Nape Hatendewi Haki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape Hatendewi Haki

Discussion in 'Great Thinkers' started by Mchambuzi, Feb 4, 2012.

 1. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #1
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Wadau,

  Imekuwa jadi kubwa humu na kwenye mitandao mingine ya kijamii (haswa facebook) kwa watu kumkatisha tamaa sana NAPE na juhudi zake za kukisafisha chama. Kazi hii ni ngumu na mnaelewa fika kwanini.

  Binafsi ninachopingana na Nape kimsingi ni kitendo chake cha kuendesha 'Siasa za midako' badala ya siasa za uenezi unaokuwa informed na itikadi sahihi ya Chama. Lakini ukweli pia ni kwamba, Siasa hizi za 'mdako' Nape amezikuta, kwani zipo tangia Mwaka 1992 pale Azimio La Arusha lilipokufa, kulipisha azimio la Zanzibar. Tatizo langu kubwa na Nape ni hilo tu – kwamba hataki kukubali kwamba CCM haina tena DIRA. Nje ya hapo, Kijana huyu anajitahidi sana, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni.

  Hakuna kiongozi mwingine ndani ya Chama mwenye uthubutu wa kufanya anayofanya Nape, na haya hakuyaanza alipoteuliwa kuingia Kamati Kuu na kisha Ukatibu Uenezi, Siasa na Itikadi. Nape amekuwa ni kijana mwenye kiu ya mabadiliko tangia akiwa umoja wa vijana, jambo ambalo lilimjengea maadui wengi na wa kudumu. Vijana wengi bado wana imani na CCM kwa sababu ya uwepo wa watu kama Nape kwamba - ‘kumbe wapo viongozi wenye ujasiri wa kukemea chama kinapokosea au kulega lega'.

  Vinginevyo nina uhakika kwamba, anachokifanya Nape leo hii ndani ya CCM, ni vijana wachache sana humu Jamii Forums wangekuwa na uthubutu huo, kwani hata katika mijadala humu, wengi hawaweki hata majina yao wala sura zao za kweli. Huku ni kukosa ujasiri kwa kile unachokiamini.

  Nape ana mapungufu yake, na kwa upande wangu ni hayo niliyoyataja kwa mfano kuzunguka nchi nzima na kupokewa na vijana wa CCM wakitimua vumbi kwa shangwe wakiimba "Kauli Yetu ni Kulinda Ujamaa na Kujitegemea", na yeye akitabsamu huku akijua fika kwamba vijana wale wamepotoka. Hili ni ‘timing bomb' kwa CCM, kwani vijana hawa, pamoja na wazee na kina mama wengi kwenye uongozi huko kwenye matawi ya Chama wanaotembea na Azimio La Arusha Kama MSaafu au Biblia, wakija kubaini kwamba kwa miaka ishirini walikuwa wanadhania Wanachokiona ni Mwezi, Kumbe ni Nyota, huo ndio utakuwa mwisho wa CCM huko kwenye matawi, kwani nguvu ya chama ni matawi na mashina. Ni huko matawini ndiko kwenye wanachama, na ni huko ndiko vijana, wazee na kina mama kwa miama 20, wanadhania wanaona mwezi kumbe ni nyota. Ni muhimu katika mabadiliko ya katiba kwa CCM kuliangalia suala hili. CCM ilikuwa na nafasi nzuri ya kuweka mambo sawa kwa kufanya mabadiliko kidogo tu juu itikadi yake ili iachane na Ujamaa wa Marx-Lenin, na badala yake kuegemea kwenye Ujamaa wa Kidemokrasia (Social Democracy), bila ya kuleta athari zozote na maneno yoyote kisiasa, huku chama kikiendeleza mengi yake ya sasa kiuchumi, kijamii na kisiasa, bila bugudha. Lakini kwa bahati mbaya, CCK wameshaidaka itikadi hiyo kutokana na maelezo ambayo tumeyaona katika katiba yao ya mpito humu Jamii Forums.

