Nape: Hakuna kukata rufaa mara mgombea atakapokatwa

Nape: Hakuna kukata rufaa mara mgombea atakapokatwa

gollocko

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
2,945
Reaction score
2,283
Katibu uenezi CCM bwana Nape Nnauye amesema leo kuwa hakuna nafasi ya kukuta rufaa mara mgombea akatwapo jina kwani katiba ya CCM haisemi hivyo.

Ameendelea kusema kuwa maamuzi ya vikao vyote huwa hayahojiwi popote hivyo kutompa nafasi mgombea yeyote kukata rufaa.

Vilevile amesema CCM watatoka wamoja baada ya vikao vya uteuzi na hakuna fujo itakayotokea kwani vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko teyari kukabiliana na rabsha yoyote itakayotokea.

Chanzo: Mwananchi Online
 
Katibu uenezi Ccm Nape Nauye amesema leo kuwa hakuna nafasi ya kukuta rufaa mara mgombea akatwapo jina kwani katiba ya ccm haisemi hivyo. Ameendelea kusema kuwa maamuzi ya vikao vyote huwa hayahojiwi popote hivyo kutompa nafasi mgombea yeyote kukata rufaa. Vilevile amesema ccm watatoka wamoja baada ya vikao vya uteuzi na hakuna fujo itakayotokea kwani vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko teyari kukabiliana na rabsha yoyote itakayotokea.
Bulaza wa goli mkono..! Weka source
 
Labada kuweka msisitizo tu. Lakini yote yako wazi na yanaeleweka.

Usalama ... hakuna wa kuutikisa.

Mambo ya rufaa yanatoka wapi. Tangu lini ufisadi ukakatiwa rufaa.
 
GAZETI LA MWANANCHI: Nape: Hakuna nafasi ya kukata rufaa majina yakikatwa - Kitaifa

Dodoma
.Chama cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwa wanachama wa chama hicho walioomba ridhaa ya chama kupeperusha bendera ya CCM katika nafasi ya Urais iwapo majina yao yatakatwa.

Kauli hiyo imetolewa mjini Dodoma leo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama hicho, Nape Nnauye alipokutana na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa ya ratiba ya vikao vya mchujo wa wagombea utakaoanza siku mbili zijazo.

Kikao hicho kitaongozwa na Katibu Mkuu CCM Abdulrahaman Kinana pamoja na kikao cha sekretarieti ya chama.

Nape alisema hakutakuwa na nafasi ya kukata rufaa kwasababu, kwanza hakuna kanuni hiyo na pia hakutakuwa na muda wa kutosha kufanya hivyo.

“Tuwe wakweli tu, muda wenyewe siuoni na kanuni haisemi habari ya kukata rufaa…uchujaji wa majini kikao hakitakiwi kutoa sababu, sasa unakataje rufaa,” alisema Nape.

Hata hivyo Nape amewapa matumaini wanachama wa chama hicho kuwa watatoka kwa umoja hata baada ya kupatikana kwa mgombea urais kupitia chama hicho.

Aidha amebainisha kuwa hakuna fujo zozote zitakazotokea, kwa kuwa vyombo vyote vya ulinzi vimejipanga vya kutosha
 
Kama hii ni taarifa rasmi kutoka kwa Nape, '' Nape kwanini huyo mtu uliyempania asipitishwe chama hakikuweka mchakato wa kumwondoa kwenye hatua za awali akashindwa kuchukua fomu? Sasa mmesubiri mpaka anakaribia kufunga goli mnataka kumkata buti na unaweka mazingira ya refa kutokutoa penalt. Huoni huo ni uonevu?
 
Ila nilimsikia Msekwa juzi clouds akisema huwa kuna nafasi ya rufaa na akamtolea mfano Malecela mwaka 2005 alikata rufaa akatos wa na halmashauri kuu
 
Katibu uenezi Ccm Nape Nauye amesema leo kuwa hakuna nafasi ya kukuta rufaa mara mgombea akatwapo jina kwani katiba ya ccm haisemi hivyo. Ameendelea kusema kuwa maamuzi ya vikao vyote huwa hayahojiwi popote hivyo kutompa nafasi mgombea yeyote kukata rufaa. Vilevile amesema ccm watatoka wamoja baada ya vikao vya uteuzi na hakuna fujo itakayotokea kwani vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko teyari kukabiliana na rabsha yoyote itakayotokea.

Izingatieni Sana Na Kwa Umakini Mkubwa Tena Uliotukuka Juu Ya Kauli au Maelezo Haya KUNTU Ya Nape Kwani Yameshaashiria Dhahama.
 
