Kwa yaliyomkuta Nape Nnauye na Mwita Waitara, je nini nafasi ya vijana ndani ya CCM? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kwa yaliyomkuta Nape Nnauye na Mwita Waitara, je nini nafasi ya vijana ndani ya CCM?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Magabe Kibiti, Oct 14, 2008.

 1. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #1
  Oct 14, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alhamisi moja ya september 2006, nilihudhuria sherehe ya kumtunuku Raisi JK Kikwete shahada ya heshima ya udakitari wa sheria kwa utumishi bora toka kwa chuo cha St Thomas - MN Marekani. Tukio zima, hotuba ya Kikwete, na hotuba ya kituo cha uwekezaji kwa wafanyabiashara na wakaazi wa MN villinipa moyo sana kuwa hatimaye nchi yetu ilikuwa inaelekea kwenye ujenzi wa misingi bora kwa ajili ya maendeleo ya Taifa.

  Baadhi ya wazee niliokutana nao kwenye hafla na mikutano hiyo walisisitiza sana muelekeo mpya wa nchi na suala la vijana na watanzania waishio nje ya nchi kuwekeza au kurudi nyumbani ili kushiriki katika ujenzi wa nchi. Mzee mmoja ambaye ni kiongozi mzito serikalini alinihakikishia kuwa vijana watakuwa na nafasi kubwa sana ya kushiriki kwenye uongozi na utendaji kazi wa serikali ya JK Kikwete.

  Miezi michache baadaye, nilifanya kitu ambacho nilikuwa nimejizuia kukifanya kwa maisha yangu yote mpaka wakati huo - nilituma maombi ya uanachama wa CCM. Bila kuchelewa, nilingia kwenye mtandao wa CCM na nikajaza fomu ya kuomba uanachama. Nilikuwa nimeshawishika kuwa mazingira ya Kikwete kwenye uongozi yangekuwa mazuri kwa kijana kama mimi ambaye jina langu la ukoo halikujulikana kokote kwenye daftari la wanasiasa na wafanyakazi wa taifa na chama cha mapinduzi.

  Kwa vile hakuna yoyote yule ndani ya ccm aliyewahi kunitumia email au jumbe yoyote ile kusema kama nimekubaliwa maombi yangu au la, niliendelea kusubiri huku pia nikiamini kuwa maombi yangu yamekataliwa. Kipindi hicho hicho, kijana na mpiganaji mwenzangu niliyepitia pamoja naye kwenye misukosuko ya uongozi na migomo ya vyuo vikuu Tanzania - Zitto Kabwe, nyota yake kisiasa ilikuwa ikiendelea kung'ara kwenye chama chake cha CHADEMA. Hii ilinipatia moyo kuwa movement yetu ya mabadiliko tuliyoianza mlimani ilikuwa bado inawakilishwa vizuri sana na sikuwa na sababu yoyote ya kuhuzunika.

  Mwaka 2007, ulianza kufunua zaidi mwelekeo wa serikali ya Kikwete. Wazee hawakuonekana kama walikuwa tayari kuingiza vipaji vipya au kukubali sera na mitizamo mipya toka kwa vijana. Baadhi ya vijana wenzangu niliokuwa nao Mlimani na ambao pia walikuwa wamefanikiwa kuingia CCM, walikuwa wakiniandikia kila mara kuwa hawapewi nafasi kabisa kwenye sera au mwelekeo wa chama na serikali yao. Muda si mrefu serikali ya Kikwete ilianza kukumbwa na kashifa moja baada ya nyingine na huku wazee ambao wamekuwa wanaendesha siasa na sera za chama wakajikuta wakirudi kwenye mchezo waliouzoa kwa miaka yote hii - kuwa wakali na wakatili kwa wapinzani wao - kama vile kumtimua Zitto bungeni.

  Kwa muda sasa (kuanzia miaka yangu Mlimani 98-01), vijana wengi wanaomaliza Mlimani na vyuo vingine, kwa njia moja au nyingine, wamekuwa wanajaribu kutafuta nafasi yao ndani ya chama tawala Tanzania - CCM. Wapo wengi waliofanikiwa kutokana na nafasi zao au za wazazi wao, wapo waliofanikiwa kutokana na kujua namna ya kupanga na kucheza karata zao vizuri, wapo wengine ambao ("tumekosa hata nafasi ya kukubaliwa kuwa wanachama") nafasi zetu kwenye chama hiki kikubwa sana Tanzania ziligonga mwamba.