  Kwa wale ambao bado wana mapenzi na CCM (kwani imani inaweza kuwa imeisha), nadhani ni muhimu tukamweleza Nape mapungufu yake ni yepi, na changamoto zake ni zipi, huku tukitambua kwamba kibarua chake, na uthubutu wake wa sasa, wengi humu hatuwezi hata kujaribu. Nape alifikia hatua ya kutaka kuvuliwa uanachama wa UVCC, na uanachama wa CCM. Hatua zilishafikia mwisho kabisa. Sasa hata kama ni kweli alitaka kujiunga kwingine, why not iwapo maamuzi ya kukutimua yamekamilika lakini wewe bado unataka kuendelea kutetea maslahi ya taifa lako? Mwenzangu ungefanya nini?

  Kibarua chake cha sasa ni cha kubadilisha Chama, na hii ni kazi nzito sana kwani katika organization yoyote, change ni kitu kigumu sana, hata iwe StarBucks, Apple, Microsost, au IBM. Hii ni kwa sababu mabadiliko ndani ya organization yoyote (CCM included), maana yake ni kubadilisha watu – kimtazamo, culture, attitudes, behavior, practice, norms, mambo ambayo yamejengeka ndani ya CCM kwa miaka zaidi ya 35 sasa, pengine hata Nape alikuwa hajazaliwa. Hata kwenye makampuni makubwa duniani, kila wanapohitaji kuleta change, huwa wanapata wakati mgumu sana, na suala hilo huwa linahitaji experts wanaolipwa fedha nyingi sana kusaidia mchakato huo, ambao mafanikio yake mara nyingi huwa ni ya kiwango kisichozidi 70%.

  Mwisho, nia yangu hapa sio kusema CCM Saaaaafiiii, hapana, CCM ya sasa ni Chafu, inanuka. Lakini ni viongozi kama Nape ambao angalau wanatoa matumaini (hata kama ni hafifu) kwa vijana ambao bado wana mapenzi na CCM (sio lazima iwe imani), kwamba kumbe wapo wachache ndani ya CCM wenye mawazo tofauti. Nawaomba sana ndugu zangu, kama hamkubaliani na Nape, basi mfanye hivyo kwa hoja, sio matusi na kejeli kwa mtu ambae ni dhahiri anajitolea sana kujaribu kuleta mabadiliko ndani ya CCM. Vinginevyo hata umweke nani katika nafasi ya Nape, ataonekana ni kilaza tu! Lakini kilicho muhimu zaidi ni lengo la mhusika katika kufanikisha anayo yaamini, ambayo ni kwa maslahi ya CCM in the long run, regardless of the hurdles encountered now. Hata yeye akishindwa na kuondoka, wapo watakaoanzia pale alipoachia.

  Wapo wengi wasiokubaliana na Mnyika, Mtatiro, n.k, lakini wanafanya hivyo kwa hoja, sio matusi na kejeli. Binafsi, ingawa kwangu mimi Mnyika stands to be one of the best leaders in our generation, bado ana mapungufu mengi tu ambayo from time huwa watu wanayaelezea kwa hoja, sio matusi na kejeli. Whether ni mapungufu ya Chadema, CCK, CUF, NCCR, CCM, kuyajadili kwa hoja itatujenga na kutufunza mengi sana, huku tukibakia na uanachama wetu wa vyama mbalimbali.

  Vyama vya upinzani bado ni vichanga, havijafikia hatua ya kuhitaji kubadilika, lakini vitafikia huko kwani the only thing that is constant in an organization is 'change'. Tusubiri kuona mchakato huo kwenye vyama vya upinzani utapitia misuko suko gani. Vinginevyo ni dhahiri kwamba sakata la kina Hamad, Kafulila, Zitto, ni dalili za mwanzo za wimbi hilo katika vyama husika.

