Nilisimulia story ya mpenzi wangu anayependa kununa ovyo. Basi Leo naona nibwage manyanga kwenye penzi hili. Tulikuwa vizuri tu na nilikuwa namjali sana tu. Ila mambo yameenda tunachat vizuri tunaongea ila usiku tulichat vizuuri kesho yake nikawa namcheki lakin hajibu Wala hapokei simu. Jioni nikaenda kuonana naye, nikamuuliza shida ni Nini? Akaniambia kuwa ni kwa sababu sikwenda kumuona Jana yake. Tukaongea yakaisha. Usiku tukapigiana simu tukaongea tukaagana vizuri. Kesho yake Tena ikawa hivyo hivyo. Hapokei Wala hajibu text. Sasa nimemfata Leo jion namuuliza tatizo lako ni Nini? Anasema hataki kuongea na hajisikii kuongea na mimi. Ikabid niondoke. Ila kwa hapa naona nibwage tu manyanga maana hajibu Wala hapokei simu yangu. Kesho ntamfata nimuambie najua hanitaki Tena iwe ndo mwisho hatonisikia Tena. Wadau mnaona je maamuzi yangu?