  Nimekuwa najaribu sana kusoma sera na utendaji wa vyama kabla sijafanya tena uamuzi (maana najutia uamuzi wa pupa nilioufanya mwaka 2006) wa kuomba uanachama wa chama cha siasa. Ninavutiwa sana na nafasi ya rafiki yangu Zitto sasa hivi kwenye siasa za chama chake na nchi yetu. Nafurahi sana kuona kuwa yeye anaendeleza mapambano na ujenzi wa nchi yetu. Natambua hata hivyo kuwa siasa ni mchezo mchafu sana (hasa baada ya yaliyotokea kwa rafiki na mbunge wangu wa Tarime - Wangwe). Nafurahia pia mafanikio ya rafiki yangu mwingine ambaye amefanikiwa ndani ya CCM - Maina Owino wa CCM - London

  Miezi michache iliyopita, shemeji yangu (ambaye ni kiongozi wa CCM Tarime) aliniuliza maoni yangu kuhusu uanzishaji wa matawi ya ccm ughaibuni na kama bado nina mapenzi na ccm kiasi cha kufikiria kuanzisha tawi la ccm marekani. Sidhani kama ingenichukua muda mrefu kumpa jibu la swali lake. Watanzania wengi ninaowajua USA wanasita sana kujiunga na CCM kwa vile hawaoni kama wana nafasi sawa na matajiri wazee walioko ndani ya ccm sasa hivi.

  Wakati nikifikiria cha kusema, stori ya vijana Nape Nnauye na Mwita Mwikwabe zikatambaa kwa kasi kwenye vyombo vya habari kabla ya wazee ndani ya chama hawajarudi kucheza mchezo wao waliouzoea wa kuwaandama hawa vijana (Mwikwabe anatuhumiwa kwa kesi ya wizi wa mamilioni huku Nnauye akitafutiwa sababu ya kufukuzwa UVCCM).

  Swali ninalowasilisha hapa kwako msomaji na mchangiaji wa Jamiiforums, je ni nini unafikiri kuwa ni nafasi ya vijana ndani ya CCM?
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Oct 14, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,205
  Trophy Points: 280
  Vijana ambao ni wanafiki ambao pia wanafikra za kifisadi na hawako tayari kuweka maslahi ya Tanzania na Watanzania mbele wana nafasi nzuri ndani ya Chama Cha Mafisadi, lakini wale ambao watakuwa wakweli wa nafsi zao na kuamua kuweka mbele maslahi ya nchi badala ya yale ya CCM na mafisadi kamwe hawatakuwa na nafasi ndani ya chama hicho.
   
 3. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #3
  Oct 14, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Please kwa nini ulijiunga ccm? Ulikuwa unatafuta fedha, madaraka, umaarufu, kinga au ulijitolea kutumikia taifa lako?

  Rafiki yaki Zitto, anatafuta fedha, madaraka, umaarufu, kinga au amejitolea kutumikia taifa?

  Mwanachama anajiunga na chama ili iweje? Unajua utofauti wa uanachama wa FMES, Makamba, Nape, na Msekwa kule CCM?

  Unaesemeaje kauli ya Sumaye kuwa maisha mazuri ya wafanyabiashara yapo ccm?

  Nashabikia chadema vibaya mno but i don think kama nitachukua kadi, pai nafikiria wengi wapo humu kwa staili hio.

  conclude nini kilikusukuma kuchukua kadi ya ccm?
   
 4. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #4
  Oct 14, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Niliomba kujiunga na ccm (bado sijakubaliwa hadi leo) kwa sababu nilikuwa naitikia wito wa kujiunga na wenzangu ili kulitumikia taifa langu. Natumaini kuwa Zitto alijiunga CHADEMA ili kulitumikia taifa analolipenda sana.

  kwa kweli sina hakika kama najua kama hao uliowataja hapo juu wamejiunga kwa nia gani - natumaini wamejiunga ili kuungana na wenzao kujenga nchi.

  kwa bahati mbaya, wakati wa uongozi wa Mkapa na Sumaye maisha mazuri ya wafanyabiashara yalionekana kuwa kama yapo ccm. Mwanzoni wa uongozi wa Kikwete kulitolewa ahadi nyingi kuwa hali itabadilika ila inaonekana mambo yanarudi kule kule.

  Katika hili naona kama tuko pamoja kwenye mtizamo huu. Kwa kutojua kama nilikubaliwa au kukataliwa uanachama wa ccm, bado sijui kama naweza kudai haki ya uanachama wa ccm sasa hivi au wa chama chochote kile Tanzania. Bado najifunza na kusoma sera za hivi vyama ili kujua nifanye maamuzi gani sasa ingawa ninaelekea kwenye kufanya kazi za kujenga nchi bila ya ulazima wa kutumia vyema

  Nia yangu ya kutaka kujiunga na wenzangu wenye mtazamo fulani ili kujenga na kuendeleza taifa langu.
   
 5. Selous

  Selous JF-Expert Member

  #5
  Oct 14, 2008
  Joined: Jan 13, 2008
  Messages: 1,322
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Then support any movement kwa hali na mali kama unahisi ina maslahi kwa Tanzania. No matter yupo chama gani. Ila i do respect wale wenye karama hio kama akina Zitto, Mnyika, FEMS, Dr. Slaa, na wale wote wenye mapenzi mema na nchi hii bila kusukumwa na personal interest na conflict within.

  Nachelea sana kumpongeza Nape na Kilango kwa sababu roho yangu tu haitaki.

  Kaka nahisi sisi tunaopigana kwenye grass roots huku pia kipato chetu kikiwa na mahusiano na mafisad ndo hali yetu mbaya. pale pa kuepuka tusiwafaidishe mafisadi tunafanya na pia tumejiandaa kwa lolote. ila hawajui waanzie wapi mana hata wao wamebanwa vilivyo na hao walioyowaleta. hope you get it correctly!
   
 6. M

  Magabe Kibiti JF-Expert Member

  #6
  Oct 14, 2008
  Joined: Jan 20, 2008
  Messages: 292
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kichwangumu,

  Mimi sijamuongelea Kilango hapa na sidhani kama Kilango anaweza kuhesabiwa kama kijana ila nimeelewa point yako ya mtizamo.

  Asante
   
 7. M

  Mwafrika wa Kike JF-Expert Member

  #7
  Oct 14, 2008
  Joined: Jul 5, 2007
  Messages: 5,194
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  kweli kabisa BAK,

  Vijana wengi wasiokuwa na pesa au majina makubwa wamejaribu kugombea nafasi za udiwani au ubunge kupitia ccm kila chaguzi na kujikuta wakitupwa mbali na mazee (mengi yao mezi tu na mafisadi) ndani ya ccm. Wazee wengi ccm hawako tayari kubadilika na kuanza kujenga nchi bali wanajali matumbo yao tu.

  Kuna mtu miaka ya nyuma aliwahi kusema kuwa ccm ina wenyewe na kadri siku zinavyoenda hili linajidhihirisha wazi. Wenye kufungua matawi ya ccm nje ya nchi endeleeni tu kufanya hivyo kwa kadri mtakavyoamua kuendelea kukaa nje ya nchi. Siku mkirudi nyumbani tu na kujaribu kusema chochote mtaishia kuwa kama Nape na wenzake wengi ambao hata sasa hawasikiki tena.
   
 8. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #8
  Oct 14, 2008
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Magabe, et al.,

  Niliwahi kuandika article ikielezea, pamoja na mambo mengine, kwa nini vijana kama Nape wanaendelea kubaki CCM. Hebu jaribu kuisoma hapa chini uone kama inajibu baadhi ya hoja zako.
  _________________________________________________________________

  CCM ya Nape ni nadharia, ya Nchimbi ndiyo iliyopo

  na
  Kitila A. K. Mkumbo (Tanzania Daima, 24 Septemba 2008)

  NIMEFUATILIA, kama ilivyo kwa Watanzania wengine, ‘mgogoro' wa kifikra na mtazamo kati ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti katika Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Nape Nnauye na mwenyekiti anayemaliza muda wake katika umoja huo, Emmanuel Nchimbi.

  Hata hivyo nikiri mapema kabisa kuwa sielewi mantiki ya mgogoro huu na hatimaye mjadala uliofuata na unaoendelea.

  Nisichoelewa hasa ni msingi wa dhamira ya Nape katika hoja yake ya kupinga mkataba wa mradi wa ujenzi wa jengo la makao makuu ya UVCCM, ambayo imevuta hisia za watu wengi, ndani na nje ya CCM.

  Najiuliza maswali mawili. Mosi, je, Nape ameibua hoja ya kupinga mkataba ‘haramu' wa mradi wa ujenzi wa jengo la UVCCM kama karata na turufu ya kumwezesha kushinda kiti cha uenyekiti wa umoja huo?

  Pili, ni kweli kwamba Nape ni miongoni mwa wana CCM wachache ‘waliokoka' na kujiunga na kundi kubwa la wananchi wanaochukizwa na kukerwa na mwenendo wa ufisadi miongoni mwa viongozi waandamizi wa CCM na serikali yake?

  Kama msingi wa hoja ya Nape ni ule wa kwanza, wa kutumia hoja yake kama turufu ya kuvuta hisia za wana UVCCM wenzake ili wamchague kuwa mwenyekiti wao, ni wazi kuwa amekwishashindwa kabla hajaanza.

  Kwa msingi huu, anachojaribu kufanya Nape ni kuvunja misingi mama ya kanuni za ushindani ndani ya CCM.

  Nape anataka achaguliwe kwa misingi ya hoja za kimantiki, uadilifu, ustaraabu, ukweli, uwazi, uhuru na kujitegemea katika kufikiri, zaidi ya yote, kutanguliza utaifa dhidi ya uchama na ukada.

  Yote hii ni misingi mizuri, lakini si misingi ya CCM na ndipo upofu wa Nape ulipo. Kwa hoja zake, Nape anajaribu kuweka mlo safi katikati ya jalala la taka.

  Hautanoga na wala hataufaidi mlo huo, zaidi ya yote anajiweka katika mazingira hatari ya kuambukizwa vijidudu hatari vitakavyompelekea augue ugonjwa hatari wa matumbo!

  Anachofanya Nape ni kupingana na misingi ya kanuni za msingi za kutafuta madaraka ndani ya CCM, ambazo kwa uchache kabisa ni pamoja na ubabaishaji, uzandiki, ujanjaujanja, njia za mkato, unafiki, ghiliba, kujipendekeza, kuiba wajumbe na kuwaficha.

  Muhimu zaidi kuliko zote, kutanguliza ukada na uchama dhidi ya uwezo wa kiuongozi na kiutendaji na uzalendo kwa nchi. Hii ndiyo CCM ambayo Nape anajaribu kuibomoa na ambayo Nchimbi na wenzake kina Makamba wanaipigania.

  Kwa hiyo utaona kwamba CCM ambayo Nape anajaribu kuipigania haipo, ni nadharia. Iliyopo ni ile CCM ambayo Nchimbi na Makamba wanajaribu kuilinda kwa mafanikio makubwa.

  Niliwahi kuwa mwanachama na kada mwaminifu wa CCM kwa muda kidogo na nilijaribu kugombea nyadhifa kadhaa katika UVCCM, kwa bahati nzuri nilishindwa zote!

  Kwa uzoefu nilioupata ni kwamba hushindi uchaguzi ndani ya CCM kwa kuwa na uwezo au kwa kujenga hoja za kimantiki zinazoweka maslahi ya nchi mbele.

  Unashinda uchaguzi ndani ya CCM kwa kujifanya wewe ni kada kuliko mwingine yeyote, kwa ujanja ujanja, kwa kujipendekeza na kujipitishapitisha kwa baadhi ya wakubwa wanaoingia kwenye vikao muhimu vya CCM kurubuni wajumbe wa vikao, ikiwemo kuwaficha wajumbe wa vikao hivyo.

  Ukitaka kushindwa kirahisi katika uchaguzi wa CCM, uonyeshe uwezo na utangulize mambo ya taifa mbele badala ya ukada. Kama kuna kiongozi wa CCM aliyeshinda uchaguzi ndani ya chama hicho kwa kujenga hoja za kutetea masilahi ya taifa dhidi ya ukada awe wa kwanza kujibu makala hii.

  Nape, wana CCM wengine makini wanajua vizuri kwamba ingekuwa ni suala la uwezo na kutanguliza masilahi ya taifa, Rais Jakaya Kikwete asingewashinda Salim Ahmed Salim, Mark Mwandosya na hata Frederick Sumaye.

  Pamoja na mambo mengine, sifa kubwa iliyomfanya Rais Kikwete awashinde wenzake katika kinyang'anyiro cha kugombea urais ni ukada wake wa muda mrefu katika CCM.

  Kwa hiyo katika CCM ukada ndiyo sifa mama na kigezo muhimu cha kuweza kuchaguliwa. Ndiyo kusema Nape anapojaribu kutanguliza utaifa, tena kwa kuzomea ufisadi, ambayo ni nguzo muhimu ya kuwepo kwa CCM, kama turufu ya kutaka achaguliwe kuwa mwenyekiti wa UVCCM, anajaribu kukata mbuyu kwa wembe. Hataweza, atajikata mwenyewe na kuuacha mbuyu umesimama kidete.

  Pengine tumpe Nape, ile Waingereza wanaita: "The benefit of doubt". Kwamba Nape ni miongoni mwa wana CCM wachache waliookoka hivi karibuni, ameamua kujitoa mwili na roho katika kujiunga na majemadari wa vita dhidi ya ufisadi.

