kwa akili yako fupi unadhan hatapita
utawajua October wakati wanahamia magogoni.Ukawa ndo nini....ni wauza viroba au mirungi tuweke sawa.
Onge wach jatelo..rit waneSiyo atapita tu,ni rais huyo ni suala la muda tu
Dodoma.Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa wanachama wa chama hicho walioomba ridhaa ya chama kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya Urais iwapo majina yao yatakatwa.
Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa wagombea utakaoanza siku mbili zijazo.
Kikao hicho kitaongozwa na Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana pamoja na kikao cha sekretarieti ya chama.
Nape alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwasababu, kwanza hakuna kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.
Tuwe wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni haisemi habari ya kukata rufaa uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa sababu, sasa unakataje rufaa, alisema Nape.
Hata hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa chama hicho kuwa watatoka kwa umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea urais kupitia chama hicho.
Aidha amebainisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea, kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi vimejipanga vya kutosha.
Kwa mujibu wa ratiba ya kikao,Kamati Kuu itakutana tarehe tisa na kutoa wagombea watano kabla ya Halmashauri Kuu kukutana tarehe 10mwezi huu, ambapo majina matatu ya wagombea yatateuliwa kabla ya kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu tarehe 11 ili kumpata mgombea mmoja atakaepeperusha bendera ya chama hicho.
My take;
Hizi ni salaam kwa mwana monduli na watu wake kisaikolojia,Lowassa kupita tano bora ni sawa na mji mkuu kuamia dodoma.
Tuonane keshokutwa hapa.Nitakukumbusha.
Yaangalie vizuri sana haya majina
1. Asha Rose Migiro
2. Mizengo Pinda
3. Billal au Augustino Ramadhan(walau mmoja wao)
4. John Pombe Magufuli
Shika sana haya majina
Mkuu akipita au asipopita wewe utapungukiwa na nini?Siyo atapita tu,ni rais huyo ni suala la muda tu
Sasa mkuu nikikureport kwa mode's upigwe ban ntakukosea?matusi ya nini sasa?
Mkuu unajiamini sana, unajua lakini kuwa ccm pesa mbele na kwao mkono mtupu haulambwi?
Ni ukweli usio fichika kwamba Lowasaa alisha wa aminisha watanzania kwamba yeye ndio rais ajaye,ni watu wachache sana tunao amini Kowassa hafai kuwa rais but always majority wins..hilo ndilo litaleta mpasuko pale itakavyo kuwa ndivyo sivyo.
Nguvu ya pesa ni kuanzia Halmashauri Kuu, kamati kuu na kamati ya maadili pesa hazikuokoi huko.
Ndivyo ilivyokuwa kwa Malecela na Horace Kolimba mwaka 1995 walipokuwa tayari wamemaliza kazi kuanzia NEC lakini wakaishia kabla na akaja kushinda Mkapa ambaye hakutuma pesa yoyote.Mwaka huu hilo linajirudia.
Nape hana ubavu kupambana na lowassa,huyu nape ni sawq na mwanamke ambaye hajakeketwa
Kwa hii hali kuwa na matumaini kuwa lowasa atapita ni ndoto za halinacha...hali mbaya sana kwa team lowasa wamemkamia sana wenye chama chao...na ndio wenye makali kwa sasa.
Pole sana kaka kwa kujiaminisha kuwa bila Lowassa kuwa rais Tanzania haipo..... Maana mnaamini Lowassa ndio kila kitu.