CCM yamwangukia Bashe! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yamwangukia Bashe!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Nov 24, 2008.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Nov 24, 2008
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mwanasiasa kijana machachari aliyekuwa mwanachama na mgombea nafasi ya Mwenyekiti taifa ya jumuya ya Umoja wa Vijana wa chama cha mapinduzi , Nape Nnauye ametangaza rasmi kumuunga mkono mgombea wa Makamu mwenyekiti wa UVCCM Taifa Ndugu Husein Bashe,

  Alitoa kauli hiyo juzi Jumamosi alipokuwa akihojiwa kuhusu masuala kadhaa yanayohusu UVCCM na CCM. Nnauye alinukuliwa akisema ndugu Bashe ni mtu makini na mwenye sifa za kuwa kiongozi kwani amewahi kuwa Rais wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu Mzumbe.

  Kuhusu wagombea wengine wa makamu mwenyekiti Beno Malisa na Zainabu Kawawa, Nnauye anasema ni kosa kubwa kwa UVCCM kumchagua Beno Malisa kuwa makamu mwenyekiti UVCCM Taifa kwa kuwa ni fisadi alishiriki kuandaa mkataba tata wa jengo la UVCCM.

  Nape alimlaumu Malisa kuwa anataka kuvuruga maadili ya uongozi kwa kuandaa safu ya wakuu wa vitengo, Nape anasema kumteua Ridhwan Kikwete kuwa katibu uhamasishaji UVCCM Taifa, nafasi inayohachwa wazi na Mhe Tom Mwangonda mbunge wa kuteuliwa na Raisi ni kosa kubwa.

  Malisa amekubaliana SWAHIBA WAKE Ridhwan Kikwete kuwa akishinda atamteua Ridhwan kuwa katibu uhamasishaji Taifa wa UVCCM (hili ni kosa kubwa)

  Beno hana sifa ya uongozi haiwezekani mtu tangu darasa la kwanza mpaka chuo kikuu haujawahi kuwa hata monita leo uombe kuwa makamu mwenyeki kwa kigezo cha kuwa karibu na mtoto wa Rais.
   
 2. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #2
  Nov 24, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,605
  Trophy Points: 280
  Kazi imeanza...wenyewe kwa wenyewe....wanaanza kuumana...kutoana macho
   
 3. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #3
  Nov 24, 2008
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wacha watwangane waparurane,hii ni nzuri kama wapinzani watatumia mfarakano wa CCM kujijenga.
   
 4. H

  Honey K JF-Expert Member

  #4
  Nov 24, 2008
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kimsingi kabla mazungumzo hayajaenda mbali niliweke wazi hili, tulipokuwa tukizungumza clouds fm, hatukutaja jina la hussein bashe, na baada ya kusoma hapa naanza kuhisi kuna watu wanakusudia kutumia hili kisiasa maana yanayosemwa juu ya kina benno na ridhiwani ni mawazo binafsi ya aliyendika hapo juu, hebu tuwe wakweli badala ya kumlisha mtu maneno, narudia sina mgombea na wala mimi mpaka sasa sio mpiga kura, haya ni uzushi
   
 5. H

  Honey K JF-Expert Member

  #5
  Nov 24, 2008
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  nDUGU YANGU oGWALUMAPESA NASIKITIKA KWA TAARIFA HII ULIYOITOA HAPA UKIDAI NIMESEMA HII NI KUSHUSHA HESHIMA YA FORUM HII, PENGINE SEMA ALIYEKUPA HAYA MAANA MKANDA WA NILIYOSEMA CLOUDS FM UPO NAWEZA WEKA HAPA IKAWA SI NZURI SANA KWAKO.

  NAAMINI UMETELEZA JITAHIDI KUTOTELEZA TENA....
   
 6. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #6
  Nov 24, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Parapanda italia parapanda...
   
 7. MwalimuZawadi

  MwalimuZawadi JF-Expert Member

  #7
  Nov 24, 2008
  Joined: Sep 1, 2007
  Messages: 643
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mazungumzo yako mbali tayari...ila usionde ukweli utajulikana vere soooon
   
 8. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #8
  Nov 24, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ogwalumapesa

  Ningeomba ui-edit hiyo post yako maana mpaka kichwa chauma kukuelewa. Huenda ulikuwa unaiandika ukiwa na usongo, ili tuichangie bila kuwa biased isome tena halafu usahihishe makosa madogo madogo ya kiuandishi.
   
 9. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #9
  Nov 24, 2008
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka hakuna kuteleza hapa. Hii ni cheap propaganda ya BASHE. Sitashangaa kama ni yeye mwenyewe. Tatizo CCM na hata wanasiasa vijana wa Tanzania bado hatujatambua umuhimu wa kuendesha siasa kitaalamu. Hii inaonyesha kuwa BASHE hana strategists makini katika campaign team yake. Ni rahisi kwa mtaalamu wa siasa kugundua kuwa propaganda ya aina hii ni hatari maana uwezekano wa kubackfire ni mkubwa mno.....

  Tanzanianjema
   
 10. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #10
  Nov 24, 2008
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wapinzani wapi hao?lol
   
 11. P

  Phillemon Mikael JF Gold Member

  #11
  Nov 25, 2008
  Joined: Nov 5, 2006
  Messages: 8,855
  Likes Received: 2,430
  Trophy Points: 280


  ..karibu bw mdogo..karibu sana tukate ishu,.utasaidia sana kuleta balance ya hoja humu ndani ambapo mara nyingi viongozi wa ccm ...hawaonekani sana hapa..sasa kwa ujio wa watu kama wewe kwa uwazi[maana tunajuwa wanaingia kwa siri]...itasaidia kuleta usawa wa hoja..humu ndani....

  kumbuka JF ...WHERE WE DARE TALK OPENLY.....
   
 12. JohnShaaban

  JohnShaaban JF-Expert Member

  #12
  Nov 25, 2008
  Joined: Aug 23, 2007
  Messages: 465
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nape, karibu sana.
  Hii ndio JF, kuna watu makini lakini pia kuna vijana wababaishaji wanaopenda kulisha wenzao maneno. Hakijaharibika kitu kwa sababu huyu kijana anaweza asirudi tena kwenye hii 'thread' kama utapenda kuthibitisha hilo.

  By the way, kama unaweza kuweka hayo mazungumzo uliyofanya CloudsFM (hata mhitasali) basi ingependeza ili tujue Bw. Ogwalu ameteleza wapi; maana inawezekana 'implication of main theme' ya mazungumzo yako ilimfanya Ogwalumapesa akatoa maoni hayo. Kumbuka mambo ya JF yako wazi, humu ndani hakuna ukiranja wa Makamba wala EL; hapa tunatoa maoni kwa uwazi na vielelezo thabiti!
   
 13. Kilbark

  Kilbark JF-Expert Member

  #13
  Nov 25, 2008
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 558
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hizi siasa zina mwisho wake. Na kwa kweli kama mtanzania wa kawaida inanifundisha kuwa watu wanagombea madaraka kwa ajili ya kudhulumu wapiga kura wao na sio kuwaletea mabadiliko. Unaweza kuona hata katika hii michakato yao siku hizi. Natamani Nyerere siku moja aamke aone huu ushenzi...By the way karibu sana Nape.
   
 14. FairPlayer

  FairPlayer JF-Expert Member

  #14
  Nov 25, 2008
  Joined: Feb 27, 2006
  Messages: 4,166
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Vumilia tu Nape. Humu JF watu makini wapo tele na watu hovyo pia wapo.

  Nimefurahi sana kwa kupinga hoja kwa hoja bila mikwaruzo. Dalili za kukomaa hiyo.
   
 15. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #15
  Nov 25, 2008
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280

  Mkuu Nape,

  Vipi hilo la kumuona Rais wetu bado ana uwezo wa kuongoza miaka mingine ijayo.Hali ya maisha wananchi wanayopitia leo hii,kweli unamuona huyo mkulu bado anafaa?
   
 16. Pilato

  Pilato Member

  #16
  Nov 25, 2008
  Joined: May 29, 2008
  Messages: 60
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Originally Posted by ogwalumapesa View Post
  Malisa amekubalihana maSWAHIBA WAKKE Ridhwan kikwete kuwa akishinda atamteua Ridhwan kuwa katibu uhamasishaji Taifa wa UVCCM ili ni kosa kubwa ,Beno hana sifa ya uongozi haiwezelkani mtu tangu darasa la kwanza mpaka chuo kikiuu haujawahi kuwa hata monita leo uombe kuwa makamu mwenyeki kwa kigeza cha kuwa karibu na mtoto wa Rai  Ogwalumapesa
  Tunaomba utueleze vizuri ili tuchangie ,jamani tusiwe tunadhalau mada labda kuna ukweli ndani yake ,ogwalu thibitiosha maneno hayo juu ili tuchangie..!!
   
