Naona sasa ning'atuke kutoka kwake

Naona sasa ning'atuke kutoka kwake

mtu bati

Senior Member
Joined
Mar 29, 2021
Posts
117
Reaction score
129
Nilisimulia story ya mpenzi wangu anayependa kununa ovyo. Basi Leo naona nibwage manyanga kwenye penzi hili.

Tulikuwa vizuri tu na nilikuwa namjali sana tu. Ila mambo yameenda tunachat vizuri tunaongea ila usiku tulichat vizuri kesho yake nikawa namcheki lakin hajibu Wala hapokei simu. Jioni nikaenda kuonana naye, nikamuuliza shida ni Nini?

Akaniambia kuwa ni kwa sababu sikwenda kumuona Jana yake. Tukaongea yakaisha. Usiku tukapigiana simu tukaongea tukaagana vizuri. Kesho yake Tena ikawa hivyo hivyo. Hapokei Wala hajibu text. Sasa nimemfata Leo jion namuuliza tatizo lako ni Nini?

Anasema hataki kuongea na hajisikii kuongea na mimi. Ikabid niondoke. Ila kwa hapa naona nibwage tu manyanga maana hajibu Wala hapokei simu yangu. Kesho ntamfata nimuambie najua hanitaki Tena iwe ndo mwisho hatonisikia Tena. Wadau mnaona je maamuzi yangu?
 
...hajibu wala hapokei simu yangu..."

"...anasema hataki kuongea na hajisikii kuongea na mimi..."

Kusanya nguvu zote hata kama ni kwa kuomba mizimu ya ukoo na kabila lenu nawe ukae kimya uone. Usimwandikie text wala kumpigia simu kabisa kabisa.

Na hata gubu likija kumuisha akaandika au kukupigia simu jitahidi ukaushe tu halafu ulete mrejesho hapa. Huyu likely ana mtu mwingine au anajua jinsi unavyompenda na amejiaminisha kuwa ni lazima tu utamtafuta. Ukiuchuna na akajua kuwa she is replaceable na kwamba unaweza kumpiga chini ndo utaona hasa yukoje. Na akirudisha komwe lake tena weka msimamo wazi kuwa hupendi hilo gubu lake na uwe imara katika msimamo wako.

Kwa jinsi unavyozidi kumtafuta ndivyo unajishushia heshima na unazidi kujidhalilisha tu kwake; na kila wiki utakuwa unakuja humu kuanzisha nyuzi. Usipogangamara huyu atakusumbua sana!
 
Kama wewe ni me..., hujamkuna eneo lake hadi ukaona gego lake na mlio wa sauti ya zeze ukatoka kwenye koo lake.

Kama wewe ni ke.....

Mwanaume anayenuna mbali mbali na Kasie.
Tufundishe ujuzi wa zamani namna ya kumkuna mpaka kuona gego mkuu
 
Kama wewe ni me..., hujamkuna eneo lake hadi ukaona gego lake na mlio wa sauti ya zeze ukatoka kwenye koo lake.

Kama wewe ni ke.....

Mwanaume anayenuna mbali mbali na Kasie.
Me mimi
 
Maelezo yako ni mimi mtupu kipindi kile nina miaka 19...huyo unayemuelezea ana umri gani?
Alikuwa hapendi pia ile tabia na alikuwa ananiambia mara nyingi lakini sikubadilika...akafikia maamuzi kama yako ya kubwaga manyanga...nikaachwa teh!

One thing for sure ni kwamba anakupenda,hivyo ni vijitabia ambavyo huwa tunakuwa navyo tu na havielezeki inakuwaje vinajitokeza...with time atabadilika tu

Mimi nilimpenda sana yule mwanaume lakini vile vitabia vya kununa vilinipenda zaidi,vikaharibu kila kitu
 
She is 20.
 
Nilisimulia story ya mpenzi wangu anayependa kununa ovyo. Basi Leo naona nibwage manyanga kwenye penzi hili. Tulikuwa vizuri tu na nilikuwa namjali sana tu. Ila mambo yameenda tunachat vizuri tunaongea ila usiku tulichat vizuuri kesho yake nikawa namcheki lakin hajibu Wala hapokei simu. Jioni nikaenda kuonana naye, nikamuuliza shida ni Nini? Akaniambia kuwa ni kwa sababu sikwenda kumuona Jana yake. Tukaongea yakaisha. Usiku tukapigiana simu tukaongea tukaagana vizuri. Kesho yake Tena ikawa hivyo hivyo. Hapokei Wala hajibu text. Sasa nimemfata Leo jion namuuliza tatizo lako ni Nini? Anasema hataki kuongea na hajisikii kuongea na mimi. Ikabid niondoke. Ila kwa hapa naona nibwage tu manyanga maana hajibu Wala hapokei simu yangu. Kesho ntamfata nimuambie najua hanitaki Tena iwe ndo mwisho hatonisikia Tena. Wadau mnaona je maamuzi yangu?
Mkuu mbona unataka kucomplicate Mambo, ushaenda akakwambia hataki na hajiskii kuongea na wewe, yani mtu hujamfanya chochote ila hajiskii kuongea naww kwa mtu mwelewa ulitakiwa kuelewa nini anamaanisha, kwani kuna haja gani ya kwenda ili umuambie eti unajua hakutaki ilhali ye pia anajua hakutaki? Unataka ufunge safari unafata nini? Ukikuta yupo na Mshakaji ambae ndio anafanya ye akukatae utafanya nini?

