Nape-chadema wamekiuka katiba yao wenyewe!

ray jay

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2011
Posts
1,084
Reaction score
485
"UANZISHWAJI WA KANDA ZA CHADEMA NI KINYUME NA KATIBA YAO,,
Kama Chadema wanaweza kukiuka katiba yao wenyewe wataweza vipi kuiheshimu katiba ya Nchi?"-Nape aliyasema haya alipokuwa akiwahutubia umati wa wakazi wa mji mdogo wa makambako jana,alisema anashangazwa na kitendo cha chadema kuanzisha kanda na viongozi wa kanda hizo kutolewa mfukoni kwa mwenyekiti wa chadema ndugu mbowe huku wakifahamu wazi kuwa huo ni ukiukwaji wa katiba yao,,!!!
 
Nape! Si uhamie CHADEMA? Mbona kila siku umejikita kuihubiri CHADEMA badala ya CCM yetu? Kazi tuliyo kupa ni kuipigia praganda CCM ila inaonyesha una mapenzi makubwa na CHADEMA. Kwa vile umeonyesha mapenzi makubwa sana kwa CHADEMA kiasi kwamba kila siku unapo pata nafasi ya kuzungumza na waTanganyika ni kuitaja taja CHADEMA ni vyema ukachukua uamuzi wa kuhamia huko. Sio kila siku kubwabwanya habari za CHADEMA huku ukiamini kwamba unakibomoa kumbe unakijenga CHADEMA.

Tuachie CCM yetu maana tunajua wewe ni mmoja wa waasisi wa CCJ.
 
Hili la kanda limewatisha na lita zidi kuwayeyusha kama bonge la barafu kwenye jua! Wameozoea kuona chadema makao makuu wakifanya kila kitu na kuwapangia mbinu chafu kupitia kile chombo chao walicho shauriwa na mkuu wao kuwa "...Na nyie muache kutegemea polisi..."

Kwa sasa kanda zinajiendesha zenyewe kwa ufanisi na zimeshusha zaidi mamlaka ya chama kwa wanachama kwenye ngazi za msingi.

Nape akae atulie sindano ziingie, alikuwa mstari wa mbele kusema chadema ni chama cha kikanda! Leo povu linamtoka anaziongelea kanda kuwa zimetoka mfukoni kwa mwenyekiti! Huku ni kuweweseka na hakuhitaji shahada ya chuo kikuu kuona kuwa mtoto wa kiume ana lia huku kang'ata kidole akiugulia maumivu.
 
Utaratibu wa chadema wa kanda unawatesa sana kina nape na ccm kwa ujumla.

Sent from my BlackBerry 9700 using JamiiForums
 
Curiously, Mohamed Mtoi. Mbona sioni harakati za maana za viongozi wa kanda, namsikia zitto na tabora yake pamoja na mabere marando viongozi wa kanda nyingine vipi? Unaweza ukatumia fursa hii kutuhabarisha ni nani ni viongozi wakuu wa kila kanda.
 
Hili la kanda limewatisha na lita zidi kuwayeyusha kama bonge la barafu kwenye jua! Wameozoea kuona chadema makao makuu wakifanya kila kitu na kuwapangia mbinu chafu kupitia kile chombo chao walicho shauriwa na mkuu wao kuwa "...Na nyie muache kutegemea polisi..."

Kwa sasa kanda zinajiendesha zenyewe kwa ufanisi na zimeshusha zaidi mamlaka ya chama kwa wanachama kwenye ngazi za msingi.

Nape akae atulie sindano ziingie, alikuwa mstari wa mbele kusema chadema ni chama cha kikanda! Leo povu linamtoka anaziongelea kanda kuwa zimetoka mfukoni kwa mwenyekiti! Huku ni kuweweseka na hakuhitaji shahada ya chuo kikuu kuona kuwa mtoto wa kiume ana lia huku kang'ata kidole akiugulia maumivu.

