Kwanini Rais Samia ni mzito kuchukua hatua?

Mdude_Nyagali

Member
Dec 11, 2022
60
1,237
๐‘ด๐‘ฎ๐‘ถ๐‘ด๐‘ถ ๐‘พ๐‘จ ๐‘ฒ๐‘จ๐‘น๐‘ฐ๐‘จ๐‘ฒ๐‘ถ๐‘ถ ๐‘ต๐‘ฐ ๐‘ด๐‘จ๐‘ป๐‘ถ๐‘ฒ๐‘ฌ๐‘ถ ๐’€๐‘จ ๐‘ผ๐‘ฒ๐‘ฐ๐‘ด๐’€๐‘จ ๐‘พ๐‘จ ๐‘น๐‘จ๐‘ฐ๐‘บ.
Ni miaka miwili imepita tangu Samia aapishwe kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika miaka yake miwili tumeshuhudia Rais akiwa mzito wa kuchukua hatua za kinidhamu kwa watumishi na viongozi wasiokuwa waaminifu kwa Jamhuri ya Muungano. Sijui ni kigugumizi gani au uwezo wake wa kiutendaji umewekwa kwenye koma/ICU na wala nchi?

Kuna mambo mengi sana Rais yuko kimya na kwa uchache ngoja nizungumzie mambo matatu ambayo ni Mauwaji mikononi mwa polisi, Tozo na mfumuko wa bei pamoja na ufisadi.

1. ๐Œ๐€๐”๐–๐€๐‰๐ˆ/๐”๐“๐„๐Š๐€๐‰๐ˆ ๐Œ๐ˆ๐Š๐Ž๐๐Ž๐๐ˆ ๐Œ๐–๐€ ๐๐Ž๐‹๐ˆ๐’๐ˆ.
Kumekuwa na mwendelezo wa utekaji pamoja na mauwaji ya watuhumiwa katika vituo vya polisi. Baada ya Rais Samia kuchukua ofisi pale ikulu Machi 2021 watu wengi waliamini kwamba ule ulikuwa mwisho wa watu kutekwa, kuteswa na kuuwawa. Lakini baada ya muda mambo ya mauwaji na utekaji yalijirudia. Tena safari hii wahanga wakubwa wakiwa raia wa kawaida na si wakosoaji wa serikali kama enzi za Magufuli. Wakati mwingine nawaza kwamba huenda Rais Samia kubadilisha viongozi na wakuu wa vyombo vya dola kulilenga kusuka safu yake mpya ya uongozi na sio kukomesha mauwaji na utekaji unaofanywa na baadhi ya watumishi vyombo vya dola.

Tulishuhudia vijana watano wafanyabiashara wa Kariakoo wakikamatwa na watu waliodaiwa kuwa ni polisi kisha wakapelekwa kusikojulikana. Hata ndugu zao walipoenda polisi kujua hatima majibu waliyopewa yaliwashitua kwani polisi walikana kuhusika kuwashikilia. Ni mwaka mmoja na miezi sasa hawa vijana hawajapatikana. Pamoja na kelele tulizopiga mitandaoni, kelele za ndugu pamoja na vyombo vya habari hazijasaidia kuwarudisha vijana hao. Rais ambaye ndiye amiri jeshi mkuu na moja ya majukumu yake ni kuhakikisha raia wake wako salama hajawajibika na wala hajamwajibisha yoyote sio waziri au IGP ni kama vile kuku zimepotea. Amekaa kimya kana kwamba hausiki au hawajibiki na usalama wa raia.

Sio hao tu orodha ya watu kutekwa na wengine kufia vituo vya polisi iliendelea kila kona ya nchi. Mauwaji ya raia Mtwara baada ya kelele nyingi kwa mbaaali angarau akamwagiza waziri mkuu aunde tume ambayo mpaka leo ni mwaka hakuna ripoti ya hiyo tume. Sijui tatizo ni yeye au waziri mkuu?

Baada ya kuona ripoti ya tume mauwaji ya Mtwara imefungiwa maandazi kashfa za watu kufia vituo vya polisi ziliendelea huku polisi wakisingizia watuhumiwa hujinyonga wenyewe. Ilifika mahali polisi walidai wengine walijinyonga kwa kutumia chupi lakini bado Rais Samia kakaa kimya. Orodha ya watu waliofia vituo vya polisi na wengine kutekwa na polisi kwa upande wangu peke yangu nimepokea majina 20 ndani ya miaka miwili ya Samia. Juhudi zetu pamoja na kelele za kutaka hatua kuchukuliwa haijazaa matunda kana kwamba najiuliza hivi kweli tuna Rais au tumeweka shati golini?

