Nape: CHADEMA wajiandae kuingia msituni

Nape: CHADEMA wajiandae kuingia msituni

Fnayeni mpango mkisajili na wawezeshwe kuwa na silaha ili ulinzi uimarishwe zaidi kwa viongozi wenu.
 
.....Nilisikia Nape siyo mtoto wa mzee Nnauye ndo maana hajatajwa hapo juu. Eti wanadai Nape ni mtoto wa nanihii, Mzee Nnauye alisakiziwa tu!!.
Kwenye hayo maelezo Nape anaangukia kwenye kundi la jamaa na marafiki angekuwa ni mtoto wake angetajwa miongoni mwa wenzake. Msimlazimishe mtu kuwa mkiwa wakati babaye yupo
 
KATIBU wa Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye amerusha kombora kwa Chama cha Demokrasia na Maendekeo (CHADEMA) akidai makundi ya vijana wa ulinzi vya chama hicho (Red Brigade) yameandaliwa kwa ajili ya kuingia msituni kwa shughuli za ugaidi. Kauli hiyo aliitoa juzi wilayani Mpwapwa kwenye ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, inayoendelea mkoani Dodoma.

"CHADEMA wanaandaa vijana kupitia Red Brigade ili kuingia msituni na kuchukua madaraka ya nchi kwa mabavu. Wanafanya hivyo kwa sabababu wanajua hawawezi kuchaguliwa kwa njia ya kura wakati wa uchaguzi mkuu," alisema Nape na kuongeza: "Hawa wanaopiga kelele huko mitaani eti Red Brigade wanaandaliwa kwa ajili ya kulinda kura, naomba niwaulize hizo kura wanazotaka kulinda nani atawapigia? Hata hizo kura za kuiba zitatoka wapi," alisema.

Nape alidai kwamba tayari CCM wamepata taarifa nyeti za mpango ovu unaoandaliwa na CHADEMA kuelekea kwenye Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu kwamba kuna mpango wa kuwatumia vijana wa Red Brigade.

"Taarifa tulinazo ni kwamba Red Brigade ni vikosi vinavyoandaliwa kwa ajili ya vitendo vya ugaidi na shughuli nyingine za ovyo. Taarifa ni kwamba hili ni kundi la kigaidi, wataanzishaje kundi la usalama wakati tunavyo vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi yetu?" alihoji Nape.

Nape alikituhumu pia chama hicho kwa kujihusisha na vitendo vya kuvunja amani katika matukio mbalimbali nchini ikiwamo yale yaliyotokea kwenye uchaguzi mdogo wa Igunga na maeneo mengine kama Morogoro na kusababisha kuuawa kwa kijana muuza magazeti.
Mkuu Invisible tusaidie ku-attach hii habari hapo juu kwenye uzi huu.

CC: Moderator
 
Last edited by a moderator:
Akiongea leo mkoani Dodoma katika mkutano wa hadhara,katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,bwana Nape Nnauye , amekielezea kikundi cha Red Brigade kama kikundi cha kigaidi kinachoweza kuvunja amani ya nchi na kuwataka wananchi kuwa macho na vikundi vya aina hiyo.

CHANZO:ITV

My take;
Hivi kati ya Red Brigade na watuhumiwa wa Escrow,nani anahatarisha amani ya nchi hii?!

Aliyetangaza hadharani kuwa kama katiba ya Warioba ingepita atakuwa wa kwanza kwenda msituni hakuwa mwananchama wa CHADEMA. Unfortunately, ametangulia huko ingawa sijui ni msituni au la! Na Nape anayedai kuwa Red Brigade imeandaliwa kuingia msituni kufanya mambo ya kigaidi ni unafiki kwa sababu yeye Nape alikuwa ni mmoja wa wale waliomsindikiza (less than 2 weeks ago) tena kwa nyimbo yule aliyejitangaza publicly (ndani ya Bunge) kuwa atatangulia msituni. Unafiki wa Nape ni kuwa anajua kabisa huyo jamaa aliyejitangaza publicly kuwa angetangulia msituni hakuwa one of the Red Brigade members. Huku ni kujitoa ufahamu kwa uzuzu tu.
 
Vikundi vyote vipigwe marufuku iwe green, red, au kile cha cuf (sijui kinaitwaje), vyote hivi ni vikundi vya kigaidi ambavyo vitatugharimu sana hapo baadaye! Sasa ukiangalia hao red brigade ni kama magaidi fulani hivi, makoti meusi, miwani mieusi na makofia meusi sasa hiyo ndo nini? Hapo CHADEMA tumekurupuka, hatukutafuta ushauri mzuri! Kwani kungekuwa na ubaya gani kama wangevaa magwanda tu au T-shirt za M4C? Tukubali kubadilika bwana! Hizo sura hazinivutii kabisa!!