  Otherwise, Do Not Speak Unless You Can Improve the Silence.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,611
  Likes Received: 3,913
  Trophy Points: 280
  Sio hivyo tu, Nape alivyoingia kwenye game, at least tukaanza kuona kumbe CCM bado wapo

  Ameleta siasa za ushindani, ametetea mpaka wapinzani na amekuwa muumini wa siasa za vijana

  The guy is real smart, ana respond haraka kwenye issues za kitaifa na kusema maoni yake waziwazi

  Niliwahi kusema huko nyuma upinzani wawe waangalifu kwani CCM wakipata akina Nape wengine watatu, upinzani chali

  kuchukiwa na kutukanwa na kukebehiwa ni kutokana na ufahamu mdogo wa wanachama wa vyama vya upinzani wakidhani ni zamu ya chama fulani kushika nchi

  Chuki za watu kwa Nape na CCM yeyote ile ni vile vidonda ambavyo havijatibiwa bado, vidonda vya ufisadi, CCM as to do something with, swala la kuvua gamba...limekaa kichama zaidi, kitaifa halina maslahi kwani we need those guys in court!
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Feb 4, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  let Credit be given when it is due............Hongera Nape , simamia dhamira yako na mapenzi mema kwa nchi yetu!
   
 4. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #4
  Feb 4, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  He is just being used by mkweree to fullfil his political agenda and then he will flush him down the toilet like a used condom!! Mnakumbuka jinsi alivyoshuhulikia issue yake kule umoja wa vijana wakati ule wa bif ya Nape na Nchimbi??
   
 5. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #5
  Feb 4, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  As you know, flushing a condom down the toilet isn't as easy as you may think, haiendi kwenye sewage kirahisi hivyo.
   
 6. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #6
  Feb 5, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ni Kweli ......
  Na aliyezuia kutumuliwa kwa Nape naye ana busara sana(Ki -CCM) maana kama kitendo hicho kingetokea CCM ingekuwa na hali mbalya zaidi kuliko sasa. Machoni pa jamii CCM ingekuwa na sura ya "wazee", isoykuwa na jipya na matumaini yeyote. Kama ulivysema figue kama za ina nape japo kidogo zinasaidia.....

  Lakini yanayotokea CCM yanaweza kutokea hata CDM, CUF na NCCR . kile kile kinachoweza kuitikisa CCM ndio kinachweza kuibomoa CDM, CUF na NCCR..............
   
 7. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #7
  Feb 7, 2012
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mchambuzi,

  Sidhani kama watu ndio wanamkatisha tamaa. Nape mwenyewe ndiye anayekatisha watu tamaa. Kama Nape anataka atendewe haki, basi na yeye atende haki. Nilishawahi ku-quote baadhi ya posts zake humu humu JF na kuziweka kwenye thread nyingine. Labda niziweke hapa, halafu utuambie tumtendee haki gani Nape.

  Zamani kabla ya kupata cheo alichonacho sasa Nape alikuwa anaita WanaJF wakubwa. Pia alikuwa ni mtu wa kushukurusa kwa maoni aliyokuwa anayapata hapa JF.

  Zaidi Nape alikuwa hupendezwi na wakubwa fulani:

  Katika posts zake alikuwa anatanguliza shukrani kwanza na kueleza misimano yako dhabiti tena with reference:

  Alikuwa naita watu ndugu:

  Alikuwa unaiheshimu hii JF:

  Lakini tokea apate hiki cheo posts zake sijui kama zinajenga au kuiharibu JF. Kwa mfano:

  Tofauti na zamani wakati mwingine sasa Nape anaona baadhi ya watu kama wanafiki. Mfano:

  Japokuwa kuna wakati huwa anaamkia mguu wa kulia:

  Japokuwa wakati mwingine huwa anaamkia mguu wa kushoto kiasia kwamba tofauti na zamani hataki ushauri:

  Lakini Nape mwanasiasa kijana unayemsema ni yupi hasa? Je ni huyu?

  Au ni huyu?

  Hapo Nape anakupa matumaini yapi mpaka kufikia extent ya kusema kuwa anaishi nchi tofauti na tunayoishi sisi? Au keshabadilika?
   
