Nape: Hakuna kukata rufaa mara mgombea atakapokatwa

Nape: Hakuna kukata rufaa mara mgombea atakapokatwa

Hakuzungumzia goli la mkono?

Hilo Goli lipo na Huyo huyo Nape ndiye kupewa kazi na Waganga wa Asili wa Membe ataingia na Hirizi kule kwenye mchujo ili kuhakikisha jina la membe linapenya hadi kupiga Goli la mkono , Mda huu membe yupo na waganga wake wanawashughurikia cc kwa speed ya kutisha.
 
Wagombea wote 40 wanataka wawe marais mwaka huu, haiwezekani wote wakatoka wamefurahi, wapo watakaotoka na vinyongo haswa wale ambao hawataingia ata 5 bora.

Ebu fikiria wazoefu hawa

1. Lowassa
2. Wasira yupo serikalini toka miaka ya 60
3. Samweli Sitta,yupo ndani ya serikali toka miaka ya 60
4. Prof Mwandosya
5.Magufuli-waziri kwa miaka 20 mfululizo-mwenye utendaji wa viwango
6. Billal-Makamu wa Rais miaka 5 na Waziri Kiongozi miaka 10
7. Pinda-Waziri Mkuu kwa miaka 8
8. Frederick SUmaye, waziri mkuu kwa miaka 10
9. Asha Rose Migiro,Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
10. Augustino Ramadhan -Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania
11. Dr Mwakyembe
12-42: List inaendelea..

Hivi wakikatwa7 miongoni mwa hawa, utalalamika?nani hapa ana uzoefu kuliko mwingine?hivi waziri mkuu kwa miaka miwili ana uzoefu kuliko Waziri Mkuu kwa miaka 10,au Waziri Mkuu kwa miaka 8?utasema waziri mkuu kwa miaka 2 ana uzoefu mkubwa kuliko waziri kwa miaka 15+Naibu katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kwa miaka 5?

Ni lazima miongoni mwao hawa watakatwa, na wakatwe tu maana hakuna namna nyingine haiwezekani wakapitishwa wote.Kumbuka wote hao ni wazee, lazima chama kionyeshe kuwa kinajali vijana pia, kwenye 5 bora lazima awepo kijana walau mmoja.

Sasa kwenye kuchuja kupata tano bora lazima chama kiangalie makundi maalum yaliyopo nchini.

1 Lazima kuwe na mwanamke-Asha Rose Migiro atapita

2. Lazima kuwe na Mzanzibar walau mmoja (Billal, Augustino Ramadhan au wote)

3. Waziri Mkuu aliyeko madarakani-lazima apitishwe 5 bora-Pinda

4. Dr John Pombe Magufuli

5. Ongeza mmoja kati ya hawa au mmoja wa 2..kumbuka kigezo cha ujana kuonyesha chama kinajali vijana

(a) Lowassa (b) Prof Mwandosya (c) Magufuli (d) Wasira (e) Membe (f) Sumaye (e) Sitta (f) na wengineo (g) Mwigulu (f) Makamba e.tc

Sasa ebu niambie kama kigezo mtu anajivunia ni uzoefu ebu niambie ni nani hapa anapaswa alalamike kwa kigezo cha uzoefu wake?Je ni Sumaye Waziri Mkuu mfululizo kwa miaka 10?je ni Waziri Mkuu wa miaka 2 Lowassa aliyetoka kwa kashfa?je ni Sitta aliyeko Serikali kutoka awamu ya kwanza?je ni Wassira aliyeko serikalini toka awamu ya kwanza na mtetezi mkubwa wa serikali kwa miaka 10 sasa?je Pro Mwandosya?

Utagundua hapa huwezi kupata sababu ya kulalamikia kwa kigezo cha uzoefu.

Mchanganuo wako ni sawa na mimi nikisema hivi:
utasema korea ina uzoefu kuliko tanzania wakati tumepata uhuru wakati unaofanana?
utasema marekani wana uzoefu kuliko tanzania wakati wote ni binadamu?

Mtu anaweza kufanya kazi miaka miwili akaleta Tija kuliko mtu aliyefanya kazi miaka 10. ila kwa hoja yako wewe unaangalia namba, na ni kweli 10>1
 
Baada ya polisi kutumika kupiga wapinzani,sasa kuna kila dalili ya polisi hao kuwageukia watu wa chama chao.

Hii itakuwa poa sana.
 
siwezikubishana na watu wasiojua siasa hujui kwenda na wakati yaani upo upo tu!nakushauri rudi shule ukasome
 
Baada ya polisi kutumika kupiga wapinzani,sasa kuna kila dalili ya polisi hao kuwageukia watu wa chama chao.

Hii itakuwa poa sana.

Safari hii Polisi watawapiga sana ccm Kwa ccm maana hata chaguo la Nape mwenyewe asipopita atajisikia vibaya .
 
Baada ya polisi kutumika kupiga wapinzani,sasa kuna kila dalili ya polisi hao kuwageukia watu wa chama chao.

Hii itakuwa poa sana.

Ni zamu yao sasa kupigwa nafikiri kauli ile ile ya wapigwe itatumika na huku pia..sio Ukawa peke yake
 
Ccm ni ya nape na makonda wakushirikiana na walafi wengine. Lowasa kitu gani bana
 
Dodoma.Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa wanachama wa chama hicho walioomba ridhaa ya chama kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya Urais iwapo majina yao yatakatwa.



Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa wagombea utakaoanza siku mbili zijazo.

Kikao hicho kitaongozwa na Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana pamoja na kikao cha sekretarieti ya chama.

Nape alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwasababu, kwanza hakuna kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.


“Tuwe wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni haisemi habari ya kukata rufaa…uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa sababu, sasa unakataje rufaa,” alisema Nape.

Hata hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa chama hicho kuwa watatoka kwa umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea urais kupitia chama hicho.

Aidha amebainisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea, kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi vimejipanga vya kutosha.

Kwa mujibu wa ratiba ya kikao,Kamati Kuu itakutana tarehe tisa na kutoa wagombea watano kabla ya Halmashauri Kuu kukutana tarehe 10mwezi huu, ambapo majina matatu ya wagombea yatateuliwa kabla ya kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu tarehe 11 ili kumpata mgombea mmoja atakaepeperusha bendera ya chama hicho.

My take;
Hizi ni salaam kwa mwana monduli na watu wake kisaikolojia,Lowassa kupita tano bora ni sawa na mji mkuu kuamia dodoma.

Kwa CCM ya leo Lowassa hana mpinzani, subirini
 
Nilishawaambia hawa mafisadi kuwa wajiandae kisaikolojia. Maumivu yanakuja
 
Ccm ni ya nape na makonda wakushirikiana na walafi wengine. Lowasa kitu gani bana

Ni kweli kabsa Nasikia hao Watu wamepewa Kazi maalum na Membe kuhakikisha kuwa Lowasa hapenyi kokote wameziba kona zote kuna Mseto wa waganga wa kienyeji membe kaamua Kufa na Lowasa kaweka mitego kote.
 
Back
Top Bottom