Ndio kusema Pius Msekwa aliwadanganya wanaCCM kwa kusema kuwa mgombea atakayekatwa jina lake na kamati kuu anayo nafasi ya kukata rufaa katika Halmashauri kuu, na kusema hilo sio jambo jipya kwa kuwa kanuni na taratibu za CCM zinaruhusu hilo na kwenda mbele zaidi kwa kutoa mfano hai kuwa 2005 jina la Malecella lilipokatwa na Kamati kuu alikata rufaa ndani ya Halmashauri kuu na rufaa yake hiyo ikasilizwa although alishindwa.
Hawa UKAWA wanajipotezea muda wao kuota ndoto za siku moja kuja kushika dola, Ila huwa najiuliza hivi kule ukawa ni nani anafaa kutuongoza watanzania!!!Usiwe mjinga hakuna maarufu wa kuizidi ccm
Jumapili? Jumapili ni siku ya mkutano mkuu, ambapo wagombea watakuwa wanatoka 3 - 1, vikao vya kukata kata majina vinaanza Alhamisi, hapo mtashuhudia hao mnaowaita "waadilifu" wakienda na maji
CCM hii iliyotetea ESCROW!! leo iwatetee "waadilifu"? Makongoro anakumbuka kilichomtokea 2012, baada ya kujifanya Nyerere 2010 kwenye Mkutano wa NEC
Dhahma ipi tena kaka, na ameshasema vyombo vyote vya ulinzi na usalama viko makini?
hawa vijana sasa wataiuwa ccm mda sio mrefu,matusi wao,tabia mbaya wao,kutoshimu wakubwa wao ni wao pia,SIJUI NI NANI ANAYEWATUMA KUFANYA HAYA???
Msekwa Ni Nani Katika Chama Sasa Kihadhi Na Kiutendaji Ukilinganisha Na Katibu Mwenezi Na Itikadi Wa Chama Cha Mapinduzi CCM Ndugu Nape Nnauye? Mimi Nayaamini Ya Nape 100% Na Siyo Ya Huyo Mzee Aliyechoka Na Ambaye Hata Hivyo Amekaribishwa Tu Kwa Kazi Maalum Na Baada Ya Hapo Anajipumzikia Zake. Comrade Nape Hebu Tupe Raha Sisi Wapenda UZALENDO, HAKI, UADILIFU Na UKWELI Kwa Kutuchinjia Huyo FISADI Na Kutupa Mtu Makini Atakayefuata Nyayo Za Hayati Baba Wa Taifa Mwalimu Julius Kambarahe Nyerere Na Nakuamini Kuwa Wewe Na Mangula Mtafanya MUWEZALO Mtuchinjie Huyo Mtu Huku Na Sisi Na Kamati Zetu Zile Za KITAMADUNI Tukimmaliza Mtu.
Hahaha, huyu jamaa anakuwaga na mshawasha wa ajabu... Sasa demokrasia iko wapi? Wenyewe si wanakuwaga wanajisifu ni chama chenye demokrasia pana? Ushuzi mtupu!Nape anasumbua kama ng'ombe jike aliekuwa kwenye heat
Mkuu unajiamini sana, unajua lakini kuwa ccm pesa mbele na kwao mkono mtupu haulambwi?
ni wenye uwezo wa kufikiria kwa kina ndio wanaweza kutambuwa hili, rufaa ya watu 35 sio kitu cha kuweza kufanyika kwa siku moja
Kuna watu wanasema ana uzoefu kuliko wote,ndio logic yangu.
Ni kweli yawezekana mtu akafanya miaka michache kama ilivyokuwa kwa Sokoine lakin akawa na impact kubwa, lakini uzoefu huo wa Lowassa wa miaka miwili ndio uliishia na Richmond,hivyo miaka hiyo miwili ni ya aibu.Ndio maana huwezi kumlinganisha na Sumaye au Pinda ambao ni wazoefu kuliko yeye kwa kigezo hicho.