CHADEMA yamkaba koo Nape. Amwangukia Kinana kumwokoa

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Hali ya Mbunge wa Mtama Nape Nnauye kisiasa Jimboni Mtama imezidi kuwa mbaya baada ya Chadema kupitia kwa kijana msomi Stephen Kamillius Membe kufanya operesheni kila Kijiji na Sasa kila nyumba kutaka wananchi wamkatae Nape na CCM yake.

Operesheni hiyo imefanyika kwa miezi miwili Sasa na kubadili upepo ambapo siku ya jaza Nape alifika Mtama akitaka kukutana na kina mama na wazee lakini akiambulia patupu baada ya kuambiwa atoe hela ya kukutana nao. Wachache walioenda Kijiji Cha Rondo waliambulia 20,000 kila mmoja wakiambiwa ni ya sikuu.

Pale pale Nape akaanzisha shindano la mchezo wa bao Ili kuwanasa wazee ambapo ameahidi kutoa 500,000/= Kwa mshindi na 30,000/= kwa kila atakayeshiriki tarehe mosi ya mwaka Mpya.

Hata hivyo taarifa zilizopo ni kwamba mwanasiasa huyo mwenye majivuno amemuomba Kinana kufika Mtama kushawishi wana CCM wanaotimkia Chadema na kumwambia hadharani, "hatukujui, tulikupigia kura Kwa heshima ya Membe Sasa hayupo". Rudi kwenu.

Wakati Kinana atakapounguruma siku hiyo tarehe 7/1/2024 Mbowe naye atatua Rondo Chiponda kuhani kaburi la Membe kabla ya kufanya mkutano mkubwa wa hadhara.

My take: Nape usipoteze fedha zako Mtama imeitika Kwa Membe. Tafuta Jimbo ugombee using'ang'anie Mtama. Godfather wako hayupo tena.
 
Mtama waache Ujinga, Sugu Mbeya siyo kwao lakini wanampenda kupindukia

Mchungaji Msigwa Iringa siyo kwao lakini kura zetu anazo

Lema Arusha siyo kwao

Devotha Minja Morogoro siyo kwao nk...nk
 
Nipo masasi naenda zangu newala,nikataka kujua kuhusu ccm masasi inakubarikaje?aiseeh Yule dada hakunihudumia Tena eti kwanini naongelea ccm.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom