe hata siyo hivyo bali ni mfumo wa kulindana na kuendeleza maovu yale yale huku mazuri kiduchu sana wakiliazimisha kuyapa coverage kubwa, watu wameshaamka!
   
Loading...