Naona nikienda kuwa academician, nimechoka ajira kwenye private sector

Ukiwa kwenye NGO unaona ni mdogo maana unatumika mno na kuwa subjected into a lot of stress... Unaona kabisa unachopata doesn't worth your mental health
Napingana na hii dhana ya kunyonywa. Kinachofanyika ni kuwa NGO nyingi zinatumia International standards. Ambapo kama working hours ni 8 ni kweli inakuwa 8 na labda upate lunch break ya 1 hour. Kama ni kazi ni kazi kweli siyo kulembalemba. Hiki ndicho kinachofanyika kwenye nchi za wenzetu walioendelea.

Sisi tumezoea kufanya kazi saa 8 halafu katika hizo saa 8, saa 3 umezitumia kwenye social media na 2 hours kupiga stories kazini. Mambo kama haya utayakuta nchi maskini kama bongo tu. Sasa ukiwa subjected kwenye mazingira yenye system ya kazi kweli utaona mateso na kunyonywa.

Mie nitakubaliana na wewe kama muda wako wa kazi ni 8 hours halafu unafanyishwa kazi zaidi ya 8 hours na hulipiwi overtime. Otherwise ni ile dhana tu ya nchi maskini kama sisi ambao tumezoea uzembe na kupiga soga kazini huku tukizirura kwenye social media kama ilivyo wafanyakazi wengi wa Umma!
 
Kimsingi that was my dream job ila sasa sikufanikiwa kuokota the required grades. Nilimiss 3.8 Gpa by a few points it hurt me alot sababu naelewa nilihujumiwa tu na uwezo ninao. Huwa nawaza sijui nifanye post graduate na masters niweze ingia huko ila nikiwaza competition ilivyo dah.
Ila walimu wa chuo wana enjoy sana muda wao hasa wanaoishi campus.
Kilaza unajifariji 😂😂😂😂
 
Mleta mada nadhani uendelee kufanya research yako vizuri hasa unapodhani ukiwa academician unakuwa free zaidi na workload inapungua. Workload ukiwa academician inaweza kuwa kubwa pengine kuliko hata huko kwenye NGOs unazosema. Lecturers wengi huwa wanakosa hata muda wa kujibu emails. Wakati mwingine wanajibu hata baada ya wiki kutokana na wingi wa majukumu yao. Wanafanyia kazi emails zilizo urgent tu na ambazo zipo kwenye circle ya mazingira yao ya kazi.

Sema utofauti wa huko kwenye NGO na kwenye U-lecturer ni kuwa;

i) Kwenye mazingira ya vyuo vikuu mambo mengi yanakuwa well organized na more cordinated. Kwahiyo unakuta mambo ni mengi ila yanaenda very systematic tofauti na ilivyo huko kwenye NGO
ii) Kwenye vyuo vikuu mostly una-work independently na pressure iliyopo ni kati yako na majukumu yaliyo mbele yako. Tofauti na huko kwenye NGO ambako, tofauti na workload kuwa kubwa, bado unakuwa na pressure za boss wako.
iii) Ukiwa chuo kikuu hasa vyuo vya serikali na ukafikia level ya kuwa lecturer unakuwa huru zaidi kufanya maamuzi ya kipi ufanye kwa wakati upi, unaweza hata kuahirisha kipindi ukaendelea na shughuli nyingine mfano kazi za research na ukakipanga hicho kipindi wakati mwingine na wanafunzi wako. Tofauti na kwenye NGO ambako huwezi jifanyia maamuzi mwenyewe bila kuwa ana consequences.
iv) Hata hivyo, haimanishi ya kuwa unakuwa huru jumla. Na kwenyewe kunakuwa na administrators kama wakuu wa idara, college n.k ambako unawajibika kwao.

Mambo mengine kama kupanda vyeo, kuongeza elimu, maslahi naomba nisigusie maana watu wengi wameyazungumzia huko juu.
 
Daaah sema hapo vigezo sasa walivoweka.. labda private universities huwa wana relax conditions za GPA ila vyuo vya serikali naona wapo static kwenye GPA
Ndoivyo naona option nzuri ni kuongeza masters huku ukitafuta gpa above 4
 
Mafao ya kujitoa yanaitwa unalipwa ela yako yote ndio imeisha hyo sasa hela ikiisha sijui utafanyaje


Wakati mwenzako wa gavoo kila mwisho wa mwezi anachukua bado kiinua mgongo chake
Nani alikudanganya watu wa private hawapati mafao ya kila mwezi??
 
Nani alikudanganya watu wa private hawapati mafao ya kila mwezi??
Watanzania wengi hatuna utamaduni/tabia ya kufuatilia vitu kwa undani na kuujua ukweli.Ndio maana ni rahisi sana kuwadanganya Watanzania.
Mara nyingi huwa nasikia watu wanadanganyana hivi kuwa walio private hawana kiinua mgongo. Na mbaya zaidi, wengine hata ukijaribu kuwaelewesha wanakua wabishi bila facts.
 
Daa yaani mtu Ni muhasibu Kwenye UN agencies analipwa 6m, na allowance Kama zote, umlinganishe,na muhasibu wa Tamisemi anayelipwa laki 7
Hata mimi nimeshangaa.
Tatizo la wasomi wa Tanzania wana lack of confidence,uoga wa maisha.
Wanataka wapate kazi serikalini kwenye taasisi moja miaka yote hadi wazeekee hapo hapo.
 
Mafao ya kujitoa yanaitwa unalipwa ela yako yote ndio imeisha hyo sasa hela ikiisha sijui utafanyaje


Wakati mwenzako wa gavoo kila mwisho wa mwezi anachukua bado kiinua mgongo chake
Hiyo kiinua mgongo si hadi ufikishe miaka 60 na mvi zishakutoka hizo hela utaenjoy wapi.
 
Sidhani aisee, ni mmoja kwny watu 1000
Salary za private zinatofautiana sana kutokana na ukubwa wa kampuni na pia culture ya kampuni.
Pale Tanzania Breweries kuna waswahili walikuwa wanalipwa mishahara hadi 15m for managers.
So mishahara ya 4m,5m,6m ilikuwa ni ya kawaida sana.
Ila sijajua sasa hivi maana kampuni iliuzwa na kumilikiwa na watu wapya.
 
Back
Top Bottom