Awamu ya 6 inayoongozwa na Rais Dkt. Samia imetenga Tshs. Trilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa shule za msingi nchini

The Sunk Cost Fallacy 2

JF-Expert Member
Nov 8, 2022
7,382
8,437
Habari wanajukwaa..

Serikali ya awamu ya 6 Inayoongozwa na Rais wa Maneno kidogo na matokeo makubwa mh.Dk Samia S.Hassan imetenga Shilingi Tilioni 1.5 kwa ajili ya Kuimarisha elimu ya Msingi Nchini..

Kiasi hicho Cha Pesa kitatekelezwa chini ya mpango wa BOOST ambapo shule Mpya zitajengwa,kongwe zitakarabatiwa kulingana na mahitaji..

Hivyo kile kilio Cha uha a wa vyumba vya madarasa na watoto kukaa chini na kurundikana linaenda kupatiwa ufumbuzi..

Angalizo mradi huu Ni wa Miaka 5 kuanzia mwaka 2022/23-2026/27..

Pia ikumbukwe kwamba ili kukabiliana na changamoto za Elimu Serikali imeanzisha Program 3 kwenye Ngazi mbalimbali za Elimu Kama ifuatavyo.

1.Elimu ya Msingi-Boost 1.5Tilion,

2.Elimu ya Sekondari-Sequip 1.1 Tilion,

3.Elimu ya Kati na Juu-Heet -Bil.925.

Hongera Sana mh.Rais kwa Kuchapa kazi zinazoonekana,hakika historia itaandika jina lako kwa wino usiofutika..👇
Kairuki.jpg


========

Trilioni 1.5 Kujenga na Kukarabati Shule za Msingi nchini’ Kairuki

Na Fred Kibano, Pwani

Serikali imetenga shilingi Trilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya shule za msingi zenye uchakavu kupitia mradi wa kuimairisha elimu ya msingi na awali (Boost).

Kauli hiyo ya Serikali imetolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Angellah Kairuki leo tarehe 10 Januari, 2023 mkoani Pwani wakati akizungumza na Maafisa Elimu Wilaya na Kata, Wakuu wa Shule za Sekondari na Walimu Wakuu wa Shule za Msingi na viongozi wa Elimu ngazi ya Halmashauri wakati wa kikao kazi cha Uboreshaji wa Usimamizi wa Elimumsingi na Sekondari katika viwanja vya shule ya sekondari kibaha.

Waziri Kairuki amesema tathmini ya kina inaendelea kufanyika chini ya Ofisi yake ili kujua uchakavu wa miundombinu ya shule za msingi ambapo baada ya tathmini hiyo kuna shule ambazo zitapata ukarabati mkubwa, ukarabati mdogo na nyingine kuvunjwa kabisa kwa kuwa hazikidhi viwango vya kutolea elimu.

“katika kuimarisha miundombinu ya elimu ya awali na msingi kupitia mradi wa BOOST, tumetenga jumla ya shilingi Trilion 1.15 ambazo zitatumika katika ujenzi na ukarabati wa shule katika kipindi cha miaka 5 na kwa kuanzia kwa mwaka huu wa fedha tutaanza na shilingi Bilioni 259 ” amesema Kairuki.

Aidha, Waziri Kairuki alifanya ziara fupi kujionea ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Sofu iliyopo Mji wa Kibaha ambayo ujenzi wake umekamilika na wanafunzi wamekwisha anza masomo kidato cha kwanza.

Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa mkoa wa Pwani Mheshimiwa Abubakar Kunenge amesema mkoa wake ulifanya tathmini na kuona baadhi ya mila za wananchi sio nzuri hasa kwa watoto wa kike ambapo wameanza kuchukua hatua na kuanzisha kampeni za kumuokoa mtoto wa kike ikiwa ni pamoja na wazazi kuwekewa mazingira salama majumbani na shuleni.

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Elimu Ofisi ya rais TAMISEMI bw. Vicent Kayombo amesema kuwa kikao kazi hicho cha Uboreshaji wa Usimamizi wa Elimumsingi na Sekondari kina lengo la kuweka
 
Ni jambo jema

Haiwezekani 1977 tulikalia Mawe kwa upungufu wa madawati na leo 2023 Watoto wetu na wajukuu wakalie Mawe au Ndoo
Mama ameliona Hilo na mkono wa mama Ni wa malezi,hizo shida zinaenda kwisha ikiwemo kumtua mama ndio kichwani..

Leo hii Huduma za X Ray zinapatikana Hadi Vituo vya Afya,huyo ndio Mama Sasa 👇
---

Kituo cha Afya Hombolo chaanza kutoa huduma za Mionzi

OR-TAMISEMI

Kituo cha Afya Hombolo kilichopo katika Jiji la Dodoma kimeanza kutoa huduma za mionzi kwa wananchi wa kata hiyo na maeneo ya jirani mara baada ya kupokea mashine ya X-ray kutoka Serikali kuu.

Akizungumza baada kupokea Mashine hiyo Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Dkt.Andrew Method amesema hapo awali wananchi wa hombolo walilazimika kuja mpaka vituo vya mjini ambapo ni mbali na makazi yao mara tu wanapohitaji huduma hiyo.

“Lakini kwa sasa huduma hiyo imesogezwa karibu kabisa na wananchi hao hivyo itakua imewapunguzia adha ya kusafiri umbali mrefu kufuata huduma ya mionzi, Dkt. Andrew.

Mashine hiyo ya X-ray ni miongoni mwa mashine 137 zilizopelekwa kwenye vituo vya kutolea huduma nchini kote.

Tunamskuru Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuendelea kusogeza huduma za Afya karibu kabisa na wananchi.
 
Ni jambo jema

Haiwezekani 1977 tulikalia Mawe kwa upungufu wa madawati na leo 2023 Watoto wetu na wajukuu wakalie Mawe au Ndoo
Yaani mimi nikiona kuna shule wanafunzi hawana madawati, au matundu ya choo machache nahisi kuna tatizo kubwa kwenye kamati ya shule yaani wale ndio wakulala nao mbele.m kabla ya mkurugenzi wa eneo husika.
 
Back
Top Bottom