Mkuu umemaliza. Sirudi tena kwenye hii thread. Asante sana
 
Naomba huyo mropokaji wa Magamba arejee yafuatayo; Katiba ya Chadema toleo la mwaka 2006, Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama, Miongozo kutoka ofisi ya Katibu Mkuu kwa mujibu wa Kanuni. Mamlaka ya Baraza Kuu ya kutunga Kanuni na Miongozo mbalimbali (ukiwemo mpango wa Kanda) na utaratibu wa uchaguzi. Atuambie jambo gani limekiuka Katiba? sio kutoa lugha nyepesi na za kitoto, huo usemaji wa chama?
 
Bwana NAPE wewe ni mtaalamu wa vyama vingapi? Tuliambiwa na kauli ya Mwenyekiti wako wa CCM kwamba wewe na Sitta ndo mlianzisha CCJ mkamwacha mwenzenu kwenye mataa, na sasa naona tena unanyemelea mambo ya CHADEMA.

Je CCM imevunja Katiba mara ngapi?
1. Kuwaambia wezi wa EPA warudishe fedha bila kuchukuliwa hatua si
kuvunja Katika?
2. Kutumia Jeshi la wananchi JWTZ kutuliza ghasia DSM, na sasa Mtwara si
kuvunja Katiba?
3. Kuingia Mikataba ya kifisadi na raslimali za asli kutowanufaisha
watanzania si kuvunja Katiba?
4. Kuua Tembo wetu na watuhumiwa kuendelea kutumia raslimali za
wanyonge si kuvunja Katiba?
5. Vyombo vya dola kushindwa kuwakamata watuhumiwa wa kuteka watu
maarufu kama Dr. Ulimboka na Kibanda si kuvunja Katiba ?
6. Polisi kuwaua wanahabari kama Mwangosi hadharani na Mtuhumiwa
aliyesimamia mauaji hayo si kuvunja Katiba?
7. Kuingilia utaratibu wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya Katiba mpya
na CCMkuhakikisha mnapata wajumbe wengi si kuvunja Katiba?

BWANA NAPE WEWE CHUKUA CHAKO MAPEMA NADHANI DALILI ZA ANGUKO LENU KWA SASA NI DHAHIRI. Mojawapo ninazoweza kukupa kwa sasa ni
a) Matumizi makubwa ya nguvu na kutumia vyombo vya dola kwa usirisiri
b) Kukosa ushawishi na matumizi makubwa ya rushwa ili kuchaguliwa
c) Migawanyiko ndani ya CCM na makundi hayo hata mwende kwa waganga hayawezi kumalizika
d) Ni vitendo vya kujisifia ninyi wenyewe kuwa mmefanya maendeleo makubwa wakati sifa hizo mngesifiwa na watu wengine.
e) Hotuba za watawala kujaa lawama kwa wapinzani wenu ambao hawana hazina, wala vyombo vya dola.
f) Kufanya juhudi za makusudi kutumia hata Bunge kupindisha ukweli na kugandamiza demokrasia
g) Kushindwa kutekeleza ajenda zenu kuu kwenye ilani na kudandia ahadi za watu wengine kama ya Katiba mpya na sasa nasikia mnaongelea elimu bure na ujenzi wa reli ya kati
h) Kuwapa nafasi kubwa wafanya biashara kuwa sehemu ya viongozi wa umma na matokeo yake unaona Bunge linakuwa tupu jamaa wako kwenye biashara zao.

TAFAKARI
 
"UANZISHWAJI WA KANDA ZA CHADEMA NI KINYUME NA KATIBA YAO,,
Kama Chadema wanaweza kukiuka katiba yao wenyewe wataweza vipi kuiheshimu katiba ya Nchi?"-Nape aliyasema haya alipokuwa akiwahutubia umati wa wakazi wa mji mdogo wa makambako jana,alisema anashangazwa na kitendo cha chadema kuanzisha kanda na viongozi wa kanda hizo kutolewa mfukoni kwa mwenyekiti wa chadema ndugu mbowe huku wakifahamu wazi kuwa huo ni ukiukwaji wa katiba yao,,!!!

aisifiaye mvua imemnyea......
 
Siku hizi JJ Mnyika ana wasaidizi wengi mpaka akina Nape, mtu ambaye anatoa kauli kwa kutumia tumbo na sio fikra na hoja za msingi. Aje atuambie ni ibara gani imekiukwa na ni viongozi wangapi na akina nani wametoka mfukoni kwa Mwenyekiti
 
Je alishawaona wataalamu wa vinasaba kumwezesha kumpata biological dad wake? Au ziarani huko ndo anatafuta ukoo wake wa kiukweli. Ipo shida kubwa sana kwa watoto tunaolelewa na single parents. Pengine tusimlaumu sana ndugu yetu.....
 
Bwana NAPE wewe ni mtaalamu wa vyama vingapi? Tuliambiwa na kauli ya Mwenyekiti wako wa CCM kwamba wewe na Sitta ndo mlianzisha CCJ mkamwacha mwenzenu kwenye mataa, na sasa naona tena unanyemelea mambo ya CHADEMA.

Je CCM imevunja Katiba mara ngapi?
1. Kuwaambia wezi wa EPA warudishe fedha bila kuchukuliwa hatua si
kuvunja Katika?
2. Kutumia Jeshi la wananchi JWTZ kutuliza ghasia DSM, na sasa Mtwara si
kuvunja Katiba?
3. Kuingia Mikataba ya kifisadi na raslimali za asli kutowanufaisha
watanzania si kuvunja Katiba?
4. Kuua Tembo wetu na watuhumiwa kuendelea kutumia raslimali za
wanyonge si kuvunja Katiba?
5. Vyombo vya dola kushindwa kuwakamata watuhumiwa wa kuteka watu
maarufu kama Dr. Ulimboka na Kibanda si kuvunja Katiba ?
6. Polisi kuwaua wanahabari kama Mwangosi hadharani na Mtuhumiwa
aliyesimamia mauaji hayo si kuvunja Katiba?
7. Kuingilia utaratibu wa kuwapata wajumbe wa mabaraza ya Katiba mpya
na CCMkuhakikisha mnapata wajumbe wengi si kuvunja Katiba?

BWANA NAPE WEWE CHUKUA CHAKO MAPEMA NADHANI DALILI ZA ANGUKO LENU KWA SASA NI DHAHIRI. Mojawapo ninazoweza kukupa kwa sasa ni
a) Matumizi makubwa ya nguvu na kutumia vyombo vya dola kwa usirisiri
b) Kukosa ushawishi na matumizi makubwa ya rushwa ili kuchaguliwa
c) Migawanyiko ndani ya CCM na makundi hayo hata mwende kwa waganga hayawezi kumalizika
d) Ni vitendo vya kujisifia ninyi wenyewe kuwa mmefanya maendeleo makubwa wakati sifa hizo mngesifiwa na watu wengine.
e) Hotuba za watawala kujaa lawama kwa wapinzani wenu ambao hawana hazina, wala vyombo vya dola.
f) Kufanya juhudi za makusudi kutumia hata Bunge kupindisha ukweli na kugandamiza demokrasia
g) Kushindwa kutekeleza ajenda zenu kuu kwenye ilani na kudandia ahadi za watu wengine kama ya Katiba mpya na sasa nasikia mnaongelea elimu bure na ujenzi wa reli ya kati
h) Kuwapa nafasi kubwa wafanya biashara kuwa sehemu ya viongozi wa umma na matokeo yake unaona Bunge linakuwa tupu jamaa wako kwenye biashara zao.

TAFAKARI

Hii sio size ya NAPE hata kidogo, ingekuwa vyema zaidi kama ingemfikia Mwenyekiti wao ili aitafutie mtu stahili wa kuifanyia kazi.
 
nape ni kiliza wa ajabu...kila kukicha anakuwa msemaji wa chadema.....hawa ndio aina ya viongozi waandamiz wa ccm. mm nlizani ataeleza namna ya kudhibi ujangili, utoroshwaji wa wanyama,mauwaji kwa raia na mambo mengine mengi.lakini kila kukicha yeye na chadema tu..kama sio upuuzi ni nini?
 
Nape kawa mtetezi wa katiba ya CHADEMA!
Haya ni maajabu nayo.
 
Nape Moses Nnauye ni Katibu mwenezi Kivuli wa Chadema. Kazi hii anaifanya kwa weledi wa hali ya juu sana. Hongera kwa kujitolea kufanya kazi hii bila malipo.
 
