Nape-chadema wamekiuka katiba yao wenyewe!

Nape-chadema wamekiuka katiba yao wenyewe!

Hold on a minute; hii ni hoja ambayo hata mimi nimeitoa nyuma hata nilipotoa pendekezo la kuundwa Kanda za chama. Nilipendekeza kuwa Kanda ziundwe baada ya Mabadiliko ya Katiba ambayo yangeainisha mahusiano kati ya Kanda na Mikoa, Kanda na Taifa n.k. Lakini ni la muhimu kwa sababu Kanda zinatakiwa kuwa na madaraka na madaraka yanakuja kutoka kwenye Katiba.

Baraza Kuu ni kweli linaweza kuwa liliagiza kuundwa kwa Kanda lakini zikiwa na mamlaka gani? Uongozi wake unapatikana vipi? Kilichotokea kuwa baadhi ya viongozi wale wale wa kitaifa - wengine ni wabunge - wamekuwa tena viongozi wa Kanda ina defeat the whole pupose of relegating or delegating authority kwenda kwenye kanda.

Lakini kubwa zaidi ni kuwa CDM itajikuta kwenye matatizo litakapokuja suala la nidhamu (discipline); Je Kanda inaweza kusimaia nidhamu kwa viongozi wa mikoa na wilaya katika kanda hizo? Kanda zinapata wapi madaraka hayo? Madaraka hayaji kwa kuwa chombo kipo bali kwa kuanishwa mahsusi nini kinawezekana.

Nni kweli mfumo wa Kanda za CDM ni tishio kubwa zaidi la mfumo wa CCM kwani kwa wanaojua historia mara baada ya kuundwa kwa TANU kazi mojawapo ilikuwa ni kuunda Kanda za chama kwa hiyo mfumo huu si mgeni Tanzania ni CCM waliuacha. Ni mfumo unaokisogeza chama karibu zaidi na wananchi lakini siyo alama za chama tu bali pia uhuru na mamlaka ya chama.

Badala ya kumkejeli Nape kisiasa ni vizuri tujibu hoja yake kuhusu Mamlaka ya Kanda - uundwaji wake na utendaji kazi wake - yanapatikana wapi katika Katiba ya CHADEMA? Kwanini CDM na Baraza Kuu hawakufanyia maabdiliko katiba ili kuunda vyombo hivi vya kanda?

Sasa hoja hii wala haikutakiwa kutolewa na watu wa CCM kabisa; ilikuwa ni hoja iliyotakiwa kuibuliwa na wana CDM wenyewe.
 
Nape Moses Nnauye ni Katibu mwenezi Kivuli wa Chadema. Kazi hii anaifanya kwa weledi wa hali ya juu sana. Hongera kwa kujitolea kufanya kazi hii bila malipo.

Hapo umenena mkuu,
Na hii inafurahisha kwamba anafanyia kazi kampuni A lakini mshahara anapokea kampuni B. mfano kama kuna mtu alikuwa hajawahi kuisikia CDM inabidi amfahamishe ili aweze kuelewa anachokisema mwisho wa siku watu wanajawa na shauku ya kuwaona CHADEMA ni akina nani.Ongera nape kwa kazi nzuri.
 
Huyu Kinda, katiba ya CCM hata hajui inasema nini anarukia ya CHADEMA? Mitoto mingine bwana!

Hii ni kama kuoa/Kolewa na mke/mume ambae si chaguo lako mtu unabaki kumfuatilia hata kama hakuhusu!Katiba ya CHADEMA Nape anaitafuta ya nini?Nape ng'ooka CCM ubaki shujaa na sio mganga njaa a.k.a mchumia tumbo!!!
 
Hold on a minute; hii ni hoja ambayo hata mimi nimeitoa nyuma hata nilipotoa pendekezo la kuundwa Kanda za chama. Nilipendekeza kuwa Kanda ziundwe baada ya Mabadiliko ya Katiba ambayo yangeainisha mahusiano kati ya Kanda na Mikoa, Kanda na Taifa n.k. Lakini ni la muhimu kwa sababu Kanda zinatakiwa kuwa na madaraka na madaraka yanakuja kutoka kwenye Katiba.