Kama majambazi wa kwenye bongo movie.
 
Kumbe FUTUHI huwa wanamuigiza yeye, mzee wa kukurupuka

Ha ha haaa. Hii kiboko. Lakini wakati mwingine Nape naye awe anakuwa makini kwenye kauli zake. Mbona viongozi wengine wana-consult ubongo kabla ya kiongea? Ina maana alisahau Green Guards na yule kamanda wao anayevaa mavazi ya jeshi la China? Nape kwa kweli hakitendei chama chake haki.
 
mbona jina halionekani hapa

attachment.php

Huyu ni mwanaharamu.
 
Hivi ukimsiliza Nape huwezi kupata hata neno moja zaid ya pumba inaonesha aliko hakuna washauri wa kumshauri maana kila kukicha yeye na pumba. Ni kubwabwaja tu hakuna hoja yeye akisimama asipokisema Chadema hajisikii au Cuf Kilaza ni Kilaza tu
 
Nimesoma yote yalio andikwa nime baki na ???????????????????????????? paka nimechoka tonapo enda sijuwi ni digitali or What
 
Kwanza atueleze lile Jengo jipa la UVCCM ni ufisadi wa Lowassa ama upofu wa CCM. Kelele alizopiga bado anazisimamia? Tume ya Andrew Chenge Makengeza ilishatoa ripoti ama bado? Gamba CCM limeshavulika ama bado? Akishajibu haya, aende "kwao" Iramba Magharibi kwa Lameki Madelu ili ajiandae kugombea Ubunge, labda huko ataambulia kura. Ubungo ASAHAU!
 
Akiongea leo mkoani Dodoma katika mkutano wa hadhara,katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM,bwana Nape Nnauye , amekielezea kikundi cha Red Brigade kama kikundi cha kigaidi kinachoweza kuvunja amani ya nchi na kuwataka wananchi kuwa macho na vikundi vya aina hiyo.

CHANZO:ITV

My take;
Hivi kati ya Red Brigade na watuhumiwa wa Escrow,nani anahatarisha amani ya nchi hii?!

sijapata kuona mwenez plain brain kama nape,propaganda ijengee hoja bt jamaa linalopoka tu,hata mwenyekit wake aliwaikir kuwa jamaa mropokaji,women exposively arque by perception!!huyu bwana anadeserve kua kwenye hilo kundi.
 
Nape yule angefaa kuwa muimbaji wa taarabu
 
“CHADEMA wanaandaa vijana kupitia Red Brigade ili kuingia msituni na kuchukua madaraka ya nchi kwa mabavu. Wanafanya hivyo kwa sabababu wanajua hawawezi kuchaguliwa kwa njia ya kura wakati wa uchaguzi mkuu,” alisema Nape na kuongeza: “Hawa wanaopiga kelele huko mitaani eti Red Brigade wanaandaliwa kwa ajili ya kulinda kura, naomba niwaulize hizo kura wanazotaka kulinda nani atawapigia? Hata hizo kura za kuiba zitatoka wapi,” alisema.

Juzi tu ilikuwa 39 kwa 5
Bado anauliza nani atachagua upinzani
 
Mi sijaelewa mirathi inasemaje!ktk mali alizoacha marehemu kaputeni jonii komba hili la kuingia msituni aliwapa chadema ???Aliandika kwenye mirathi au ni mambo ya kusikia?
CC. salary slip,mkirua,Bak,boss,meandu et al
 
Hivi kwa nini jina la nape halipo kwenye picha ya kumbukumbu?nijulishwe wadau?
 
Mara nyingi maneno yake yasiyo na hoja huwa anaangalia pa kuyatoa na huwa atoi nafasi ya kuulizwa maswali. Ila I.T.V nayo ijiandae kisaikolojia kwa namna ya uchambuzi wa habari zao kuna AZAM
 
Yaani Nape ndio anawaweka busy ?kichaa akikukuta mtoni unaoga akachukua mavazi yako na ww ukamkimbiza wewe ndio utakuwa kichaa. Nape ni reject kama hamuamini agombee hata mtaa au kijiji akiahinda nahama nchi..
 
Kati ya huo upuuzi alioongea kipi ni Sera ya chama chake ni kipi kinaleta maendeleo kwa wananchi? Anateketeza pesa uma kuzunguka nchi mzima kutishia maisha watanzania.
 
Back
Top Bottom