Nape Nnauye: Rais Samia amefuta ada kuanzia awali mpaka kidato cha 6. Mlioguswa nendeni mtandaoni mkaseme 'Tunasimama na Samia'

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
121,947
95,237
Anasema kipindi kilichopita kilikuwa na kikundi kinaitwa task force.

TRA walikuwa wanafunga account za wafanyabiashara kwa kisingizio cha kukusanya kodi kwa kutumia Task force hivyo kufilisi wafanyabiashara.

Ila kwa utawala wa mama yetu hilo jambo limekomeshwa.

Hakika nimeamini kuwa kila masika ina mbu wake.

Nape Nnauye amesema kuwa huko nyuma kulikuwa na wafanyabiashara ambao waliteseka kwa kufungiwa akaunti zao na kikosi kazi cha TRA. Sasa hivi wafanyabiashara chini ya utawala wa Rais Samia mambo yao yanakwenda sawasawa.

Nape ameongeza kuwa wafanyabiashara ambao wameguswa na jambo hilo waende mtandaoni wakaandike mema ambayo wanadhani Rais Samia amewagusa na waandike Hashtag ya #TunasimamaNaSamia

Ameongeza kuwa huko nyuma tulikuwa yunakimbizana kuchangishana pesa za kujenga madarasa, lakini sasa hivi Mama Samia ameleta hela madarasa yamejengwa na wanafunzi wanasoma vizuri. Pia ni Rais Samia ambaye amesema watoto wasome bure kuanzia darasa la awali mpaka kidato cha sita, na wanachuo wapatiwe mikopo.

Hivyo amewataka wote walioguswa na Rais Samia kwenda mtandaoni na kuandikwa jinsi walivyoguswa na kumalizia na Hashtag ya #TunasimamaNaSamia

Pia soma: Kampeni za Uchaguzi 2025 zimeanza?
 
Hawa wanaomsifu Sana mama mchana usiku Wana Jambo lao na yule binti anayeishi Marekani.

Mwendazake kamteua uwaziri leo mbele za watu anamsema vibaya as if waziri hahusiki kwenye mabaya ya serikali.

Mchunguzeni huyu kwa kauli ya makonda.
 
Anasema kipindi kilichopita kilikuwa na kikundi kinaitwa tusk force.

TRA walikuwa wanafunga account za wafanyabiashara kwa kisingizio cha kukusanya kodi kwa kutumia Tusk force hivyo kufilisi wafanyabiashara.

Ila kwa utawala wa mama yetu hilo jambo limekomeshwa.

Hakika nimeamini kuwa kila masika ina mbu wake.

View attachment 2964739

Ni task siyo tusk
 
Ukishaona jina la Rais linageuzwa wimbo wa taifa basi jua pana tatizo mahala
 
Hawa wanaomsifu Sana mama mchana usiku Wana Jambo lao na yule binti anayeishi Marekani.

Mwendazake kamteua uwaziri leo mbele za watu anamsema vibaya as if waziri hahusiki kwenye mabaya ya serikali.

Mchunguzeni huyu kwa kauli ya makonda.
Huyu huyu Nape alipotimuliwa kazi na Jiwe,nakumbuka alienda kuangukia
 
Ndio ukweli wenyewe huo ,Sasa Jambo Hilo halipo na makusanyo yamepaa mara 2.

Mwisho angejikita kumkosoa Mange kuliko kulinganisha na awamu ya 5 unless wafuasi wa awamu ya 5 ndio wanashirikiana na Mange kuandika upuuzi na shit Kwa Samia.
wewe si juzi kati ulipandisha uzi mama atumie task force leo unaungana na waziri mpuuzi,yeye na january ndio wanaotoa taarifa kwa Mange Magufuli aliwashtukia akawatupilia mbali watu wapuuzi unaapa kulinda siri za serikali bado unazitoa!
 
Sasa wafanyabiashara wameanza kucheza Rafu baada ya kupewa fair play..

Wakiendelea naunga mkono tusk force ila sio kupora pesa za watu.
 
Anasema kipindi kilichopita kilikuwa na kikundi kinaitwa tusk force.

TRA walikuwa wanafunga account za wafanyabiashara kwa kisingizio cha kukusanya kodi kwa kutumia Tusk force hivyo kufilisi wafanyabiashara.

Ila kwa utawala wa mama yetu hilo jambo limekomeshwa.
Aweza Nape kuwa ana hoja lakini.mambo mengine aachie waziri anayehusika hizo hoja ni za waziri wa fedha ndie hasa mwenye haki ya kuyaongelea
 
Ndio ukweli wenyewe huo ,Sasa Jambo Hilo halipo na makusanyo yamepaa mara 2.

Mwisho angejikita kumkosoa Mange kuliko kulinganisha na awamu ya 5 unless wafuasi wa awamu ya 5 ndio wanashirikiana na Mange kuandika upuuzi na shit Kwa Samia.
Hilo la wa "awamu ya tano " ni wazi kabisa wala halihitaji "rocket science" kulielewa.

Wapo wengi wamepenya kwenye awamu hii lakini wanaishi kama kunguru waliyekatwa mbawa, wanakoroma tu kuruka hawawezi
 
Anasema kipindi kilichopita kilikuwa na kikundi kinaitwa tusk force.

TRA walikuwa wanafunga account za wafanyabiashara kwa kisingizio cha kukusanya kodi kwa kutumia Task force hivyo kufilisi wafanyabiashara.

Ila kwa utawala wa mama yetu hilo jambo limekomeshwa.

Hakika nimeamini kuwa kila masika ina mbu wake.

View attachment 2964739
Labda kwakuwa hayupo kwenye biashara ndo maana anayaongea hayo ila ukweli ni kuwa kufungia akauntil za bank za wafanyabiashara (Urgency notes) kupo pale pale hasa kama unadaiwa na hulipi kwa muda mrefu asidanganye umma. Wafanyabiashara siku zote hawapendi kulipa kodi huo ndio ukweli kuendelea kuwachekea ni sawa na kucheka na nyani kwenye shamba la mahindi akafanye utafiti Kkoo watu hawatoi receipt ukidai wako radhi kutokukuuzia bidhaa au unaambiwa ulipie receipt ya kutembezea huo mzigo ulionunua na wengine wanakwambia kabisa wanakufikishia mzigo mpaka unapotaka ila receipt hakuna halafu uendelee kucheka nao?

Suala la kodi lazima liangaliwe kwa umakini sio porojo za wanasiasa na kingine makada wa chama tawala wafanyabiashara wako na kinga inapigwa simu moja mizigo inapita bila kizuizi chochote au bidhaa zinauzwa bila receipt. Kila siku rais analalamika juu ya wakwepa kodi hasa wafanyabiashara wakubwa bila kubanwa hakika hayupo mfanyabiashara aliyetayari kulipa kodi kwa moyo mweupe.
 
Back
Top Bottom