2.๐“๐Ž๐™๐Ž ๐๐€ ๐Œ๐…๐”๐Œ๐”๐Š๐Ž ๐–๐€ ๐๐„๐ˆ.
Tumeshuhudia baada ya Rais Samia kuapishwa kwa haraka alifanya mabadiliko makubwa ya baraza la mawaziri japokuwa mawaziri wengi alirithi kutoka kwa mtangulizi wake akiwemo waziri mkuu. Watu walianza kuwa na matumaini kwamba huenda angepunguza ukata wa maisha ulioletwa na mtangulizi wake lakini mambo hayakuwa hivyo.

Siku 40 za mwanzo tu serikali ya Samia ilipandisha gharama za vifurushi vya internet DATA mara mbili kuliko ilivyokuwa awali. Shilingi elfu moja ambayo ilikuwa na uwezo wa kununua GB moja ya internet sasa ikawa inanunua MB 400 tu. Wananchi wakaanza kulalamika kelele zikawa nyingi lakini ndio kwanza Rais alikausha kimya kana kwamba haishi Tanzania na malalamiko hayaoni. Waziri wake sijui anaitwa Nape anajibu kwa kiburi kwamba kama vifurushi ni gharama zimeni data na Rais yupo kimya tu.

Wakati kidonda cha kupanda kwa data kikiendelea kuuma likafuata pigo lingine la tozo kwenye miamala ya simu na bank. Unatumiwa buku 5 unatoa buku 3 buku 2 imeishia kwenye makato achilia mbali aliyekutumia naye kukatwa tozo. Katikati ya kilio cha tozo likapigwa kombola lingine la mfumuko wa bei. Gharama za maisha zikaongezeka vilio vya machinga na wakulima bei za mbolea lakini bado Rais akaendelea kukaa kimya kana kwamba hahusiki na wala hawajibiki na chochote. Hata akiongea basi naye analalamika kama sisi mpaka najiuliza pale ikulu tuna Rais kweli au tumeweka shati golini?

3. ๐”๐…๐ˆ๐’๐€๐ƒ๐ˆ
Wengi waliamini kwamba pengine serikali ya Rais Samia kuongeza tozo na kodi mbalimbali kwa wananchi alikuwa analenga kupunguza deni la taifa kama ambavyo Rais Mkapa alifanya katika utawala wake kwa kutokukopa na kupunguza deni la Rais Mwinyi. Takwimu za deni la taifa zikatushitua. Rais Magufuli ndio alishikilia rekodi ya Rais aliyekopa pesa nyingi kwa kipindi cha miaka mitano kuliko watangulizi wake. Lakini rekodi hiyo ilivunjwa na Rais Samia kwa mwaka mmoja tu. Yani pesa ambayo Rais Magufuli aliikopa kwa miaka mitano Samia kaikopa kwa mwaka na wakati huo hata matumizi ya mikopo hiyo hayaeleweki .

Wakati tumepigwa butwaa tukijiuliza imekuwaje mara anaibuka mkaguzi mkuu na mdhibiti wa hesabu za serikali CAG anatusanua namna ambayo watumishi wa umma na viongozi wa serikali walivyovuja pesa za umma. Wengi wakaamini kwamba Rais angechukua hatua kwa ripoti ile lakini hakuchukua hatua yoyote zaidi ya kuwataka wezi hao kula urefu wa kamba zao.

Mwaka mmoja baadaye inatoka ripoti nyingine ya CAG ikionyesha uvujaji na wizi mkubwa wa pesa za umma kukiwa na zaidi ya trillion 2 zilizoibiwa. Hapa Rais angarau alichukua hatua kidogo kwa kuwatukana wezi stupid lakini hakuwawajibisha kwa kuwafukuza kazi au kuwasimamisha ama kuwapeleka mahakamani.