Juzi nakumbuka niliwapa maelekezo yeye Nape na mwenzie KINANA(A.K.A NDOVU) nini cha kuzungumza katika ziara yao ili anainchi wawaelewe vizuri na waichukie CHADEMA nilisema waseme haya

By ebaeban katika ziala yenu ya majukwaani mkoa wa njombe pambaneni na chadema kisayansi bahati nzuri mtakutana na mwenzenu mzoefu deo filikunjombe, kamwe msiitete serikali kama inakosea na wala mda mwingi msiutumie kuitaja taja chadema. Waelezeni wanainchi maana ya:

  1. maisha bora kwa kila mtanzania sera hii ya ccm ni nzuri sana ikitekelezwa ipasavyo ila chama kinakwamishwa na watumishi wasiowaaminifu wa halimashauri zipatazo 136, maana wanakwiba hela zote zinazotumwa katika halimashauri zao ili kutekeleza miradi ya maendeleo, hii ni fursa nzuri kwenu(kinana, nape ) kuwasisitiza madiwani wasimamie vizuri hela za miradi, waambieni madiwani wawaangalie sana watendaji na wahoji hizo nyumba na magari wanayonunua.
  2. pia ni fursa kwenu kuwaambia wanainchi jinsi serikali yao inavyoshghurika na kudhibiti mfumko wa bei kwani nao ni kikwzo katika utekelezaji wa sera ya maisha bora kwa kila mtanzania
  3. kwamwe msijihusishe na matusi hasa wewe nape mambo yako ya kusema eti chadema ni nguruwe kamwe wanainchi hawawezi kukuelewa na ndo utalikoroga kabisaaaa
  4. pia waelezeni wanainchi jinsi serikali yao inavyojishughulisha na kupiga vita masuala ya rushwa ambayo imeshamili kiasi taasisi nzima kama bunge linahongwa.

mwisho waelezeni wanainchi namana serikali yao inavyoshughurika na wale wanaofuja raslimali ya taifa kama majangili wanaouwa tembo na kusafirisha vipusa, masuala ya kusaini mikataba mibovu ya kinyonyaji na wale wanaotorosha hela na kuweka banki za inje wote hawa wanakwamisha utekelezaji wa sera ya maisha bora kwa kila mtu.

Mukisema yote haya majukwaani bila matusi hakika chadema kwisha na tegemeeni kuvuna kadi nyingi sana toka upinzani,

nawatakia kazi njema

ebaeban
Tel.Aviv
Kwa nini hawasikii?
tel.aviv.
 
"UANZISHWAJI WA KANDA ZA CHADEMA NI KINYUME NA KATIBA YAO,,
Kama Chadema wanaweza kukiuka katiba yao wenyewe wataweza vipi kuiheshimu katiba ya Nchi?"-Nape aliyasema haya alipokuwa akiwahutubia umati wa wakazi wa mji mdogo wa makambako jana,alisema anashangazwa na kitendo cha chadema kuanzisha kanda na viongozi wa kanda hizo kutolewa mfukoni kwa mwenyekiti wa chadema ndugu mbowe huku wakifahamu wazi kuwa huo ni ukiukwaji wa katiba yao,,!!!

Administrators do right things right (Only law) but Leaders do things right (Law and Situation).
Tafakari!!!!!!
 
Hili la kanda limewatisha na lita zidi kuwayeyusha kama bonge la barafu kwenye jua! Wameozoea kuona chadema makao makuu wakifanya kila kitu na kuwapangia mbinu chafu kupitia kile chombo chao walicho shauriwa na mkuu wao kuwa "...Na nyie muache kutegemea polisi..."

Kwa sasa kanda zinajiendesha zenyewe kwa ufanisi na zimeshusha zaidi mamlaka ya chama kwa wanachama kwenye ngazi za msingi.

Nape akae atulie sindano ziingie, alikuwa mstari wa mbele kusema chadema ni chama cha kikanda! Leo povu linamtoka anaziongelea kanda kuwa zimetoka mfukoni kwa mwenyekiti! Huku ni kuweweseka na hakuhitaji shahada ya chuo kikuu kuona kuwa mtoto wa kiume ana lia huku kang'ata kidole akiugulia maumivu.

Mngoshi Mtoi!

Mosie!

Una matata sana iwe!!!! Ne utatoa mwe magutwi du!
 
Back
Top Bottom