Naongea na mwenye mbwa siongei na mbwa

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Dec 29, 2015
18,488
13,608
Kuna mtu mmoja shombe shombe (chotara/zero point five), yeye ni mmoja wa watu wenye ushawishi ndani ya klabu ambayo zamani iliitwa Sunderland. Huyu mtu ni mmoja wa wadau muhimu wa sekta ya usafirishaji, ni mmoja wa wamiliki wa magari makubwa yanayopeleka mizigo katika nchi jirani.

Wakati wa awamu ya nne aliingia kwenye mzozo na aliyekuwa waziri wa barabara, akafikia hatua ya kuongea kwa dharau akisema kwamba yeye haongei na mbwa bali anaongea na mmiliki wa mbwa, ilibidi aliyekuwa waziri mkuu aingilie kati na kuutatua ugomvi ule.

Mungu si athumani siku za kuishi huwa zinakwenda kasi sana, leo hii yule aliyeitwa mbwa ndiye mwenye mbwa, na ana sauti ya juu kabisa na yenye mamlaka.

Shombe shombe yupo kwenye wakati mgumu, kwani huyu mwenye mbwa wa sasa, anafahamu fika dharau aliyokutana nayo wakati akiwa kazini katika wizara ya barabara.

Nyeti zinahabarisha kwamba mwenye mbwa yupo njiani kuandaa mapigo yatakayorudisha heshima aliyoipoteza baada ya kudharauliwa mpaka kufananishwa na dogi.

Somo muhimu kwa shombe shombe na wengine wote wenye kupenda kuropoka hovyo bila ya kuitazama kesho inafananaje, ni kwamba mdomo ulikiponza kichwa.
 
Nakumbuka mtu mmoja Alisema weka akiba ya maneno. Huyo jamaa alitakiwa aweke akiba ya maneno. Lakini kumbuka jamaa alinyemelea madaraka wakati wa awamu ya kwanza, alitaka kuingia madarakani yeye na wenzake Kwa njia haramu!!!
 
Acheni kuandika kiumbembea, huyu mtu anaitwaa hance pope. Dini inatufundisha kusamehe saba mara sabini. Magufuli sii mjahaidina, magufuli ni mkristo safi.
Mawazo yenu nyinyi wachonganishi, hayapo kwa magufuli.
 
Amsamehe bure maana alikuwa hajui alitendalo ila achunguzwe kama amelipa kodi hawezi akawa na jeuri namna hii
 
hata mie natamani ningemjua, hebu tujuzeni jamani hata kwa darubini au kwa vinasaba ili nasi tumfahamu wajameni
 
Acheni kuandika kiumbembea, huyu mtu anaitwaa hance pope. Dini inatufundisha kusamehe saba mara sabini. Magufuli sii mjahaidina, magufuli ni mkristo safi.
Mawazo yenu nyinyi wachonganishi, hayapo kwa magufuli.
Kwahiyo Wajahidina hawasamehi? na mbona imeandikwa Kisasi ni haki na Msamaha ni bora. na wameambiwa wafuate vitu bora...
 
Acheni kuandika kiumbembea, huyu mtu anaitwaa hance pope. Dini inatufundisha kusamehe saba mara sabini. Magufuli sii mjahaidina, magufuli ni mkristo safi.
Mawazo yenu nyinyi wachonganishi, hayapo kwa magufuli.
Tusichanganye mambo dini haisemi wanaovunja sheria wasamehewe sabini mara saba.
 
Back
Top Bottom