 17. H

  Honey K JF-Expert Member

  #17
  Nov 25, 2008
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Naiheshimu sana forum hii kwani inasaidia kutoa mambo ambyo wakati mwingine hayasemwi na vyombo vingine.Nawashukuru kwa kunikaribisha, napokea kwa heshima kubwa karibu yenu wakubwa, naahidi ushirikiano mkubwa kwa kadri ya uwezo wangu wote.
  SASA MAMBO MUHIMU TULIYOONGEA KATIKA KIPINDI CHA MLANGO WA DHARURA NI;

  1). Niliunga mkono uteuzi wa wagombea kutoka Zanzibar kugombea Uenyekiti UVCCM. Baadhi ya sababu ni kuwa haya ni maamuzi ya kikao halali cha chama NEC, kwa kuzingatia kuwa hakuna uteuzi ambao usingekuwa na mapungufu, hata huu ninaouunga mkono una mapungufu yake mengi tu, lakini ukilinganisha na uteuzi mwingine kwa MTAZAMO WANGU huu ulikuwa nafuu kuliko mingine. Lakini nilikumbusha kuwa mwaka 2003 niligombea mimi uenyekiti uvccm na kulikuwa na wagombea toka znz ambao hawakurudishwa hivyo sioni sababu ya bara kulalamika leo.
  2).Utendaji wa Makamba, nilichosema ni kuwa si dhambi kujadili utendaji wa Makamba kama katibu mkuu wa CCM, tena hata wanachama wa kawaida wana nwajibu wa kujadili hali ya chama chao, KWANI NAAMINI HICHI NI CHAMA CHA WANA CHAMA NA SI VIONGOZI. N a nikaongeza kuwa kikao chenye mamlaka ya kumwajibisha Katibu mkuu wa ccm ni NEC huu ndio utaratibu, hivyo hata baada ya kujadili mwisho lazima malalamiko yaletwe NEC ndo wanaweza kumwajibisha Katibu Mkuu.

  3). Nikasema KUGOMBEA URAIS 2010 SI DHAMBI ni huru kwa mwana chama yeyote kwa mujibu wa katiba ya CCM ambayo ndio sheria mama, kwani hata ilani ya uchaguzi inatengenezwa mpya, hivyo sitashangaa kuona watu wanachukua fomu kuomba uteuzi, ndio demokrasia.

  4). Nikasema pia si kweli kwamba wanaokosa wanakumbatiwa, inawezekana kwa upande mmoja lakini sio katioka kesi zote, nikatoa mfano wa waliowajibishwa kwa makosa ya Richmond, nikasema hawa walisaliti chama kwani tuliwatuma kutekeleza ilani ya chama wao wakaenda kutekeleza yao.

  5.) Nikajibu swala la kufukuzwa uana chama uvccm, nikasema MWENYE AKILI NAJUA NANI MKWELI NANI MWONGO kwani UJENZI MPAKA SASA UNAENDELEA BILA MKATABA, MAPUNGUFU NILIYOYAELEZA NDIYO YALIYOUNDIWA TUME KUREKEBISHWA, SASA MWONGO NA MKWELI IKO WAZI, lakini najua mtu mzima kukiri kosa ni ngumu...maji marefu hapa kwa mzee wangu....

  HAKIKA HATUKUMTAJA KABISA HUSSEIN BASHE KATIKA MAZUNGUMZO YOTE, SI MIMI, WALA OMARY KIMBAO AU JERRY SILAA NA HATA MTANGAZAJI KIBONDE, NIMESIKITISHWA NA TAARIFA HIZI KUZIKUTA HUKU, GAZETI LA TANZANIA DAIMA WALICHAPA PIA LAKINI KIMAKOSA, SIKUKANUSHA KULE COZ INGEATHIRI UCHAGUZI KWA UPANDE MMOJA NA HASA MGOMBEA MMOJA.

  Namwomba ndugu yangu asituharibie heshima ya forum hii, naamini nimeeleza kwa kifupi yaliyotokea.
  Nnauye Jr
   
 18. H

  Honey K JF-Expert Member

  #18
  Nov 25, 2008
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kingine nillichozungumza ni swala zima la kufungwa kwa vyuo vikuu nchini....nilisema naamini kinachopigiwa kelele sio SERA YA UCHANGIAJI YENYEWE bali ni UTEKELEZAJI WA SERA, hivyo sioni sababu ya serikali kutumia ubabe kufunga vyuo badala yake wakae chini na wadau kujadili namna bora ya kutekeleza sera hii. Najua kuwa iko katikati ya mwaka wa fedha wa serikali lakini muhimu kukubali kuwa yapo matatizo katika utekelezaji wa sera hii, ili njia bora itafutwe kisha tuwe na utekelezaji bora zaidi mwaka ujao wa fedha. Maghembe aache ubabe si jambo la buisara kila mara kufunga vyuo hivi maana tunaanzisha utamaduni mbovu wa kutojadiliana kumaliza matatizo yetu hili sio jema.....
   
 19. k

  kaujore New Member

  #19
  Nov 25, 2008
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnauye,
  unasubiri nini kujitoa sisiemu? chama kimeoza hicho.
   
 20. C

  Chuma JF-Expert Member

  #20
  Nov 26, 2008
  Joined: Dec 25, 2006
  Messages: 1,330
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  AJitoe then ajitoe upinzani arudi tena CCM...? Kama ameamua kupambana ndani ya CCM, let it be....
   
Loading...