Naongea na mwenye mbwa siongei na mbwa

Hahaaaaa manosaaaaaaaa katumbua jipu sioo menfine tetekuwanga yanaitaji dawa yaponee
 
Acheni kuandika kiumbembea, huyu mtu anaitwaa hance pope. Dini inatufundisha kusamehe saba mara sabini. Magufuli sii mjahaidina, magufuli ni mkristo safi.
Mawazo yenu nyinyi wachonganishi, hayapo kwa magufuli.
Hao wajahidina umewamiss sana na utawaona hapa
 
HUYU NDIYE ZACHARIA HANS POPPE WA SIMBA SC

au kuna Hans Poppe mwingine?

Zacharia Hans Poppe

Hans Poppe
 
Kuna siku nikiwa Lusaka kipindi cha kampeni mkurugenzi wa jiji la Lusaka alimyima sata kibali cha kufanya kampeni, sata akatinga hadi jiji akamwabia yule mkurugenzi kuwa hawaambie waliomtuma kuwa siku akiwa rais atakomesha tabia ya watumishi kuwa sehemu ya vyama tawala, alichoambulia sata ni tusi toka kwa yule mkurugenzi kuwa, wewe mbwa asiye na Elimu nani akupe urais wa nchi, kama siyo walinzi wa sata ngumi zingelika, bahati mbaya kwa mkurugenzi sata akashinda urais.
 
Nadhani Kwa sasa badala ya kupumulia pua anapumulia masikio!!! Kibri si maungwana

Mkuu na wewe unaamini habari ya kulipizana visasi kwa sababu ya nafasi ya madaraka uliyopata.
Angalieni msije kumwingiza Rais kwenye mtego mbaya. Kwa Nchi yetu Rais ana madaraka makubwa sana
akiyatumia kama mleta mada na wengine wanavyotaka tutavuruga "Uongozi".
Kwanza mleta mada ametumia maneno ya kibaguzi "chotara".

Kama kweli Hans Pope alisema hayo sioni ni kwa vipi alipe kisasi, hata sisi kwa nyakati tofauti tumewajibu vibaya
marafiki/Viongozi wetu kwa viwango mbalimbali, je tulipizane kisasi? Kama ni suala la wao kufanya makosa
wakati wa kuendesha biashara lisifanywe "target" kwa Mtu mmoja. Sheria na taratibu zifuatwe. Wakati anatenda kazi
alikuwa Waziri na si Magufuli, sasa ni Rais atatenda kama Rais na si kulipiza aliyofanyiwa huko nyuma.

Kuna Watu kwa pace hii ya Rais wanaweza kutuingiza mtegoni kwa malengo yao na chuki zao binafsi.Nchi hii ina
Watu zaidi ya Milioni 45, kila Mtu ana mtazamo, udhaifu na hulka yake. Huwezi kuhukumu wote, kama ambavyo
Watu wa Kigamboni waliambiwa wapige mbizi kama hawana nauli!
 
Kuna siku nikiwa Lusaka kipindi cha kampeni mkurugenzi wa jiji la Lusaka alimyima sata kibali cha kufanya kampeni, sata akatinga hadi jiji akamwabia yule mkurugenzi kuwa hawaambie waliomtuma kuwa siku akiwa rais atakomesha tabia ya watumishi kuwa sehemu ya vyama tawala, alichoambulia sata ni tusi toka kwa yule mkurugenzi kuwa, wewe mbwa asiye na Elimu nani akupe urais wa nchi, kama siyo walinzi wa sata ngumi zingelika, bahati mbaya kwa mkurugenzi sata akashinda urais.
Eeeh bwana eeeh...duh
enhee ikawaje?
 
Kumbe ni mdingi hivyo, sikuwahi sikia kama alishawahi kufanya siasa na kutaka kumpindua jk1
 
Mkirudi mmelewa viroba msilazimishe kuanzisha thread za kijinga na zenye negative impact kwa rais wetu. Ulivyoandika watu wengi watakuwa na mawazo kuwa rais Magufuli anajindaa kulipa kisasi. Na jambo lolote baya au litakalomkuta huyo ''mwenye malori'' uliyesema itaonekana kama ni mheshimiwa rais ametumia wadhifa wake kulipa kisasi. Au hata akifanya uhalifu wowote na akakamatwa kwa mujibu wa sheria na vyombo vya dola, wengi wataona kuwa ni rais wetu amejibu mapigo (kwa mujibu wa thread yako). Tunaomba sana moderators wawe wakali kwa thread za kijinga na kichochezi kama hizi. Narudia kusema tena fikirini kwa mapana kabla hamjaanzisha thread kwani hapa sio klabu ya wanzuki!
Kaka usijifanye unaipenda sana nchi hii kuliko kila mtu hapa jamii forum. Ukifuatilia maandishi utaona mahali nimeandika "nyeti zinahabarisha". Na hii ni forum, kila mtu ambaye anajihesabu kama great thinker anao uwezo wa kuchambua kila kinachoandikwa. Hii sio klabu ya wanzuki na wote waliochangia sio walevi wa wanzuki.
Ndugu yangu jifunze kusoma maandiko na kuyapima kama mtu mwenye upeo mkubwa wa kuelewa mambo. Mimi nimeandika kwa mujibu wa nyepesi nyepesi nilizosikia, ina maana nisiandike kitu eti kwa sababu ya impact ya baadae?.
 
Hapana hapana hapana. Umekosea kabisa. Hata kama umeambiwa kutoka kwa malaika lakini kuna namna ungeweza ku-present thread yako na ikaeleweka. Wewe umeumba picha ya kuwa rais Magufuli yupo tayari kujibu mapigo kwa sababu aliambiwa msemo ambao haukumpendeza tena siku za nyuma! Hapa ni kama unamweka rais kwenye kundi la walipa kisasi. Ungeweza tu kusema jamaa ana kosa A na una fununu kuwa atatumbuliwa siku za karibuni. Na labda ungeweza kukumbushia mwishoni kuwa ''mnakumbuka huyu ndiye aliyekuwa na jeuri ya kusema blah blah blah siku za nyumba!

Jaribu kurudia tena maandishi yako:
Shombe shombe yupo kwenye wakati mgumu, kwani huyu mwenye mbwa wa sasa, anafahamu fika dharau aliyokutana nayo wakati akiwa kazini katika wizara ya barabara.

Nyeti zinahabarisha kwamba mwenye mbwa yupo njiani kuandaa mapigo yatakayorudisha heshima aliyoipoteza baada ya kudharauliwa mpaka kufananishwa na dogi.
 
Hapana hapana hapana. Umekosea kabisa. Hata kama umeambiwa kutoka kwa malaika lakini kuna namna ungeweza ku-present thread yako na ikaeleweka. Wewe umeumba picha ya kuwa rais Magufuli yupo tayari kujibu mapigo kwa sababu aliambiwa msemo ambao haukumpendeza tena siku za nyuma! Hapa ni kama unamweka rais kwenye kundi la walipa kisasi. Ungeweza tu kusema jamaa ana kosa A na una fununu kuwa atatumbuliwa siku za karibuni. Na labda ungeweza kukumbushia mwishoni kuwa ''mnakumbuka huyu ndiye aliyekuwa na jeuri ya kusema blah blah blah siku za nyumba!
Nimekusoma mzee na nitafanyia kazi ushauri, pamoja.
 
Back
Top Bottom