Nape ni kama msafisha vyoo vya stendi harufu za mikojo zinamlevya
 
Kama hii ni taarifa rasmi kutoka kwa Nape, '' Nape kwanini huyo mtu uliyempania asipitishwe chama hakikuweka mchakato wa kumwondoa kwenye hatua za awali akashindwa kuchukua fomu? Sasa mmesubiri mpaka anakaribia kufunga goli mnataka kumkata buti na unaweka mazingira ya refa kutokutoa penalt. Huoni huo ni uonevu?

Wamechelewa sana ..yaani EL kishaingia kwenye penati box kabaki yeye na kipa
 
Ila nilimsikia Msekwa juzi clouds akisema huwa kuna nafasi ya rufaa na akamtolea mfano Malecela mwaka 2005 alikata rufaa akatos wa na halmashauri kuu

Msekwa Ni Nani Katika Chama Sasa Kihadhi Na Kiutendaji Ukilinganisha Na Katibu Mwenezi Na Itikadi Wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Nape Nnauye? Mimi Nayaamini Ya Nape 100% Na Siyo Ya Huyo Mzee Aliyechoka Na Ambaye Hata Hivyo Amekaribishwa Tu Kwa Kazi Maalum Na Baada Ya Hapo Anajipumzikia Zake. Comrade Nape Hebu Tupe Raha Sisi Wapenda UZALENDO, HAKI, UADILIFU Na UKWELI Kwa Kutuchinjia Huyo FISADI Na Kutupa Mtu Makini Atakayefuata Nyayo Za Hayati Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Kambarahe Nyerere Na Nakuamini Kuwa Wewe Na Mangula Mtafanya MUWEZALO Mtuchinjie Huyo Mtu Huku Na Sisi Na Kamati Zetu Zile Za KITAMADUNI Tukimmaliza Mtu.
 
Huyo Nape mala nyingi ni Mzee wa Kubwabwaja tu bana hakatwi mtu hapa aisee hata iweje aiseeeeeee
 
Safari hii CCM kweli mmedhihirisha double standard na jinsi wakubwa walivyo na mtu wao kwenye briefcase kwani mmepiga hata marufuku wageni kuja Dodoma,swali wageni wa kawaida ni wapiga kura??!

Kwa nini Dodoma kumejaa vitisho,hila,ushenziushenzi na kuviziana??!!
 
Ila nilimsikia Msekwa juzi clouds akisema huwa kuna nafasi ya rufaa na akamtolea mfano Malecela mwaka 2005 alikata rufaa akatos wa na halmashauri kuu

Wagombea wapo 40,watakatwa 35,ukiruhusu rufaa hivi rufaa za watu 35 utazishughulikia kwa siku ngapi?siku moja tatu hizo za vikao vyote zitatosha?common sense tu inaonyesha kuwa rufaa haitawezekana.Muda haupo.
 
Msekwa Ni Nani Katika Chama Sasa Kihadhi Na Kiutendaji Ukilinganisha Na Katibu Mwenezi Na Itikadi Wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Nape Nnauye? Mimi Nayaamini Ya Nape 100% Na Siyo Ya Huyo Mzee Aliyechoka Na Ambaye Hata Hivyo Amekaribishwa Tu Kwa Kazi Maalum Na Baada Ya Hapo Anajipumzikia Zake. Comrade Nape Hebu Tupe Raha Sisi Wapenda UZALENDO, HAKI, UADILIFU Na UKWELI Kwa Kutuchinjia Huyo FISADI Na Kutupa Mtu Makini Atakayefuata Nyayo Za Hayati Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Kambarahe Nyerere Na Nakuamini Kuwa Wewe Na Mangula Mtafanya MUWEZALO Mtuchinjie Huyo Mtu Huku Na Sisi Na Kamati Zetu Zile Za KITAMADUNI Tukimmaliza Mtu.

Mkuu Msekwa ni makamu mwenyekiti, akitoka Kikwete anayefuatia ni Msekwa, Nape ni msemaji tu.
 
Nape bana.....si anaruhusiwa kugombea 2025? Atasemaje hakuna rufa....

Hizi ni dalali kuna kuku mkubwa anachinjiwa dodoma...hahaha
 
Tunamjua huyo...kateni jina tuwatie adabu...EL yupo na goli....kipa kaenda malikiti....EL akichukua nchi nepi tutamtandika bakora kariakoo mchana kweupee
 
Back
Top Bottom