Napata wasiwasi na mchumba wangu aendae chuo kikuu

Napata wasiwasi na mchumba wangu aendae chuo kikuu

Chuo changamoto babii, huyo demu wako labda awe mtu wa kujitegemea kwa kila kitu na anayejitambua.

Kama demu wako ana asili ya ushamba au wale wa kushikwa maskio yani mtu wa kuongozana na mashosti andika maumivu. Pia kama alikuwa anabanwa sana nyumbani ni tatizo jingine hilo.

Chuo ni sehemu nzuri ya kujifunza maisha ila mademu malimbukeni hufanya vituko vya kila aina hebu ona.

1. Kama alikuwa hajui club ataenda tu na pombe atakunywa...

2. Wewe au kwao hamna gari akibebwa kwenye na vijana wenye hayo mamlaka hachomoki...

3. Bata za kila weekend guaranteed kwa viwanja na mahoteli makubwa ya town, lazma sponsor akiomba utamu anapewa tu huku demu akidanganywa ataolewa na huyo jamaa baada ya chuo so hatokuwaza tena...

4. Akiwa kilaza jua kuna kipanga fisi wa darasani atapata fursa akimbana ghetto/hostel na kumpiga pindi kisha kulipwa penzi juu ya deka.

5. Kama alikuwa hajui kuvaa kuna mashosti atakutana nao huko watamvisha viwigi,makucha mpaka skin jeans na vikondom ili aonekane wa kisasa...

6. Kuna vijana wakishua watanashati 24/7 wenye mvuto na mamlaka kama wanaomiliki mageto makali,pesa,magari. Sio ajabu demu wako akakuona kolo tu huendani nae baada ya kuwa anatongozwa sana na watu highclass zaidi na kupelekwa viwanja vya maana.

7. Akiangalia we uwezo wako ghetto t.v chogo, full majaba outing mnaenda beach kimba kula madafu na azam chokstik na diamond karanga. Lazma aone unamchelewesha maisha tu.

ANGALIZO:
Mwaka wa kwanza unaeza maliza nae freshi ila hayo mara nyingi hutokea ndani ya mwaka wa pili wa chuo, we sikilizia tu! Nikushauri tu andaa backup plan in case haya yatatokea maana odds ni 90% likely kwa wasichana wengi!
Ukiona meseji hazijibiwi kwa wakati, namba inatumika sana kuanzia saa 4-6 usiku na pia hakujulii hali siku nzima mpaka umuanze na ukiulizia shida ni nini anakuwa mkali na visingizio ambavyo havikuwepo mwanzoni jua tayari.
 
Wewe kama huna hata degree andika tu maumivu tayari umeshamkosa
 
Mkuu kama unafeel kupungukiwa bila huyo mwanamke,
Kuwa na imani ya kumpata kama ukijipanga vema kimaisha(uchumi) akimaliza akukute mtu wa tabaka fulan, jipange mara 3 kwa mwez kumtembelea kama chuo karibu kila weekend ni bahati sana kumaliza chuo akiwa na tabia yake ya sasa.
Chuoni wanakuwaga very cheap(nasema nilichokiona)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiandae kisaikolojia kwa hali yoyote, ili ikitokea basi isikuumize ukaja kulia humu.
 
Ushaur ni bora uanze kutafta replacement mapema saana, chuoni siyo pazur kabisa hasa kwa mabint hata kama ana msimamo watamchukua, japo wapo wanaoweza lakin hiyo inategemea ukoje kuanzia pesa na vngne ving

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo huna mchumba tena kijana, wakisha enda chuo andika maumivu..

Hubadilika tabia pindi wafikapo chuo yaani ataenda kukutana na wenye hadhi kubwa na vishawishi vya hapa na pale........

Labla kama wewe unafanya kazi BOT, na Baba yako ni mmiliki wa Oilcom na Mama yako anafanya kazi Bank ya dunia hapo ndiyo hatakusaliti hata kidogo.....


Otherwise jiandae kwa msiba.....
Nimecheka sana....[emoji28][emoji28][emoji28] ulichosema ni sahihi kwa asilimia 99 japo wasichana/wanawake kukikubali hapa siyo rahisi.
Anyway ushauri wako ni sahihi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom