Mbwa alaumiwa kwa kumnyima Mkenya ushindi katika mbio za marathon

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,615
Je, ilikuwa ni hujuma au ilitokea bahati mbaya?

Habari kamili;

Seneta mmoja nchini Kenya amekosoa mashirika ya michezo kwa kushindwa kuchukua hatua baada ya mbwa kumfukuza mwanariadha Robert Kimutai Ng’eno wakati wa mashindano ya riadha wiki iliyopita huko Buenos Aires, Argentina.

Ripoti zinasema mwanariadha huyo alionekana akiongoza akiwa amesaliwa na kilomita 4 kukamilisha mbio hizo, wakati mbwa alipojitokeza na kuanza kumfukuza.

Licha ya juhudi za baadhi ya watazamaji kumfukuza mbwa huyo, lakini tukio hilo lilionekana kumfanya Ng’eno kupoteza mwelekeo na hatimaye kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio hizo.

Raia wenzake wa Kenya Cornelius Kiplagat na Paul Kipngetich Tanui waliibuka katika nafasi ya kwanza na ya pili mtawalia.

Picha inayoonyesha mbwa akimfukuza Ng’eno imesambaa sana katika mitandao ya kijamii na baadhi wameuliza kwanini juhudi zaidi hazikuchukuliwa kuwalinda wanariadha.

“Mwanariadha hakupewa heshima yake na kukabiliwa na kejeli,” alisema Seneta Samson Cherargei kwenye mtandao wa X (zamani uliokuwa ukijulikana kama Twitter).

Alisema kwamba Waziri wa Michezo wa Kenya Ababu Namwamba na shirika la wanariadha la Kenya hawakusimama na mwanariadha huyo, huku akiongeza kwamba hawajachukua hatua kwa kueleza malalamishi yao au kutoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi na mamlaka za Argetina.

BBC Swahili: 29 Sept, 2023.
View attachment 2766907
 
Bila video au picha ni Umbea tu kama wa famikia ya Sepetu
Nimeichukua hii habari BBC Swahili kama ilivyo ikiwa na picha japo lazima ipatikane You Tube
2302779f-c73e-4552-acf8-92d158256fb0.jpg
 
Back
Top Bottom