  Kuokoka kupo si tu katika siasa na dini, lakini pia katika nyanja nyingine za maisha ya kijamii. Lakini unapoamua kuokoka lazima ujue na uzingatie misingi ya wokovu, vinginevyo utaanguka tena.

  Kuokoka kisiasa na kidini kunahitaji ujasiri wa kukubali kusutwa na kuacha mazoea. Ili ukamilishe wokovu lazima ukubali kubadilika kimwili na kiroho.

  Ninachokiona hapa ni kwamba Nape amekwisha kutoka CCM kiroho, kiakili na kisaikolojia lakini bado amebaki kimwili. Hili ni tatizo linalowakumba wana CCM wengi.

  Ninaamini kuna wana CCM wengi waliokwisha kukihama chama chao kiroho, kiakili na kisaikolojia, lakini wameendelea kubaki huko kimwili kwa kukosa ujasiri au kwa sababu zingine, ikiwemo kuamini kwamba ipo siku CCM itabadilika.

  Nikiri kuwa mimi ni mmojawapo, ambaye ilinichukua takriban miaka mitano kuhama CCM kimwili. Nilikuwa nimeachana na CCM kiroho, kiakili na kisaikolojia tangu mwaka 2000, lakini ilinichukua miaka mitano hadi 2005 nilipoamua kujitoa hadi mwili na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

  Binafsi nilijitoa CCM baada ya kujiridhisha bila shaka kuwa CCM imefikia hatua ya usugu, na haiwezekani kubadilika. Ni hatua ambayo vyama dada kama KANU, ZANU-PF na UNIP vilipitia na ambayo ni wananchi pekee wenye uwezo wa kuibadilisha.

  Kama kweli tumechoshwa na madhira ya CCM, ikiwemo ufisadi, inabidi tufike mahala tukubali kuachana na CCM. Kuendelea kuibakisha CCM madarakani ni kukubaliana kwamba, pamoja na kwamba tumeumia kama nchi, bado tunaweza kuendelea kuwavumilia CCM, hatujaumia vya kutosha.

  Kufikiri kwamba CCM inaweza kubadilika ni njia nzuri ya kujiridhisha kisaikolojia baada ya kushindwa kuitoa madarakani, lakini haisaidii kubadili hali ya mambo katika nchi yetu.

  Kwa hiyo, Nape ana mambo mawili ya kuchagua. Mosi, anaweza akaendelea kubaki CCM kimwili na kuisaliti dhamira yake ya ndani na akaendelea kupiga kelele za ufisadi, ambazo zitazidi kumtenga na wenzake ambao ‘hawajaokoka' katika CCM, na hivyo kuendelea kuonekana kituko! Pili, anaweza akauvaa ujasiri kwa kuamua kuutoa mwili wake kutoka CCM na kuupeleka kule ambapo akili na roho zipo. Uamuzi ni wake.

  Inapatikana pia hapa: http://www.chadema.net/makala/mkumbo/kitila_18.html
   
 9. T

  The Golden Mean Member

  #9
  Oct 14, 2008
  Joined: Sep 15, 2008
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mugabe Kibiti naomba unifafanulie ujuzi wako kuhusu mambo haya kwani mimi yananifanya nisite kuwapigia makofi vijana hawa:

  je unadhani Nape na waitara ndio vijana pekee ccm?
  kama nimekuelewa vizuri kwenye swali lako la msingi, unaonyesha hiyo kama ndio tabia ya ccm kuwaadhibu vijana, na hivyo kuwatisha wenyine kuingia kwenye chama hicho kikongwe.
  naomba uzingatie ya kwamba ccm kuna vijana wengi sana wanakitumikia chama hicho, naomba usiniuliza dhumuni lao kwa sababu sijui kwa kweli kama na wao ni mafisadi wajao, ila msingi ni kwamba wapo.

  haafu zingatia pia kuwa watazidi kuongezeka, hasa mwishoni mwa mwaka huu. uvccm inafanya uchaguzi na age limit ya wagombea wake ni miaka 29, yeyote juu ya hapo haruhusiwi kugombea.

  kuwepo wapo, ila kuonekana kwao kwenye jamii, hilo ni suala lingine.