Mgomo wa wafanyabiashara Kariakoo ni matokeo ya ukimya wa Rais. Kushindwa kusikiliza, kutafuta majawabu na kuchukua hatua ni mambo yaliyopelea mgomo huu. Baada ya kikao cha waziri mkuu na uongozi wa wafanyabiashara wa Kariakoo siku ya jumatatu kushindwa kuzaa matunda na mgomo kuendelea siku iliyofuata, nilitegemea Rais angechukua point 3 kwa kwenda kuwasikiliza mwenyewe na kuchukua hatua. Lakini kama kawaida yake kakaa kimya. Pengine hajui madhara yake. Kuna siku mgomo hautakuwa wa Kariakoo pekee bali utakuwa mgomo wa nchi nzima utakaozalisha maandamano yanayoweza kuangusha serikali yake.

Vipi Rais Samia angeibuka mwenyewe pale MnaziMmoja kusikiliza kero za wafanyabiashara wa Kariakoo zilizopelekea wao kugoma kufungua maduka? Halafu baada ya mkutano avunje bodi ya TRA, afukuze waziri na kamishina wa TRA. Ingempandisha chati kiasi gani? Angepata sifa kiasi gani? Tukio hilo lingerudisha nidhamu kwa viongozi na watumishi wa umma kiasi gani?

Shida ya Samia nini kutochukua hatua?

๐‘ด๐’…๐’–๐’…๐’† ๐‘ต๐’š๐’‚๐’ˆ๐’‚๐’๐’Š ๐Ÿ• ๐’™ ๐Ÿ•๐ŸŽ ๐‘บ๐’–๐’Ž๐’– ๐’š๐’‚ ๐‘ต๐’š๐’Š๐’ˆ๐’–.

20230516_183816.jpg
 
Tatizo la kimfumo haliwezi badilishwa na mtu mmoja tena ndani ya miaka miwili! Tu!

Mfumo ukibadilika utaua changamoto zote!

Tatizo kuu ni uwajibikaji yaani watu wanaharibu halafu hawawajibiki HADI Rais awawajibishe SASA yeye atashika mangapi!!?

Yaani awe anakaa na kuchunguza nani asie wajibika!!?je KAZI NYINGINE atafanya NANI!!?

Hivyo tu!viongozi wateuliwa wawajibike wenyewe sio hadi Rais awawajibishe!!!
 
Poroji ndeefu ilinuweje?

View attachment 2626057
Porojo ndeefu ili iweje? Hii ni "social media" siyo "thesis". Weka mada moja fupi ueleweke, unakimbilia wapi?

Unataka awe mkurupukaji kama bwana yule? Matokeo hasi ya ukurupukaji bado hujayaelewa?

Umeyaongelea ya Kariakoo, ni kipi kimecheleweshwa katika kufanyiwa kazi ya Kariakoo?
 
Rais wa awamu ya sita hicho kiti sio chake mfumo umemlazimisha kukaa mahali ambapo sio pake.. Nashangaa watanzania wanavyomsifia.. umaskini hauwezi kuwaisha..
 
Hata wewe mtoa mada ungekuwa kwenye mfumo, na wewe ungekuwa kama yeye tu.

Au nikuulize swali jepesi tu lililo nje ya hii mada; mbona nyinyi kule kwenye chama chenu Mwenyekiti hataki kustaafu kwa hiyari?
Maana yake wanachama wote mna uwezo mdogo wa kuongoza kuliko yeye?

Kwa nini msianzishe azimio la kumuondoa kwa lazima? Inawezekana chama chenye mamilioni ya wanachama kukosa Mwenyekiti mbadala?

Au ndiyo kusema siku akichukuliwa hapa duniani na kwenda kwa Baba Muumba, na chama nacho kitakufa?
Hii hoja haiendani, hakuna mahali kasema watu wanaogopa kumshauri au kumkosoa au kumpindua ndio ingefanana na swali la kwanini hatumuondoi Mbowe.

Yeye anachouliza ni kwanini Rais ni mzito kuchukua hatua so Hilo swali lingeendana kama ungeuliza pia kwanini Mbowe ni mzito kuchukua hatua?

Bottom Line Mbowe alishatangaza kuacha uenyekiti 2023 katika mkutano mkuu wa chama, so sidhani kama anaogopwa otherwise asingesema anapingwa na wahafidhina kule Mwanza.
 
Ndivyo alivyo niliwah mshuhudia akizindua stend flan iliyokuwa imejengwa chini ya kiwango na upigaj ulifanyika wa kutosha wala hakuzindua Ile stend wala kuchukua hatua yoyote๐Ÿคฃ๐Ÿคฃndivyo alivyo๐Ÿค”๐Ÿค”
 
Back
Top Bottom