Baraza Kuu ni kweli linaweza kuwa liliagiza kuundwa kwa Kanda lakini zikiwa na mamlaka gani? Uongozi wake unapatikana vipi? Kilichotokea kuwa baadhi ya viongozi wale wale wa kitaifa - wengine ni wabunge - wamekuwa tena viongozi wa Kanda ina defeat the whole pupose of relegating or delegating authority kwenda kwenye kanda.

Lakini kubwa zaidi ni kuwa CDM itajikuta kwenye matatizo litakapokuja suala la nidhamu (discipline); Je Kanda inaweza kusimaia nidhamu kwa viongozi wa mikoa na wilaya katika kanda hizo? Kanda zinapata wapi madaraka hayo? Madaraka hayaji kwa kuwa chombo kipo bali kwa kuanishwa mahsusi nini kinawezekana.

Nni kweli mfumo wa Kanda za CDM ni tishio kubwa zaidi la mfumo wa CCM kwani kwa wanaojua historia mara baada ya kuundwa kwa TANU kazi mojawapo ilikuwa ni kuunda Kanda za chama kwa hiyo mfumo huu si mgeni Tanzania ni CCM waliuacha. Ni mfumo unaokisogeza chama karibu zaidi na wananchi lakini siyo alama za chama tu bali pia uhuru na mamlaka ya chama.

Badala ya kumkejeli Nape kisiasa ni vizuri tujibu hoja yake kuhusu Mamlaka ya Kanda - uundwaji wake na utendaji kazi wake - yanapatikana wapi katika Katiba ya CHADEMA? Kwanini CDM na Baraza Kuu hawakufanyia maabdiliko katiba ili kuunda vyombo hivi vya kanda?

Sasa hoja hii wala haikutakiwa kutolewa na watu wa CCM kabisa; ilikuwa ni hoja iliyotakiwa kuibuliwa na wana CDM wenyewe.

ha ha sema wewe maana hao ma-chadema wenzako hawanaga akili ya kupambanua mambo na hapa watakushukia nawewe muda sio mrefu
 
"UANZISHWAJI WA KANDA ZA CHADEMA NI KINYUME NA KATIBA YAO,,
Kama Chadema wanaweza kukiuka katiba yao wenyewe wataweza vipi kuiheshimu katiba ya Nchi?"-Nape aliyasema haya alipokuwa akiwahutubia umati wa wakazi wa mji mdogo wa makambako jana,alisema anashangazwa na kitendo cha chadema kuanzisha kanda na viongozi wa kanda hizo kutolewa mfukoni kwa mwenyekiti wa chadema ndugu mbowe huku wakifahamu wazi kuwa huo ni ukiukwaji wa katiba yao,,!!!
nape anaweweseka sana, kwani ccm wanaheshimu katiba ya nchi?
 
Hili la kanda limewatisha na lita zidi kuwayeyusha kama bonge la barafu kwenye jua[/QUOTE]
moto wa hizi kanda umeshaanza kuwaunguza na sasa wameanza kuweweseka!!
 
Hakuna sehemu yoyote ndani ya katiba ya chadema inataja neno KANDA,,!!

Sawa ndugu mwenezi nakuona una vipaji vingi sana. Kipaji cha kuungaunga shule. Kipaji cha kuungaunga majina. Kipaji cha kuimba kwaya kanisani na kipaji kikubwa zaidi kuliko vyote ni hiki cha Multiple IDs za JF.
Ahsante kwa kuineza Chadema na uendelee na moyo huo huo japokuwa nakuomba uisome katiba yetu kwa umakini kidogo ili uielewe vizuri.
 
Haya Ndugu Nape itikadi ya CCM ya UJAMAA na KUJITEGEMEA mnaifuata? Je kutokana na hila za CCM mahakama ipo huru wakati wameteuliwa majaji wasio na sifa? Viongozi wa polisi wanaotuhumiwa kwa mauaji wamepongezwa na kupandishwa vyeo hiyo inamaanisha nini Ndugu Nape? Nakushauri Nape jikite kwenye kuhimiza utekelezaji wa ilani ya CCM ya 2010 maana muda umebaki mfupi, kuendelea na mambo nje ya hapo unazidi kujidhalilisha na kuiweka katika nafasi mbaya CCM.
 