  je unafikiri wamesema waliyoyasema kwa maslahi ya watanzania au yao binafsi?
  hapa zingatia: kwanza, nape alikua na nafasi ya kuibua suala la jengo la uvccm mapema lakini akasubiri hadi mchakato wa kutafuta mwanykiti wa uvccm ulipoanza ndio akaibua suala hilo, unadhani alikua na nia gani?
  pili, bahati nzuri namfahamu bwana waitara tangu alipokua raisi daruso hadi sasa, mengi ya aliyoongea kwenye shutma zake dhidi ya viongozi wa uvccm ni uongo kama kusema kuwa nchimbi alimtoa yeye kwenye nafasi ya katibu wa uvccm dar es salaam akamuweka ndugu yake, mi nnachojua ni kwamba, waitara hajawahi kushikilia nafasi hiyo na alimkuta katibu aliyepo yeye alipojiunga kuwa katibu wa wilaya ya ilala, na katibu huyo hana undugu hata wa kupakana mashamba na nchimbi! sasa je huyu ni mtu anayefaa kuingia chadema kama ni muongo kiasi hicho.
  i stand to be corrected, ila mi naona mwaita waitara ataleta matatizo chadema... time will tell!

  nadhani ni vyema, kabla ya kushangilia watu wanaoikosoa ccm, hasa wale wa ndani ya ccm, tukaangalia kwanza nia yao kufanya hivyo, tusije tukawa tunawashangilia mafisadi waliovaa ngozi ya kondoo, hao ni wabaya zaidi ya wale tuwajuao waziwazi! na mbaya zaidi ni pale wanapohama na ugonjwa wao wa ufisadi kwenda kwenye vyama vingina ambavyo tunavitegemea kukaripia ufisadi!
   
 10. BongoTz

  BongoTz JF-Expert Member

  #10
  Oct 14, 2008
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 272
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  First of all, asante kwa hii thread. It's a great thread maana inauliza swali la msingi ambalo vijana wengi [wakereketwa wa CCM] bado hawajaketi chini na kujiuliza.

  Hapa ninakubaliana na wewe kabisa. Binafsi, nimekutana na watanzania wengi sana [waliobahatika kuishi kwenye nchi zinazo cherish demokrasia] ambao hawako tayari kabisa kuingia ndani ya kokoro la CCM kwasababu [kwa kuishi kwao ng'ambo] tayari wameishaona mazuri yanayoweza kufanywa na vyama tawala ktk nchi hizo.

  Pretty sad, huh!?

  Nafasi ya vijana ndani ya CCM ni sifuri. Zero. Nada. Why? Kwasababu wazee wa chama bado hawajawa tayari kuweka kando personal interests zao ili kukijenga chama. I mean, let's be serious here for a moment. Take, for example, hii issue ya Nape. Waliomchezea Nape mchezo mbaya [ukiacha Nchimbi], sio wengine ila ni wazee wenye nafasi za juu ndani ya chama. Na wamefanya hivyo for one and only one reason: "If nape gets his way, then all our crooked ways will be exposed." Forget this whole "amekiuka maadili ya chama" thing. Hawa wazee wanaoshikiria nafasi za juu ndani ya CCM ni wachafu wa kupindukia, na wanajua kuwa akiingia outsider [kama wewe ulivyoomba uanachama kisha wakakataa hata kukujibu kama umekubaliwa au lah...]; ata-leak madhambi mengi waliyoyakalia/kumbatia, and as a consequence, ulaji wao utaota mbawa.

  May be it's a wishful thinking on my part, but suppose kama Nape angetendewa haki at a time being [which is unlikely], je ni wanachama wangapi wanaojua siri ambazo sisi tulioko nje ya CCM hatujui wange-come out next? The so-called wazee wa chama aren't stupid. Ndio maana waliamua kumu-punish/shut up Nape ili wengine wanaofikiria kufuata nyayo zake wafyate mikia yao.
   
 11. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #11
  Oct 14, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mimi ninavyodhani vijana ndani ya CCM wananafasi ingawa inaweza kuwa finyu ila wanapoingia wanakuwa ni wasamaria wema na wapenda maendeleo wasiojua rushwa ni nini ila CCM inaishia kuwa corrupt their decence!
   
 12. H

  Honey K JF-Expert Member

  #12
  Oct 14, 2008
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wakubwa nawashukuru kwa maoni yenu mazuri na ya kutia moyo, lakini kubwa maoni mengi ni ya kufundisha na kuonyesha njia,ntajibu kwa kuanzia na hili kwanini nimesema wakati nachukua fomu za kugombea kiti uvccm.
   
