Nape: Hakuna kukata rufaa mara mgombea atakapokatwa

Nape: Hakuna kukata rufaa mara mgombea atakapokatwa

Wagombea wapo 40,watakatwa 35,ukiruhusu rufaa hivi rufaa za watu 35 utazishughulikia kwa siku ngapi?siku moja tatu hizo za vikao vyote zitatosha?common sense tu inaonyesha kuwa rufaa haitawezekana.Muda haupo.

Kwahiyo, watakaokatwa maumivu ni kimyakimya, una uhakika ccm watatoka wamoja kweri?
 
Jana tumeona hatua ya kwanza ya kuzuia wapambe wa jamaa wasije mjini na sasa hii ni hatua ya pili kwamba vyombo vyote vya usalama vishasogea front ..Lwasahaaaa didi yuuu geti mai mesejji? ..CCM kama gaucho vile ama JJ okocha. Leteni jina twende jamani ila kateni kwanza, kateni kabisa ili nchi yetu isipelekwe WTO badala yake kule tupeleke kahawa tu na korosho ..kama namuona mzee zungu a.k.a white na bi mkubwa Tiba
 
Ni kweli; Nape ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akiwakaribisha waandishi wa habari katika ukumbi mpya uliokamilika wa CCM wenye uwezo wa kuingiza watu 3000 wakiwa wameketi.

Nape aliulizwa kuwa kuna mtia nia mmoja ambaye ameshaona dalili za kukatwa na kamati kuu ya CCM huku yeye akiwa akubaliani na hilo hivyo kupewa mbinu kuwa ana uwezo wa kukata rufaa halmashauri kuu ambapo ana uhakika wa kupita.

Nape amesema kuwa ratiba inabana sana na hata
hivyo hakuna anayekatwa bila kuwepo sababu hivyo hamna haja ya kukata rufaa kwani ni kupoteza muda.
 
Jana tumeona hatua ya kwanza ya kuzuia wapambe wa jamaa wasije mjini na sasa hii ni hatua ya pili kwamba vyombo vyote vya usalama vishasogea front ..Lwasahaaaa didi yuuu geti mai mesejji? ..CCM kama gaucho vile ama JJ okocha. Leteni jina twende jamani ila kateni kwanza, kateni kabisa ili nchi yetu isipelekwe WTO badala yake kule tupeleke kahawa tu na korosho ..kama namuona mzee zungu a.k.a white na bi mkubwa Tiba

Itakua vipi Membe akikatwa na Lowasa kuwemo, Nape atakubali kweri?
 
Ni kweli; Nape ameyasema hayo leo wakati alipokuwa akiwakaribisha waandishi wa habari katika ukumbi mpya uliokamilika wa CCM wenye uwezo wa kuingiza watu 3000 wakiwa wameketi.

Nape aliulizwa kuwa kuna mtia nia mmoja ambaye ameshaona dalili za kukatwa na kamati kuu ya CCM huku yeye akiwa akubaliani na hilo hivyo kupewa mbinu kuwa ana uwezo wa kukata rufaa halmashauri kuu ambapo ana uhakika wa kupita.

Nape amesema kuwa ratiba inabana sana na hata
hivyo hakuna anayekatwa bila kuwepo sababu hivyo hamna haja ya kukata rufaa kwani ni kupoteza muda.

Vipi akikatwa Membe, Nape atavumilia?
 
Nape bana.....si anaruhusiwa kugombea 2025? Atasemaje hakuna rufa....

Hizi ni dalali kuna kuku mkubwa anachinjiwa dodoma...hahaha

Nashukuru Kwa Kuling'amua Hilo Na Kuweza Kusoma Alama Za Nyakati Mkuu Ni Mvivu Wa Kufikiri Atakayeshindwa Kulijua Fumbo Hilo La Nape.
 
Katibu uenezi Ccm Nape Nauye amesema leo kuwa hakuna nafasi ya kukuta rufaa mara mgombea akatwapo jina kwani katiba ya ccm haisemi hivyo. Ameendelea kusema kuwa maamuzi ya vikao vyote huwa hayahojiwi popote hivyo kutompa nafasi mgombea yeyote kukata rufaa. Vilevile amesema ccm watatoka wamoja baada ya vikao vya uteuzi na hakuna fujo itakayotokea kwani vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko teyari kukabiliana na rabsha yoyote itakayotokea.

ngoja tuone kati ya Nape na Low asa nani atakataa rufaa
 
Dodoma.Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa wanachama wa chama hicho walioomba ridhaa ya chama kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya Urais iwapo majina yao yatakatwa.



Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa wagombea utakaoanza siku mbili zijazo.

Kikao hicho kitaongozwa na Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana pamoja na kikao cha sekretarieti ya chama.

Nape alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwasababu, kwanza hakuna kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.