Inaonekana alikuwa anajaribu kukupenda ila imeshindikana, wanawake waga hawapendi mtu ghafra ispokuwa anaanza kumpenda mtu taratibu kadri wanavyozidi kutumia muda pamoja, shukuru Mungu huyo mwanamke amekuwa mkweli na hajataka kukupotezea Muda, Mtumie sms mwambie unashkuru kwa muda aliokupa mkautumia pamoja na unamtakia maisha mema full stop, Move on brother
 
Tafuta demu mwingine mkaliii ikiwezekana zaidi yake then mpange tu mjifanye kama MNA mahusiano uone kitakachotokea.huo ni utoto tu,Ila una moyo sana yaani hapokei unafuata Mara zote hizo bado anakwambia hajiskii kuongea na ww.?
Kweli mapenzi upofu nimeamini.
 
Mkuu mbona unataka kucomplicate Mambo, ushaenda akakwambia hataki na hajiskii kuongea na wewe, yani mtu hujamfanya chochote ila hajiskii kuongea naww kwa mtu mwelewa ulitakiwa kuelewa nini anamaanisha, kwani kuna haja gani ya kwenda ili umuambie eti unajua hakutaki ilhali ye pia anajua hakutaki? Unataka ufunge safari unafata nini? Ukikuta yupo na Mshakaji ambae ndio anafanya ye akukatae utafanya nini?

Inaonekana alikuwa anajaribu kukupenda ila imeshindikana, wanawake waga hawapendi mtu ghafra ispokuwa anaanza kumpenda mtu taratibu kadri wanavyozidi kutumia muda pamoja, shukuru Mungu huyo mwanamke amekuwa mkweli na hajataka kukupotezea Muda, Mtumie sms mwambie unashkuru kwa muda aliokupa mkautumia pamoja na unamtakia maisha mema full stop, Move on brother
Yeah, I'll do it bro. This is the advice now.
 
"...hajibu wala hapokei simu yangu..."

Kusanya nguvu zote hata kama ni kwa kuomba mizimu ya ukoo na kabila lenu nawe ukae kimya uone. Usimwandikie text wala kumpigia simu kabisa kabisa. Na hata gubu likija kumuisha akaandika au kukupigia simu jitahidi ukaushe tu halafu ulete mrejesho hapa. Huyu likely ana mtu mwingine au anajua jinsi unavyompenda na amejiaminisha kuwa ni lazima tu utamtafuta. Ukiuchuna na akajua kuwa she is replaceable na kwamba unaweza kumuacha ndo utaona hasa yukoje. Na akirudisha komwe lake tena weka msimamo wazi kuwa hupendi hilo gubu lake na uwe imara katika msimamo wako.

Kwa jinsi unavyozidi kumtafuta ndivyo unajishushia heshima na unazidi kujidhalilisha tu kwake; na kila wiki utakuwa unakuja humu kuanzisha nyuzi...
Mtoa mada leta mada nyingine jibu lako ndo hilo apo juu ukitaka lingine ni wewe sasa
 
Yeah, I'll do it bro. This is the advice now.
Ndio hivo brother, we usimtamkie maneno mabaya wala usitake kumkumbusha ni vitu gani ulifanya kwake asije akaona Kama unataka kulipwa, kuwa Gentleman na msifie mazuri yake na ajue utamkumbuka kwa yapi na ofcoz ulienjoy kwa muda wote mliotumia pamoja

ye pia ni mwanadamu anajua kuna mengi mazuri ulifanya kwa ajili yake na kuna matukio mlipitia na akapata furaha ata kama alikuwa hakupendi, so mfanye abakie na kumbukumbu ya busara zako ili yakimfika ya kumfika huko aendako au alipo maana kuna wajuba wanajua kuwaacha kwa manyanyaso wanawake hadi we mwanaume unajiskia vibaya

NB. Kwa namna alivo kutreat na maneno aliyokutamkia ni wazi kuwa huyo mwanamke Hana HISIA na wewe na hakupendi, kumbuka mwanamke anaweza ishi au kuolewa na mtu asiempenda na akamuigizia fresh tu, kwahiyo hatutaki uje ulete Tena uzi humu eti ohhh yule mwanamke amenifata anataka turudiane utakuwa MJINGA
 
"...hajibu wala hapokei simu yangu..."

"...anasema hataki kuongea na hajisikii kuongea na mimi..."

Kusanya nguvu zote hata kama ni kwa kuomba mizimu ya ukoo na kabila lenu nawe ukae kimya uone. Usimwandikie text wala kumpigia simu kabisa kabisa. Na hata gubu likija kumuisha akaandika au kukupigia simu jitahidi ukaushe tu halafu ulete mrejesho hapa. Huyu likely ana mtu mwingine au anajua jinsi unavyompenda na amejiaminisha kuwa ni lazima tu utamtafuta. Ukiuchuna na akajua kuwa she is replaceable na kwamba unaweza kumpiga chini ndo utaona hasa yukoje. Na akirudisha komwe lake tena weka msimamo wazi kuwa hupendi hilo gubu lake na uwe imara katika msimamo wako.

Kwa jinsi unavyozidi kumtafuta ndivyo unajishushia heshima na unazidi kujidhalilisha tu kwake; na kila wiki utakuwa unakuja humu kuanzisha nyuzi. Usipogangamara huyu atakusumbua sana!
Umetowa ushauri mzuri saana ila nilichogundua unamshauri mtoto wa darasa la tatu C kuacha kutembea na ufutio
 
Back
Top Bottom