 13. H

  Honey K JF-Expert Member

  #13
  Oct 14, 2008
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Swali la kwanini nilizungumza swala la Mradi UVCCM wakati nachukua fomu limekuwa likiulizwa sana, hasa kwanini wakati huu. Ikumbukwe mimi ni mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM(T) toka mwaka 2002, Mradi wa UVCCM ni moja ya mipango ya kazi za UVCCM kwa kipindi cha 2003/2008,kwahiyo nimekuwepo kwenye mchakato wa hili na sina tatizo na uwekezaji wa mradi huu TATIZO NI TARATIBU ZA KUFIKIA UWEKEZAJI HUU NAAMINI HAZIKUFUATWA, MBILI MKATABA HAUNA MASLAHI KWA UVCCM, CCM NA VIJANA WA CCM NA WAKITANZANIA.
  Sikuanzia pale nilipochukua fomu kuupinga mkataba huu, bali nimeanza siku nyingi vikaoni sio publicly. Wakati huo nilikuwa masomoni India kila nilipokuwa nikija likizo na kuhudhuria vikao vinavyonihusu nimekuwa nikipinga Utaratibu uliotumika kumpata mwekezaji na contents za mkataba, narudia ndani ya vikao, na si kupinga tu bali kuhamasisha bila kificho wala unafiki wengine kupinga pia, nikiamini TUNAPASWA KUWA WAZALENDO ZAIDI KWA KUWEKEZA NA MASHIRIKA YETU YA UMMA KAMA NSSF,PPF NK ILI PESA WAKIPATA ZIBAKI KUJENGA NCHI YETU PIA KULIKO WAGENI WAPATAPO FAIDA HUPELEKA KWAO.
  Nasikitika, baadae wakubwa wachache wakaamua kuvizunguka vikao na kuamua kusign mkataba tulioukataa baraza kuu la UVCCM na kuagiza marekebisho.
  Niliwaonya mara kwa mara hawakutaka kusikiliza kwa kulewa na tu madaraka, nilipochukua fomu haikuwa mara ya kwanza kwa hili kusemwa hadharani, lilisha wahi kuandikwa na KULIKONI GAZETI, tofauti tu hapa nilitoa wanaohusika na dhuluma hii kwa UVCCM,CCM NA NCHI YETU.
  NA IKUMBUKWE HAPA NDO NILIKUWA NIMERUDI TOKA INDIA MASOMONI KAMA WIKI MBILI TU, NIKAKUTA WAKUBWA WANAENDELEA NA MRADI NINAOAMINI NI WA HOVYO, NI UKWELI USIO NA MASHAKA BILA KELELE ZILE MKATABA USINGEPITIWA UPYA........sijui kama nimekidhi mahitaji yenu...
   
 14. J

  Jamco_Za JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2008
  Joined: Jul 14, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ukiwa CCM hata kama si kijana ukiwa na fikra tofauti na wenyewe basi ujue kuwa hawatakubaliana na wewe watakufukuza tu kwani wako pale kwa ajiri ya kulinda masirahi yao.

  Vijana wa tanzania inabidi ukae mbali na CCM unless wewe ni mmoja wao, ukiwa na msimamo tofauti na wao then hama chama kabla hata hajasema chochote.
   
 15. K

  Kithuku JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,395
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Kwanza hongera kwa ujasiri hadi hapo ulipofikia na asante kwa kujiunga JF. Swali moja tu ndugu: Umeshaona msimamo wa hao 'wakuu' wako, sasa msimamo wako binafsi ni upi: baada ya kushindwa kuwapinga, je sasa utajiunga nao rasmi? (The adage goes "if you can't fight them, join them!")
   
 16. deny_all

  deny_all JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2008
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 428
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lakini naona kelele zake Bw. Nape zimesaidia huo mkataba kuangaliwa upya, nadhani ndio uamuzi uliopitishwa na kikao cha mwisho chini ya Kikwete.

  Kwa maana hiyo kwa yeye kusema aondoke ndani ya chama inaweza kuwa sio tija na itaonekana amewaogopa wahusika, apambane nao ndani kwa ndani kama anaweza na anajiamini.

  Haya ni mawazo yangu yanaweza kuwa sio sawa.
   