 8. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Mkuu EMT,

  Nashukuru kwa compilation yako ambayo nadhani hata kwa Nape itakuwa na manufaa pia. Nadhani ni muhimu sana kwa Nape na viongozi wengine kutoka vyama vyote vya siasa, wakaanza kuwa makini sana na kauli zao kwani zitakuja kuwahukumu baadae kisiasa. Katika demokrasia zilizokomaa, 'flip flopping' ya wanasiasa huwa inawagharimu sana career wise, na mara nyingi huwa ni technical knock-out tosha kwenye ulingo wa siasa.

  Media industry yetu inazidi kuwa modernized, inapanuka, ina converge katika different technologies, ambapo sasa imekuwa rahisi sana kufanya archiving ya content, na vile vile suala la retrieving such content limekuwa rahisi sana. Evidence ni jinsi EMT ulivyoweza kufanya ulilofanya. Ni matumaini yangu kwamba wanasiasa, hasa vijana ambao wame embrace technology kufanikisha shughuli zao, watalichukulia suala hili seriously.
   
 9. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Majibu yako kuhusu post ya EMT nadhani umejifunza zaidi kuhusu "haki" na namna ya wanasiasa wetu (vijana kwa wazee) wasivyotabirika!

  Mkuu Mchambuzi, pole sana naona Nape kakuvua nguo hapa jamvini, nina imani moja tu kuwa wakati unajenga hoja za "haki juu ya Nape" hukutegemea kama angekuja mtu kama EMT na kukuwekea kile ambacho mara kadhaa kina mulika katika nyota ya mwanasiasa huyu ambacho ni zaidi ya nuru ya kawaida ndio maana wengi hawakubaliani naye katika uwasilishaji wake na namna anavyojipambanua.

  Kuna kitu umeamua kukifanya kidogo kwenye thread yako kwa post # 1, hebu nieleweshe ni namna gani mtu ambaye anasimama pembeni akishuhudia chombo kikipoteza dira na yeye akiendelea kusifu kwa mapambio?

  Hapo nisaidie unalenga kujenga hoja gani juu ya mtu huyu?

  Binafsi nljitoaga kujadili kitu chochote kinachohusu wakina Nape na kundi la wazee wake, ila leo kwa namna ya pekee nimevutiwa ulivyoiweka hili bandiko lako, ila kilichonivuta zaidi na kunifurahisha ni kwamba katika bango zima ulisahau upande wa pili wa mambo kwamba "kwanini hasa mambo yapo hivyo kama yalivyo linapokuja suala la Nape na anavyojipambanua"

  Ila namshukuru EMT amekukumbusha, pia nimefurahi umekumbuka.

  NB; Liangalie tena hilo suala la Dira ya Taifa (sio ya chama tena) na nafasi ya huyo mtu.
   
 10. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Mkuu JouneGwalu,

  Ni wapi Nape amenivua nguo humu jamvini? Kuna sehemu amejibu hoja yangu yoyote? Pengine nimepitiwa kidogo lakini sijaona hilo. Vinginevyo hoja yako kuhusu Nape kuwa kiongozi wa chombo kisichokuwa na dira, hata mimi nimekuwa nalieleza hilo kwa muda kwamba hili ni moja ya mapungufu yake, hasa pale anapotetea kwamba CCM ina dira na ina itikadi sahihi yani ya Ujamaa wa Marx-Lenin.

  Kuhusu EMT kutuletea content inayo onyesha 'dual personality' ya Nape, hili ni jambo zuri kwani Nape atajifunza kwambe pengine hilo nalo ni pungufu lake lingine. Na kwa kweli katika hilo, linaweza kumgharimu kisiasa huko mbeleni. Vinginevyo matukio yote haya hayabadilisha hoja yangu ya msingi kwamba Nape hatendewi haki, kwani katika hoja yangu ya msingi, nilihimiza umuhimu kwa wale wote ambao bado wana mapenzi na CCM (siyo lazima iwe imani), basi wamsaidie Nape kwa hoja, na sio matusi, kama vile tunavyofanya kwa Vijana wengine kutoka vyama vya upinzani, ambapo huwa mapungufu yao yanajitokeza, lakini wana jamvi humu hutoa mawazo na ushauri wao kwa hoja zisizo na matusi wala kashfa. Lakini muhimu zaidi nikahoji kwamba, je kuna kijana au mtu yoyote humu ambae angefanya anayofanya Nape kama angekuwa katika nafasi yake? hakuna aliyejibu hilo. Ni dhahiri kama watu hao wapo, basi ni wachache sana, kwani hata katika kujenga hoja zao ambazo ni radical, wengi humu hawatumii majina yao (au hata picha), na wengine wanaenda mbali zaidi na kusema wanaogopa kupoteza kazi zao. Mapinduzi ya kweli hayawezi kufanikiwa kwa njia hii, sana sana kitakuwa ni kijiwe cha soga kuhusu matukio ya siasa na harakati.

