Matamko ya wansiasa kama haya ni hatari zaidi kuliko hata ugaidi wenyewe. hii ni kwa sababu yanochochea hofu, chuki na hata ugaidi.
Kiongozi mkubwa wa chama kikubwa kinachotawala anatakiwa kupeleka taarifa na ushahidi kwenye vyombo vya usalama ili wahalifu wakamatwe. kesho chadema nao watakuja kwa namna hiyohiyo na kufanya hatari izidi.
Vyombo vya habari viende mbali zaidi ya kutoa habari vibainishe waziwazi kwa wanachi athari za matamko ya wanasiasa wote bila kujali chama.
Je, taarifa za kipolisi kuhusu hili zinasemaje na je, polisi wanaweza kumtaka Nape aende kituoni kutoa maelezo? maana maana matamshi yake yanaelezea kuwepo kwa uasi au maandalizi yake.