"UANZISHWAJI WA KANDA ZA CHADEMA NI KINYUME NA KATIBA YAO,,
Kama Chadema wanaweza kukiuka katiba yao wenyewe wataweza vipi kuiheshimu katiba ya Nchi?"-Nape aliyasema haya alipokuwa akiwahutubia umati wa wakazi wa mji mdogo wa makambako jana,alisema anashangazwa na kitendo cha chadema kuanzisha kanda na viongozi wa kanda hizo kutolewa mfukoni kwa mwenyekiti wa chadema ndugu mbowe huku wakifahamu wazi kuwa huo ni ukiukwaji wa katiba yao,,!!!

Tumshukuru huyo ofisa mdogo wa uenezi nje ya CHADEMA. Maana yeye na Katibu Mkuu wake sasa wameamua kuitangaza CHADEMA kweli kweli. Wanatusaidia kupima pressure waliyonayo sasa na kudhihirisha kuwa wanajua kuwa muda wao wa kung'oka umeshawadia. Tuwashukuru kwa dhati.

Mlio karibu muulizeni, akimaliza kupayuka, sasa atulie atueleze ni kipengele au kifungu cha katiba kimekiukwa.

Na je, atuambie serikali ya chama chake imefikia hatu gani katika kutekeleza ilani ya CHADEMA juu ya katiba mpya?
 
Mbowe akubali ukweli kwamba katika hili la Kanda katiba imevunjwa na haya ni mapungufu makubwa kwa mwenyekiti wa chama,,!
 
Hivi CCM bado ni Chama cha WAKULIMA na WAFANYAKAZI kinachofuata SERA YA UJAMA NA KUJITEGEMEA?Ukijibu haya Nape utajua ni cahama gani kinachovunja katiba yake.
 
Nape sijui una akili kiasi gani. We ukiwa kati ya watendaji wakuu wa ccm unatakiwa kuwaeleza watanzania namna gani serikali inatatua matatizo lukuki yanayotukabili. Je baada ya kuwaeleza watu wa makambako huo ujumbe wako, matatizo yao yametatuliwa? Wamekuwa na matumaini zaidi na siku zijazo? Mbona unawapa Chadema kazi nyepesi sana ya kupangua hoja za CCM? Tatizo la CCM yetu nafasi nyeti za utendaji zinagawiwa kwa kujuana kuliko uwezo.
 
Katiba ya CCM imevunjwa sana na wao wenyewe lakini hawalioni hilo mfano mmoja wa waliyoyakiuka ni sura ya kwanza ibara ya 4 kipengere cha 3.
4. Chama Cha Mapinduzi kinaamini kwamba:
(1) Binadamu wote ni sawa.
(2) Kila mtu anastahili heshima ya kutambuliwa
na kuthaminiwa utu wake.
(3) Ujamaa na Kujitegemea ndiyo njia pekee ya
kujenga jamii ya watu walio sawa na huru.
J e bado wanaifuata?

Pia Sura ya kwanza ibara ya 5 kuhusu azimio la Arusha.
5. Kwa hiyo Malengo na Madhumuni ya CCM
yatakuwa yafuatayo:-
(1) Kushinda katika Uchaguzi wa Serikali Kuu
na Serikali za Mitaa Tanzania Bara na
Zanzibar ili kuunda na kushika Serikali Kuu
Katiba ya Chama Cha Mapinduzi
5
Jina la Chama
Makao Makuu
ya Chama
Bendera ya
CCM
Imani ya CCM
Malengo na
Madhumuni ya
CCM
na Serikali za Mitaa katika Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa upande
mmoja na Zanzibar kwa upande wa pili.
(2) Kulinda na kudumisha Uhuru wa Nchi yetu
na raia wake.
(3) Kuhimiza ujenzi wa Ujamaa na Kujitegemea
kwa mujibu wa Azimio la Arusha.
(4) Kusimamia utekelezaji wa Siasa ya CCM
pamoja na kuendeleza fikra za viongozi
waasisi wa vyama vya TANU na ASP, kama
zilivyofafanuliwa katika maandiko mbali
mbali ya Vyama hivyo.
(5) Kuona kwamba kila mtu anayo haki ya
kupata kutoka katika Jamii hifadhi ya maisha
yake na mali yake kwa mujibu wa sheria.
(6)

Hawa wanawadanganya wasiojua.

Unaweza ukaisoma http://ccmuk.org/files/Katibaccm.pdf http://www.ccm.or.tz/images/upload/katiba.pdf (Toleo la 2010)
 
Back
Top Bottom