  Pia nikasema kwamba watu kama Nape, hata kama hawatafanikiwa na harakati zao za kubadilisha Chama, wakiondoka, watakuwa wameacha msingi mzuri ambao wapo wengi watakaoanzia pale alipoishia kwani pamoja na ugumu wa shughuli yake hiyo, bado hiyo ndio njia pekee ya kurudisha imani ya CCM kwa watanzania wengi waliopoteza matumaini.

  Sijakuelewa kuhusu dira ya taifa vis-a-vis ya chama. Kwani wengine nje ya CCM dira yao (zao) za taifa ni ipi(zipi)?
   
 11. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2012
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mchambuzi,

  Bila shaka kama Nape asingesimama na kuongea anayoongea, CCM sasa isingekuwa katika hali iliyonayo. CCM ina hope, au watu wana hope ya CCM kuwa CCM ile ya zamani kutokana na watu kama kina Nape wanaojaribu kupinga ufusadi waziwazi. Mimi naweza kumtetea Nape kwa kuwa double faced, kama kweli yeye ni double faced.

  Ukiangalia watu waliopo CCM wengi ni kutokana na kutaka kuweka mkate mezani. Na sio kuwa wanakubaliana na wanayofanya CCM. Ni lazima uonekane unakubaliana nayo ili usijeshindwa kuweka mkate mezani na ili usije-jeopardize political future yako. Ukiangalia itikadi ya ujamaa na kujitegemea wanayoitaja viongozi wetu, unaweza kusema labda ni chizi anaongea. Wapi kuna ujamaa Tanzania, nani CCM anafuata au kiutekeleza sera ya ujamaa, angalia Kingunge aliyekuwa last bastion of Ujamaa na kujitegemea alivyotupiga madole. Kama yeye mwenyewe ameacha sera na itikadi hiyo na kuwa capitalist nani atakayeifuata, Nape?

  Kwa hiyo ni haki kwa Nape kusema kimoja na kufanya kingine, he is more realistic. Anajua what is going on, what is right and what is wrong, lakini anafanya political mathematics za kumfanya aendelee kuelea asizame. Anaweza kuwa na mawazo mengine sahihi kuhusu namna ya kuendesha chama na nchi, lakini bado yeye si decision maker, so he has to be within and fight from within.

  Si kweli kuwa CCM yote imeoza, kuna watu ndani ya CCM bado wanafaa sana. Kama uwanja ukiwa mzuri wanaweza kutoa maoni yao wazi. Si kila mwanaCCM anaweza kuwa wazi kama mchambuzi, Mchambuzi na wewe ukivaa nafasi moja ya chama bila shaka utalazimika kuwa kimya, au kuwa "double faced" kama walivyo wengine.
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Mchambuzi, Nape kachimba kaburi lake mwenyewe kwa kauliz zake zisizoangalia kesho.... ana nia njema sawa, lakini kauli zake hazina filter

  Ni sawa na mimi eti kesho niseme nasimamia chama chochote, kutokana na kauli zangu mwenyewe ntakuwa nimejimaliza kabla sijaanza

  He needs to change and understand kwamba theories anazotumia zinatakiwa kuwa acclimatize to Tanzania context, otherwise atahangaika na hatapata plain level field
   
 13. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #13
  Feb 20, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu!