 17. H

  Honey K JF-Expert Member

  #17
  Oct 14, 2008
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kwanza nakushukuru kwa mawazo yako. Naomba niweke wazi msimamo wangu hapa pia kwamba...UZALENDO WANGU NA KWAKWELI WA VIJANA WA KITANZANIA LAZIMA UVUKE MIPAKA NA MINYORORO YA ITIKADI ZETU...Tanzania kwanza chama baadae...
  Kwahiyo kuhama chama naamini si suluhisho la matatizo ya Tanzania.Inawezekana leo usinielewe vyema lakini time will tell one day...mimi naamini yanayotokea leo kwenye CCM na kwakweli hata kwenye baadhi ya vyama vya siasa hasa vilivyopigania uhuru ni Mvutano mkubwa uliopo kati ya kizazi ninachoamini "kipya"...kinachoamini CHANGES... na kizazi "chazamani" kinachotaka kubaki na mambo ya zamani na wakati huo wakijikuta wanapitwa na wakati hivyo wanakosa mwelekeo hata kufanya mambo bila "busara" na kushindwa kujua kuwa wanapaswa kama chama kukidhi mahitaji ya mazingira na wakati wa sasa...Ukumbuke mvutano huu ni chachu ya kutoa zao bora"sera" kwa ukombozi "mpya" wa kiuchumi wa nchi yetu...Mao aliwahi kusema...ni muhimu kukawa na msuguano kati ya kizazi kipya na cha zamani ili kupata maendeleo..positive...
   
 18. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #18
  Oct 15, 2008
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  Saafi sana mkuu tupo ukurasa mmoja hapa.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Oct 15, 2008
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nnauye Jr,
  Mkuu kwanza nakupongeza sana kwa kujitokeza kama kijana mwenye mtazamo wenye nuru....Karibu JF, karibu sana.
  Kitu kimoja tu nakushauri ufahamu toka leo ni kwamba hao wazee unaosema wanaendeleza fikra za kizamani usifikirie kabisa kuwa wao hawapo ktk dunia hii na hawaelewi kinachotakiwa leo hii - WANAFAHAMU sana na wamekulia ktk malezi ya elimu ya wananchi kujikomboa..
  Tatizo kubwa ndugu yangu ni kwamba hao wazee kwa sababu wanafahamu tactics zote na wao kama walimu wa ukombozi wa fikra za kimapinduzi wanakuwa mbele yenu kwa kila mnalojaribu kulifanya kwa sababu leo hii watawala, Mabepari, makabaila, Mirija na kadhalika ni WAO sio walowezi tena. Tofauti ni hali ya nchi toka koloni ama Huru, toka mzungu kuwa mtu mweusi lakini Utawala na hali ya kimaisha kwa wananchi haijabadilika...
  Kwa hiyo, vita mlokuwa nayo ni nzito sana tofauti na jinsi mnavyoipima..

  Nakuomba fikira upya kuwa:- Hivi kweli sisi Waafrika tungeweza kujikomboa Kiutawala na Kiuchumi kwa kupigania haki hizo ndani ya vyama vyao vya kisiasa?.. Hivi kweli Nyerere angepewa wadhifa ndani ya Utawala wa Mkoloni tungeweza kuupata Uhuru kirahisi!...SIDHANI! na kama ingewezekana basi ingechukua miaka mingi zaidi.. Mnapotumia kuwa ndani ya CCM kuna viongozi wazuri haipishani na kusema kati ya viongozi wakoloni walikuwepo wazungu viongozi wazuri wenye moyo na uchungu.. Yet, hakuna historia ya nchi hata moja iliyokombolewa na jitihada za wazungu hao! kwa sababu wao wenyewe wamefungwa na mihuri iliypigwa rohoni mwao.

  Hiki ndicho vijana wengi Tanzania mnapotoka. Bado fikra zetu kuwa adui wa uchumi wetu ni Wageni wanaokuja kuwekesha nchini... Laa hasha, adui wetu ni sisi wenyewe Watanzania, hao viongozi wetu, wazee wetu ambao leo hii ndio wao wanaokuribisha Ukoloni mamboleo kwa kuzawadiwa shanga (10%)..Kumsimamisha mtu kama huyu ni kuwa kinyume naye kwa maneno na matendo laa sivyo nawe unazidi kujenga jina la Utawala wao..
  Mkuu sina maana utoke CCM ujiunge na chama kingine lakini jitihada zako kusema kweli ni sawa na kaa (crab) aliye ndani ya kapu - hawezi kutoka wala kuokoa kaa wenzake wote wanasubiuiri kukaangwa..
   
 20. Zakumi

  Zakumi JF-Expert Member

  #20
  Oct 15, 2008
  Joined: Sep 24, 2008
  Messages: 4,817
  Likes Received: 327
  Trophy Points: 180
  Mkandara:

  Mbona unazunguka sana. Wazee wengi ni washamba tu (period). Madaraka ya viongozi wa Tanzania yana mamlaka makubwa lakini wanashindwa kutumia kuleta maendeleo kwa jamii na kwa wao wenyewe.

  Hata China watu wanavuta 10% lakini wanajua kuizungusha 90%. Hata Marekani watu wanavuta lakini kwetu watu wanakomba.
   
Loading...