“Tuwe wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni haisemi habari ya kukata rufaa…uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa sababu, sasa unakataje rufaa,” alisema Nape.

Hata hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa chama hicho kuwa watatoka kwa umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea urais kupitia chama hicho.

Aidha amebainisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea, kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi vimejipanga vya kutosha.

Kwa mujibu wa ratiba ya kikao,Kamati Kuu itakutana tarehe tisa na kutoa wagombea watano kabla ya Halmashauri Kuu kukutana tarehe 10mwezi huu, ambapo majina matatu ya wagombea yatateuliwa kabla ya kupigiwa kura na wajumbe wa mkutano mkuu tarehe 11 ili kumpata mgombea mmoja atakaepeperusha bendera ya chama hicho.

My take;
Hizi ni salaam kwa mwana monduli na watu wake kisaikolojia,Lowassa kupita tano bora ni sawa na mji mkuu kuamia dodoma.
 
Kwahiyo, watakaokatwa maumivu ni kimyakimya, una uhakika ccm watatoka wamoja kweri?

Wagombea wote 40 wanataka wawe marais mwaka huu, haiwezekani wote wakatoka wamefurahi, wapo watakaotoka na vinyongo haswa wale ambao hawataingia ata 5 bora.

Ebu fikiria wazoefu hawa

1. Lowassa
2. Wasira yupo serikalini toka miaka ya 60
3. Samweli Sitta,yupo ndani ya serikali toka miaka ya 60
4. Prof Mwandosya
5.Magufuli-waziri kwa miaka 20 mfululizo-mwenye utendaji wa viwango
6. Billal-Makamu wa Rais miaka 5 na Waziri Kiongozi miaka 10
7. Pinda-Waziri Mkuu kwa miaka 8
8. Frederick SUmaye, waziri mkuu kwa miaka 10
9. Asha Rose Migiro,Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa
10. Augustino Ramadhan -Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania
11. Dr Mwakyembe
12-42: List inaendelea..

Hivi wakikatwa7 miongoni mwa hawa, utalalamika?nani hapa ana uzoefu kuliko mwingine?hivi waziri mkuu kwa miaka miwili ana uzoefu kuliko Waziri Mkuu kwa miaka 10,au Waziri Mkuu kwa miaka 8?utasema waziri mkuu kwa miaka 2 ana uzoefu mkubwa kuliko waziri kwa miaka 15+Naibu katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kwa miaka 5?

Ni lazima miongoni mwao hawa watakatwa, na wakatwe tu maana hakuna namna nyingine haiwezekani wakapitishwa wote.Kumbuka wote hao ni wazee, lazima chama kionyeshe kuwa kinajali vijana pia, kwenye 5 bora lazima awepo kijana walau mmoja.

Sasa kwenye kuchuja kupata tano bora lazima chama kiangalie makundi maalum yaliyopo nchini.

1 Lazima kuwe na mwanamke-Asha Rose Migiro atapita

2. Lazima kuwe na Mzanzibar walau mmoja (Billal, Augustino Ramadhan au wote)

3. Waziri Mkuu aliyeko madarakani-lazima apitishwe 5 bora-Pinda

4. Dr John Pombe Magufuli

5. Ongeza mmoja kati ya hawa au mmoja wa 2..kumbuka kigezo cha ujana kuonyesha chama kinajali vijana

(a) Lowassa (b) Prof Mwandosya (c) Magufuli (d) Wasira (e) Membe (f) Sumaye (e) Sitta (f) na wengineo (g) Mwigulu (f) Makamba e.tc

Sasa ebu niambie kama kigezo mtu anajivunia ni uzoefu ebu niambie ni nani hapa anapaswa alalamike kwa kigezo cha uzoefu wake?Je ni Sumaye Waziri Mkuu mfululizo kwa miaka 10?je ni Waziri Mkuu wa miaka 2 Lowassa aliyetoka kwa kashfa?je ni Sitta aliyeko Serikali kutoka awamu ya kwanza?je ni Wassira aliyeko serikalini toka awamu ya kwanza na mtetezi mkubwa wa serikali kwa miaka 10 sasa?je Pro Mwandosya?

Utagundua hapa huwezi kupata sababu ya kulalamikia kwa kigezo cha uzoefu.
 
Kwa kipindi hiki Nape anahasira na lowassa kuliko ukawa
Acha picha iendelee ukawa tunawasubiri tu waje ulingoni tuwatoe minundu tu
 
Kwanini Mpasuko Mkuu?

Ni ukweli usio fichika kwamba Lowasaa alisha wa aminisha watanzania kwamba yeye ndio rais ajaye,ni watu wachache sana tunao amini Kowassa hafai kuwa rais but always majority wins..hilo ndilo litaleta mpasuko pale itakavyo kuwa ndivyo sivyo.
 
Back
Top Bottom