  Heshima mbele, kwanza kabisa napenda kumpa heko EMT kwa kutoa reference nzuri kuhusu huyu kijana wetu NAPE tumeona na tumeshuhudia jinsi kijana alivyokua muungwana kipindi anatoka masomoni mpaka alipotangaza nia yake ya kugombea uenyekiti UVCCM mpaka alipokuja kua Katibu wa itikadi na uenezi, tumeona mabadiliko ya kauli zake na hii imeonyesha jinsi gani mtu akipata nafasi anavyoweza kubadilika na kua na kiburi, hapo hapo anasahau kua bila mawazo ya watu ambao anawajibu kejeli na maneno ya ki mipasho asingekua hapo alipo....

  na hapo kwenye Blue hebu nitajie viongozi angalau kumi tu ambao ndani ya CCM wanafaa na wanaweza kuleta mabadiliko endapo watapewa nafasi....
   
 14. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Mchambuzi!

  Pole sana kama majibu yangu yamekutatiza, niliposema Nape amekuvua nguo nililenga katika tamathari ya lugha tu kuwa ulitumia juhudi kubwa kwenye kujenga hoja za Nape kutendewa haki huku ukilenga "mapungufu yake madogomadogo" kwamba unayaelewa na yanasameheka, ila upande wa pili ni wazi hukutarajia demonstration ya EMT kuhusu ni mlango gani Nape kauacha wazi ambapo kupitia hapo ndi haki aliyostahili kupewa inavujia!

  Hiyo tofauti kati ya ulichokieleza juu yake na record zake mwenyewe anavyojichora kwenye majukwaa haya ndio nkakiita "umevuliwa nguo".
  Ila uniwie radhi kama nmetumia lugha ya kukera.

  Pili mkuu, pamoja na kuendelea kwako kusisitiza ubora wa Nape ambacho sina tatizo nako ila bado hujanielewesha ni namna gani yeye ni bora kama bado anasimama katika chombo ambacho hakina dira na bado anapigia debe watu wapande chombo hicho hicho??
  Hapo ndio sikuelewi kabisa, naomba unieleweshe zaidi sababu kiukweli wewe umekuwa ni miongoni mwa walimu wangu hapa jamvini, ila hili haliingii kichwani kabisa. Umeeleza mambo mengi ila mi kichwa changu kimejikita hapo kwenye suala la dira, ni vipi unaweka suala la dira ya chama chake kama ni upungufu mdogo??
  Kwamba kwako mtu anayeshabikia kitu kisicho na dira bado unamuweka kwenye kundi la kuvishwa taji??

  Tumekuwa na tatizo kwenye mijadala yetu saa zingine, tunalazimisha kuwa na washindi katika hoja zetu ilimradi tu utosheleze hoja zako, kukosekana kwa wanasiasa madhubuti katika mda husika hulazimisha hata wabovu kuonekana wanafaa mfano utendaji wa JK ambavyo upo kwenye kilele cha kuvurunda umelazimisha Mkapa aonekane jembe hata makosa yake ya kusahau "uti wa mgongo wa Taifa" yakahalalishwa na kufanywa "madogo"....
  Nadhani na wewe umetumia kanuni hyo hapa kwamba kwasababu "hamna" kijana mwenye uthubutu kama wa Nape katika masuala hayo uliyoyataja basi imekuhalalishia kuona kuwa "kutokuwa na dira" ni upungufu mdogo!

  Marazote nitaendelea kusema kuwa ni bora tusiwe na shujaa yeyote yule kuliko kuchagua shujaa kwa shinikizo la kukosekana mbadala wake.

  Nape ni kijana wa kawaida sana ambaye kwa nafasi ya aina za siasa anazocheza kijana yeyote kwenye nafasi yake atafanya hayo aliyoyafanya.

  Mwisho hata kama hamna hao vijana walioonyesha kusimamia dira ya nchi (kwa maana ya kwamba siwezi kutaja jina) hyo haimaanishi kuwa taji ntamvalisha mbwa mwitu aliyevaa vazi la kondoo, ni bora taji hlo nlichome moto na niingie gharama za kutengeneza jingine wakati namsubiri shujaa wa kweli na halisi.
  Hlo la ID na Images tunazotumia hapa hebu tuliache tu, yah inawezekana labda JF ni kijiwe cha kupigia zogo tu.
   
 15. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2012
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo neno ....... Sasa ili baadae na JK aje kuonekana ni jembe itabidi atayemfuata awe.............
   
 16. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #16
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Kuhusu Kingunge, well said. Yule ndio 'ideologue' wa chama, hivyo matendo yake ndio itikadi sahihi ya chama.

  Kuhusu mimi kubadilika iwapo nitapewa nafasi ya uongozi katika Chama, upo sahihi kwani 'power corrupts', especially ukizingatia kwamba unaweza kujikuta upo na wenzako ambao agenda zao ni tofauti kabisa, na zisizokuwa na maslahi kwa chama wala taifa. Ni ngumu sana kufanya kazi katika mazingira kama hayo, hasa ukiwa ni mtu mwenye msimamo. Mbali na hayo, pia ukweli uliowazi pia ni kwamba sina uwezo wala uzoefu wa kuniwezesha kufanikiwa katika nafasi kubwa kama walizonazo kina Nape. Kutokana na kutokuwa na uzoefu, nitakataa cheo chochote kikubwa kinachohusiana na mimi kuwa na ofisi yangu pale CCM Lumumba, iwapo itatokea nikateuliwa. EMT, naomba msimamo wangu huu uuweke kwenye records. Sitakuja ku 'flip flop' katika hili.
   
 17. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe, ni matumaini yangu watu walio karibu naye wanamshauri haya.
   
 18. Mchambuzi

  Mchambuzi JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2012
  Joined: Aug 24, 2007
  Messages: 4,819
  Likes Received: 1,140
  Trophy Points: 280
  Bila samahani Mkuu, kwani hoja yako ipo sahihi, nimekuelewa sasa.

  Hakuna sehemu ambayo nimesema kwamba Nape ni kiongozi Bora. Sina vigezo vyovyote bado vya kuhitimisha hivyo juu ya Nape. Nilichosema ni kwamba ana uthubutu ambao wengi hawana, na anasimamia kitu anachokiamini. Na nikasema pia kwamba hata kama hatafanikiwa na kuondoka katika nafasi yake, msingi huu aliouweka ni moja ya njia kuu za kukiokoa chama, na wengine watafuata mle mle. Vinginevyo sioni ubora wa Nape, na kinachochangia hilo ni suala la kuhubiri itikadi ambayo haipo. Nilishalielezea hili sana kama moja ya mapungufu ya Nape lakini ya CCM pia kwa ujumla. Hivyo, upungufu huu unaondoa neno 'bora' kwa Nape kama kiongozi, na 'bora', kwa CCM, kama Chama.

  Sijamvisha Nape taji, nimesema tu kwamba hatendewi haki na kutoa sababu zake. Lakini katika hoja yangu ya msingi, nimeelezea mapungufu yake kwa ufasaha.

  Upo sahihi iwapo hoja yako itasomeka kwamba .."akitokea kijana yoyote mwenye uthubutu kama wa Nape..." Vinginevyo sio kweli kwamba kijana yoyote angekuwa katika nafasi ya Nape basi na yeye automatically angewashambulia watuhumiwa wa ufisadi namna hii, na kuhimiza waondoke katika chama. Kwahili naomba tukubaliane.

  Mwisho ni msisitizo wangu tu kwamba pamoja na mapungufu yake, tumpe credit kwa uthubutu, na kama tuna nia nzuri ya kumsaidia, iwe kwa hoja na sio kebehi, matusi na kashfa. Lakini nimegundua baada ya demonstration ya EMT, Nape pia huwa anatoa matamshi ya kuchochea chuki dhidi yake. Hili ni tatizo.
   
 19. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Ok Brother Mchambuzi, nmekubaliana na wewe katika hayo maeneo uliyotaka tukubaliane.!
   
Loading...